Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


100 Greatest Africans.

Kuna wapuuzi wengi tu ngoja niwataje kidogo.

Bob Marley, Pele, Maria Mutola, Michael Jackson, Miriam Makeba, Jay Okocha, Bill Cosby, Oliver Mthukuzi, Venus William, Serena William, Luambo Makaidi, Manu Dibango.

Ngoja niishie hapa nisitaje wengine.
 
WC,

Ala kumbe haya ni mazito.

Wakati naandika kitabu haikunipitia kuwa
iko siku haya yatahangaisha watu.

Hizo nyaraka nimeziona na ziko katika rejea
kama nilivyoonyesha.

Nimeweka taarifa ya Kaunda na Kenyatta.
Zisome.

Mpaka wanatia huruma haya yote ni mapya kwao lazima wapate mshutuko.
 
Mag, Unaandika kwa hamaki. Sijajua umekusudia nini. Labda utulie uandike upya.
Neno "mchochezi" "unaona matusi" yanafunika mantiki.

Mbona hili jambo linakutoa nje kiasi hiki? Ni historia tu ya wazee wangu isikuumize kiasi hiki.
mohamed hata dakika hii ukikiri kuwa uliyoyaandika ni historia tu ya wazee wako, huu mnakasha hata haungefikia hapa...lakini kudai kuwa ndiyo historia ya kweli ya harakati za uhuru wa Tanganyika, hapana hapo hatukuachii. Ingawa unadai Dar es Salaam unaijua lakini kumbuka wengine tumeingia humu wewe ukiwa bado kwenye mbeleko. Dar es Salaam tuliyoikuta siyo hii unayoiona leo...kama si mipango madhubuti ya awamu ya kwanza, kwa mfano "operation makuti", hadi leo sehemu kama Kariakoo, Ilala, Magomeni (Mapipa, Mikumi na Makuti), zingekuwa na sura ingine kabisa!

Zaidi ya hapo hakuna tusi kubwa kwetu wazee tuliokuwapo kama kudai Baba wa Taifa aliwapiga vita Waislaam kwa kuwanyima elimu!...sasa inapofikia hapo sina jina lolote kwako zaidi ya muongo na mchochezi...ndivyo nilivyo mimi Mag3, I call a spade a spade, sina ule uswahili wa kufunika kombe mwana haramu apite. Wewe Mohamed Said, ni zao la mdini kutoka Pakistan, mchochezi through and through bila samahani...hawa wakina Ilunga, Ponda, UAMUSHO ni matunda ya hila zako, you are the brain behind it all...kisa? Wazee wako hawakukwaa uongozi wa juu serikalini!
 
Nakuuliza, na kwa kunywa kikombe cha Babu sio Ushirikina?
Wewe na yeye wote wajinga na washirikina wa kutupwa! nakushangaa kijana wa kisasa bado unakumbatia ujinga huo! shame on you. Na ndio maana unayakumbatia maupuuzi ya mzee woko Mohamed Saidi bila hata kufikiri!
 
Mwanakijiji na wenzako mmeikosa ile golden chance ambayo mlipewa!!
Kuleta ile audio, kutoileta mpaka sasa kumetupa nafasi sisi wafuatiliaji kuamini kwamba kuna mambo yanayofichwa.
Huna unachokijua zaidi ya uchochezi wa Mohamed Saidi, pole mwanakwetu!
 

Ritz,

Mashaallah.

Hakika Allah amekujalia akili.
Quick thinking...

Allah akuzidishie.

Mimi ninachokiona kwa huyu ndugu yangu ni kibri na jeuri.

Imenishtua kwa kweli kwa kuwa kwangu mimi hapa nakuchukua
kama barza ya kubadilisha mawazo.

Bahati mbaya naona huyu mwenzangu pamekuwa pa uadui na
pa kutukaniana wazee wetu.

Ndiyo nikasema naona ameghadhibika atulie kidogo.

PS:

Rafiki yangu alinichukua hadi Brooklyn Heights New York mahali ambako
walikuwa wanatengeneza zile series za Cosby Show.

