Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Wild Card,

Kuna mambo kamwe hutayaelewa hadi uwe Muislam.
Unazungumza kuchomoka...

Unadhani Ponda anajuta kuwa pale alipo?

Ponda ameingia katika orodha ya waja wema wa Allah
ambao kawataja katika Qur'an.

Wale wanaosimama kuipigania dini yake kwa mali na nafsi
zao.

Ponda hakuvamia kiwanja kile.
Kiwanja hicho ni mali ya Wakfu ni mali ya Waislam.

Mtu havamii mali yake.

Ama mie kuwa shahidi wa Ponda hilo naliomba kila nikenda sijda.

Nikilipata hilo nami nitakuwa nimeunganishwa na kipenzi changu
marehemu Sheikh Hassan bin Amir.

Nasikitika Allah bado hajanikubalia dua yangu.
 

Naomba kuwajua hao waislamu wanafiki ambao mzee huyo wa Tabora aliwataja wote hapo mahakamani.
 

Mohamed Said,

Mara ya mwisho kumuona huyu Mzee wetu mzalendo ilikuwa mwaka 1990.

Hawa ndugu zetu humu ukumbini watasema hizo ni ngano.

Lakini bahati nzuri watu wamemuona na kumsikia Mzee wetu Bilal Waikela.
 

Nasikia Manji ndie hasa alikua anangoja Ponda aingie ktk kumi na nane zake. Bakwata wamepewa viwanja vingi sana hasa mijini na wajane na watu mbalimbali waliotoa wakfu viwanja they are so good at selling them to businessmen hata kariakoo nasikia kuna viwanja vingi wameuza. sasa ponda kama alikichukua kwa nguvu hakuwa sahihi kukitwaa kwa Manji angewafuata Bakwata na wao ndio wana jurisdiction
 
Umeona kesi inakoelekea? Kulekule kwenye simulizi zako. Ushahidi kama huu utamsaidiaje Ponda? Hachomoki!
 
Unadhani Ponda anajuta kuwa pale alipo?Akili na mawazo ya wafia dini haya. Mzee Mohamed, una tofauti gani na Osama bin Laden?
 
Mwambie Sheikh Ponda akuorodheshe kama shahidi wake. Sijda haitakufanya uwe shahidi! Sijui kwa nini serikali nayo imekuacha katika hili wakati Ponda ni mtekelezaji tu wa maandiko yako!
 
Umeona kesi inakoelekea? Kulekule kwenye simulizi zako. Ushahidi kama huu utamsaidiaje Ponda? Hachomoki!

WildCard,

Uislam umetakaza kufanya dhulma wa kuruhusu dhulma anachofanya Ponda nikupambana na dhulma.

Huko kuchoma au kutokuchoma siyo issue Sheikh Bilal Waikela aliwekwa ndani na Nyerere leo yupo wapi na Nyerere yupo wapi.

Allah ana njia nyingi za kuwasaidia waja wake.
 
Dhulma kwenye kiwanja hiki kafanya nani na kafanyiwa nani? Aliyekiuza BAKWATA, taasisi ya Kiislam. Aliyekinunua Muislam safi kabisa ambaye kila kilipo kiwanda chake na msikiti upo!
 
Mwambie Sheikh Ponda akuorodheshe kama shahidi wake. Sijda haitakufanya uwe shahidi! Sijui kwa nini serikali nayo imekuacha katika hili wakati Ponda ni mtekelezaji tu wa maandiko yako!

Unataka kusema Ponda naye ni victim wa mandiko hayo duh!!
 
Unataka kusema Ponda naye ni victim wa mandiko hayo duh!!
Sheikh Ponda haoni wala hasikii kwa maandiko ya mzee Mohamed. Nadhani katika vitabu alivyonavyo huko rumande, hiki cha mzee Mohamed ni cha pili kwa umuhimu baada ya Quran Tukufu
 

Mzee Saidi kuna wakati nikisoma maandishi yako najikuta nacheka peke yangu, ngoja nikukumbushe kidogo hapo nyuma nilikuuliza swali, ukazuga kama hujasikia kama kawaida yako. Baadae Son of Alaska akasisitiza.


