Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Habari za saa hizi Yericko, kuna dossier naitayarisha kuiwasilisha kwenye uzi huu, sasa kuna vitu vidogo vidogo vinahitajika ili niweze ku-tie loose ends.

Hivi Yericko mzee wako aliwahi kukufafanulia ni nani au shirika gani lilichangia hela nyingi kama nauli ya kumuwezesha Mh.Kambarage kwenda UN kwa mara ya kwanza, wakati wa harakati zake za kudai uhuru. Najua kuna baadhi ya raia wa kawaida walio changa walicho kuwa nacho - lakini mimi niko interest na aliye toa lion's share, Asante.

Katika mada hii mimi nimesimama kama mtanzania yeyote anaekereka na upotoshwaji wa Mohamed Said juu ya historia ya nchi yetu, hivyo sijasimama kutetea undugu damu wala maslahi binafsi.

Nimelieleza kwakifupi tu pale juu kuwa pamoja na juhudi kubwa za Idd Faiz Mafongo mweka hazina ea TANU za kukusanya michango ya wanachama kwaajili ya safari hiyo, lakini walioratibu safari hiyo kwakukata tiketi ya ndege yakwenda na kurudi ni kanisa katoliki kupitia shirika la maryknoll sisters la USA chini ya padre Art Wille ambae ni kama vile alimlea Mwalimu.
 
Yericko,

Hiyo ni safari ya pili 1956 ndiyo kanisa lilitoa tiketi.

Kwa safari ya kwanza 1955 TANU ilikuwa kama mtoto yatima
ilikuwa bado haijakubalika.
 
IN person,eeeeh mola tuepushe............................

Said_2011.gif

Son...

Ungenitoa ile nimetia kanzu na kofia.
Hii kichwa wazi hujanifurahisha sana.

Tia basi na clip nazungumza jamvi
lichangamke.

Huenda Ritz akaja na halua.
 
Mohamed,
Asante kwa taarifa hii. Kumbe umeanzia Lutheran Primary School, ukaenda St. Joseph Middle/ Secondary School. Sasa mbona huwaambii akina Ritz humu jukwaani kwamba wewe ni product ya Christian schools? Kwa nini huzungumzii manufaa ya Nyerere kutaifisha shule za misheni ili watu kama wewe nao wanufaike na elimu: matunda ya uhuru wetu? Jana nimeweka humu bandiko makusudi jinsi wakristo wa Ethiopia walivyowafadhili Waislamu waliokuwa wananyanyaswa na wapagani wa Saudi Arabia. Pia kulikuwa na hotuba aliyoitoa Muislamu mbele ya kadamnasi wa Wakatoliki. Lengo langu lilikuwa ni kutaka kujenga kile ambacho unahangaika kukibomoa. Hakuna popote pale kwenye kitabu cha Sivalon aliposema kuwa Uislamu ni uadui wa Wakatoliki. Nimekisoma tena hii wiki iliyopita sikuona madai yao hayo. Historia imeonyesha moyo wa ushirikiano kati ya Wakristo na waislamu. Jinsi mfalme Negus alivyowakaribisha waislamu na kuwahifadhi ndivyo hivyuo hivyo wazee wetu akiwemo Abdulwahid, walivyomkaribisha Julius Nyerere mjini Dar-es-salaam kushiriki katika harakati za kutafuta uhuru wa Tanzania. Ni ushirikiano huo ambao tunapaswa kuujenga na kurithisha watoto wetu na wajukuu wetu. Lakini huko unakoelekea wewe unataka kubomoa halafu sijui kitakachojengwa katika maporomoko hayo kitakuwa ni kitu gani. Nimeona nifunguke kidogo hapa.

Jasusi,

Mbona wengi tumesoma shule hizo si ndiyo Waingereza
wakishirikiana na Wamishionari katika elimu?

Sasa tungesoma wapi wakati shule ndiyo hizo za serikali
na misheni?

Si jambo la kushangaza.

