Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Hapana huijui historia hii.

Ni suala la mdomo kutomkataa bwana wake.

Kisa cha uchaguzi wa tarehe 17 April 1953 kati ya Abdulwahid Sykes nimekieleza kwa kirefu hapa ukumbini
labda kwanza kama useme hukubaliani na yale niliyoandika.
 
Nina ushahidi umetunga! Nikiweka ushahidi huo utaamuomba mwenyezi mungu radhi? Kuna mahali hakuna research niweke hapa na ikithibitika uombe jamvi radhi?
 
Inakuaje mtu anaji-quote mwenyewe kila sehemu?

Kwa kuwa ni ''authority'' katika somo hili.

Kama unae mtu kafanya tafiti na kaandika kunishinda
katika somo hili nifahamishe na mimi nimfuate kwa nukuu zake.

Ni hilo tu.

1. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.

2. Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi 2006

3. Contributing Author African Anthology, The Mermaid of Msambweni, Oxford University Press, 2008 Nairobi

4. Uamuzi wa Busara, Abantu Publications, Dar es Salaam, 2009

PART OF RESEARCH PAPERS/ARTICLES

In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).


1. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London)

2. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)

3. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam)

4. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam)

5. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).

6. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000' (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15[SUP]th[/SUP] – 17[SUP]th[/SUP] 2003)

7. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27[SUP]th[/SUP] February – 4[SUP]th[/SUP] March 2004)

8. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11[SUP]th[/SUP] April 2004).

9. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8[SUP]th[/SUP] - 10th February 2006)

10.The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (Paper Presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa, University of Johannesburg 1 - 3 September, 2006 (the paper was again presented to Islamic Propagation Centre International)
 
nina ushahidi umetunga! Nikiweka ushahidi huo utaamuomba mwenyezi mungu radhi? Kuna mahali hakuna research niweke hapa na ikithibitika uombe jamvi radhi?

sasa kama una ushahid si uuweke ili tuuone ukweli?kuombwa radhi kutakuongezea ama kukupunguzia nini??mbona watu wamekaa kishabiki shabiki hivi,kama una ushahidi weka watu waone,kama utaonekana una mantiki ukweli utadhihiri tuh,sasa vitisho wamtisha nani??
Kila mtu yupo hapa kujadili hoja.
 

Kuna ushahidi gani mwengine zaidi ya PUBLISHED work?

Au kwa kitu kuqualify kuwa ni ushahidi, kitu gani kinatakiwa? labda nikuulize
 
Unawakosea sana Viziwi na Bubu kuwaweka kwenye kundi la wajinga. Mjinga ni mtu yeyote asiyefahamu kitu au jambo fulani, ----, Jura, Galagula, Bozi, Mpumbavu, Juha.

Hakuna uhusiano kati ya ujinga na Kiziwi na Bubu.

Wamfahamu Ustadh Ilunga Hassan?
Napenda sana mihadhara yake...ofcourse, huwa haihusu dini.
Pale hata Ponda haoni ndani....kawaita wazenji Mbwa na viongozi waislamu wanaoongoza zenji nao ni mbwa.....ni mbwa wa mfalme ..mfalme being Rais wa Muungano,, rais wa mfumo kristu, so wakina Shain ni mbwa wa mfalme ambao among wazenji ambao ni mbwa, Shain anakuwa mfalme wao.

Very funny.....eti Shekhe wa Mombasa kauwawa, anawaambia watu wa mombasa wasipige mawe magari ya watu, kama wanataka revege wakamate padre mkoja au askofu au kardinal wachinje. Wakichinja kama wanne hivi watakuwa wametuma ujumbe.

The likes of ustadh Ilunga ni wengi sana ila labda hawanivutii.
 
Nina ushahidi umetunga! Nikiweka ushahidi huo utaamuomba mwenyezi mungu radhi? Kuna mahali hakuna research niweke hapa na ikithibitika uombe jamvi radhi?

Kuna haja gani ya vitisho.
Weka ushahidi hapana tabu.
 
Kuna threads tatu humu za Mzee Mohamed Said, Mag3 na hii ya Yericko Nyerere. Zimesheheni kila kitu. Ni zaidi ya kitabu cha mzee huyu mfia dini.

You cannot be serious!!

Nadhani shule itakua umeeenda kuangalia majengo, ku-mingle na kujua watu tofauti si kutafuta 3ilmu.
Msomi, "great thinker" yoyote hawezi hata kufikiri let alone kusema au kuandika ulichokiandika. Nakuonea huruma sana kijana.

Mungu akuongoze inshaaAllah Ameen
 
Last edited by a moderator:
Hizi threads ni akili, fikra, michango na mawazo ya watu wengi. Kitabu chako kile ulijifungia mahala ukakiandika akili na vionjo vyako mwenyewe. Najua ukipewa nafasi ya kukiandika upya na baada ya kupitia humu JF kuna ambayo utasahihisha, utaondoa au kuyaongeza. Kitabu chako kile sio msahafu. Kuna mambo mengi mle sio kweli.