Rafiki yangu mwingine alikwenda kunionyesha ukumbi alokuwa akipiga Bob Marley
Finsbury Park, London wakati Marley hajawa maarufu na huyu rafiki yangu wakijuana
vyema.

Manu Dibango kaja kufanya Show Harare mimi niko pale.
Mji umepata wazimu na Makosa Man!
 

Ah, sasa nimekuelewa - mkuu nilisha sema humu kwamba Ndugu Mohamed Said is not some monster; sijui kwa nini baadhi ya wana JF wanamuogopa kupindukia - yeye kaandika kitabu chake baada ya kufanya utafiti kwa madhumuni ya kurekebisha pale palipo pinda, sasa kama baadhi ya wasomaji wanaona kuna vitu ambavyo havijafafanuliwa vizuri, cha kufanya ni kumuomba atoe maelezo ya ziada au wenye kujua mengine ya ziada wamshauri arekebishe vipengere ambavyo vimekaa ndio sivyo alafu msikilizeni anatesema nini, lakini tujikita katika malumbano ambayo hayana tija yoyote au kumsema vibaya, actually ninacho ona mimi ni as if kuna ushindani wa aina fulani vile - kama dunia inakubali kihistoria kwamba Wamerikani ndio walikuwa wa kwanza kutua mwezeni, sasa tatizo liko wapi!! Hata mimi zamani nilikuwa na mawazo kama hayo hayo kwamba ukombozi wa Taifa letu dhidi ya Waingereza alianzia mwaka 1954 na akina Paul Bomani, Rashid Kawawa, Titi Mohamed, Kambona na Nyerere nk - hiyo ndiyo historia tulikuwa tunaisikia tukiwa shule ya msingi!! Nilikuja kushtuliwa kutoka usingizini baada ya kukutana na mzungu mmoja (Mwingereza) nikiwa nje masomoni, ikabidi nifanya kazi ya ziada kuelewa ni kitu gani hasa kilikuwa kinajiri wakati wa ukoloni wa Waingereza ndani ya Tanganyika, hicho ndio kilinifanya kidogo nitofautiane na nyinyi katika misimamo yenu.

Hili la bwana Jericko kusema kwamba ndugu Mohamed Saidi ana uwezo wa kunilisha ngano za masika (hapa sijui unamanisha nini!! Najua kiswahili changu kiko a bit rusty lakini hapo nimetoka kapa)! Mkuu Jericko naweza kuelewa your concern katika hilo, lakini nataka kukuhakikishia kwamba ndugu Moh hana uwezo wa kulisha watu mambo ambayo hawayataki kuyasikia - lakini ukiona wasomaji zaidi ya 8K wamepitia uzi huu so far ujue kuna jambo, kumbuka wengi wao wanasoma tu bila ya ku-comment chochote!

Mkuu labda nikufahimishe kwamba najua mambo mengi kuhusu Taifa letu, kwa kulezwa na baba yangu mzazi ambaye aliwahi kuwa Mwalimu pale Tabora mmoja wa wanafunzi wake alikuwa ni Baba wa Taifa, Mh.Kambarage alipokwenda masomoni Makerere mzee wangu alihamishiwa Sekondary ya Bwiru Mwanza - hapo alikutana na mwalimu mwenzake ambaye alikuwa sijuhi ndugu au mjomba wa Kambarage sikumbuki vizuri (lakini nafikili Andrew anaweza kuwa na kumbukumbu kama aliwahi kuzungumza na baba yake kuhusu huyo mwalimu jamaa yao) sasa Kambarage alipokuwa anakuja likizo kutoka Uganda alikuwa na kawaida ya kupitia Bwiru kwa jamaa/ndugu yake huyo kumtembelea na kukutana na mzee wangu kwa mara nyingine, baadae mzee wangu alibadirisha kazi na kuajiliwa katika mambo ya Public Relations na Serikali ya Kingereza na akawa na access kubwa ya Public Addressing Systems na vifaa vingine, kwa hiyo Kambarage alipokuwa anatembelea mikoani akifika kwetu mzee wangu alikuwa anampatia Nyerere system hizo kutangazia wananchi kinyume cha matakwa ya mwajiri wake i.e Wakoloni hivyo hakujali kupoteza ajira yake pindi Waingereza wangepata tetesi kwamba anamsaidia Kambarage, hivyo mzee wangu alikuwa anamfahamu vizuri Kambarage.

