Kama unaamini historia ni lazima iwe kwenye kitabu kimoja tu basi wanasema imekula kwako. Wewe umesoma kitabu kimoja na ukajiridhisha kuwa kilipaswa kuandika kila kitu (kikubwa na kidogo) kilichotokea katika historia. Huu ni uelewa finyu wa uandishi wa kihistoria. KUweza kuelewa historia ya TANU ni muhimu kusoma katika sehemu mbalimbali na ni katika kufanya ihvyo ndivyo tunavyoweza kuelewa histtoria yote.
Leo hii mtu akitaka kuandika historia ya Uhuru wa Tanganyika atafanya makosa kama hatosoma kitabu chako. Kwa sababu na wewe umechangia kwa sehhemu yako kuielewa historia hiyo. Ni makosa kudhani kuwa wewe umeandika historia yote na kweli tupu. Abdu Sykes, na ndugu zake wametajwa kwenye maandishi mengine ya historia ya TANU au ya matukio muhimu ya TANU.
ILikuwa makosa kwako kudhani kuwa kwa vile hicho unachoita "Historia ya Kivukoni" hakikutaja baadhi ya majina basi TANU haikuwahi kuwapa heshima na kuwataja kwa hadhi zao kina Sykes. Umeongozwa mno na hisia kiasi kwamba umeacha kuandika historia.
MM,
Sheikh Hassan bin Amir katajwa?
Vipi Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Halima Selengia, Fundi Muhindi,
Shariffa bint Mzee, Amina Kinabo, Abdallah na Maulid Kivuruga, Sued
Kagasheki, Abdallah Rutabanzibwa, Salum "Ndege Mwema" Abdallah...
Umekutana na majina haya?
Omar Suleiman, Haruna Taratibu, Ali Migeyo, Shariff Attas, Msham
Awadh, Bantu Group, Saniyyat Hubby, Al Watan, Egyptian, Bomba
Kusema...
Ingekuwa mimi naamini nimeandika historia yote nisingekuhimizeni
nanyi muandike.
Mikasa kabla na baada ya uhuru...
Nimekusoma hata hivyo.