Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed huko kwa watu wanaojua kwanini hawakujua kuwa takwimu zako ni za kiwango duni na hazipo katika kiwango cha utafiti wa aina yoyote?

Free for all (JF)Jukwa nene na la heshima wamekusimamisha na umekiri, narudia umekiri kuwa yalikuwa makosa.
Havard wanajua mabucha ya nguruwe! sisi wenye nchi ndio tutakwambia kama hivi:

Mohamed umesema maandamano ya kuvunja mabucha ulikuwepo kuanzia msikiti wa mtoro( maandishi yapo hapo juu bila ubishi). Tunakubana ueleze maandamano yalianzia kwa Mtoro unabadili kauli na kusema siku ya pili.
Unabadili kauli kama ulivojifungia na kubadili takwimu Christian vs Muslim kuwa Muslim vs non muslim.

Hata kwa kubadili kauli bado upo wrong! hii hapa nakupa
Msafara wa kwenda kuvunja mabucha ulianzia msikiti wa kichangani magomeni.
Msafara huo ulianza majira ya jioni kuelekea kagera kupitia bara bara ya Morogoro.
Vijana walikuwa wakisema ''takri allah akbaru''.

Malalamiko ya ilikuwa kutosikilizwa kwa madai ya uwepo wa mabucha ya nguruwe katika maeneo ya makazi.
Katika ushahidi wa walalamikaji, waliweza kutoa barua waliyoandika na ambayo haikushughulikiwa na serikali za mitaa.

Baada ya uvunjaji, baadhi ya watu walisema kuwa lile lilikuwa suala la chuki dhidi ya wakristo.
Waislam walijibu vizuri sana kwa kusema, msafara ulipita bara bara ya morogoro na eneo la mwembechai lina makanisa kama lile lililokaribu na kwa marehem sheikh Yahya pale mwembechai na la Wasabato eneo hilo.

Wakaendelea kusema hakuna kanisa hata moja lililorushiwa jiwe au kuhalifiwa na kwa mantiki hiyo madai yao yalikuwa dhidi ya kupuuzwa kwa hoja zao za mabucha ya nguruwe na serikali licha ya kwamba waliandika barua na wala si chuki dhidi ya wakristo.

Hoja hiyo iliingia akilini mwa watu wenye fikra na ni ukweli kuwa hakukuwa na uhalifu mwingine.
Hili limeandikwa katika sehemu nyingi ikiwa ni pamoja na kitabu au makala( sikumbuki ni kutoka kumbu kumbu gani).

Maana yake ni kuwa maandamano yalikuwepo na wewe hukuwepo, isipokuwa kama ulishiriki siku ya pili hilo sijui.
Mohamed, maandamano yalikuwepo na nilishuhudia kwasababu zama hizo nikiishi maeneo hayo.

Ulichotaka kusema ni kuwa ulishiriki kuanzia kwa Mtoro. Baada ya kuona hilo halitaingia akili kwa wenye kutumia akili ukabadili na kusema siku ya pili. Sina tatizo na siku ya pili, ukweli ubaki pale pale kuwa siku ya kwanza hukushiriki kwasababu hujui hata uwepo wa maandamano hayo.

Labda niweke sawa haikuwa maandamano kwa maana hiyo, ilikuwa ni watu waliokuwa wanakwenda kwa kundi kuelekea kule. Kama hii si kweli, iweje waislam walisema kuwa hakukuwa na kanisa hata moja lililohalifiwa jambo ambalo ni kweli kabisa. Hata viongozi wa makanisa hayo walikiri kuwa hakukuwa na uhalifu katika maeneo yao.

Sasa kauli hiyo ya waislam ambayo iliungwa mkono na viongozi wa makanisa yaliyokuwa jirani ilitokeaje endapo hakukuwa na maandamano.
 

