Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Nilipo Blue.Al akhiy Gombesugu umegusa saaaaaana saaana kama nawaona hawa baadhwi ya masheikh uliowataja. naona umesaha vitongoji vngine Muhimu kama Ndumi na darini kisiwani kwani huko ndio chimbuko na bahri kubwa ya ilmu kwa wengi.Mimi nashauri tuweke uzi maalum tuichambue TANGA ilivyokuwa kabla ya uhuru na baada ya uhuru kwanini Tanga imedidimia kiuchumi wakti kila kitu wanacho kuanzia bandari na hali ya hewa safi kuona dhulma walizofanyiwa.Upande wangu nitachambua sana kiuchumi kwani nina data nyingi sana za huko na wapi waliwakona na kuwadhulumu.Nimefurahi sana uchambuzi wako na Allah akubariki sana.maa salaam
Kokote ambako UISLAM umetamalaki na kukomaa kwa sana nchi hii hakuna maendeleo KIELIMU. Kwa maana hiyo na maendeleo mengine hayapo. Huu ni ukweli mchungu kidogo ambao hata hivyo ulianza kufanyiwa kazi na Mwalimu kwa kutaifisha mashule mengi tu na kutenga nafasi maalum za sekondari kwa ajili ya watoto wa maeneo haya kama ilivyokuwa kwa jamii za wafugaji.Haisaidii sana kuukana ukweli huu au kuhamishia matatizo haya kwa mtu/watu au jamii nyingine.
 
Nyirabu ni Mkurya, Warioba hakuwa Mzanaki kama Nyerere kwa hiyo suala la Ukabila halipo. Na hapa kwenye Kitabu chake anasema kipindi Warioba anateuliwa kuwa Waziri Mkuu hakuwa akijulikana wakati iko wazi tayari alikuwa mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa hivyo anaingia moja kwa moja Bungeni, utasemaje mtu huyo hafahamiki? Na hilo la Mtihani tulishalimaza siku nyiingi. Kaka yangu (alikuwa mtoto wa jirani yetu na hivyo tulikuwa kama ndugu) amemaliza darasa la saba kwa mara ya kwanza 1980 kabla hajarudia na alitumia namba za mtihani, na tena haya wakiongea na Kaka yangu wa kuzaliwa nawasikia kabla hata uvumi huo unaousema haujasikika.Na nikuulize kitu kimoja ni nani aliyemteua Warioba kuwa Waziri Mkuu na Nyirabu Gavana?
Nikusaidie kitu.Enzi za Nyerere professional hazikuwa zinazingatiwa bali mambo yote Chama kimeshika hatamu za uongozi. Kila pahala siasa inatawala.Lakin kumbuka nimekulia Tz na kuzunguka karibu nchi nzima wila zote za Tz Bara najua mengi. Kumbuka kuwa unaposema Mbeya mtu yoyote huko atakwambia wanatoka wanyakyusa lakin kumbuka kuna makabila mengi sana wakiwemo wapangwa, wasafwa na wengine.Unaposema Mara watu wote watakwambiia wanatoka wakurya, lakin kuna makabila mengi sana kule wakiwemo wang'oreme, waikizu, wazanani na wengine wengi tu.Kwa bahati najua sana utendaji na uwezo wa Nyirabu na hata warioba kwani kwa namna moja au nyingine niliwahi kufanya nao kazi hivyo ninachozungumza nalinganisha na uwezo wao kikazi na utendaji wao. wapo wengi lakin naona tuishie hapa kwani ni upendleo wa dhwahir.
 
Katika kitabu chake bwana Mohamedi ametoa shutuma nyingi sana kwa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo ya eti Mwalimu katika hotuba yake ya kuaga taifa alitamka wazi kuwa hamjui ABDUL SYKES, Inashangaza sana kwani Mohamed Said anajua wazi ameudanganya umma na kudhihaki wanaukombozi wetu.

Ilikujiridhisha ndugu zangu wadau pitieni sehemu ya Hotuba ya Mwalimu Nyerere ya kuaga taifa tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais aliyoitoa mbele ya wazee wa Dar es Salaam,




‘"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.

Niliporudi nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini nikiwa shuleni – Chuo Kikuu – nilijua. Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ya siasa. Niliamua hivyo: Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda na kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.

Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.

Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.

Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima. Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Kwa hiyo la maana siyo kuanzisha matawi, maana chama kipo na matawi yameenea; la maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.

KUVUNJWA KWA TAWA

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere. Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.

Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA?
Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo Anautouglou. Kwenye mkutano huu wakanichagua kuwa Rais wao – wa TAA.

Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana – katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.

Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).

WAZEE NA MSIMAMO

Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi. Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano.

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz – waliokuwa wengi ni wazee.

Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: Wazee na Ndugu zangu! Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU. Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa! Hawakuyumba hata kidogo! Vijana walikuwa na mashaka. Wengine walikuwa na vikazi vyao, waliogopa kuvipoteza.

Nalo jambo lenyewe ni la hatari – la kuzungumzia uhuru! Unaweza ukakosa kazi; na wapo waliopoteza kazi; wengine wakaacha kazi. Akina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.

Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.

Nilikwenda Songea mwaka 1955 mara baada ya kujiuzulu. Huko wazee walinipokea na kunielewa. Nilianza safari za kuitembelea Tanganyika nzima. Nilikwenda Mbeya. Mkutano wangu niliufanya na wazee; kikundi kidogo cha wazee, ndani ya nyumba ya mtu.

