Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Na kweli hili hata mimi nimeliona, sasa hivi anakuwa mwangalifu sana. Lakini nimejifunza kitu, si vizuri
kukaa kila mara na watu wanaokusifu tu au kukusikiliza bila kuhoji....Unaishia kuwa arrogant.

Na ukishakuwa arrogant na ukawa na darsa la aina hiyo wanameza kila kitu, kama Warioba hakuwa
anafahamika kabla ya kuwa Waziri Mkuu watu wanameza, Kigoma Malima alianzisha namba za Mtihani
watu wanameza, Nyerere aliingia Dar 50's watu wanameza, Utafiti uliopinda Watu wanameza n.k n.k.

BTW: Ameshakuweka kwenye "shit" list yake?
 

Platozoom,
Mimi ni yule yule na ikiwa unadhani nimebadilika mimi
hili kwa kweli silijui.

Kuhusu Malima na hayo mengineyo nasimama katika
kauli zangu zote na hiyo ni pamoja na historia ya Nyerere,
Warioba nk.

Tatizo ni kuwa mnaojibu si mliokusudiwa maneno hayo na njia
nzuri ya kuweza kupambana na kitabu changu si hii mnayotumia
ya mistari kumi JF.

Namna hii tutakesha.
Andikeni historia yenu ijibu kitabu changu.

Kuhusu jeuri.
Hakika kuwa wakati nakuwa jeuri na hii inategemea.

Na huo ujeuri huwa nimedhamiria kabisa.
Muungwana huwezi kumfanyia jeuri.

Anaenistahi na mimi humfanyia staha.
Huu ndiyo ustaarabu.
 

Heshima yako mzee MS. kwa kusema kuwa ikiwa kitabu kimekuchoma HILI NILILITEGEMEA NA HALINISHANGAZI hapa sasa una-qualify my calling you a LIAR. Hukunijua wakati unatunga kitabu hiki. Period.
 

Wimana,
Naona hili la Ukristo katika Wamanyema limekukaa.

Ama mimi kukubali...
Sasa nimekubali nini?

Umenipa mfano wa Mmanyema Mkristo.
Sawa mie nani nikukatalie?

Lakini inajulikana fika kuwa kumpata Mmanyema Mkristo ni shida.
Unaweza ukamkuta Mrufiji Mkristo na wala hilo halitozamisha jahazi.

Au Mmashomvi Mkristo na zaidi sana inakuwa kitu cha ajabu.

Lakini mimi hadi nafika umri huu wangu wa uzee sikupata kusikia au
kushuhudia Mmanyema Mkristo hadi uliponitanabaisha.

Kwa hili nakushukuru.
 
RITZ;
we kila mara unapogusia msosi nami ndio huwa nala! hapa nanywa maziwa mgando (Nyati) na nyama choma (bata mzinga) hii kwa leo Alhamdulillahi inatosha! unajua tena zaidi ya hapo ni kuongeza uzito!

Kadogoo, I like this. Bwana nimeshacheka mno. Bwana nimekumiss sana. Take care
 
Heshima yako mzee MS. kwa kusema kuwa ikiwa kitabu kimekuchoma HILI NILILITEGEMEA NA HALINISHANGAZI hapa sasa una-qualify my calling you a LIAR. Hukunijua wakati unatunga kitabu hiki. Period.

Wickama,
Kuniita muongo sawa hivyo ndivyo unavyoona.

Hakika kuna wengi kama wewe wametabika sana na kitabu changu.
Akili zao hazikubali kabisa kama hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa.

Wako waliokuja kuzungumza na mimi uso kwa macho...

Dunia ndiyo ilivyo kuna wakati mpaka uijue sababu ya ajabu ndipo
hiyo ajabu inapoondoka.
 

Wimana,
Hapana sina sababu ya kujibaraguza.

Hiyo nimekupa ni mifano ya mfano wa Wamanyema.

Mie sina mfuasi mie naandika kama uandikavyo.

Naungwa mkono na kupingwa kama wapingwavyo
wengine.

Sijawa na makamu ya kuwa na wafuasi.
 