Mkuu kuna mambo mengi ninayo yafahamu lakini siyasemi, nilipata bahati ya kwenda nje na kukutana na na Mzee mmoja Mwingereza ambaye aliwahi kuwa PC wakati wa ukoloni, yeye ndiye aliye nishtua kuhusu harakati za wenzetu Waislaam kuhusu kupinga ukoloni - alisema walikuwa wanawapa wakoloni wakati mgumu kwa kuwa walikuwa well organised na ilikuwa si rahisi kuvunja mikakati yao kwa kuwa walikuwa na mbinu nyingi sana - walijaribu kuwatumia baadhi ya Waislaam
katika mambo ya upelelezi kuhusu nyenendo zao bila mafanikio ya kulidhisha mmoja wao nadhani alikuwa ni mtu Kutoka Kagera - Kweyamba kama sikosei, ndugu Moh anaweza kutusadia katika hilo. Sasa mzungu wa watu alikuwa na maslahi gani katika kunieleza ukweli huo; kwa nini hatutaki kukubali kwamba mambo mengi aliyo andika ndugu Moh yana ukweli ndani yake - ndugu zangu kwani tukikubali tutapoteza nini? Turekebisha pale penye mapungufu au palipo sahaulika bila ya kujali kama mleta marekebisho ni mwislaam, mkristo au mpagani.
 

ni wapuuzi kwako, ila sio kwa wengine... Sio wote wana mtazamo kama wako...
 
NATAMANI WATUNGE MTIHANI MASHEHE wasahihishe mashekhe alafu tuhakiki kama sio madudu tu tutaona,,waislamu wenye maendeleo wenyewe hawataki hii kitu wanaita itikadi kali,,,,
 
Jamani ni uendawazimu kujaribu kuulinganisha mlima na kichuguu...

 

Na hutamsikia anaenda kuwatetea wenzake mahakamani, au kumsikia anasimama kuandamana kupinga kufungwa kwao...
 

Mohamed Said,

Huyu jamaa juzi alisema wewe unaleta uchochezi yeye na wenzake wanahubiri upendo kwa Waislam na Wakirsto.

Leo huyo huyo anajitapa kuwa anahubiri upendo anakuambia kwake ni tusi kubwa wewe kuwataja Abdulwahid Sykes na Mshume Kiyate.

Huyu mtu ni wakumpuuza tu.
 
Msamehe kasoma harakaharaka.
Darwin, mimi nililiacha nikidhani kuwa limeeleweka lakini inaonekana kana kwamba mimi ndiye sijui kusoma. Kuna uwezekano sijui na naomba msaada ndio ilm yenyewe.
Tafadhali sana soma sentensi, angalia koma na nukta halafu uniambie wewe umeelewaje
Kwanza lengo kubwa lilikuwa kumwambia Mohamed kuwa anapotaja orodha ya watu halafu wengine akawawekea majina ya kabila wasomaji makini wanaelewa kwa mtazamo tofauti na wasomaji tu ili mradi kasoma.

Katika majina yote ni mawili ameyawekea kabila.
Mohamed anachotaka kuueleza ulimwengu ni kuwa ukombozi wa nchi hii ulitegemea sana ukabila na dini.

Baada ya kuwaondoa wakristo katika maandishi yake kilichofuata ni kuingiza ukabila yaani Umanyema na Unubi ili baadaye aunganishe na ujio wao kama waislam kukamilisha azama yake.

Jiulize kwanini wafuatao hawakuwekewa makabila yao! Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Raikes Kusi, Rawson Watts and Cecil Matola!