Kwa mkutano huu wa Mbeya, wazee wakauliza: Unatafuta nini? Nikawaambia natafuta uhuru. Wale wazee, kwa sababu ya vita vya Maji Maji, na wanakumbuka, kabisa, wakaona mimi ninatafuta jambo la hatari. Tulifanya mkutano wa makini kweli. Wakauliza: Wewe unawezaje kuleta uhuru? Wewe una njia gani kudai uhuru na usitiwe kitanzi na Waingereza?

WAINGEREZA WAONGO

Tulielezana. Nikawaambia ninyi wazee, Waingereza wanawadanganya, Waingereza wametumwa na ule Umoja wa Mataifa uliokufa (League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari, watuachie tukajitawale.

Waingereza wanafanya ujanja; hawasemi. Vita vimekwisha (vya Pili) na Umoja wa Mataifa mwingine – mpya (United Nations Organisation – UNO) umewakabidhi Tanganyika kwa shabaha ileile. Sisi siyo koloni lao. Wamepewa dhamana tu.


Kwa hiyo nikawaambia wazee, hakuna haja ya kumwaga damu. Tuwaseme tu! Tuwashitaki kwa waliowaleta hapa kwamba hawafanyi kazi yao; wamesahau kabisa!

Wazee wakauliza: Eh, inawezekana? Nikasema inawezekana. Kazi yetu ya kwanza ilikuwa kuwaambia watu kwamba uwezekano wa kujitawala upo. Hilo lilikuwa la kwanza. Wazee walijua maana ya kujitawala. Walitamani kujitawala, lakini hawakujua waanzie wapi.

Vijana hawakuwa na habari kwamba kujitawala kunawezekana. Kwa hiyo kwa wazee sikuwa na matatizo. Wao hawakuwa na kazi; hawakumwogopa Mwingereza. Hawakuogopa kufukuzwa kazi. Baadhi walikuwa wafanyabiashara.

Mzee John Rupia (marehemu) alikwua mfanyabiashara na kaidi kidogo. Aliwahi kutishwa na kunyang’anywa leseni yake ya biashara. Akaambiwa akiendelea kushirikiana na kijana mwenda wazimu (Julius Nyerere), atanyang’anywa leseni moja kwa moja. Rupia aliwajibu: Potelea mbali!

Nasema yote haya ikiwa njia ya kutoa shukrani kwa wazee na imani yao kwa vijana wakati huo.

Imani hujenga imani. Na mambo haya makubwa ya nchi, kama hayana baraka za wazee hayaendi. Magumu sana. Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani. Tangu awali kabisa.

TWAININGI AMEKWISHA

Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.

Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee – za jadi.

Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, “Twining (Twainingi) umekwisha!” (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!

Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama. Twaining hawezi tena!

Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo. Kwenye makaburi kule! Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.

Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa. Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo. Tufunge! Tukafunga. Hakuna kula. Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko. Tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni.

Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia. Mimi nikamuuliza mzee: Sheikh, una Aspro? Akajibu: Kwa nini unataka Aspro? Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kwelikweli. Akasema subiri.

Tulisubiri hadi saa ya kufuturu. Tukafuturu vizuri. Mzee Ramia akaniuliza: bado unataka Aspro? Nikajibu kichwa sasa hakiumi. Kumbe ilikuwa njaa.

Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee."’



Mohamed Said kuwa mkweli, waambie ukweli watanzania (waislamu) kuwa umetumia mgongo wa Uislamu na Hayati Abdul Sykes, kwakumkashifu na kumdhihaki Hayati Mwalimu Julius Nyerere na kuwasafisha wazee wako walioasi serikali mpya ya Mwalimu ambapo ndipo madhila hayo wakayapata.

Mtu yeyote mwenye akili timamu akisoma hiyo hotuba ya Nyerere ataelewa kwamba huyu jamaa alikuwa mnafiki sana.

Haiingii akilini kumfahamu Abdul Sykes eti wakati amerudi kutoka Uingereza na baada ya kukaa pale Pugu kwa mda ndio aje Dar es Salaam kutaka kujua viongozi wa TAA ni kina nani. Alifahamishwa kuhusa TAA tangu yuko Makerere na akashauliwa kuacha kuanzisha chama kingine badala yake afungue tawi la TAA pale. Baada ya kurudi Makerere akachaguliwa kuwa Katibu wa TAA wa jimbo la Tabora. Aliwezaje kufungua tawi kule Makerere na baadaye kukubali kuwa Katibu wa TAA wa jimbo bila kumfahamu Abdul Skyes ambaye katika kipindi chote hicho alikuwa Katibu wa Chama?

Labda kama akili zake zilikuwa sio nzuri hivyo akakubali kuacha chama chake alichotaka kuanzisha na akajiunga na chama kingine bila kujua viongozi wa juu ni kina nani na nini malengo ya chama chao.
 
gombesugu,

Kwa kweli nikisoma bayana zako humu jamvini walaahi najisikia murua raha mstarehe.

Hawa ndugu zetu wanasema tusitumie neno "sisi" au "nyie" wanasema siyo uzalando wakati huo huo hao wanaotoa kauli hizo ndiyo wanaotuita sisi wafuasi wa Mohamed Said na wale wote wanaopingana na fikra za Nyerere.

Kwa maana hivyo hawa wote ambao ni Wakirsto ni wafuasi wa Nyerere. Sisi watu wa madarasa akili zetu na fikra zetu zinafanana kama machinas..ha haa haa.

Kuna jamaa mmoja humu yeye alienda mbali zaidi akasema kuwataja hao wazee wa kariakoo humu jamvini kwake ni matusi makubwa huyu huyu ndiye anatoa darsa kwa Waislam, ha ha haaa.