Tatizo la vitabu vingi ni kuwa "static". Usijali sana juu ya wazungu kukienzi na kukitukuza kitabu chako hiki. Wazungu hawaijui Tanganyika/Tanzania kuliko sisi.
 

Mzee wangu Mohamed Said,
Kama mtu kaweza kusema kuwa thread tatu ulizojadiliana na Yeriko zinausambamba na kitabu chako, huyo mtu shule alikwenda kutalii na si vinginevyo.

Athari za mfumokristo ndo hizi. kuzalisha madudu
 

Tusichanganye hoja.
Tumalize ya Mkapa kisha Insha Allah tutaweza kuja kwa Bilal.

Hiyo kuwa Mkapa kakataa ushahidi wa Waislam kwa kuwa ni ''tungo''
na ''hisia'' kauli hiyo umeipata wapi?

Tafadhali nifahamishe.
 
Mzee wangu Mohamed Said,
Kama mtu kaweza kusema kuwa thread tatu ulizojadiliana na Yeriko zinausambamba na kitabu chako, huyo mtu shule alikwenda kutalii na si vinginevyo.

Athari za mfumokristo ndo hizi. kuzalisha madudu

Wewe bado kijana hujaona mengi.

Mimi nimekutana na hao wengi sana maishani.
Wasojua hadhi ya Cambridge wala Oxford.

Ndiyo maana unaona humu mimi sipati shida hata kidogo.

Ni wepesi kutukana.
Ni wepesi kukejeli.

Kibri kimewatangulia.
 

WC

Huu ndiyo ushahidi ulionitisha nao?
Kama upo mwingine hebu nifahamishe.
 
Unaponiita kijana wakati nimeshatafuna nusu karne unanikosea adabu. Kwani kitabu cha Mzee wetu Mohamed ni msahafu? Amekosea mengi tu mle. Kumbuka Mzee Mohamed alizaliwa miezi kadhaa kabla TANU haijazaliwa tarehe 7.7.1954. Hadi tunapata uhuru alikuwa hata shule ya msingi hajamaliza. Yoote kasimuliwa na mengine katunga ili kusukuma mbele agenda yake kuu ya UDINI na kumbomoa Mwalimu.
 

Kijana unatisha!

Fikra za mtu kama wewe unadhani zitaingia kwenye kitabu ambacho ni authority kama cha mzee wetu?
Mtu unayesema kuwa threads ni sawa sawa na kitabu?
Mtu ambaye hujui the significance of a work of academia being published?
Mtu ambaye hutambui the weight of Cambridge, Oxford na Harvard kukipitisha?

Kama utajaaliwa kufanya research na utabeza research yako from threads za JF, mdogo wangu utafeli vibaya na utachekwa
 
Kusomeshwa kwa kitabu chako huko ughaibuni kwa wasiojua ukweli, sio turufu yako kwetu katika mnakasha huu mzee wangu

Huyo Mzee Mohamed Said, kitu muhimu kwake ni kuwa kitabu chake kimekubaliwa na kusomwa USA na UK tu! Lakini ajabu analalamika kuwa UDsm Wahadhiri hawakubali kufanyiwa marejo, na kwa kuwa Wahadhiri hao wamekataa kitabu chake; basi ni Wakristo.
Ajabu ni kuwa hao wa UK na US ambako kinatumika kwenye vyuo vyao, hawataji kwa dini zao!
 
Sio mimi Mzee Mohamed. Fanya subira au kapumzike leo.

Nakuomba radhi.

Angalia unavyojiharibia muruwa wako.
Ilitosha kunambia kuwa siyo mimi.

Mimi nikakutaka radhi.
Hapakuwa na haja ya kuongeza hayo mengine.

Huo ni ujuvi.
Na ujuvi si sifa ya mtoto aliyefunzwa adabu na mama yake.

Usiwatukanishe wazee wako kuwa hawakukufunza adabu.
Adabu, tabia njema ni silaha utapendwa popote.
 
hoja ipo wazi sana,sijui nini kinachowakwaza.Hapa namkumbuka paulo alipokuwa anawashangaa Wagalatia kwa namna wasivyoelewa mpaka kufikia kuwauliza,hivi nyie wagalatia msiokuwa na akili ni nani aliyewaroga.....

Huna weledi, sana sana umeonyesha mlengo wako wa kidini kiasi cha kumuingiza Mtume Paulo na barua yake ndani ya Biblia.
 

Kama umetafuna nusu karne na unamawazo haya, nakuonea huruma kwako na vizazi vyako

Au labda ulimwengu wa academia huufaham vizuri na hufaham taratibu zake ndo mana unasema haya, kiasi cha kusema thread tatu za Yeriko na Mzee Mohamed Said ni sawa na kitabu chake.

Ungejua uzito wa the Golden Triangle kule Uingereza au Ivy League kule Marekani, nadhani ungekiangalia kitabu kwa mtazamo mwengine kabisa

Nawasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…