Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Shukrani sana ndugu.

Ritz,

Karibu.
Tumekutandikia busati jipya.

Tumeagiza kahawa safi toka
Ethiopia.

Zomba kaahidi kuja na halwa
ya lozi.

Uje na rafiki yangu Yericko.
Insha Allah.
 
BAKWATA ilianzishwa kuwanusuru na janga la bloodbath between yourselves.Mzee Masasi alijitahidi sana kwa cause ya waislam Tanzania

Son...
Nina kisa kizima lakini tukikianza hapa tutakesha.

Amini upendavyo.
Ila leo Waislam wamejua kisa cha kuvunjwa EAMWS.

Na wanajua nani alitoa ruksa akina Sawaya wapite
majimboni wakihonga fedha BAKWATA ikubaliwe.

Mengi. mengi leo yanafahamika.
Kabla hawajafa akina Rashid Kayugwa walieleza yote.
 
Mimi mzee nikikusupport wanasema nilamba viatu vyako lakini mzee kuhusu ili swala la BAKWATA yaani umeongea points sana NYERERE NDIE ALIYEANZISHA BAKWATA hilo swala wala halihitaji tochi ishaalah mzee MS mungu akujalie umri.

BH,

Amin ndugu yangu.

Ndiyo maana hadhi ya Nyerere imeshuka mbele
ya macho ya Waislam.

Huu ni ukweli.

Unatisha unaogopesha lakini huu ndiyo ukweli
unaotukabili hivi sasa.
 
BH,

Amin ndugu yangu.

Ndiyo maana hadhi ya Nyerere imeshuka mbele
ya macho ya Waislam.

Huu ni ukweli.

Unatisha unaogopesha lakini huu ndiyo ukweli
unaotukabili hivi sasa.
Na inazidi kupanda mbele ya Watanzania wanaoitakia nchi hii mema. Wiki chache zilizopita, wiki ya mwisho ya mwezi Februari hapa Marekani wanaadhimisha president's day. Wakati natembea kwa mazoezi nilishangaa jirani yangu mzungu kaweka picha kubwa ya George Washington mlangoni kwake, ingawa president's day ni ya marais wote waliotangulia mbele ya haki Marekani. Nikajiuliza, iweje huyu jamaa kaamua kuadhimisha George Washington peke yake? Jibu likaniijia haraka, "founding father." Ndiyo Nyerere huyo. Licha ya laana tulla zenu Nyerere ataendelea kuenziwa na majority ya Watanzania.
 

Mzee Said, this is too low kwa Mwandishi na 'Mtafiti' kuamini kuwa watuhumiwa hao Wislamu wamekamatwa kwa kuonewa kwa kusikiliza wanavyojitetea mbele ya Hakimu. Ni dni baya mno, na inaonyesha dhahiri kuwa kwako linapokuja suala linalohusu Waislamu basi unalihusisha moja kwa moja na kuonewa kwa Waislamu, hili si jema katu na linaonyesha jinsi gani jinsi ulivyo 'biased' linapokuja suala la Uislamu.

Kama 'utafiti' uliopelekea Kitabu chako ni wa aina hiyo, kusikiliza upande mmoja na kuhitimisha kuwa ni ukweli basi unafanya kosa kubwa sana kiutafiti maana hata katika uandishi wa kawaida wa habari tu, unamdai Mwandishi kudi taarifa na upande wa pili.

Umenisikitisha sana kkabisuchukua utetezi wa vijana hao waliokamatwa Ijumaa kuwa ni kweli na amina, hili linakuondoa kabisa ktk ethics za uandishi na utafiti.
 
Mohamed Said umesema wakati wa kugombania uhuru,kabla nyerere ajahutubia kulikuwa na mtu anapandisha munkhar/kuhamasisha kabla nyerere ajaingia kufunga kazi.Tumekuomba utumie lugha ya ki academia hii lugha "hadhi ya nyerere imeshuka mbele ya waislam"kama vile unaongea kariakoo shimoni waachie vichwamaji akina Ritz wewe shusha nondo
 
Last edited by a moderator:

Yakhe, ulichotuwekea hapa hakisomeki. Inahitaji miwani ya darubini.
 
Ritz,

Karibu.
Tumekutandikia busati jipya.

Tumeagiza kahawa safi toka
Ethiopia.

Zomba kaahidi kuja na halwa
ya lozi.

Uje na rafiki yangu Yericko.
Insha Allah.

Mohamed Said,

Shukrani sana maalim wetu na mie nimekuja na zawadi ya bokoboko la mbuzi na swamri kidogo, pamoja na vipopo, jerebi, pera maziwa pamoja na radu.

Ndugu yetu Yericko atafaidi sana ngoja nimwambie zomba, ampe kwanza ngisi wa kuchoma.
 