Kuna mwingine yeye bingwa wa tambo na majingambo anawaita wazee wetu "mwanameka" yeye anaita kukata kisu na mfupa, ha haa ha.

Karibu sana mie napata uji wa shurba na mkate wa ufuta.
Wanachekesha sana!.
Kila tunachokifanya sisi sicho.
Tukipokea misaada inaitwa pesa za kigaidi na haramu.Lakini zile zao ndio safi.
Tukiandika vitabu vya kwetu sivyo,vya kwao ndio sahihi hata kama vinapotosha msingi wa jambo.
Tukitangaza.Sisi hatujui na hatujafikia viwango.Wao ndio wanaojua kazi hiyo.
Tukichapisha magazeti wanasema tunaandika vibaya,wao ndio wanaojua kuandika.
Tukijenga chuo wanasema hatufundishi vizuri kama wao.
Ilimradi kila tunachojenga wao wanabomoa.Imesema kweli Qur'an kuhusu tabia zao za husuda.
Akina Nguruvi wanajidai kututolea machozi ya mamba.Eti tufanye kama fulani na fulani tusilalamike......kama kwamba tuliyofanya huko nyuma tulifundishwa na yeye(wao).Na kama kwamba hayo tuliyofanya tayari yamesalimika na fitna zao.
 
Ngongo,Naona vibaya kuja na maneno ambayo kwa wengine yanachoma.Kwa ajili hii nitasema kitu kimoja tu.Kama ni kutaka kusema kuwa Nyerere alisimama kwa miguu yakemwenyewe alipofika Dar es Salaam na hakuwa muhitaji hii si kweli.Hayo ya umaarufu kabla ya kutoka UNO Machi 1955 wala sitatia neno.Ila jiulize kipi kilichofanya Tanzania ya leo impe Abdu na Ally Sykes medalibaada ya miaka 50 ya uhuru?Kipi kikubwa walichofanya?
Medali aloopewa Abdu na mdogo wake ni ile ya wao kuwa miongoni mwa waasisi 17 wa TANU. Miaka 50 ya uhuru ndio ilikuwa mahala pake. Kwani ulitaka wapewe lini hasa! Mzee Mohamed, wewe ni wa kuhangaishwa na mambo madogo kama haya? Hata Mwalimu alipewa medali ile siku hiyohiyo na Mama Maria akaipokea kwa niaba yake. Mwalimu hakuwa mtu wa kujikweza na kujitukuza mwenyewe. Aliacha tuzo hizi wazitoe watu wengine.
 
Ngongo,
Naona vibaya kuja na maneno ambayo kwa wengine yanachoma.
Kwa ajili hii nitasema kitu kimoja tu.

Kama ni kutaka kusema kuwa Nyerere alisimama kwa miguu yake
mwenyewe alipofika Dar es Salaam na hakuwa muhitaji hii si kweli.

Hayo ya umaarufu kabla ya kutoka UNO Machi 1955 wala sitatia neno.

Ila jiulize kipi kilichofanya Tanzania ya leo impe Abdu na Ally Sykes medali
baada ya miaka 50 ya uhuru?

Kipi kikubwa walichofanya?

Mohamed,
Umeuliza swali zuri. Kipi kilichofanya Kikwete ampe marehemu Abdulwahid na Ally Sykes medali baada ya miaka 50 ya uhuru? Jibu lake linaweza kuwa VERY interesting. Lakini nadhani ni bora kila mtu aspeculate kivyake vyake.
 
Kokote ambako UISLAM umetamalaki na kukomaa kwa sana nchi hii hakuna maendeleo KIELIMU. Kwa maana hiyo na maendeleo mengine hayapo. Huu ni ukweli mchungu kidogo ambao hata hivyo ulianza kufanyiwa kazi na Mwalimu kwa kutaifisha mashule mengi tu na kutenga nafasi maalum za sekondari kwa ajili ya watoto wa maeneo haya kama ilivyokuwa kwa jamii za wafugaji.Haisaidii sana kuukana ukweli huu au kuhamishia matatizo haya kwa mtu/watu au jamii nyingine.

WC,

warabu wanasema hivi " Ujinga usio na khasara ni bora sana Kuliko Ilmu isiyo na Faida".

Unajuwa katika sehemu zilizofata na kutamalaki mila na desturi za Uislam ndizo sehemu zilizostaharabika sana hakuna mauaji ya vikongwe, watu kutembea na magovi, kukeketa, kuchuna ngozi na kunyofoa viungo vya albino na hata mateso kwa akina mama. Kwani Utamaduni wa kiislam unahimiza sana Utu na kuthamini hilo.
 
WC,

warabu wanasema hivi " Ujinga usio na khasara ni bora sana Kuliko Ilmu isiyo na Faida".

Unajuwa katika sehemu zilizofata na kutamalaki mila na desturi za Uislam ndizo sehemu zilizostaharabika sana hakuna mauaji ya vikongwe, watu kutembea na magovi, kukeketa, kuchuna ngozi na kunyofoa viungo vya albino na hata mateso kwa akina mama. Kwani Utamaduni wa kiislam unahimiza sana Utu na kuthamini hilo.
Misri wanakeketa, wewe!
 
Mtu yeyote mwenye akili timamu akisoma hiyo hotuba ya Nyerere ataelewa kwamba huyu jamaa alikuwa mnafiki sana.