Hata siku moja hutamsikia Mohamed akimzungumzia Nyerere na Uzanaki wake. Sababu kubwa ni kuwa uzanaki hauwezi kumtia Nyerere katika hatia na hukumu inaweza kuwa ndogo kuliko inavyotakiwa.

Badala yake utamsikia akimnasibisha na Ukristo na Kanisa ili kuunganisha dot zake hasa kwa wale wanaosoma maandishi na sio wale wanaosoma na kuelewa.Kwa bahati mbaya kundi linalosoma tu maandishi bila kutafuna ni dogo sana hapa JF

That's my the main point. Sasa bila kuondoa nukta Mohamed anakana maneno yake na kusema nimemuwekea.
Hajibu hoja anatueleza majirani zake. Yote hiyo ni kutaka kufunika contradiction na hiden agenda niliyoieleza.

Niambie ndugu yangu, hivi hapo juu kwenye quote maneno hayo ni ya watu wawili tofauti au ni mmoja
 
Ritz, mapovu ya nini? anayeandika vitu hapa bila ushahidi ni huyo mzee wako Mohamed Saidi. Akidaiwa ushahidi amekuwa ama ananukuu ngano zake au akijibu majibu ya kihuni.. andikeni na nyie historia ya wazee wenu..si shindani hapa.. mimi ni scholar nimetembea nchi nyingi.. zomba wape dozi... Ritz wajibu hao..
 
Wewe mtoto wacha uzushi, ukweli unaouimba hapa uko wapi? rudi shule kajifunze kufikiri kwa kutumia akili yako na sio ya kuzima kutoka kwa Mohamed Saidi! anakupoteza wewe, ona vijana wenzako wanavyo kudharau!
 

Ritz,

Hawa jamaa wako katika mshtuko mkubwa.

Kuwa Abdulwahid akijuana na Kenyatta mdogo wake Ally
akiandikiana na Kaunda...

Baba yao kakutana na watu maarufu wa wakti wake Donald Cameron,
Dk. Aggrey, kaasisi African Association kaandika maisha yake leo hii
ni moja ya nyaraka muhimu...

Haya naona yanawapa shida achilia mbali ile historia ya Abdu Sykes
mwenyewe.

Njia ya kutokea kwao ni hizi kejeli, matusi nk.nk.

Wanafananisha na wazee wao kwa wakati ule walikuwa wanafanya nini...

Wanashindwa kukubali kuwa Allah humpa amtakae bila ya hesabu.
Mimi simjibu tena huyu ndugu yangu.
 
Hili lilikuwa ni zoezi lililoendeshwa na New African kwa wasomaji kutoka kila pembe ya Afrika na dunia...kuna majina tunayataja humu ya watu ambayo hayakuweza hata kujitokeza kwenye orodha ya watu milioni moja! Hilo ndilo linanipa taabu...kwa nini hakuna hata jina moja la wazee Mohamed Said wa Gerezani lililojitokeza?

 
Last edited by a moderator:

umetoa mfano mzuri sana; mchango wa babako ni muhimu katika historia ya Uhuru wa nchi yetu. Kumbe Nyerere alikuwa anapta msaada wa watu wengine nje ya Dar-es-Salaam. Swali kwako: Je familia yako inamchukuliaje Nyerere baada ya uhuru? Je aliidhulumu familia yako kwa kutowapa upendeleo maalum? Je Nyerere aliamuru jina la babako lisitajwe kwenye historia yetu ya Uhuru? Unafikiri Nyerere ana chuki dhidi ya familia yako kwa vile hakuwakumbuka baada ya Uhuru?
 
Huna unachokijua zaidi ya uchochezi wa Mohamed Saidi, pole mwanakwetu!

Sina ninachojua mimi nimsikilizaji tu ;-))
Wewe umeprovide nini hapa?
Afadhali huyo MS anaumiza kichwa au tuseme working hard kuelezea anachokijua.
Wewe umeandika nini kikawaingia watu akilini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…