Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Nyambala,

Kunijibu au kutonijibu hiyo ni khiyari yenu.
Juu ya hayo kama kunijibu mbona mmechelewa sana?

Hiki kitabu kimechapwa Uingereza kwa mara ya kwanza
kwa Kiingereza mwaka 1998.

Kimechapwa Kenya kwa Kiswahili 2002.

Sasa anapokuja mtu na kusema ananijibu leo mie nauliza
siku zote alikuwa wapi?
 
Mohamed,
Umemtaja mzee Aikaeli Mbowe. Ngoja nikupe kisa kimoja kumhusu huyu mzee na ulinganishe na malalamiko yako ya Nyerere kuwasahau akina Dosa Aziz wakati alipokuwa Ikulu. Mzee Mbowe alikuwa na shida sana kukutana na Nyerere kila alipokwenda Dar-es- Salaam. Alitumia kila mbinu, akipiga simu Ikulu kuomba appointment lakini wale wasaidizi wa Mwalimu ambao hawakumjua, walimzuia. Mzee Mbowe aliamua siku moja kusubiri pale nje ya gate wakati Nyerere anakwenda Ikulu. Nyerere akamwona pale nje, akashuka kwenye gari lake na kumuuliza mbona anasubiri nje. Akamwelezea shida aliyokuwa nayo kukutana naye. Basi akamshika mkono akaenda naye Ikulu. Akawaambia wale maafisa wake kuwa kuanzia siku hiyo, kama huyo mzee anataka kuonana naye asiwekewe pingamizi.
 
Inatosha tu kukuambia kuwa kama umekutana na nyaraka za wazee
wangu huko ulikozikuta mbona basi Kivukoni College walipoandika
wazee wangu hawakutajwa katika kitabu chao ''Historia ya TANU 1954-
1977?''

Kama unaamini historia ni lazima iwe kwenye kitabu kimoja tu basi wanasema imekula kwako. Wewe umesoma kitabu kimoja na ukajiridhisha kuwa kilipaswa kuandika kila kitu (kikubwa na kidogo) kilichotokea katika historia. Huu ni uelewa finyu wa uandishi wa kihistoria. KUweza kuelewa historia ya TANU ni muhimu kusoma katika sehemu mbalimbali na ni katika kufanya ihvyo ndivyo tunavyoweza kuelewa histtoria yote.

Leo hii mtu akitaka kuandika historia ya Uhuru wa Tanganyika atafanya makosa kama hatosoma kitabu chako. Kwa sababu na wewe umechangia kwa sehhemu yako kuielewa historia hiyo. Ni makosa kudhani kuwa wewe umeandika historia yote na kweli tupu. Abdu Sykes, na ndugu zake wametajwa kwenye maandishi mengine ya historia ya TANU au ya matukio muhimu ya TANU.

ILikuwa makosa kwako kudhani kuwa kwa vile hicho unachoita "Historia ya Kivukoni" hakikutaja baadhi ya majina basi TANU haikuwahi kuwapa heshima na kuwataja kwa hadhi zao kina Sykes. Umeongozwa mno na hisia kiasi kwamba umeacha kuandika historia.
 
Sasa anapokuja mtu na kusema ananijibu leo mie nauliza
siku zote alikuwa wapi?

Labda hhawakujua hatari ya yale unayoyadai kwani kwa muda mrefu wengi walidhani ni kitabu ambacho umewalenga Waislamu tu. Ni mpaka watu wengine nao walipoanza kukisoma na kuelewa upotoshaji mkubwa uliofanya ndani yake ndio maana leo unapingwa. Utawala wa histohisia umefikia tamati!
 

MM,
Nimekusoma.

Ikiwa ndiyo tumehitimisha hiyo ni kheri sana kwetu
sote kwa maana mjadala kuhusu kitabu umekamilika.

All is well that ends well.
 
MM,
Nimekusoma.

Ikiwa ndiyo tumehitimisha hiyo ni kheri sana kwetu
sote kwa maana mjadala kuhusu kitabu umekamilika.

All is well that ends well.

kwa mfarakano baina ya Wakristu na Waislamu ambao umeuanzisa kweli unaamini 'all is well that ends well"? It hasn't ended well yet sir.. you brew trouble unhindered...
 

MM,

Sheikh Hassan bin Amir katajwa?

Vipi Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Halima Selengia, Fundi Muhindi,
Shariffa bint Mzee, Amina Kinabo, Abdallah na Maulid Kivuruga, Sued
Kagasheki, Abdallah Rutabanzibwa, Salum "Ndege Mwema" Abdallah...

Umekutana na majina haya?

Omar Suleiman, Haruna Taratibu, Ali Migeyo, Shariff Attas, Msham
Awadh, Bantu Group, Saniyyat Hubby, Al Watan, Egyptian, Bomba
Kusema...