Haiingii akilini kumfahamu Abdul Sykes eti wakati amerudi kutoka Uingereza na baada ya kukaa pale Pugu kwa mda ndio aje Dar es Salaam kutaka kujua viongozi wa TAA ni kina nani. Alifahamishwa kuhusa TAA tangu yuko Makerere na akashauliwa kuacha kuanzisha chama kingine badala yake afungue tawi la TAA pale. Baada ya kurudi Makerere akachaguliwa kuwa Katibu wa TAA wa jimbo la Tabora. Aliwezaje kufungua tawi kule Makerere na baadaye kukubali kuwa Katibu wa TAA wa jimbo bila kumfahamu Abdul Skyes ambaye katika kipindi chote hicho alikuwa Katibu wa Chama?

Labda kama akili zake zilikuwa sio nzuri hivyo akakubali kuacha chama chake alichotaka kuanzisha na akajiunga na chama kingine bila kujua viongozi wa juu ni kina nani na nini malengo ya chama chao.
Kama alivyomwaga mboga na Ugali wake umemwagwa.Yeye sie muasisi wa TAA iliyozaa TANU.
 
Wanajamvi leo tumeingia page # 649,Mzee wetu Mohamed Said anaelekea kukubali makosa ya kitabu chake namwona hatu lugha anayoitumia si ile ya mwanzo ana weka tahadhari kubwa kabla hajachangia hoja si kama kule mwanzo.

Napenda kuwapongeza Mag3 Nguruvi3 Mzee Mwanakijiji Jasusi platozoom WildCard Wickama .......Kazi mliyoifanya si haba Mzee wetu Moh kajivunza mambo mengi hakujua Nyerere alishaingia Dar kabla ya mwaka 1950.Hakuwa anajua Nyerere alikuwa kiongozi wa AA mwaka 1945 huko Tabora.Hakupenda wasomaji wake wafahamu Rais wa kwanza wa AA alikuwa Cecil Matola angetokea Gerezani angeandika page 10 kumwelezea uhodari wake,usomi wake ......Mzee wetu kwa maksudi alitaka kutudanganya kwamba Abdul Sykes ndiye aliyemtambulisha Nyerere katika siasa za Dar hakujua Nyerere alionana na Dossa Aziz mwaka 1945 bila shaka Abdul Sykes wakati huo hakuwa na ushawishi wowote na kama alikuwa nao basi ulikuwa hauvuki Gerezani.

Nasema tena nawashukuru sana kazi mliyoifanya ni kubwa na mnastahili nishani ya uraia wema uliotukuka.Uchambuzi na hoja mbali mbali hakika ni funzo kubwa kwa anayetaka kujifunza.

Naona sasa unataka kulazimisha Bao.

Pole sana
 
Mtu yeyote mwenye akili timamu akisoma hiyo hotuba ya Nyerere ataelewa kwamba huyu jamaa alikuwa mnafiki sana.

Haiingii akilini kumfahamu Abdul Sykes eti wakati amerudi kutoka Uingereza na baada ya kukaa pale Pugu kwa mda ndio aje Dar es Salaam kutaka kujua viongozi wa TAA ni kina nani. Alifahamishwa kuhusa TAA tangu yuko Makerere na akashauliwa kuacha kuanzisha chama kingine badala yake afungue tawi la TAA pale. Baada ya kurudi Makerere akachaguliwa kuwa Katibu wa TAA wa jimbo la Tabora. Aliwezaje kufungua tawi kule Makerere na baadaye kukubali kuwa Katibu wa TAA wa jimbo bila kumfahamu Abdul Skyes ambaye katika kipindi chote hicho alikuwa Katibu wa Chama?

Labda kama akili zake zilikuwa sio nzuri hivyo akakubali kuacha chama chake alichotaka kuanzisha na akajiunga na chama kingine bila kujua viongozi wa juu ni kina nani na nini malengo ya chama chao.

Rudia kuisoma hotuba hiyo kwa umakini na kwa utulivu kijana,

ukikurupuka hivyo bila shaka utaibuka na dhana hiyo.

Tofautisha kipindi yupo Makerere na kipindi yupo Scotland, ukifanya hivyo utaielewa hiyo hotuba ndugu yangu.
 
Mtu yeyote mwenye akili timamu akisoma hiyo hotuba ya Nyerere ataelewa kwamba huyu jamaa alikuwa mnafiki sana.

Haiingii akilini kumfahamu Abdul Sykes eti wakati amerudi kutoka Uingereza na baada ya kukaa pale Pugu kwa mda ndio aje Dar es Salaam kutaka kujua viongozi wa TAA ni kina nani. Alifahamishwa kuhusa TAA tangu yuko Makerere na akashauliwa kuacha kuanzisha chama kingine badala yake afungue tawi la TAA pale. Baada ya kurudi Makerere akachaguliwa kuwa Katibu wa TAA wa jimbo la Tabora. Aliwezaje kufungua tawi kule Makerere na baadaye kukubali kuwa Katibu wa TAA wa jimbo bila kumfahamu Abdul Skyes ambaye katika kipindi chote hicho alikuwa Katibu wa Chama?

Labda kama akili zake zilikuwa sio nzuri hivyo akakubali kuacha chama chake alichotaka kuanzisha na akajiunga na chama kingine bila kujua viongozi wa juu ni kina nani na nini malengo ya chama chao.
Sasa hapo mbona na ninyi mnapingana na Mohamed Said? Yeye anasema Nyerere alifahamiana na Abdul Sykes mwaka 1953 or thereabouts. Therefore alipokuwa Makerere hakufahamiana na Abdulwahid Sykes. Kipi msichoelewa hapo? Mwageni mboga lakini msimwage akili zenu.
 
Misri wanakeketa, wewe!

Uijui Misri naomba uisome vizuri.