Nimepata kuandika paper kuhusu matatizo ya elimu kwa Waislam wa
Tanzania: TheQuestion of Muslim Stagnation in Education in Tanzania
- A Muslim Riddle
(Paper presented at the Conference of the Global
World of the Swahili
Intercultural Dialoguemon the Indian Ocean Zanzibar,
February 20 - 23, 2003).

NB: Nimeshangazwa jana kuna mtu kaniletea link na nimeiona hii paper ikinasibishwa
na BBC.j
 
Mohamed,
Asante kwa taarifa hii. Kumbe umeanzia Lutheran Primary School, ukaenda St. Joseph Middle/ Secondary School. Sasa mbona huwaambii akina Ritz humu jukwaani kwamba wewe ni product ya Christian schools? Kwa nini huzungumzii manufaa ya Nyerere kutaifisha shule za misheni ili watu kama wewe nao wanufaike na elimu: matunda ya uhuru wetu? Jana nimeweka humu bandiko makusudi jinsi wakristo wa Ethiopia walivyowafadhili Waislamu waliokuwa wananyanyaswa na wapagani wa Saudi Arabia. Pia kulikuwa na hotuba aliyoitoa Muislamu mbele ya kadamnasi wa Wakatoliki. Lengo langu lilikuwa ni kutaka kujenga kile ambacho unahangaika kukibomoa. Hakuna popote pale kwenye kitabu cha Sivalon aliposema kuwa Uislamu ni uadui wa Wakatoliki. Nimekisoma tena hii wiki iliyopita sikuona madai yao hayo. Historia imeonyesha moyo wa ushirikiano kati ya Wakristo na waislamu. Jinsi mfalme Negus alivyowakaribisha waislamu na kuwahifadhi ndivyo hivyuo hivyo wazee wetu akiwemo Abdulwahid, walivyomkaribisha Julius Nyerere mjini Dar-es-salaam kushiriki katika harakati za kutafuta uhuru wa Tanzania. Ni ushirikiano huo ambao tunapaswa kuujenga na kurithisha watoto wetu na wajukuu wetu. Lakini huko unakoelekea wewe unataka kubomoa halafu sijui kitakachojengwa katika maporomoko hayo kitakuwa ni kitu gani. Nimeona nifunguke kidogo hapa.
Tawire baba! Mohamed amelenga kuwa na Bosnia na Herzegovina, Nigeria na Somalia. Yeye anasimulia hazina zilizoachwa wakati anataka kurithisha kizazi maafa.

Imesemwa katika hadithi za dini kuwa katika shughuli ngumu kufanya ni biashara kwasababu punje moja katika pishi ya mchele inaweza kukutia matatani. Inasemwa mizani iwe ya haki.Ni biashara ndiyo ugumu wa biashara!
 
WC,

Unataka tubishane kwa kitu ambacho waliasisi wazee wangu
na mie kuijua historia yake?

Hivi wewe utaijua AA kuliko mimi mjukuu wa waasisi hawa?
Hivi wewe utaujua undani wa TANU kunishinda?

Huo ni muhali.
Mohamed Said, nani anakupa mamlaka ya kumiliki "historical knowledge"? kwanini uamini kuwa wewe ni mtu pekee mwenye uwezo na akili ya kufahamu historia ya AA na TANU ati kwa sababu wazee wako walihusika?Nakusihi acha kiburi na majivuno ya jinsi hiyo!
 
