Hilo halipo huku bara tu. Ni tatizo katika jamii nyingi. Na ndio hasa sehemu ya huu mnakasha. Watu wanaacha kutafuta kiini cha tatizo, wanabaki kutafuta simple solutions. Mfumo wa kifisadi unamnyima kazi kijana wa kikristo/kiislam/asiye dini, badala ya watu kuangalia tatizo la ufisadi kwa ujumla wake, mwingine anaibuka anasema Yule kijana wa kiislam amenyimwa kwa sababu ya dini yake. Wakristo na waislam wa Lindi hawataki shule labda wanapendelea kuvua samaki zaidi, au wakristo na waislam na wapagan kwenye jamii za wafugaji wanakataa shule kwa kupenda zaidi ufugaji na uwindaji, halafu mtu anaibuka na kusema, waislam kwenye jamii hiyo wamebaguliwa na mfumo kristo… Nafikiri hata huko Oman uliko, kuna watu wana mentality hiyo, ikitokea uprising because of social discontent, kuna watu hawatawia kuilaumu Marekani, badala ya kuangalia kiini cha matatizo ya wananchi…
Mohamed Said mara kadhaa amesema Nyerere hakuasisi TANU! Tukipinga hili mnasema tunamtetea Nyerere kwasababu ni mkristo mwenzetu, na tuna chuki na uislam. Na kila anayepingana nanyi, mnafikiri ni mkristo tu
Na sisi hatukatai kuwa kulikuwa na waasisi wengine. Walikuwepo lakini Nyerere alikuwa ndio kinara. Au unataka kinara awe Abdul ambaye hakuwa na uongozi wowote ndani ya TANU kuanzia 1954???
Kama umemsoma Mohamed Said vizuri, na umetusoma na sisi vizuri bila jicho la udini, utaona kuwa hatupingi hadithi za nani alimpa Nyerere baiskeli, au nani alikuwa anampokea kikapu pale sokoni. Hata akidai kuwa Nyerere alikuwa anaenda sokoni bila pesa, kama ni ndio ukweli, sisi ni nani hata tupinge? Tunachopinga ni kufichwa baadhi ya facts ili kumdunisha mmoja na kumkweza mwingine. Tunapinga hisia zinazoingizwa kwenye masimulizi na kufanywa kama sehemu ya ukweli. Mathalan anaposema "the speech was farce, the TRUTH was muslims were no better than they were before independence" bila kueleza hiyo TRUTH ameipataje. Kuna bandiko analirudi rudia eti "The church declared islam as its enemy" wakati hiyo declaration is his own imagination. Anaposema watu walifungwa kwa uislam wao wakati actually walifungwa kwa kukaidi sheria za wakati huo (ikiwa ni pamoja na wasio waislam), huoni kuwa ni hisia tu ambazo zina lengo la kugawa wananchi? Mpaka amefikia hatua ya kutuma vijana na masheikh kuzunguka misikitini kuwaambia waislam wasichague Chadema ili wamchague muislam Kikwete? Hayo bwana
Barubaru ndio tunayoyapinga
Nimekusoma
Nilikuuliza lile suala la your treatment as Zanzibari arab by your Oman hosts. Je wanakuona ni mwarabu kama wao, au na wewe wanakuita mwarabu pori? (Najaribu kulinganisha na wanaoitwa wangazija pori kule Comoro)