Itazame haponchini kwenu maeneo ya pewani kama Mtwara, lindi, Pwani, Znz na tanga mambo niliyobainisha hapo juu yote yapo na linganisha na mara, Mbeya na kwengineko.


Pole sana
 
Uijui Misri naomba uisome vizuri.

Itazame haponchini kwenu maeneo ya pewani kama Mtwara, lindi, Pwani, Znz na tanga mambo niliyobainisha hapo juu yote yapo na linganisha na mara, Mbeya na kwengineko.


Pole sana

Sijakuelewa. Unabisha kuwa Misri hawakeketi wanawake zao? Unabisha?
Soma hiki kipande:

Despite being legally banned, female genital mutilation in Egypt is on the rise, causing lifelong pains, health problems and even death for the women who undergo it. Islamists are pushing to legalize the procedure again.
Umm Mohamed lives in a part of Cairo where others dump their garbage. The 47-year-old Muslim woman has experienced many hardships in her life. Putting on a brave face, she says she is used to being daily surrounded by dirt and misery. But what really hurts, she admits, is the pain she personally had to endure 35 years ago.
When Mohamed was 12, nearly all parents from the quarter where she lived brought their daughters of the same age to a hair dresser. "We didn't know why," she says, "but we were all very excited, as each girl had just been given a new, white dress."
In celebration of the day, the girls' hands had been painted with henna. They were ever so proud. But then came the moment of shock: "Suddenly this man, who was really a stranger to us, started to undress us," she recalls. "Then he got out his razor blade." All the girls underwent the procedure which mutilated them for life - without narcotics and without even minimal hygene standards.
'How can my family do this to me?'
Mohamed bled for three days. When it didn't stop, her father went to the local baker for some ashes to cover up the wound. But the dirt only made everything worse. "I still remember asking myself how my family could do this to me," Mohamed says, tears clouding her eyes. Another girl from her neighbourhood, she adds, even died after the procedure.
 
Wanaukumbi,

Naomba tujikumbushe baadhi ya mambo huenda tukajenga fikra zetu upya na kwa utulivu:

Tanganyika Kama Nchi Chini ya Udhamini waUmoja wa Mataifa


Mwanzowa Siasa Katika Tanganyika: 1950- 1954

Tanganyika African Association: 1950-1954

Kamati Ndogo ya Siasa Ndani ya TAA: 1951- 1954
Baadaya Vita Vya Pili Vya Dunia Uingereza ilikabidhiwa Tanganyika chini ya kifungu76 na 77 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Kama mamlaka tawala Uingerezailitarajiwa kuanzisha na kuendeleza maendeleo ya siasa, uchumi na ya kijamii yaTanganyika hadi kufikia wakati ambao watu wake wangekuwa tayari kujitawala. Lakini Waingereza walifanya khiyana na hawakutimiza ahadi hiyo.

Walijihusisha na kulinda maslahi yao wenyewe yakikoloni na yale ya watu weupe wachache na wakaendelea kuwapuuza Waafrika waliokuwawengi na wenye nchi. Wakati Wazungu na Wahindi walikuwa na jumuia zao kuendeleza maslahi ya watu wao katika Tanganyika, Waafrika walikuwa hawana uwakilishi wowote.

Wazungu walikuwa na European Association na Wahindi walikuwakilishwa naIndian Association. Vyote viwili vilishugulika na watu wao wenyewe. LakiniWaafrika hawakuwa na chama kama hicho kuwatetea. Katika Baraza la Kutunga Sheria Waafrika waliwakilishwa na mmishionari Mzungu jina lake Father Gibbons, aliyekuwa akifanya kazi Misheni ya Minaki maili kadhaa nje ya Dar es Salaam, Mzungu huyu hakuwa na uhusiano wowote na Waafrika aliokuwa akiwawakilisha na akikaa Minaki Misheni nje ya Dar es Salaam.

Kwa ajili hii Waafrika walipohisi hawawakilishwi na hawana chama kama kile cha Wazungu na Waasia kutafuta haki zao, walikutana na kuamua kuunda chama chao wenyewe. Gavana wa Donald Cameron ambae alitawala Tanganyika kuanzia mwaka wa 1925 hadi 1929 ndiye aliyeanzisha Baraza la Kutunga Sheria la kwanza katika mfumo wa IndirectRule.

Gavana Cameron hakupinga kuanzishwa kwa African Association pale ilipoanzishwa mwaka wa 1929 ila aliiasa kuwa chama kisijiingize kabisa katikasiasa. Vipi sasa Waafrika wataikomboa nchi yao ikiwa hawaruhusiwa kufanya siasa?

Waafrika vijana waliotoka vitani na vijina wasomi waliomaliza elimu yaMakerere College Uganda hawakukubaliana na msimamo huu wa kujiweka mbali na siasa. Mwaka 1950 vijana hawa walifanya mabadiliko makubwa katika Tanganyika African Association (TAA) kama ilivyokuwa ikijulikana baada ya kubadilisha jina mwaka 1948

Katika uchaguzi uliofanyika Dar es Salaam Dr Vedasto Kyaruzi na Abdulwahid Sykes walichaguliwa rais na katibu. Hakuna nyaraka zozote zinazoonyesha kama African Association ilikuwa imetayarisha mpango wakushughulikia hali ya siasa.