Ukadai nimeuliza kwa kukupima uwezo au? Swali bado hujajibu!!!!!
Nikakujibu
By Nyambala
Hapana Mzee Saidi sijauliza kwa kupima uwezo wako bali ni kwa nia nzuri tu ya kutaka kuweka mambo sawa. Na ni muhimu vijana wetu wafahamu historia nzima mpaka uhuru wenyewe ulipopatikana.

Ukajibu majibu yangu lakini si swali la msingi


Nikakukumbusha

Ukajibu majibu lakini swali la msingi holaaaaaa!!!!!!!!!!


Sasa naomba nikujibie maana najua jibu unalijua ila linakuumiza. Unajisikiaje unapokuta kwenye negotiations hakukuwa na wazee wala akina Skyes It was again the same man, himself alone and solo. How does that feel???? Nyerere again and was there by himself. Waambie tu vijana Mzee Saidi ndiyo maana ya historia. But what a coincidence? Nyerere huyu huyu anakuwa mwenyekiti wa kwanza wa TANU ambayo unadai iliasisiwa na kina Sykes, Nyerere tena huyu huyu anakwenda kutuwakilisha watanganyika milioni tisa UNO na kama unavyodai kwa nauli zilizotolewa na kina Sykes. Sasa inakuwaje tena mtu huyo huyo ndiyo negotiator by himself akiwakilisha watanganyika wote dhidi ya wakoloni?, Do you wanna know how old was he by then? Why, why, why? Kuna mlinganisho wowote wa mtu huyu na mtanganyika yeyote achilia mbali akina Sykes.

Mzee Saidi una haki kabisa ya kuwa obsessed na Abdu kwa sababu zako binafsi lakini huna haki hata kidogo kutaka kulazimisha ukuu wa Abdu dhidi ya Nyerere, au kudunisha ushujaa wa Nyerere ili kuelevate umahiri wa Abdu. Watu hawa wawili hawalinganishiki, na hawafanani ni sawa na Bahari na maji ya kikombe. Hata zije historia milioni na baada ya miaka alf, Nyerere bado around this time hakuna aliyekuwa mfano wake. Endelea kuchapa ngano mkuu lakini eneo hili umekwama.
 
Mzee wangu Mohamed Said utetezi wa Sheikh Bilal Rehani Waikela hauna mashiko wala hauwezi kuwasaidia watuhumiwa.Ikiwa watuhumiwa walikuwa wakisubiri utetezi wa aina hii hakika bado wana safari ndefu,hata hiyo mipango ya ujenzi wa Chuo kikuu itabidi mtafute vichwaa vingine akina Sheikh Ponda na kundi lake watazidi kuwaangamiza katika lindi la ujinga na mtabaki na ngonjera za mfumo kristo milele.




 
Last edited by a moderator:
Ahahahahahah..Naamini mpaka mtanange huu ukifika mwisho watu watakuwa wamejifunza mengi sana.Wakuu mwanakijiji,nguruvi3,mag3 na yericko nyerere na wote wenye mlengo wa aina yenu nawaombeni sana muweze kuandika kitabu chenye title ya hii thread.Na Mzee Mohamedi Saidi nakupongeza sana kwa kuendelea kuwepo hapa jukwaani,nimependa umekuwa muwazi.Safi sana.
 

Twende Kazi,

Ahsante kwa maneno yako mazuri.
Sifa ya Uislam ni ukweli.

Haki daima itakuwa juu.
Haki si kitu cha kuwa chini ya kitu kingine.

Ndiyo maana unaona nimeweza kuwa hapa
na kueleza yale yote niliyokuwa nayajua kuhusu
wazee wangu bila hofu.
 

Waache waendelee kutapa tapa wafa maji..
Ati wanajigamba wamemweka moh said kwenye kona..!
Sasa hiyo kona iko wapi?
Yan wanachosubiri ni kutafuta point of weakness na wao kuanza kuishambulia kama wanacheza chandimu.,
ni kazi kubwa sana kuupinga ukweli,
bure wataumiza mikono ukuta wakijipigia,
maji ya shingo yamewafika..
 