Mzee Mwanakijiji;5976827]Historia - na ulinukuu maneno ya Sykes huko nyuma - akisema TANU iliasisiwa 1954.
Tena akasema ''.......I was one of the founder of TANU 1954''hakusema founder of TANU mwaka 1948 au mwingine. Abdul Sykes hakuwa mjinga wa kutaja mwaka! alimaanisha alichokusudia akifahamu kuwa historia ndivyo ilivyokuwa na yeye hakuwa na uwezo wa kuibadili isipokuwa itajieleza yenyewe
Historia ya TANU kama chama cha siasa imeanza na Nyerere; sasa hii si kumpa sifa Nyerere au kumtukuza Nyerere bali ni kuwa wakweli wa HIstoria. Kusema kuwa Tanzania ilianza 1964 si kukataa kuwa huko nyuma akukuwepo na Tanganyika au Nchi ya Watu wa Zanzibar! NI kuwa mkweli tu wa historia. Vita ya Kagera ilianza 1978 sasa hii ni kweli; lakini 'chokochhoko' za Idi Amin hazikuanza 1978!
Ni historia hiyo anayoieleza Mohamed ndiyo ismeayo kuwa kulikuwa na mhausiano ya vyama vya kisiasa vya Tanganyika na Zanzibar kuanzia zama za AA. Hii kama tutaifanya Mohamed itakavyo basi yupo atakayeandika kuwa muungano wa mwaka 1964 ulianza miaka ya 1940 na kwamba CCM ambayo ni zao la TANU na ASP nayo ilianza miaka ya 1930. Hapo ni laghai tu kwenda kwa mbele.
TANU ni zao la vyama vilivyokuwepo nyuma yake na ni matokeo ya mawazo yaliyokuwepo kabla yake. Historia yake imetanguliwa na historia ya vyama vingine kabla yake. Hivyo, kuisoma historia ya TANU ni kusoma historia ya political development in Tanganyika na katika kufanyahivyo mtu ni lazima asome historia ya AA, TAA na vyama vya wafanyakazi na vyama vingine vya kikabila. Mwanzo wa TANU basi siyo zao la AA peke yake kama unavyotaka watu waamini; ni zao la vyama vya kikabila (tribal associations), vyama vya wafanyakazi na vyama vya maslahi ya Waafrika (AA kikiwemo).
Sidhani kama utaeleweka maana utakuwa umeondoa dhana nzima ya uzulu na umanyema hata kama mantiki inalazimisha hali iwe hivyo.
Imefika mahali sasa tumeanza kutengeneza tabia kama ya baadhi ya ndugu zetu.
Wamekubali kuwa wao wananyanyaswa, wamekubali kuwa wanadhulumiwa; wamekubali kuwa wanatengwa; wamekubali kuwa wao hawawezi kufanikiwa katika nchi yao! Na maskini tunaweza kuona humu jinsi makundi ya vijana na labda wazee wakikubali porojo hizi bila kuzihoji na wakiamini kabisa kuwa wao ni duni mbele ya Wakristu huku wakihofia jinamizi lisilokuwapo la Mfumo Kristu
Wataalam wasaikolojia wanasema ukitaka kumshinda mtu kwanza kabisa hakikisha unamfanya duni na dhalili.

Mohamed anadhani kuwa asemayo ni kuwajenga vijana wa kiislam. Anapingana na kanuni za asili kuwa hadi hapo atakapoamua kuwaambia ukweli, zao la uchochezi na ulaghai halina siku za usoni.

Leo mwanafunzi aitwaye Halima au Najmira hata kama ameshinda kulala mhula mzima basi anafaa kwa masomo na kazi. Kwamba certificate si uwezo ni jina la imani ya mtu
Mohamed amewafanya wajsikie duni bila sababu .
 
By Mohamed Said WC,Unataka tubishane kwa kitu ambacho waliasisi wazee wangu
na mie kuijua historia yake?Hivi wewe utaijua AA kuliko mimi mjukuu wa waasisi hawa?
Hivi wewe utaujua undani wa TANU kunishinda?Huo ni muhali
Mohamed, knowledge haingii akilini kwa njia za kurithi. Knowledge ni kitu kinatafutwa. Hatujui mtoto wa G.Washington, Churchil, Gandhi, Mandela, Nyerere, Reagan nao watasemaje.

Hili ndilo tatizo kubwa sana, kwamba ukizaliwa Dar unajua kiswahili. Utashangaa anatoka mtu bara anakuwa mwalimu wa kiswahili hapo hapo uswahilini. Hii kutokana na kuamini kuwa maarifa yanaingizwa kichwani kwa njia za osmosis.