Kumbe Nyerere alikuwa Dar mwaka 1945 na akakutana hapo na kina Dossa pia; hii ni kabla ile safari akiwa mwakilishi wa TAA kutokea Tabora 1946. Watu wa Dar walikuwa wameshaisikia habari zake.

Moja ya mambo anayoyatambua fika Mzee Mohamed kuwa Kama atawaeleza ukweli huo wafuasi wake basi misheni yake itavurugika
 

MS, heshima tena kwako. The central issue hapa MS ni moja. Ukishaji-commit kuwa ULITEGEMEA a THAT and THIS reaction from a person you have never known while publishing your book, then ABSOLUTELY you are not TELLING the TRUTH (with all respects). The least you could say as a scholar Mzee MS, ni kuwa you RESPECT my position. Which is what you are NOW DOING and my deepest respects to you for the courage to utter that. Nimeshasema MANY TIMES, kwamba much as sina tatizo na mtiririko wa matukio, i just DO NOT SHARE your analysis and interpretation of some. SIO lazima watu wawe wamoja kwenye INTERPRETATION, never tofauti na wapambe fulani wanavyobamiza watu humu wasitofautiane. I HONESTLY BELIEVE ABDUL SYKES WOULD STILL HAVE BEEN A HERO HATA kama ANGEKUWA A HINDU. I refuse to associate his vission and strength to his Muslim faith. Martin Luther King, Mao-Tse-Tung, Mandela and Mahatma Ghandi their and each belonged to different faiths. That is where i will always stand. That aside, and in recognition of your scholarly achievement I have ALWAYS stood on your side kuwa EFFORTS zako za kuandika kitabu LAZIMA zipewe their due share of RESPECT (Soma threads zangu zote on this matter). We tanzanians have just too few books in the worldshare. Anybody trying it including Yericko lazima tum-encourage. It is for this reason, and with utmost respect to you that i refuse to be stereotyped by your last posting kwa sababu you just dont know my educational path and neither did you know it at the time of publishing this book and i stand by THAT. It is obvious uliandika posting yako in anger and possibly some hurry. Wanasema it is not personal stritcly business. Haya tuendelee na darsa. I love your both arguments (you, Mwanakijiji and Nguruvi). Lets forget this and move on.
 

Mimi ni mkristo lakini mpka leo nalaumu Marekani na vita hii na naipinga kwenda kutumia drones zao Pakistan, somalia Afghan na sehemu nyingine, hata juzi kwenye Boston Bombs niliwaonea huruma wamarekani na felt very bad for kid and those who lost thier lives and i got to think that what they went through is what Pakistan,somalia and other countries go through almost daily and to top up wamerikani wana wabomb na drone zao, i empathize with Iraq and Afghan people. But i have never looked at it as Muslims being oppressed, but i look at it as a Powerfull nation kuonea taifa dogo.

So huo ni udini when you look at it as Muslims being oppressed.
 


Wickama,
Nadhani unajua kuwa sie Wamanyema wawili uzito
wetu unatosha kuzamisha jahazi na kina Kasulwa
ni ndugu zangu...

Sasa ile mie kusema "nilijua" sikukusudia wewe.
Nilikusudia wote watakaosoma kitabu changu.

Hili la Uislam limerefushwa kuliko kusudio lenyewe
na baya zaidi ndio mwiba wenyewe.

Ama kuhusu Yericko ulosema sawa tunawajibika kumtia
ghera na huo ndiyo utu.
 
The history shows that,under the British,the tables were turned against muslims.
while germans considered Muslims their allies,the british regarded them as their enemies,as oliver (1965;206)says
Also in 1959,two years before Tanganyika's independence,a section of muslims(AMNUT),Expressd fear that after indpendence African christians would use their educationa advantage to perpetuate themselves in power and to undermine muslims.AMNUT urged the British to stay on,until Muslims were educationally at par with Christians,Nyerere argued,and his argument made a lot of sense,that the British who discrimated Muslims in education could not be expected to rectify that imbalance.The Muslim question could only be resolved in Independent Tanganyika.The majority of Muslims agreed with nyerere.
The muslim question,with which our country is plauged,is centred on that promise.Whether or not that promise has been kept.?
But what we see now is nothing rather than several ways of avoiding that question..
 