Ingekuwa mimi naamini nimeandika historia yote nisingekuhimizeni
nanyi muandike.

Mikasa kabla na baada ya uhuru...
Nimekusoma hata hivyo.
 
MM,

Sheikh Hassan bin Amir katajwa?

Vipi Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Halima Selengia, Fundi Muhindi,
Shariffa bint Mzee, Amina Kinabo, Abdallah na Maulid Kivuruga...

Mikasa kabla na baada ya uhuru...
Nimekusoma.

Hivi kweli unafikiri kuna historia inawataja kila mtu ili kuonekana mtu yuko fair? Hakuna mtu anayeandika historia akaweza kuwataja wote hadi watu aliokuwa anasalimiana nao subject. Kweli kabisa katika uelewa wako wote ulitegemea historia ni lazima iwataje watu wote wa Dar-es-Salaam ambao walifahhamiana na Nyerere? Hivi kweli unafikiri wote ambao waliotoa mchango wao kwa namna moja au nyingine katika harakati za uhuru wametajwa au walipaswa kutajwa?

Kwa kweli ungeweza kabisa kuwataja wale wengine waliotoa mchango katika harakati za Uhuru bila a. Kumshambulia Nyerere na b. Kuwaacha wengine kwa sababu ya dini zao. Ulichokifanya kwa kweli ni disservice to the nation. Umeingiza udini kwenye historia na sasa historia ya Tanganyika inasomwa katika sehemu mbili "Waislamu Vs. Wakristu". Ulichokifanya ni kibaya zaidi kuliko unavyofikiria. Unaweza ukafikiri umepata sifa na heshima mbele ya Waislamu lakini kwa kweli umewafanyia faraka ndugu zako na utakuwa muungwana ukitambua hilo na kulirekebisha. Hakuna sifa katika faraka.
 
Jasusi,
Inasisimua sana.

Nikimfahamu Mzee Mbowe ndani ya Mercedes yake
nyeusi na katia suti.

Siku zote.
Natoka shule napita pale ofisini kwake.
 
Soma historia uone nani aliyefarakisha watu.
Namba moja ni wewe unayetoa madai usiyoweza kuyathibitisha bali kunukuu maandishi yako mwenyewe.
Ni wewe usiyeweza kutoa tafiti bali tafiti ya warsha ulioifanya wewe chini ya usimamizi wa raia wa Pakistan.

Ni Mohamed Said anayefundisha watu kulalamika bila kuweza kutetea malalamiko yako.
Ni wewe unayechukia wanadam kwasababu tu hawafuati imani yako
Ni wewe unayedhani Umanyema, uzulu na Unubi ni bora kuliko raia mwingine.

Ni wewe unayeeneza uongo, chuki, farki na kufitinisha jamii ili uuze vitabu.
Ni wewe mwenye kiu ya kuona damu ya mwanadamu inamwagika kwa gharama zozote.
Ni wewe usiyetaka kuleta utangamano wa taifa bali kuligawa kwa makundi.

Ni wewe uliyejipa haki miliki ya kuamua nani mwislam nani kafir! hata kama maneno na matendo yako hayakupi nafasi

Anayedhani wewe ni wa kudharauliwa basi ajiulize tena. Wengine wakitumia kalamu kugundua maarifa ya kumkomboa mwanadam wewe unatumia kalam ya kumwangamiza.
Kalamu yako ni kubwa maana ina rangi nzuri na za kuvutia hasa kwa wale wapendao rangi hata kama haina wino.
 

Nguruvi,
Umeghadhibika.

Mtu akighadhibika uungwana ni kumtuliza kwanza.
Utakapotulia Insha Allah ntakujibu yote.
 
MM,

Vipi kuhusu yalosemwa na Njozi, Bergen, Sivalon...
Na wao wamezua uongo?

Kuna tofauti kubwa kati ya walichoandika wengine na unachohfanya wewe. Njozi anakaribiana na wewe lakini unaona siku hizi ameback down na yuko more sober. Yeye aliyedai kuwa Wakristu wanapendelewa kwenye Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro alikuwa na asilimia 80 ya wakufunzi Wakristu! Hamkuwahi kumuuliza kwanini.. kina Bergen na Sivalon hawajesema unachosema wewe.

Kuna tofauti kati ya facts na opinions; they dealt with some certain facts, you on the other and have tried to create facts out of your own opinions.
 

MM,
Nimekusoma.
 
kwa hiyo wazee wangu mnakasha umeisha au?
kwa mara ya kwanza naona mnakubaliana.

Z,

Mimi sikuja humu kutafuta suluhu.

Mimi nimekuja hapa kueleza yale
ambayo hayakuwa yanafahamika.

Itakapofika wakati kuwa waloweka
uzi huu wataona pametosha basi
hapo ndipo tutahitimisha Insha Allah.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…