Mtu anadhani historia ya Nyerere lazima mtoto wake aifahamu sana, utashangaa watu wanaoandika historia ya Mwalimu wengine walimuona akipita kwa mbali au gazetini. Vipi umewahi kusikia watoto wangapi wa Mkwawa, Mwinyigumba na wengine wakijinasibu kwa maeneo au sifa za baba zao.

Mtu anaamini kuwa kwakuwa babu yake alikuwa karani shirika la reli au bandari basi yeye ni lazima awe mkuu wa shirika hilo kwasababu anaufaham zaidi hata kama hajawahi kukanyaga darasa stahiki.
 
Mzee Mwanakijiji,

Naona unataja tu majina ya viongozi Waislam kama ushahidi wa maandiko yako.

Wewe ni muandishi mahiri usiishie kutaja tu majina zama zaidi mpaka Wizara zote za serikali na mashirika uje na "Ratio" Waislam na Wakirsto kina nani wamejaa serikalini hapo ndiyo tutafahamu nani anafaidika na matunda ya uhuru.
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said, nani anakupa mamlaka ya kumiliki "historical knowledge"? kwanini uamini kuwa wewe ni mtu pekee mwenye uwezo na akili ya kufahamu historia ya AA na TANU ati kwa sababu wazee wako walihusika?Nakusihi acha kiburi na majivuno ya jinsi hiyo!

Gwalihenzi, nionyeshe mahali mzee MS amesema yeye ndiye mwenye"historical knowledge"peke yake ya AA na TANU baba ficha upumbavu wako onyesha busara zako angekuwa na majivuno asinge jadiliana na vilaza kama wewe huku jf
 
Katika mada hii mimi nimesimama kama mtanzania yeyote anaekereka na upotoshwaji wa Mohamed Said juu ya historia ya nchi yetu, hivyo sijasimama kutetea undugu damu wala maslahi binafsi.

Nimelieleza kwakifupi tu pale juu kuwa pamoja na juhudi kubwa za Idd Faiz Mafongo mweka hazina ea TANU za kukusanya michango ya wanachama kwaajili ya safari hiyo, lakini walioratibu safari hiyo kwakukata tiketi ya ndege yakwenda na kurudi ni kanisa katoliki kupitia shirika la maryknoll sisters la USA chini ya padre Art Wille ambae ni kama vile alimlea Mwalimu.

Yericko mimi wala nilikuwa sifikilii mambo ya undugu wa damu, nimejaribu kusoma tena kwa makini makala yako - inaelekea mzee wako alikuwa anakueleza mambo mengi ambayo wengi wetu hatuyajui au tunayajua kijuu juu tu! Kama nilivyo wahi kusema humu, Mzee wangu alikuwa anafahamiana vizuri na baba yako, kuna mambo mengi nayafahamu lakini siyasemi i.e swali hili nililihuliza 4 a reason.

Kitu ninacho kushukuru ni kwamba licha ya mimi wakati mwingine kuwa abrasive, lakini hujawahi kunijibu vibaya; wakati mwingine unahamua kukaa kimya bila kunijibu chochote - hii inadhihilisha una analytical mind inayo chemka SANA!

Nashukuru kwa kunijibu - nategemea kukuhuliza swali lingine jioni hii - CHEERS.
 
Yericko,

Hiyo ni safari ya pili 1956 ndiyo kanisa lilitoa tiketi.

Kwa safari ya kwanza 1955 TANU ilikuwa kama mtoto yatima
ilikuwa bado haijakubalika.

Za saa hizi mkuu Said, hivi Mh.Kambarage alipo hacha kazi pale Mwakanga na kujikita katika mambo ya siasa full time, kumbuka wakati huo alikuwa na familia changa yaani mkewe, watoto na mama yake mzazi wote hao walikuwa wanamtegemea! Sasa swali nani alikuwa anampatia hela za kijikimu kimaisha yeye na familia yake kwenye wakati mgumu aliyo kuwa nao.

Ni nani aligharimia safari yake ya kwanza ya kwenda UN. Ndio hayo mkuu wangu.
 