Last edited by a moderator:
Jasusi,

Citation iko hapo na pg. no.
Mohamed,'
Samahani kama nitakuwa nakusumbua. Umesema hiyo citation ya kanisa kuona uislamu kama adui iko page 37 katika toleo la 1992. Mimi nina toleo la 2001 na page 37 inazungumzia jinsi viongozi wa kanisa walivyounga mkono ujamaa: 1967- 1977. Hapa nitakutajia chapters (sura) zilizomo kwenye hicho kitabu ili uniambie ni sura gani kwa sababu huenda page zinatofautiana kati ya toleo la 1992 na 2001 ambalo ndilo ninalo. Sura ya 1 ni Utanguliz. Sura ya 2 Viongozi wa Kanisa Katoliki na Watawala wa TANU/CCM. Sura ya 3: Mafundishi Rasmi ya Maaskofu Juu ya Siasa na Uchumi 1953-1966. Sura ya 4: Viongozi wa kanisa walivyounga mkono ujamaa: 1967-1977. Sura ya 5: Viongozi wa kanisa walivyosita kuunga mkono ujamaa: 1967-1977. Sura ya 6: Viongozi wa kanisa na hali ngumu ya maisha 1977-1985. Sura ya 7: Muhtasari. Ningependa kujua ni sura gani hiyo quote inapatikana ili niisome na kuona mukhtadha wake. Asante sana.
 

Jasusi,

Hunisumbui hata kidogo.

Ni wajibu wetu pale tunapoona jambo
halijakaa sawa kusahihishana.

Nipe muda nikitafute kitabu kisha Insha
Allah tutalinganisha notes zetu.
 
Mohamed Said,

Shukrani sana maalim wetu na mie nimekuja na zawadi ya bokoboko la mbuzi na swamri kidogo, pamoja na vipopo, jerebi, pera maziwa pamoja na radu.

Ndugu yetu Yericko atafaidi sana ngoja nimwambie zomba, ampe kwanza ngisi wa kuchoma.

Ritz,

Jamani msilete hatari kisha lawama ikaniangukia mie.

Huyu Jericko itabidi tumuulize kwanza asifakamie akaja
kuamkia Muhimbili.

Mimi nitakuwa simo.

La akisema hawezi vyakula hivyo bora nimchukulia nyama
choma mbuzi na ndizi za kuchoma.
 

Son....

Una nongwa!
Sawa nimekusikia sahib yangu.

Maana mie ndiye ''academician'' humu.

Najua unanipaka mafuta kwa mgongo
wa chupa.

Lakini ujue fumbo mfumbie nani vile?
Utamalizia.
 

Wimana,

Mvaaji ndiye ajuae wapi kiatu kinabana.
Labda nikuongezee.

Huku kwetu jeshi la polisi linachukuliwa
kama ''armed wing of the Church.''

Unajua ndugu yangu kwa hali yako kama
Mkristo hujaonja kubaguliwa.

Siku hiyo hapakuwa na maandamano hapa
Dar es Salaam kote.

Huyo alokamatwa ananihusu na ninajua mie
nikisemacho.
 
Mohamed Said,

Shukrani sana maalim wetu na mie nimekuja na zawadi ya bokoboko la mbuzi na swamri kidogo, pamoja na vipopo, jerebi, pera maziwa pamoja na radu.

Ndugu yetu Yericko atafaidi sana ngoja nimwambie zomba, ampe kwanza ngisi wa kuchoma.

WEWE unavamia,jelebi,pera maziwa(penda) na ladu ni shuguli za wadosi
 

Jasusi,

Nilifika George Washington Memorial hapa Washington na nikaona
ile video inayoonyesha mapambano yake na Waingereza.

Najua ushafika hapo na unayajua vyema makumbusho hayo.

Nilichukua muda mrefu katika makumbusho haya na kwa hakika huyu
shujaa anastahili kuenziwa na Waamerika.

Nimepita George Washington Bridge nikielekea New Jersey kutoka New
York nimeona sanamu ya Washington na farasi wake na nikaonyeshwa
sehemu alipowachenga Waingereza wakati wa vita vya ukombozi.

Lakini Washington anaenziwa kwa kile alichowafanyia wananchi wake.

Nyerere ataenziwa na hakuna awezae kuzuia hilo.

Lakini juu ya kuenziwa kwake atakumbukwa halikadhalika kwa yale aloacha
nyuma.

Jamii moja imeneemeka nyingine hohehahe na hata kuandika historia yao
walikuwa wanatishwa.

Najua hili linakuhusu.
Leo nilikwenda mazikoni makaburi ya Kisutu.

Nimefika katika kaburi la mzee wako Abdu Sykes na mwanangu ndiye aliyesoma
dua.

Pembeni yake liko kaburi la mama yetu, mkewe mama yake Kleist Bi. Mwamvua
Mrisho Mashu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…