Wewe unadhani hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa kwa kuwa umeyatoa kwa Abdu! Unaamini pia kwamba wengi wametaabika na kitabu chako. Taabu tunayoipata na kitabu chako hiki ni hiyo ya wewe kuamini kuwa yote uliyoyaandika mle ni kweli. Mzee Mohamed, hakuna kitakaibadili historia ya nchi hii iwe kama ilivyo kwenye kitabu chako.
 



Well said mkuu

Yaani wauwe watu halafu end of the day wategemee peace what peace wata suffer kama wengine wanavyosuffer
 
Winama,
Inawezekana pia wapo Wanyagatwa Wakristo.

Sasa nifute kwa ajili gani ingawa sijamuona Mnyagatwa
Mkristo.

Sheikh Mohammed Said,

Salaam sana.

Hapa pana mambo mengi mno yenye kuleta rabsha kiduchu na vichekesho vingi. Nafikiri unakumbuka ile bayana yangu ya awali kwako,sababu nilichelea kuingia mambo kama haya ya udini,kutaja majina na kuwaadhiri jamaa zetu toka family mbalimbali tunazozistahi na mikanganyiko mingi saana,na matokeo yake tupo nje kabisa na hii mada/shutuma dhiki yako.

Imekua kama mtego wa panya sasa,anangia alokuwamo na asokuwamo!ahaha!!

Nimecheka pasi kiasi na yale majibu ulotoa kuhusu hiyo habari ya mmanyema mkristo. Nafikiri Sheikh Mohammed labda kitambo hujenda tembea pale Ujiji kuona "mabadiliko". Mimi binafsi pia pana pahala kwingi nahitaji nikatupie jicho Insha Alaah penye uhai na maajaliwa.

Hii habari ya makabila, ama kwa hakika imenichekesha kiduchu hasa ulipotaja Wangazija Wakristo. Unajua pale Comoro siku hizi pana wale "Wangazija pori" ambao huenda pale "kununua baraza" na kujinasibu Ungazija pasi kiasi. Ukizungumza na Bwana Ahmed Rajab atakuchekesha zaidi juu ya habari hizi.

Nafikiri hata ndugu zetu wa kiZaramo zamani nao walikua na dasturi na ustaarabu kama huo wa kukaribisha "wabweshu" na kuita "udugu wa khiyari". Tena walikua wakifanza na sherehe kubwa mno siku ya kutimiza huo "udugu". Napenda saana tamaduni na mapenzi yalokuwapo zamani baina yetu.

Sijui lini utapata fursa tuwekee na habari za mapinduzi ya Zanzibar,hasa wale wamakonde wa Kipumbwi,Ushongo na Sakura walotumiwa kuua ndugu zetu na kumuweka madarakani yule Mnyasa alokuja Unguja mtoto wa mgongoni(yaleyale ya Musharaf kuja Pakistani mtoto wa mgongoni halafu kuwafanzia watu hadaa). Ndugu na jamaa zetu wengi walitolewa roho na yule dhalim.

Uncle yangu Commando Amour Dougheish,ndo alokua akamkamate yule Mnyasa toka pale Ikulu na kumpeleka pale Idara ya habari - Rahaleo, halafu atangaze kuwa nchi isharejeshwa na imo mikononi kwa wananchi wenyewe. Wallahi,lile jambo mpaka leo najuta halikufanikiwa.

Basi Insha Allah tuendelee na mnakasha.

Ahsanta.
 
Well said mkuu

Yaani wauwe watu halafu end of the day wategemee peace what peace wata suffer kama wengine wanavyosuffer

But Dont get me wrong, just t clarify

I do not condone any violent au terrorist act kwa jamii au watu wowote, in the name of anything.


Violence is violence, act of terror is act of terror, it has no justification whatsoever.
 


Wild Card,
Kama kubadilika ndiyo nishaibadili.

Leo historia ya TANU na Nyerere mwenyewe watu wanaisoma vingine.
Haya ndiyo mabadiliko yenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…