Yericko mimi wala nilikuwa sifikilii mambo ya undugu wa damu, nimejaribu kusoma tena kwa makini makala yako - inaelekea mzee wako alikuwa anakueleza mambo mengi ambayo wengi wetu hatuyajui au tunayajua kijuu juu tu! Kama nilivyo wahi kusema humu, Mzee wangu alikuwa anafahamiana vizuri na baba yako, kuna mambo mengi nayafahamu lakini siyasemi i.e swali hili nililihuliza 4 a reason.

Kitu ninacho kushukuru ni kwamba licha ya mimi wakati mwingine kuwa abrasive, lakini hujawahi kunijibu vibaya; wakati mwingine unahamua kukaa kimya bila kunijibu chochote - hii inadhihilisha una analytical mind inayo chemka SANA!

Nashukuru kwa kunijibu - nategemea kukuhuliza swali lingine jioni hii - CHEERS.

Bukyanagandi,

Umeipata wapi kuwa Yericko ni mtoto wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere?

Julius Kambarage Nyerere mpaka anaondoka duniani alikuwa na watoto saba tu.

Cha kushanganza hata mtoto wa kwanza wa Julius Kambarage Nyerere, Andrew Nyerere amfahamu Yericko.

Nyie endeleeni kupeana ngano tu.
 
Mkuu wa Republic of Nauru umenichekesha karibu nizimie, mkuu mbona mambo yenyewe bado kabisa - tuwe na subira mkuu, kadiri tunavyo kwenda mengi yatajulikana.
 
its unfortunate tht we even do discuss abt muslims and christianity stuff. hivi vitu tumeletewa didnt we have any identity b4 this white guys came to Africa? lets stick to our own beliefs sidhani kama tutakuwa na matatizo.period.
 
Za saa hizi mkuu Said, hivi Mh.Kambarage alipo hacha kazi pale Mwakanga na kujikita katika mambo ya siasa full time, kumbuka wakati huo alikuwa na familia changa yaani mkewe, watoto na mama yake mzazi wote hao walikuwa wanamtegemea! Sasa swali nani alikuwa anampatia hela za kijikimu kimaisha yeye na familia yake kwenye wakati mgumu aliyo kuwa nao.

Ni nani aligharimia safari yake ya kwanza ya kwenda UN. Ndio hayo mkuu wangu.

Buk,

Nakuomba usome kitabu changu kuna historia nzima ya viongozi wa TAA na TANU.
Yote kuhusu safari ya UNO yamo mle.

Nachelea kuleta ugomvi barzani.
 
Mohamed, knowledge haingii akilini kwa njia za kurithi. Knowledge ni kitu kinatafutwa. Hatujui mtoto wa G.Washington, Churchil, Gandhi, Mandela, Nyerere, Reagan nao watasemaje.

Hili ndilo tatizo kubwa sana, kwamba ukizaliwa Dar unajua kiswahili. Utashangaa anatoka mtu bara anakuwa mwalimu wa kiswahili hapo hapo uswahilini. Hii kutokana na kuamini kuwa maarifa yanaingizwa kichwani kwa njia za osmosis.

Mtu anadhani historia ya Nyerere lazima mtoto wake aifahamu sana, utashangaa watu wanaoandika historia ya Mwalimu wengine walimuona akipita kwa mbali au gazetini. Vipi umewahi kusikia watoto wangapi wa Mkwawa, Mwinyigumba na wengine wakijinasibu kwa maeneo au sifa za baba zao.

Mtu anaamini kuwa kwakuwa babu yake alikuwa karani shirika la reli au bandari basi yeye ni lazima awe mkuu wa shirika hilo kwasababu anaufaham zaidi hata kama hajawahi kukanyaga darasa stahiki.[/COLOR]

Nguruvi,
Mfano wako si sawa.

Ujuzi nilionao katika historia ya TANU hauendani na urithi.

Nimeijua kwa kuona, kusikia kutoka wenye TANU yao na
kwa kutafiti.

Hizo ni daraja tatu za uelewa.
 
Back
Top Bottom