Mzee Saidi kuna wakati nikisoma maandishi yako najikuta nacheka peke yangu, ngoja nikukumbushe kidogo hapo nyuma nilikuuliza swali, ukazuga kama hujasikia kama kawaida yako. Baadae Son of Alaska akasisitiza.
Ukadai nimeuliza kwa kukupima uwezo au? Swali bado hujajibu!!!!!
Nikakujibu
Ukajibu majibu yangu lakini si swali la msingi
Nikakukumbusha
Ukajibu majibu lakini swali la msingi holaaaaaa!!!!!!!!!!
Sasa naomba nikujibie maana najua jibu unalijua ila linakuumiza. Unajisikiaje unapokuta kwenye negotiations hakukuwa na wazee wala akina Skyes It was again the same man, himself alone and solo. How does that feel???? Nyerere again and was there by himself. Waambie tu vijana Mzee Saidi ndiyo maana ya historia. But what a coincidence? Nyerere huyu huyu anakuwa mwenyekiti wa kwanza wa TANU ambayo unadai iliasisiwa na kina Sykes, Nyerere tena huyu huyu anakwenda kutuwakilisha watanganyika milioni tisa UNO na kama unavyodai kwa nauli zilizotolewa na kina Sykes. Sasa inakuwaje tena mtu huyo huyo ndiyo negotiator by himself akiwakilisha watanganyika wote dhidi ya wakoloni?, Do you wanna know how old was he by then? Why, why, why? Kuna mlinganisho wowote wa mtu huyu na mtanganyika yeyote achilia mbali akina Sykes.
Mzee Saidi una haki kabisa ya kuwa obsessed na Abdu kwa sababu zako binafsi lakini huna haki hata kidogo kutaka kulazimisha ukuu wa Abdu dhidi ya Nyerere, au kudunisha ushujaa wa Nyerere ili kuelevate umahiri wa Abdu. Watu hawa wawili hawalinganishiki, na hawafanani ni sawa na Bahari na maji ya kikombe. Hata zije historia milioni na baada ya miaka alf, Nyerere bado around this time hakuna aliyekuwa mfano wake. Endelea kuchapa ngano mkuu lakini eneo hili umekwama.
Nyambala,
Mimi sioni sababu ya kuniuliza maswali ndiyo mimi nikataka kujua iweje uniulize swali
kama hilo lina tija gani?
Kwani mimi si kawaida yangu kuwa najibu kila kitu niulizwacho tungefahamiana kitambo
hili ungelijua.
Kwa hakika mimi nimekuwa na obsession na Abdu Sykes toka udogo wangu.
Baba yangu akimpenda sana Bwana Abdu na mara nyingi akihadithia habari za kupigania
uhuru akimtaja Abdu Sykes.
Ikitokea kuwa katika marafiki wa baba yangu hapa Dar es Salaam nikatokea kumuusudu
sana Bwana Abdu.
Tuje kwa Nyerere.
Hapana popote pale mimi nilipojaribu kumdunisha Nyerere na kumweka Abdu juu yake.
Siwezi kuwa na ujinga huo.
Na hilo isingewezekana kwa kwa uongozi wao ulipishana.
Nayajua alofanya Nyerere katika ulimwengu kama sote tunavyojua.
Hili halijapata kuwa na shaka kwangu hata kidogo.
Isipokuwa katika historia ya kuunda TANU siku zote na hata ninapohadhiri ndani na nje
ya nchi nikisema na shingo naitoa kuwa Nyerere hangeweza kumwangalia Abdu Sykes
machoni na akasema, ''Mimi Nyerere ndiye niliyounda TANU.''
Nyerere asingeweza.
TANU haikuanza mwaka 1954.
Historia ya TANU inaanza na baba yake Abdu Sykes mwaka 1929 katika kuunda African
Association.
Hapa ndipo ilipo tofauti yangu na yako na wengi sana pamoja na Nyerere mwenyewe.
Na sikusema haya kwa kificho.
Nimesema haya Nyerere yu hai na magazeti yakachapa na watu wakasoma.
Nishaweka hapa rejea za magazeti hayo sina haja ya kurudia tena.
Sasa tuje safari ya UNO ya 1955.
Ikiwa umekisoma kitabu changu utaona kuwa safari ile iliratibiwa na Baraza la Wazee
wa TANU chini ya uenyekiti wa Sheikh Suleiman Takadir na mweka hazina wa Al Jamiatul
Islamiyya na TANU Idd Faiz Mafongo ndiye aliyekuwa akikusanya fedha na katika fedha
zilizotiwa katika mfuko ule ni kutoka hazina ya Al Jamiatul Islamiyya.
Sasa hapo wala mimi sitotaka kukuuliza swali lolote isipokuwa hili dogo sana.
Swali lenyewe ni hili hapa: Kabla mimi sijasema haya ulikuwa ukiijua historia hii?
Nyambala,
Wewe na mfano wa wewe si wa kunikwamisha mimi na ukipenda nakupa changamoto njoo
na historia uijuayo wewe mimi nitakupa majibu yake.
Hivi haikushangazi hata chembe kuwa hata Idara ya Historia ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
hadi leo hawajaweza kuandika chochote kuhusu historia ya kudai uhuru?
Wewe hushangazwi na hilo?