weka hapa jamvini acha porojo kaka,kama nidhamu ya majadiliano uliivunja mapema sana kwa Mohamed Said kwa maneno yako ya kejeli na dharau.Kulitaja kanisa ktk kuleta uhuru wa tanganyika ni kiroja.ushiriki wake ulikuwa wa kinafiki na kiini macho.Historia itabaki na haitabadilishwa kama mnavyotaka kufanya.
Sio muamini wa viroja, bali mimi ni muamini wa mang'amuzi ya nera! Una haki yakutomjua Shehe Issa bin Amir kwakuwa umelishwa yamini kwa ngano za chukizo! Shehe Issa mmoja wa wasomi wakiislamu wa mwanzo kabisa mwishoni mwa himaya ya dola ya kijerumani aliyejengwa kwa busara ya pwani, ndie aliyekuwa tunu ya hekima za waungwana mnamo miaka ya 1928 hadi miaka ya 1950! Ikiwa utaonyesha nidhamu ya majadiliano, Nikipata wasaa nitakupa habari za shehe huyu ambae alikuwa kiungo muhimu kati ya kanisa na uislam Tanganyika!
Last edited by a moderator:
