Mimi ni mgeni katika JF, lakini kila nikiingia humu naona Mohammed Said anapigwa vita juu ya kitabu chake au publications zake, true scholars would counteract by writiing books by enlisting facts, humu sioni ni firimbi tu, kiandikwe kitabu ambacho kita counter facts zilizoandikwa na Mohammed Saidi, , kama nyinyi ni wasomi toeni academic and historical evidence za ku counter Saidi's writings and we can go even, further lets talk about far and beyond.
Sintofahamu,
Hawa ndugu zetu wana tatizo kubwa sana la saikolojia.
Nimesoma hapa mengi sana ya kustaajabisha na wao yanawataabisha sana.
Ngoja nikupe mfano.
Abdu Sykes ''contemproraries'' wake wote pamoja na baba yangu wanajua TANU
kwa hakika imeundwa na Abdu na harakati zile aliaanza muda mrefu.
Marehemu Mzee Mavemba wa Mtaa wa Mahiwa kila siku akilieleza hili.
Hawa wote wanajua mchango wa baba yake Abdu katika kuanzisha African Association
1929.
Hawa wanajua haya kwa kuwa wamekulia Dar es Salaam na haya yote yametendeka wao
wakiyaona kwa macho yao.
Ndugu zangu wanakuja na hoja kuwa TANU imeasisiwa na Nyerere 1954.
Kuna mtandao mmoja wa Nyerere umeandika kabisa kuwa TANU imeasisiwa Pugu.
Huu ni mfano mmoja mdogo sana.
Kuna suala la hotuba ya Nyerere UNO 1955 na maandalizi ya safari ile.
Hawa ndugu zangu inawawia tabu kukubali kuwa hotoba ile imetokana na mapendekezo ya
katiba ya 1950.
Nyoyo zinawauma kusoma kuwa katika mapendekezo yale ya TAA kuna sahihi ya Sheikh Hassan
bin Amir.
Wanaleta kila aina ya visa, kebehi, kejeli na hata matusi wanaghadhibika kwa jambo dogo sana
kama hilo.
Wao wanataka iwe Nyerere kafika New Street kakuta hakuna chochote na yeye ndiye akafanya kila
jambo kuanzia kuitisha mkutano wa July 1954 hadi kutafuta wanachama wa TANU.
Mimi nawaambia wanachama wa mwanzo wa TANU wametoka Rufiji na aliyekwenda kuwaandikisha
ni Said Chamwebyewe.
Mimi nawaambia hilo haliwezekani hakuna aliyekuwa anamjua Nyerere katikaDar es Salaam ya 1950
asingeweza kumpata mtu.
Mambo ya kuanzisha chama cha siasa kunataka wasaa na fedha za kutosha.
Nawaambia Abdu ni mojawapo wa viongozi wa TAA waliokuwa wakitoa fedha hizo na mikutano ya siri
ikifanyika nyumbani kwake Mtaa wa Stanley na Sikukuu.
Nawaeleza kuwa mimi nayajua haya kwa kuwa mkewe Bwana Abdu Bi. Mwamvua mimi ni mama yangu
kanieleza kila kitu hadi lile kabati la kuweka fedha la Bwana Abdu ambae yeye ndiye alikuwa mshika funguo.
Nami namtania namwambia, ''Kumbe mama ulikuwa mweka hazina kivuli wa TANU.''
Mimi najua mengi kwa kuwa hawa waliofanya haya ni wazee wangu na sishi mie kuwakumbusha ukweli huu.
Nawaambia watu wa mwanzo pale Kariakoo ofisini kwa Abdu Sykes kujuana na Nyerere ni Shariff Attas mimi
huyu babu yangu.
Acha hilo pale sokoni alikuwapo mjomba wangu Bwana Hamisi Salum, alikuwapobabu yangu Shariff Mwamedi
hawa wakifanya biashara pale.
Hawa wamemjua Nyerere pale na walikata kadi zao za TANU ofisini kwa Abdu Sykes.
Nyerere akija pale sokoni anaporwa kikapu na watu hawa nje ya soko Mtaa wa Mkunguni na akirejeshewa kinakuwa
kikapu kimeshatakata anarudi nyumbani kwake Magomeni.
Wakati hawa wakizunguka sokoni pale yeye anakuwa ndani ofisini kwa Abdu Sykes wanazungumza.
Haya mie nayaeleza kwa mapenzi na kuonyesha mapenzi ya wazee wangu kwa Nyerere wao wanasema namdhalilisha.
Niishie hapa.