Mimi hata siwashangai nyinyi wafia nyerere kwa upingaji wenu. mshazoea kupinga na kupinga. Mlipinga sana kuwepo kwa MoU ya wakristo na Serikali. Makubaliano yaliyofanywa kwa siri.Mkasema hakuna kitu kama hicho, HAKUNA MAKUBALIANO HAYO, HAKUNA......!!!. Mlikuja kufedheheka pale rais Kikwete aliposema hadharani pale dodoma mabilioni anayokupeni. Na akawahidi kuwa atawongezeeni mabilioni hayo ya umma. Baada kuona ukweli umedhihiri, mkaja na lingine ati oh pesa za MoU zinatoka makanisa ya Ujerumani na papers mkaandika. Sasa niwaulize rais kasema pesa zinatoka serikalini ni za umma nyinyi mnasema ni kutoka makanisa ya ujerumani nani yupo sahihi kati ya rais na nyinyi wafia nyerere?
 

Nguruvi3,

Mbona unapenda kujiliwaza sana kuwa umembana Mohamed Said, alichokujibu ndiyo kilichofanyika maandamano rasmi kushirikisha Misikiti yote yalifanyika kesho yake.

Siku ya kwenda kuvunja mabucha ya nguruwe vijana walijikusanya pale Mapipa kama vijana 40 tena kwa siri wakaelekea Mwembechai kuungana na wenzao.

Wewe unamuuliza Mohamed Said maandamo yameinzia Mtoro ulitaka akujibu ndiyo ili upate pakusemea. Hayo yote mbona yameindikwa kwenye kitabu cha mauaji ya Mwembechai wala huna jipya la kutueleza kuhusu Mwembechai.

Maandamano ya siku ya pili ndiyo yalishika kila Msikiti kulitokea mapambano pale kituo cha fire baina ya polisi na waandamanaji waliokuwa wanatokea Misikiti ya Kichangani, Mwembechai, Kagera, Mtambani.
 

Huyu Nguruvi anapenda sana kudowea vineno ili atangaze ushindi wakati kazi ndio kwanza imeanza ya kupata darsa.
Yeye mwenyewe alikwepa suala la sensa.
Haya mambo ya historia ya waislamu huwezi kuyapatia jawabu kutoka maandishi ya makanisani.Wasikilize waislamu wenyewe wanasemaje.
 
Mohamed, hivi maandamano ya kuvunja mabucha yalianzia kwa Mtoro?

Mimi nina temerity ya kusema mbona saizi yangu ni wewe!

Mbona unataka kulazimisha wapi amekuambia maandamano ya kuvunja mabucha yameanzia Mtoro.
 
Ni sisi wafia Nyerere ndio tuko sahihi. Maelezo ya MOU kayaweka hapa Dr. Slaa mkakaa kimya.
 

Nguruvi,

Maalim wangu Hassan Bana anasema ubishi hauna maana.

Siwezi niwe nakaa kujibu yale ya "umekiri" nami nikujibu
"sikiri ninasema nk."
 
Mzee Mohamed Said, Ritz,Kuna shule ya wa-Yemen iliyojengwa kwa kumegwa kiwanja kilekile ambacho kimemletea matatizo Sheikh Ponda na WATANZANIA wengine wanaoburuzwa na simulizi zako mzee Mohamed. Kwa nini hawa wa-Yemen hawakuvamiwa wakati wao hata sio Watanzania?
 
Last edited by a moderator:

TAKRI ALLA AKBARU ndio nini? bila shaka hayo hayakuwa maandamano ya Waislamu maana ktk Uislamu hakuna TAKRI ALLA AKBARU!!!! halafu mnauliza maswali ya kipuuzi kabisa! Waislamu wanapoandamana wanaweza kuanzia Msikiti wowote au yote kwa wakati mmoja! Waislamu wako huru kuswali ktk msikiti wowote sisi sio kama dini zingine zinazolazimishwa kuabudu ktk jengo moja tu au kufunga pingu za maisha na mwanamke mmoja! yaani hata kama hazai huruhusiwi kuoa mwingine utakufa na huyo mmoja!
 
TANU haikuanza mwaka 1954.

Historia ya TANU inaanza na baba yake Abdu Sykes mwaka 1929 katika kuunda African
Association.

Hapa ndipo ilipo tofauti yangu na yako na wengi sana pamoja na Nyerere mwenyewe.

