Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Mohamed huko kwa watu wanaojua kwanini hawakujua kuwa takwimu zako ni za kiwango duni na hazipo katika kiwango cha utafiti wa aina yoyote?Mohamed Said;5972377]Maandamano ya kuvunja mabucha yalianza Msikiti wa Mtoro?
Nguruvi,
Siku vijana walipokwenda kuvunja mabucha hawakwenda kwa maandamano.
Mandamano yalianza Msikti wa Mtoro siku ya pili kwenda polisi kuwatoa masheikh
waliokamatwa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi baada ya kuvunjwa mabucha.
Kuna pp niliwasilisha Chuo Kikuu cha Kenyatta kuhusu kuvunjwa kwa mabucha na
matokeo yake: Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the
Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern
Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21[SUP]st[/SUP] Century 1[SUP]st [/SUP]- 3[SUP]rd[/SUP] August 2006,
Kenyatta University, Nairobi.
Kukwepa swali kwa kuogopa kitu gani?
Mimi nasimama kwenye vyuo kote huko najibu maswali ya watu wenye kujua nije
nikimbie swali hapa free for all?
Free for all (JF)Jukwa nene na la heshima wamekusimamisha na umekiri, narudia umekiri kuwa yalikuwa makosa.
Havard wanajua mabucha ya nguruwe! sisi wenye nchi ndio tutakwambia kama hivi:
Mohamed umesema maandamano ya kuvunja mabucha ulikuwepo kuanzia msikiti wa mtoro( maandishi yapo hapo juu bila ubishi). Tunakubana ueleze maandamano yalianzia kwa Mtoro unabadili kauli na kusema siku ya pili.
Unabadili kauli kama ulivojifungia na kubadili takwimu Christian vs Muslim kuwa Muslim vs non muslim.
Hata kwa kubadili kauli bado upo wrong! hii hapa nakupa
Msafara wa kwenda kuvunja mabucha ulianzia msikiti wa kichangani magomeni.
Msafara huo ulianza majira ya jioni kuelekea kagera kupitia bara bara ya Morogoro.
Vijana walikuwa wakisema ''takri allah akbaru''.
Malalamiko ya ilikuwa kutosikilizwa kwa madai ya uwepo wa mabucha ya nguruwe katika maeneo ya makazi.
Katika ushahidi wa walalamikaji, waliweza kutoa barua waliyoandika na ambayo haikushughulikiwa na serikali za mitaa.
Baada ya uvunjaji, baadhi ya watu walisema kuwa lile lilikuwa suala la chuki dhidi ya wakristo.
Waislam walijibu vizuri sana kwa kusema, msafara ulipita bara bara ya morogoro na eneo la mwembechai lina makanisa kama lile lililokaribu na kwa marehem sheikh Yahya pale mwembechai na la Wasabato eneo hilo.
Wakaendelea kusema hakuna kanisa hata moja lililorushiwa jiwe au kuhalifiwa na kwa mantiki hiyo madai yao yalikuwa dhidi ya kupuuzwa kwa hoja zao za mabucha ya nguruwe na serikali licha ya kwamba waliandika barua na wala si chuki dhidi ya wakristo.
Hoja hiyo iliingia akilini mwa watu wenye fikra na ni ukweli kuwa hakukuwa na uhalifu mwingine.
Hili limeandikwa katika sehemu nyingi ikiwa ni pamoja na kitabu au makala( sikumbuki ni kutoka kumbu kumbu gani).
Maana yake ni kuwa maandamano yalikuwepo na wewe hukuwepo, isipokuwa kama ulishiriki siku ya pili hilo sijui.
Mohamed, maandamano yalikuwepo na nilishuhudia kwasababu zama hizo nikiishi maeneo hayo.
Ulichotaka kusema ni kuwa ulishiriki kuanzia kwa Mtoro. Baada ya kuona hilo halitaingia akili kwa wenye kutumia akili ukabadili na kusema siku ya pili. Sina tatizo na siku ya pili, ukweli ubaki pale pale kuwa siku ya kwanza hukushiriki kwasababu hujui hata uwepo wa maandamano hayo.
Labda niweke sawa haikuwa maandamano kwa maana hiyo, ilikuwa ni watu waliokuwa wanakwenda kwa kundi kuelekea kule. Kama hii si kweli, iweje waislam walisema kuwa hakukuwa na kanisa hata moja lililohalifiwa jambo ambalo ni kweli kabisa. Hata viongozi wa makanisa hayo walikiri kuwa hakukuwa na uhalifu katika maeneo yao.
Sasa kauli hiyo ya waislam ambayo iliungwa mkono na viongozi wa makanisa yaliyokuwa jirani ilitokeaje endapo hakukuwa na maandamano.