Kuelewa mwelekeo wa siasa kama wakati ule inabidi mtu atazame mwenendo wa viongozi wa TAA na jinsi walivyokuwa wakiyashughulikia mambo tofauti yaliyokuwa yakiwadhili wananchi.
Jambo la kwanza lililofanywa na uongozi huu mpya mara tu baada ya kuingia madarakani ni kuunda TAA Political Subcommittee (Kamati Ndogo ya Siasa ya TAA) iliyokuwana wajumbe hawa wafuatao: Sheikh Hassan bin Amir aliyekuwa Mufti wa Tanganyikana Zanzibar; Dr Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Said Chaurembo aliyekuwaLiwali wa Mahakama ya Kariakoo; John Rupia na Stephen Mhando.

Kazi ya kamati hii ilikuwa ni kushughulika na masuala yote ya siasa katika Tanganyika. Kuundwa kwake ndiyo hasa ulikuwa mwanzo wa siasa za dhahiri katika Tanganyika na mwanzo wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Kwa kipindi cha miaka ishirini namoja African Association ilifanya kazi chini ya katiba isiyokuwa ya siasa. Kwa mara ya kwanza mwaka 1950, TAA chini ya uongozi mpya, ilijipa hadhi ya chama cha siasa, siyo kwa kubadilisha katiba yake lakini kwa kuunda kamati ya siasa ndani ya chama.

Kamati hii ilikuwa na watu wenye kuwakilisha maslahi na uwezo tofauti, wakiwa halikadhalika wanatokana na uzoefu na hali tofauti. SheikhHassan bin Amir Muunguja alikuwa ndiye Mufti wa Tanganyika na aliwakilishaWaislam ambao hasa ndiyo waliokuwa wakiongoza mapambano dhidi ya serikali.

Nyuma ya Sheikh Hassan bin Amir walikuwa masheikh, makhalifa wa tarikambalimabali na Waislam wote kwa ujumla. Said Chaurembo aliwakilisha Wazaramo waDar es Salaam na vitongoji vyake.

JohnRupia kutoka Mission Quarter alikuwa mfanya biashara tajiri na mfadhili wachama. Stephen Mhando Mbondei kutoka Muheza, na aliyejulikana kwa misimamomikali aliwawakilisha wasomi wa Makerere. Alikuwapo Abdulwahid Sykes, mfadhiliwa chama ambae baba yake ndiye alikuwa katibu muasisi wa African Association.

Baadaya kuunda kamati hii, Abdulwahid akiwa kama katibu alianza kuyaandikia matawiya TAA nchi nzima kuyahuisha. Jambo kubwa lililokabili TAA ilikuwa ni hadhi yaTanganyika kama nchi ya udhamini chini ya Umoja wa Mataifa. TAA alimuingiza katika ile kamati ya siasa Earle Seaton, mwanasheria kutoka Bermuda aliyekuwa akikaa Moshi ili aishauri kamati kuhusu mambo ya sheria ya katiba ili iwezekukabiliana na serikali ya kikoloni.

Seaton alitakiwa kuishauri TAA jinsi yakuliendea shauri la kutaka Uingereza itoe uhuru Tanganyika ijitawale yenyewekwa kuwa nchi hiyo haikuwa koloni, bali nchi chini ya udhanini wa Umoja wa Mataifa. Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa tayari lilituma ujumbe wake wa kwanza kuzuru Tanganyika mwaka wa 1948 kuja kukagua hali ya siasa ya Waafrikakama wanaweza kukabidhiwa madaraka ya kuendesha nchi yao.

Lakini hakuna jambololote la manufaa lilipatikana kutoka kwa ujumbe huo. Lakini ilikuwa wazi kuwakuanzia mwaka 1950 Makao Makuu ya TAA mjini Dar es Salaam chini ya Dr Kyaruzina Abdulwahid ikiungwa mkono na kamati ya siasa sasa ilikuwa ikiamka kutoka kwenye usingizi mzito na ilikuwa imejiwekea lengo.
Uongozi wa chama cha TAA ulipata changamoto yake ya kwanza kupitia Constitutional Development Committee (Kamati ya Mapendekezo ya Katiba) iliyoundwa na Gavana Edward Francis Twining na mgogoro wa ardhi ya Wameru.

Gavana wa wakati ule Edward Twining alikaribisha mapendekezo kutoka kwa watu mashuhuri, vyama vya ustawi wa jamiina ''Native Authorities'' watoe mapendekezo vipi Tanganyika itawaliwe.

Kamati yasiasa ya TAA ilipeleka mapendekezo yake ambayo yalitiwa sahihi na wajumbe wotewa kamati ya siasa. Sheikh Hassan binAmir, Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando na Said Chaurembo.

TAA Ilitambua kuwa matatizo mengi kuhusu haki za Waafrikayalikuwa masuala ya kisheria ambayo yalihitaji ushauri wa wanasheria. Kwa mara ya kwanza kwa msaada wa Seaton, TAA kilitoa hoja zake zilozotiwa nguvu na ukweli hoja na kwa takwimu zilizoonyesha udhalimu ndani ya mfumo wa kikoloni ambao ulikuwa kinyume na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Memorandum ya TAA kwa Constitutional DevelopmentCommittee ambayo Pratt iliandikwa kwa utaalamu wa hali ya juu. TAA ilipendekez akuwa ndani ya Baraza la Kutunga Sheria Waafrika watashika nusu ya viti kwa miaka kumi na mbili na baada ya hapo wajumbe wachaguliwe kwa kupigiwa kura.
Gavana Twining iliyapuuza mapendekezo ya kamati ya TAA. Serikali iliendelea na mipango yake ya muda mrefu ya kuwaimarisha Wazungu na Waasia waliokuwa wachache na kuwasukuma kando Waafrika kinyume kabisa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi zilizokuwa chini ya udhamini.

