Katika mada hii mimi nimesimama kama mtanzania yeyote anaekereka na upotoshwaji wa Mohamed Said juu ya historia ya nchi yetu, hivyo sijasimama kutetea undugu damu wala maslahi binafsi.
Nimelieleza kwakifupi tu pale juu kuwa pamoja na juhudi kubwa za Idd Faiz Mafongo mweka hazina ea TANU za kukusanya michango ya wanachama kwaajili ya safari hiyo, lakini walioratibu safari hiyo kwakukata tiketi ya ndege yakwenda na kurudi ni kanisa katoliki kupitia shirika la maryknoll sisters la USA chini ya padre Art Wille ambae ni kama vile alimlea Mwalimu.
Yericko mimi wala nilikuwa sifikilii mambo ya undugu wa damu, nimejaribu kusoma tena kwa makini makala yako - inaelekea mzee wako alikuwa anakueleza mambo mengi ambayo wengi wetu hatuyajui au tunayajua kijuu juu tu! Kama nilivyo wahi kusema humu, Mzee wangu alikuwa anafahamiana vizuri na baba yako, kuna mambo mengi nayafahamu lakini siyasemi i.e swali hili nililihuliza 4 a reason.
Kitu ninacho kushukuru ni kwamba licha ya mimi wakati mwingine kuwa
abrasive, lakini hujawahi kunijibu vibaya; wakati mwingine unahamua kukaa kimya bila kunijibu chochote - hii inadhihilisha una analytical mind inayo chemka SANA!
Nashukuru kwa kunijibu - nategemea kukuhuliza swali lingine jioni hii - CHEERS.