TANU haikuanza mwaka 1954!! Tuifute tu HISTORIA ya TANU. Tufukue fuvu la Mzee Sykes la mwaka 1929. Tuone kama TANU ilikuwemo humo mwaka huo! Rais wa KWANZA wa TANU naye sio Mwalimu, ni Kleist Sykes. Haiwezekani HISTORIA ya TANU ianzie mwaka 1929 halafu Rais wa kwanza apatikane mwaka 1954, Mwalimu, ambaye mwaka 1929 alikuwa na umri wa miaka 7 tu.
 

We've since moved on to CCM pengine Nyerere hakutaka tukae huko. Mie nadhani Nyerere was the most ingenious character of his time in that he managed to bring all parties together and that was very distinct pengine wengine hawakua na sifa alizokua nazo yeye zilizompa kibali kwa makabila na dini zote hata wahindi. and also note that all the colonial eras that passed managed to devide us. Also, wazee wa kiislam waliweza kumsikia na kushirikiana na Nyerere because they believed his nobility status kifupi hakukua na ubaguzi ila pale tu aliposhindwa kuvumilia agenda za vikundi ndiposa alianza kuchukiwa na mie namshukuru mungu hakuwa soft kama walivyomdhania this is really what makes him standout. Nakumbuka bibi Titi ameishawahi hojiwa na tbc na alikua anamsifu sana tu Nyerere kwa hili alieleza jinsi wazee pamoja na wahindi walivyokuwa wakimsukuma Nyerere afanye mapinduzi nae aliweza kuhakikishia uhuru unakuja bila mapinduzi. Ni wazi kulikuwa na kundi lililotaka kuteka juhudi za uhuru na kumpandia mwalimu kijana and they failed.
 

We've since moved on to CCM pengine Nyerere hakutaka tukae huko. Mie nadhani Nyerere was the most ingenious character of his time in that he managed to bring all parties together and that was very distinct pengine wengine hawakua na sifa alizokua nazo yeye zilizompa kibali kwa makabila na dini zote hata wahindi. and also note that all the colonial eras that passed managed to devide us. Also, wazee wa kiislam waliweza kumsikia na kushirikiana na Nyerere because they believed his nobility status kifupi hakukua na ubaguzi ila pale tu aliposhindwa kuvumilia agenda za vikundi ndiposa alianza kuchukiwa na mie namshukuru mungu hakuwa soft kama walivyomdhania this is really what makes him standout. Nakumbuka bibi Titi ameishawahi hojiwa na tbc na alikua anamsifu sana tu Nyerere kwa hili alieleza jinsi wazee pamoja na wahindi walivyokuwa wakimsukuma Nyerere afanye mapinduzi nae aliweza kuhakikishia uhuru unakuja bila mapinduzi. Ni wazi kulikuwa na kundi lililotaka kuteka juhudi za uhuru na kumpandia mwalimu kichwani kijanja and they failed.
 
Nguruvi,Umezungumzia maandamano kuwa sishiriki maandamano.
Umezungumza mimi kupanda ndege kwenda nchi za nje na kuwaacha ndugu zangu.
Hili nitakujibu.Maandamano ya kwanza tumetokea Mtoro 1993.
Mabucha ya nguruwe.Nguruvi,Cheza na watu saizi yako.
Nguruvi3;5971952]Mohamed, hivi maandamano ya kuvunja mabucha yalianzia kwa Mtoro?
Mohamed, kuna swali hili naona unajaribu kulikwepa. Nikukumbushe kuwa umelileta wewe hivyo ufafanuzi tafadhali.Maandamano ya kuvunja mabucha yalianza Msikiti wa Mtoro?
Maandamano ya kuvunja mabucha yalianza Msikiti wa Mtoro?
Mohamed: Nguruvi,Siku vijana walipokwenda kuvunja mabucha hawakwenda kwa maandamano.
Kukwepa swali i? Mimi nasimama kwenye vyuo kote huko najibu maswali ya watu wenye kujua nijenikimbie swali hapa free for all?
Hakuna hata mmoja kati ya Mohamed na vijana wake aliyejibu au ku-dispute hoja.
Hoja yangu inasimama kwasababu inajisimamia. Haina kejeli, tusi bali facts.