Waafrika wengi walionelea kuwa mapendekezo ya TAAndiyo yangekuwa msingi wa katiba ya baadaye ya Tanganyika kama jamii ya watu wa rangi zote. Hata hivyo moyo wa mapendekezo yale ya TAA haukufa.

Mapendekezo yale yaliletwa tena katika mkutano wa kuanzishwa kwa TANU tarehe 7 Julai, 1954. Mapendekezo hayo ndiyo baadaye yalitiwa katika hotuba ya Julius Nyerere aliyoisoma mbele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, mwezi waMachi, 1955.

Baada ya mapendekezo ya TAA kukataliwa, uongozi wa TAA Makao Makuu ulielekeza nguvu zake zote katika kuimarisha matawi katika majimbo na kutafutamawasiliano zaidi na Umoja wa Mataifa la kutaka kutambulikana.
Juhudi hizi zilizaa matunda kwa sababu Umoja wa Mataifa ulianza kuiletea TAA taarifa na majarida kuhusu mambo mengi ya kamati zake tofauti. Kufuatia mwamko huu wa chama, serikali ilishtuka na ikaanza kuingia hofu, ikaamua kumpa uhamisho Dr Kyaruzi, rais wa TAA, kutoka Dar es Salaam kwenda Hospitali ya Gereza laKingolwira karibu na Morogoro.

Serikali ya kikoloni iliamini kwa kufanya hivyo itaweza kupunguza kasi ya TAA katika uwanja wa siasa. Serikali ilidhani kwa kumtoa Dr Kyaruzi Dar es Salaam, jambo hilo lingedhoofisha uongozi wa TAA pale makao makuu. Lakini Dr Kyaruzi hakuzuiliwa na huo uhamisho.

Kila mwisho wa juma alisafiri kuja Dar es Salaam kushauriana na Abdulwahid. Serikali ilipotambua kuwa uhamisho huo haukuathiri chochote katika mchango wa Dr Kyaruzi kwenye uongozi wa TAA, alihamishwa tena kutoka Kingolwira hadi Nzega mbali kabisa na Dar es Salaam.

Katika mkutanio mkuu wa TAA wa mwaka 1951 katibu wa TAA Abdulwahid aliwasilisha taarifa yake kwa mkutano mkuu. Abdulwahid aliwataarifu wanachama kuwa mwaka huo ulikuwa mgumu na wanachama walijulishwa kuwepo katikachama mwanasheria kutoka Bermuda, Earle Seaton kama mshauri wa TAA.
Wanachama walijulishwa mchango wake katika kutayarisha mapendekezo ya katiba yaliyowasilishwakwa Gavana Twining. Wanachama walijulishwa kuhusu kufufuliwa kwa matawi ya TAA, mawasiliano yake na Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa na uhusiano ulioanzishwa na TAA na wajumbe Waafrika katika Baraza la Kutunga Sheria.

Abdulwahid aliwaeleza wanachama juu ya ziara yake ya Nairobi aliyofanya mwezi Oktoba, 1950, na kukutana kwake na Balozi wa India katika Afrika ya Mashariki. Vilevile aliwaeleza kuhusu mshikamano ulioanzishwa kati ya TAA na KAU; na kutolewa nafasi za kusoma katika vyuo vikuu vya India na serikali ya nchi hiyo kwa Waafrika wa Tanganyika kwenda kusoma katika vyuo vikuu vya India. Abdulwahid alieleza kwa ufupi juu ya kuundwa kwa African Parents Association kwa msaada wa Dr Raymond na European Parents Association.
Katika safari yake ya Nairobi Abdulwahid alikutana kwa siri na Jomo Kenyatta nauongozi wa juu wa KAU lakini hili halikuweza kuwekwa bayana.

Mwaka wa 1950 utaingia katika historia ya Tanganyika kama wakati wasomi wa Makerere,waliingia TAA kwa wingi sana. Wote walikuwa vijana na walitaka kufanya mambomengi kwa haraka na kutimiza kila kitu mara moja. Migongano katika mawazo na mbinu za siasa hayakuwa mambo mageni.

Lakini migongano hii ndiyo hasa ilikuwakichocheo cha kuendesha utawala mzuri katika chama. Taarifa ya katibu ilieleza mafanikio na matatizo ya TAA. Ofisi ya TAA haikuwa na umeme na aliwaelezawanachama mipango ya kuingiza umeme, kufungua maktaba ndogo na kuanzisha masomo ya usiku kwa watu wazima.
Hatimaye taarifa ilizungumzia juu ya ukomunisti na uhusiano kati ya watu wa rangi mbalimbali. Taarifa ilitahadharisha dhidi ya taathira za ukomunisti katika siasa za Tanganyika na ilihimiza ushirikiano baina ya wanachama wa TAA na watu wa mataifa mengine.

Wakati huo baadhi ya viongozi wa TAA walikuwa wakifahamikakwa misimamo mikali. Miongoni mwao alikuwa Stephen Mhando na Hamza Mwapachu.Wakati huo Mwapachu alikuwa akiandika katika ''The Sentinel,'' jarida la Fabian Society lililokuwa likichapishwa London.

Hawa Fabian walikuwa wana mrengo wa kushoto katika Labour Party ya Uingereza. Wakati ule kulikuwa na machifu wengi katika Baraza la Kutunga Sheria na katika hao aliyekuwa mashuhuri sana wote alikuwa Chifu Kidaha Makwaia wa Shinyanga.

