Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Inawezekana wewe si mweledi katika mambo haya
ndiyo maana unasema hayo unayosema.

Kitabu changu ndicho kinachoeleza kwa umakini
"nationalism," "Islam and Politics," etc.

Hakuna kitabu kilichogusa niliyoandika mimi.

Hakuna kitabu kinachoeleza historia ya Nyerere kama
kitabu changu.

Sasa nikupe zito.

Kinachowashangaza wasomi wa historia walimu na wanafunzi
ni kwanini Nyerere aliiogopa historia hiyo?

Kiasi cha magazeti kukusanywa na kuchomwa moto?
Pamoja na hayo.

Kubwa zaidi.

Imekuwaje alisahau hata cheo cha "mentor" wake katika siasa za
Dar es Salaam?

Kwa hawa Wazungu Marekani na Ulaya hiki si kitendawili.
Jibu wanalo.
 

kaka darasa lako limeeleweka sana na ndio maana inaona watu wanaanza kutoka nje ya mada.
 

Waliofungwa ni waliokuwa jeuri tu, wapo (wakuu wa maasi) waliojirudi na kuomba msamaha hasa walipopelekwa IKULU, Nitakujuza wote subiri...
 
hoja ipo wazi sana,sijui nini kinachowakwaza.Hapa namkumbuka paulo alipokuwa anawashangaa Wagalatia kwa namna wasivyoelewa mpaka kufikia kuwauliza,hivi nyie wagalatia msiokuwa na akili ni nani aliyewaroga.....
 
Unajua hawa ndugu zetu wameathirika na propaganda kuwa
sisi Waswahili si lolote.

Haya nikiyasikia darasani walimu wangu wakifanya kejeli na
dhihaka kuhusu TAA.

Hapo chuo kikuu.

Sasa hawa ndugu zangu ukweli umewapiga kofi usoni.
Hebu jiulize matusi ya nini?
 

Nanini kakutukana Mzee wangu wewe wa hekmaa?
 
Hunijui wala hujanisikia wala kunisoma.

Waulize hata maadui zangu kuhusu hizo shutuma zako.
Uwasikie majibu yao.
 
Waliofungwa ni waliokuwa jeuri tu, wapo (wakuu wa maasi) waliojirudi na kuomba msamaha hasa walipopelekwa IKULU, Nitakujuza wote subiri...

Mkuu wa maasi alikuwa Kepteni Eugene Maganga... Ngoja tuwe na subra.
 
Hapana kaka soma kichwa kikiwa wazi.
Nyerere kaingia katika siasa za TAA New Street 1953.

Historia ya Nyerere kwenye kitabu nimeianza toka siku
ile alipopelekwa kwa Abdu Sykes na Kasella Bantu mwaka
1952.

Sasa ukivuta kwa kupenda kwako hiyo kuwa nimefuta historia
ya Nyerere toka 1947 inakuwa si sawa.

Hayo mengine wala sina haja kujibu.
 
endelea kuwapa dawa japo chungu lakini watapona.Matusi yangekuwa yanaruhusiwa humu naona wangekutukana sana.Twajua wanaumia sana.Wanaoshindwa kutukana wanajaribu kupiga vijembe na kashfa za hapa na pale.Twajua mjadala huu ulishawashinda muda mrefu wanaona haya tu kujitoa.
 
Katika historia ya TANU sina shaka hata kidogo.
Nimesomeshwa na wenyewe walioasisi TANU.
 
Mohamed Said,

Unafahamu chochote kuanzishwa kwa TANU katika Majimbo.
 
Last edited by a moderator:
Siyo staili yangu kumlenga mtu mmoja.
Ninatoa darsa nazungumza na wote.
 
Mengi sana.
Tanga, Moshi, Dodoma, Lindi, Mikindani, Tabora, Bukoba...

Unataka niweke vipande humu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…