Maandamano ya kuvunja mabucha hayakuanzia msikiti wa Mtoro kama Mohamed anavyodai! fallacy!
Mohamed hakuwepo katika msafara wa kundi lililokwenda kuvunja mabucha. Fact
Maandamano ya siku pili hayakuwa kwenda kuvunja mabucha bali kuweka dhamana! kuvunja na kuweka dhamana ni vitu viwili tofauti.

Hoja hii imekwisha na kama kawaida tumeonyesha uzushi na kuukataa kwa hoja, matiki na weledi!
I am here to set the record clear.
 

Nguruvi3,

Unataka majibu gani au umeamua kubishana mpaka dakika ya mwisho.

Mohamed Said kakwambia maandano ya mabucha ya nguruwe yalianzia Mtoro na hayo ndiyo yaliofika mpaka posta. Maandamano mengine yalivamiwa na FFU pale fire watu wakakamatwa.

Turudi kwenye uvunjanji wa mabucha ya nguruwe.

Vijana walijikusanya pale Magomeni Mapipa tena kwa siri wakapeana taarifa na wenzao waliokuwa wanawasubiri Msikiti wa Mwembechai siyo Kagera. Vijana kama 40 wakaondoka Mapipa kwenda kuungana na wenzao Mwembechai ndiyo wakaelekea kuvunja mabucha nguruwe.

Sasa sijui unataka majibu gani.
 
Ritz,
Nijibu kale kaswali kangu: Kile kiwanja kilichomtia matatani Sheikh Ponda kimegawanywa na kuuzwa marambili au zaidi. Mbona huku walikouziwa wa-Yemen hakukuvamiwa? Au hakuna wakf kule!
 
Last edited by a moderator:

Nguruvi,
Soma post yangu nimesema maandamano yanakwenda polisi.
 

Wild Card,

Hakuna tatizo.
Kila mtu ana haki ya kuisomesha historia yake apendavyo.

Sisi historia ya TANU kama tuijuavyo haianzi na Nyerere.
Hapana haja ya kugombana kwa hili.

Kivukoni wameandika historia yao na mimi nimeandika ya wazee
wangu ambayo inakwenda nyuma hadi mwaka 1929 ilipoasisiwa
African Asociation.
 
Deadly wrong! Hapa ndipo huwa nasema kusimuliwa na kuona ni vitu viwili tofauti kabisa.

Narudia tena, waislam walikusanyika msikiti wa Kichangani Magomeni( Traffic light) wakaondoka hapo wakipiga Takbri na kupita kituo cha usalama kueleke maeneo ya Kagera kupitia mwembechai.
Walikuwa bara barani na mmoja wao ninayekumbuka alivaa kanzu na kilemba kama cha Yaser Arafat.

Watu hawakujua walikuwa wanakwenda wapi na kwanini hadi ilipotokea kuvunjwa kwa mabucha.
Kama ilikuwa siri basi ni pale watu wengine waliposhindwa kuelewa nini kinaendelea na kadri kundi lilivyokuwa linaekekea kule ndivyo walivyoungana na wenzao ambao walikuwa wana taarifa za nini kinatokea.

Hawakwenda kwa siri, narudia mnapotoshwa ninyi! mnasimuliwa hadithi na ngano za uongo mnameza tu.

Mohamed is deadly wrong, siku ya kwanza ya maandamano haikuanzia kwa Mtoro.
Maandamano yalianzia Kichangani ingawa hayakuwa rasmi lakini yalipita barabarani kama mengine.

Maandamano ya kwa Mtoro ni siku yapili kwenda kuweka dhamana.
Kwahiyo hakushiriki maandamano ya kuvunja mabucha bali pengine alishiriki uwekaji wa dhamana.

Mnafahamu hili lakini mumeamua kutia manukato katika uvundo.
Hatuwezi kuendelea kulishwa uzushi baada ya miaka 15 ya maumivu makali ya ngano.
Tuendelee kukaa kimya tukilishwa takwimu za jikoni zilizowekewa tui la nazi za kisiju.

I am here to set the record clear. No more no less.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…