Chifu Kidaha ndiyo kwanza alikuwa amerudi kutoka Uingereza masomoni. Mara tu aliporudi alitoa hotuba kali katika Baraza la Kutunga Sheria, akiiasa serikaliya kikoloni ibadilishe msimamo wake wa kuwapiga marufuku wafanyakazi Waafrikas erikalini kushiriki katika siasa.

Machifu wengi wakati huo walikuwa na hofujuu ya TAA na uongozi wake uliokuwa ukiibuka kwa kasi. Waliiona TAA kama tishio kwa mamlaka yao.Serikali ya kikoloni katika utawala wake wa ''indirect rule'' ilikuwa inawatambua machifu na sio African Association kama wakilishi wa maslahi ya Waafrika.

Ilikuwakatika kipindi cha uongozi wa Abdulwahid ndipo alipomwendea Chifu KidahaMakwaia na kumuomba achukue uongozi wa chama kama rais. Abdulwahid alimwambia Chifu Kidaha kuwa endapo atachukua uongozi wa TAA, kwa kuchukua kwake uongoziwa Waafrika, angekua amefungua dimba la mageuzi Tanganyika kwa sababu machifu wengine wangemfuata.

Kidaha alikuwa chifu aliyependwa mno na serikali ya kikoloni, kwa ajili hiyo hakuweza kwa wakati ule kuona busara ya kukubali ombi hilo. Pamoja na kauli aliyotoa kuhusu watumishi Waafrika serikalini waruhusiwe kushiriki katika siasa, kauli ambayo huenda ndiyo iliyofanya uongozi wa TAA kumuomba achukuwe uongozi, Chifu Kidaha aliuamini uchifu na ushirikiano wakaribu na serikali ya Kiingereza kwa kupitia indirect rule.

Chifu Kidaha hakuwa tayari kuweka rehani nafsi yake na na maslahi ya watu wake kwa kukiunga mkono chama kilichokuwa kinapinga ukoloni. Hii ndiyo ilikuwa hali ya siasakatika Tanganyika wakati viongozi wa TAA walipokuwa wanajitayarisha kuunda TANU chama kilichokuja kuikomboa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza.

Nafyonza Ilm tu hapa.
 
Rudia kuisoma hotuba hiyo kwa umakini na kwa utulivu kijana,

ukikurupuka hivyo bila shaka utaibuka na dhana hiyo.

Tofautisha kipindi yupo Makerere na kipindi yupo Scotland, ukifanya hivyo utaielewa hiyo hotuba ndugu yangu.

Wewe ndiye unayetakiwa kuisoma hoja yangu na ukishindwa kuilewa omba msaada kwa wenzako wakueleze huyu jamaa ana maana gani? Reasoning yangu iko wazi kabisa. Haina chenga hata kidogo.
 
WC,warabu wanasema hivi " Ujinga usio na khasara ni bora sana Kuliko Ilmu isiyo na Faida".Unajuwa katika sehemu zilizofata na kutamalaki mila na desturi za Uislam ndizo sehemu zilizostaharabika sana hakuna mauaji ya vikongwe, watu kutembea na magovi, kukeketa, kuchuna ngozi na kunyofoa viungo vya albino na hata mateso kwa akina mama. Kwani Utamaduni wa kiislam unahimiza sana Utu na kuthamini hilo.
Ndio maana huwa nawashangaa sana watu kama ninyi mnaposema ni WAISLAM pekee walioachwa nyuma nchi hii! Hivi wanaofanya vitendo hivi wana ELIMU kweli? Tutafakari
 
Wewe ndiye unayetakiwa kuisoma hoja yangu na ukishindwa kuilewa omba msaada kwa wenzako wakueleze huyu jamaa ana maana gani? Reasoning yangu iko wazi kabisa. Haina chenga hata kidogo.

Mimi nimeielewa vema hotuba hiyo, sina hata chembe ya shaka, ndiomaana nimeiweka hapo ili iwe kielelezo kwa wasioelewa na waliopotoshwa na Mohamed Said.

Narudia kukusihi kuwa irudie tena kuisoma kwa umakini kisha tenganisha vipindi vya Mwalimu akiwa Makerere na akiwa Scotland
 
Sasa hapo mbona na ninyi mnapingana na Mohamed Said? Yeye anasema Nyerere alifahamiana na Abdul Sykes mwaka 1953 or thereabouts. Therefore alipokuwa Makerere hakufahamiana na Abdulwahid Sykes. Kipi msichoelewa hapo? Mwageni mboga lakini msimwage akili zenu.

Mimi sipo hapa kumuunga mkono mtu yeyote wala kumpinga mtu yeyote. Kama unataka kuchangia kuhusu hoja niliyoiweka karibu lakini usinihusishe na mtu yeyote.
 
Mimi nimeielewa vema hotuba hiyo, sina hata chembe ya shaka, ndiomaana nimeiweka hapo ili iwe kielelezo kwa wasioelewa na waliopotoshwa na Mohamed Said.

Narudia kukusihi kuwa irudie tena kuisoma kwa umakini kisha tenganisha vipindi vya Mwalimu akiwa Makerere na akiwa Scotland

Sina haja ya kuirudia. Nimeisoma nimeielewa na nikatoa hoja yangu baada ya kuisoma na kuilelewa. Kama unataka kuchangia kwenye hoja yangu basi unachotakiwa kufanya ni kuiwakilisha hoja yangu jamvini halafu uipinge hoja hiyo kwa hoja. Sasa unapotaka kupinga hoja ya mtu kisanii kwa kumwambia arudie tena kusoma haitakusaidia. Wewe chambua hoja yangu na elezea wapi nimekosea.
 
Back
Top Bottom