Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hakuna hata mmoja kati ya Mohamed na vijana wake aliyejibu au ku-dispute hoja.
Hoja yangu inasimama kwasababu inajisimamia. Haina kejeli, tusi bali facts.
Maandamano ya kuvunja mabucha hayakuanzia msikiti wa Mtoro kama Mohamed anavyodai! fallacy!
Mohamed hakuwepo katika msafara wa kundi lililokwenda kuvunja mabucha. Fact
Maandamano ya siku pili hayakuwa kwenda kuvunja mabucha bali kuweka dhamana! kuvunja na kuweka dhamana ni vitu viwili tofauti.
Hoja hii imekwisha na kama kawaida tumeonyesha uzushi na kuukataa kwa hoja, matiki na weledi!
I am here to set the record clear.
Nguruvi,
Hebu soma upya hii post.
Unafanya haraka na matokeoa yake ndiyo hayo maneno ambayo mie sijaandika:
Angalia bold:
Umeandika maneno mengi sana.
Ni vigumu kukujibu nukta kwa nukta.
Umezungumzia maandamano kuwa sishiriki maandamano.
Hunijui...
Na wala sina haja ya kukueleza.
Umezungumza mimi kupanda ndege kwenda nchi za nje na kuwaacha ndugu zangu.
Hili nitakujibu.
Maandamano ya kwanza tumetokea Mtoro 1993.
Mabucha ya nguruwe.
Siku chache kabla nilikuwa nimetoka safari...Dar- Paris - Le Havre - Paris - London - Cardiff - London -
Dar - Zanzibar.
Zanzibar ndiyo sakata la OIC nilikwenda kuchapa majibu kwa Kanisa na Serikali katika Khayria Press na
mimi ndiye nilikuwa nilorudi na majibu hayo ambayo tuliyagawa kwa Wabunge wakati huo Bunge linakaa
Karimjee Hall.
(Nina paper nzima kuhusu OIC Insha Allah kama wanaukumbi watapenda nitaiweka jamvini.)
Nimefika Dar nimearifiwa mkutano wa dharura wa kuwawekea dhamana masheikh wetu waliokamatwa kwa
kuvunjwa kwa mabucha ya nguruwe.
Sina haja ya kukeleza nini kilitokea siku ile katika msikiti wa Mtoro ambao mimi nikiswali pale toka utoto wangu.
Sheikh Waziri Ramadhani ex - police officer ndiye aliyewasomea Waislam Qur'an na alichagua aya mnasaba na
hali iliyokuwapo siku ile.
Ilisomwa dua kubwa na tuliondoka kwa maandamano kuelekea Central Police.
Mbele yetu ndugu yetu tukimwita kwa jina la Darwesh alikuwa amebeba bendera ya kitambaa cheusi imeandikwa:
Lailaha Ilallah Muhammad Rasulullah.
Allah siku ile alijibu dua yetu pale pale.
Tumeondoka msikitini jua kali.
Tunafika Uhuru na Titi Street mawingu yanatanda na mvua ikaanza kunyesha.
Tulipambana na polisi Clock Tower na mabomu ya machozi yalirindima.
Ile mvua na upepo ukawa unapeperusha mabomu yale mbali na Waislam.
Nilikuwapo pale.
Mwenzangu alikamatwa na ndiyo ikawa sababu ya yeye kufungwa na kupoteza kazi bank.
Mimi baada ya mapambano yale nilirudi nyumbani kubadili nguo na kujitayarisha zaidi nikaja Mtoro.
Mnazi Mmoja nikakutana na rafiki yangu akanisihi nisende msikitini Mtoro kwa kuwa FFU wamezingira msikiti.
Nilimjibu kuwa nachelea kukimbia vita Allah ananiona.
Sikuweza kufika msikitini kwa kuwa Mtaa wa Mahiwa, Livingstone, Narung'ombe yote ilikuwa imefungwa...
Huwa sipendi kusema haya lakini nimeona nikueleze unijue.
Uoga si katika sifa zangu na ndiyo maana unaona nimeingia hapa na jina langu kamili bila kificho.
Wakuogopewa ni Allah SW pekee na Yeye kaweka ahadi kuwa atakaemuogopa atamfanya asiogope
chochote duniani.
Nami natamani niwe katika wale wasiomwogopa yeyote katika binadamu.
Nadhani tumefahamiana.
Mengine ulosema ni yale yale majibu ni yale yale tunazungusha humo kwa humo.
Nguruvi,
Cheza na watu saizi yako.