Ngongo,

Mimi siwezi kukuuliza hukumu yako imesimama kwenye sheria ipi.

Lakini ambalo wewe hulijui na limekupita ni kuwa Waikela kaeleza
ukweli wa mambo yalivyokuwa.

Nini Waislam wamefanya katika kupigania uhuru wa Tanganyika na
aliyesimama kueleza hayo mahakamani ni Sheikh Bilali Rehani Waikela
mmoja wa waasisi wa TANU.

Unaweza kufanya kebehi na kejeli.
You can as a Christian afford to do that.

Sijashangazwa na wewe.
 

wameishiwa nguvu kabisa..
Yani kama ni kwenye ulingoni basi benchi lao la ufundi limerusha taulo kati kati ya ulingo ili kumnusuru mpiganaji wao..
 

Hili hata moyo wa Mo'h unamsuta, anajiona kavuliwa nguo hadharani
 

Nyambala,

Mimi sioni sababu ya kuniuliza maswali ndiyo mimi nikataka kujua iweje uniulize swali
kama hilo lina tija gani?

Kwani mimi si kawaida yangu kuwa najibu kila kitu niulizwacho tungefahamiana kitambo
hili ungelijua.

Kwa hakika mimi nimekuwa na obsession na Abdu Sykes toka udogo wangu.

Baba yangu akimpenda sana Bwana Abdu na mara nyingi akihadithia habari za kupigania
uhuru akimtaja Abdu Sykes.

Ikitokea kuwa katika marafiki wa baba yangu hapa Dar es Salaam nikatokea kumuusudu
sana Bwana Abdu.

Tuje kwa Nyerere.

Hapana popote pale mimi nilipojaribu kumdunisha Nyerere na kumweka Abdu juu yake.
Siwezi kuwa na ujinga huo.

Na hilo isingewezekana kwa kwa uongozi wao ulipishana.
Nayajua alofanya Nyerere katika ulimwengu kama sote tunavyojua.

Hili halijapata kuwa na shaka kwangu hata kidogo.

Isipokuwa katika historia ya kuunda TANU siku zote na hata ninapohadhiri ndani na nje
ya nchi nikisema na shingo naitoa kuwa Nyerere hangeweza kumwangalia Abdu Sykes
machoni na akasema, ''Mimi Nyerere ndiye niliyounda TANU.''

Nyerere asingeweza.
TANU haikuanza mwaka 1954.

Historia ya TANU inaanza na baba yake Abdu Sykes mwaka 1929 katika kuunda African
Association.

Hapa ndipo ilipo tofauti yangu na yako na wengi sana pamoja na Nyerere mwenyewe.

Na sikusema haya kwa kificho.
Nimesema haya Nyerere yu hai na magazeti yakachapa na watu wakasoma.

Nishaweka hapa rejea za magazeti hayo sina haja ya kurudia tena.

Sasa tuje safari ya UNO ya 1955.

Ikiwa umekisoma kitabu changu utaona kuwa safari ile iliratibiwa na Baraza la Wazee
wa TANU chini ya uenyekiti wa Sheikh Suleiman Takadir na mweka hazina wa Al Jamiatul
Islamiyya na TANU Idd Faiz Mafongo ndiye aliyekuwa akikusanya fedha na katika fedha
zilizotiwa katika mfuko ule ni kutoka hazina ya Al Jamiatul Islamiyya.

Sasa hapo wala mimi sitotaka kukuuliza swali lolote isipokuwa hili dogo sana.
Swali lenyewe ni hili hapa: Kabla mimi sijasema haya ulikuwa ukiijua historia hii?

Nyambala,

Wewe na mfano wa wewe si wa kunikwamisha mimi na ukipenda nakupa changamoto njoo
na historia uijuayo wewe mimi nitakupa majibu yake.

Hivi haikushangazi hata chembe kuwa hata Idara ya Historia ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
hadi leo hawajaweza kuandika chochote kuhusu historia ya kudai uhuru?

Wewe hushangazwi na hilo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…