Ukimtaja Mze Shekue unanikumbusha mbaali sana enzi za akina Sheikh Abdullah Ayub na nduguye Mohamed Ayub.
Barubaru,
Salaam. nafurahi na nakutazama sana bayana zako hapa jamvini. Nilifurahi kuna wakti ulitujuza yakuwa Almarhum Burhan Mtengwa alikuwa ni class mate wako. Mimi nilimfahamu uzuri kupitia kwa Dr. Ibrahim Msabah. Insha Allah Mola tamjaalia kauli thabit na Fir'daus huko alikotangulia.
Nijaalie fursa kiduchu ya kunipokelea bayana yangu hii adimu kwako.
Mimi kwa upande wa Mama yangu ni baina ya Unguja na Tanga. Ndo maana baadhi ya jamaa hapa wakizungumza na kutuchosha kwa kuitaja Tanga,basi mie husikiliza na kujichekea peke.
Hao wanaotaja kila kukicha hizo habri za Zahrau hata na Tamta yake;family yetu ndo baadhi ya waasisi na wafadhili mpaka kesho Allahmdulillahi. Zile shughuli za awali zoote za Islamic knowledge,Taqwa,Shura,Tahweed na mengineyo mengi babu zanguWazee wetu walikua ndo Wanazuoni,wanaharakati, washughulikaji na wenye kutakwa shauri kwa kila lilotaka kufanzwa.
Leo huwezi kuitaja au kuijua asili na waasisi wa Tanga mpaka kuna baadhi ya jamaa,family uzijue kwa kina. Huyo jamaa anayetaka watu wakamuulizie habari zake kwenye misikiti na baadhi ya maSheikh pale Tanga mjini mpaka Lushoto,yanini tufikie huko ya Illahi ya manani?
Nimekujuza haya machache,maana umenitajia baadhi ya jamaa zangu wa karibu na maswahib/ndugu wa karibu wa family yetu na pia hapa kuna watu kila kukicha wanatutisha na habari za Tanga.
Pamoja na kuwataja hao kina Sheikh Mohammed na Abdallah Ayoub,pia huwezi ikamilisha Tanga leo bila kuwataja kina Sheikh Shame Mbuyu wa Kwale,Bwana Vuzo Mnyimanzi wa Chumbageni,Sheikh Merei Islam Al Baajiry,Sheikh Ali Bin Muhammad Majisu,Sheikh Hemed Bin Jumaa Al Bukhry,Sheikh AbdilRahman Salim Jibran,Sheikh Maalim Pera Bin Ridhwan,Bwana Fadhil Bwanga na wengineo wengi mno. Halafu pia lazim hiyo Tanga uijue local politics zake tangu enzi ya Mwarabu, Mjerumani na enzi ya wenye mji wao. Na ujue vitongoji vya asili na tamaduni za pale,mfano;Kilindi,Vuga,Tongoni,Mnyanjani,Chumbageni,Pongwe,Mkwaja,Buyuni Kuu,Ngamiani,Chuda,Kwale,Chongoleani,Mwarongo na mambo mengi kadhaa wa kidhaa.
Kwa ufupi kwa wale wasokwisha kututajia habari za Tanga kama vile sisi wengine ni wageni hii ni home work yao. Na wakajaribu kumuuliza huyo Sheikh Shekue, nae atawafahamisha uzuri hayo majina na hizo sehemu kwa kina,kama nae anajua au ni mtu mwenye asili ya pale Tanga mjini?
Hizo sehemu za Donge,Sahare na nyinginezo si sehemu za watu wa asili ya pale. Ilikua ni viunga tu vya wazee wetu au makazi ya wageni walohamia pale Tanga,ambavyo nahisi ndivyo ilivyo sasa?
Nilistaajabu pale Nguruvi3 alipomtaka Sheikh Mohammed Said ati atake radhi kisa "alimwambia hilo neno usirudie tena". Nguruvi3 akadai ati hilo neno kwao Tanga ni tusi!? Si kweli asilani,nami nampa challenge huyo Nguruvi3 ataje Tanga ipi hiyo atokayo yeye,na anipe nasaba yake kwa kina. Au nae kahamishia tu pale Tanga na mila za kwao Tarime,kama ni hivyo itakua amezungumza kweli.
Tangia zamani haikuwa ati ni mughali kwa Mkristo,asokua na dini au mtaalamu yeyote kujua Quran,Sunah na masuala fulani kuhusu Uislamu. Haina maana yakuwa huyo mtu ati ni Muislamu. Na mfano wetu wa karibu hapa jamvini kuna huyu ndugu yetu Mwanakijiji. Yeye anajua mengi kuhusu Uislamu na Quran kutokana na sababu zake kadhaa japo anadai hana dini. Huku nje kuna wale so called Orientalists na wataalamu kadhaa hasa wa nchi za magharibi, tangia karne ambao ni Wakristo au Atheists,nao pia wanajua saana Quran na Uislamu kutokana na sababu zao kadhaa za kitaaluma na nyinginezo za kidhalim. Kwa hili tusipate taaabu kwa jamaa wengine kutaka ati kutupatia Islamic knowledge na hadith kadhaa za Mtume-SAW,hapa si pahala pake,na kama ipo haja basi ifunguliwe thread nyingine. Nachelea tusijetia udini uso kiasi hapa jamvini,kuwakera ndugu zetu wengine na pia tukaongezewa kashfa na tashtit kwenye Iman yetu. Mengi yalosemwa juu ya Uislam imeshatosha.
Niwie radhi Al Akhiy,najua mengi humu tunasababishwa tunene pasi na mioyo yetu kutamani.
Ahsanta.
Cc; Ritz,The Big Show,Nguruvi3,Ami