Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Sina haja ya kuirudia. Nimeisoma nimeielewa na nikatoa hoja yangu baada ya kuisoma na kuilelewa. Kama unataka kuchangia kwenye hoja yangu basi unachotakiwa kufanya ni kuiwakilisha hoja yangu jamvini halafu uipinge hoja hiyo kwa hoja. Sasa unapotaka kupinga hoja ya mtu kisanii kwa kumwambia arudie tena kusoma haitakusaidia. Wewe chambua hoja yangu na elezea wapi nimekosea.

Mkuu hakuna hoja ya kuichambua wala kuifikirisha akili yangu.

Endelea kuitafsiri hivyo hii hotuba,
 
Mtu yeyote mwenye akili timamu akisoma hiyo hotuba ya Nyerere ataelewa kwamba huyu jamaa alikuwa mnafiki sana.

Haiingii akilini kumfahamu Abdul Sykes eti wakati amerudi kutoka Uingereza na baada ya kukaa pale Pugu kwa mda ndio aje Dar es Salaam kutaka kujua viongozi wa TAA ni kina nani. Alifahamishwa kuhusa TAA tangu yuko Makerere na akashauliwa kuacha kuanzisha chama kingine badala yake afungue tawi la TAA pale. Baada ya kurudi Makerere akachaguliwa kuwa Katibu wa TAA wa jimbo la Tabora. Aliwezaje kufungua tawi kule Makerere na baadaye kukubali kuwa Katibu wa TAA wa jimbo bila kumfahamu Abdul Skyes ambaye katika kipindi chote hicho alikuwa Katibu wa Chama?

Labda kama akili zake zilikuwa sio nzuri hivyo akakubali kuacha chama chake alichotaka kuanzisha na akajiunga na chama kingine bila kujua viongozi wa juu ni kina nani na nini malengo ya chama chao.

Zali la Mentali,

Wewe binadamu una fikra za hali ya juu sana hakuna mtu yeyote aliyegundua hicho kitu.

Wewe ni mtu muhimu sana kweye huu mnakasha karibu sana jamvini.

JF kuna vichwa bana siyo mchezo.
 
Last edited by a moderator:
Zali la Mentali,

Wewe binadamu una fikra za hali ya juu sana hakuna mtu yeyote aliyegundua hicho kitu.

Wewe ni mtu muhimu sana kweye huu mnakasha karibu sana jamvini.

JF kuna vichwa bana siyo mchezo.

Duuuuh ndugu wewe unaelekea kokote upepo unakovuma ilimradi hauathiri udini wako,

jisimamie ndugu yangu,
 
Nanren,

Moja ya tatizo nililolibaini huko Tanzania ni watu kujigeuza mbuni yaani kuficha kichwa chini yya majani wakti mwili wote upo nje akidhani kuwa haonekani.
Hilo halipo huku bara tu. Ni tatizo katika jamii nyingi. Na ndio hasa sehemu ya huu mnakasha. Watu wanaacha kutafuta kiini cha tatizo, wanabaki kutafuta simple solutions. Mfumo wa kifisadi unamnyima kazi kijana wa kikristo/kiislam/asiye dini, badala ya watu kuangalia tatizo la ufisadi kwa ujumla wake, mwingine anaibuka anasema Yule kijana wa kiislam amenyimwa kwa sababu ya dini yake. Wakristo na waislam wa Lindi hawataki shule labda wanapendelea kuvua samaki zaidi, au wakristo na waislam na wapagan kwenye jamii za wafugaji wanakataa shule kwa kupenda zaidi ufugaji na uwindaji, halafu mtu anaibuka na kusema, waislam kwenye jamii hiyo wamebaguliwa na mfumo kristo… Nafikiri hata huko Oman uliko, kuna watu wana mentality hiyo, ikitokea uprising because of social discontent, kuna watu hawatawia kuilaumu Marekani, badala ya kuangalia kiini cha matatizo ya wananchi…
Nanren,

Nimebainisha hapo Juu kuwa Kuna mazuri ya JKN na mabaya pia. Hakuna anayepinga kuwa JKN ni mmoja wa waasisi wa Tanu, Rais wa tanganyika na Tanzania pia.
Mohamed Said mara kadhaa amesema Nyerere hakuasisi TANU! Tukipinga hili mnasema tunamtetea Nyerere kwasababu ni mkristo mwenzetu, na tuna chuki na uislam. Na kila anayepingana nanyi, mnafikiri ni mkristo tu
Na sisi hatukatai kuwa kulikuwa na waasisi wengine. Walikuwepo lakini Nyerere alikuwa ndio kinara. Au unataka kinara awe Abdul ambaye hakuwa na uongozi wowote ndani ya TANU kuanzia 1954???
Sasa unapotolewa ushahidi kuthibitisha yeye ni mmoja wa waasisi na sio kinara katika uasisi tena kwa kupewa ushahidi madh'buti unakataa sijui unataka nini. Ikumbukwe kuwa Nyerere hakuwa na uenyeji Dar na hata tunapoambiwa nyumba alipofikia baada ya kuacha ualimu pugu alipewa kwa ufadhwili tu wa watu mnabisha.

nafikiri Nanren inabidi mfunguke hata kwa ushahidi wa mazingira tu. Nyerere hakuwa na pesa wala uenyeji wa Dar jiulizeni alikuwa anaishije ishije dar? hapo utaona kulikuwa na watu waliojitolea kumfadhwili. sasa anapotokea mtu kuachambua hao wafadhwili ambao wamesahaulika katika historia usipinge bali ingzeni katika historia yenu na sio kuficha kichwa mkidhani kuwa hamuonekani. Namshukuru Al Akhiy Mohamed Said kutujuza mengi ambayo tulikuwa hatuyajui pamoja na kuisoma historia ya nchi hiyo lakin hatufahamishwi na kufundishwa.
Kama umemsoma Mohamed Said vizuri, na umetusoma na sisi vizuri bila jicho la udini, utaona kuwa hatupingi hadithi za nani alimpa Nyerere baiskeli, au nani alikuwa anampokea kikapu pale sokoni. Hata akidai kuwa Nyerere alikuwa anaenda sokoni bila pesa, kama ni ndio ukweli, sisi ni nani hata tupinge? Tunachopinga ni kufichwa baadhi ya facts ili kumdunisha mmoja na kumkweza mwingine. Tunapinga hisia zinazoingizwa kwenye masimulizi na kufanywa kama sehemu ya ukweli. Mathalan anaposema “the speech was farce, the TRUTH was muslims were no better than they were before independence” bila kueleza hiyo TRUTH ameipataje. Kuna bandiko analirudi rudia eti “The church declared islam as its enemy” wakati hiyo declaration is his own imagination. Anaposema watu walifungwa kwa uislam wao wakati actually walifungwa kwa kukaidi sheria za wakati huo (ikiwa ni pamoja na wasio waislam), huoni kuwa ni hisia tu ambazo zina lengo la kugawa wananchi? Mpaka amefikia hatua ya kutuma vijana na masheikh kuzunguka misikitini kuwaambia waislam wasichague Chadema ili wamchague muislam Kikwete? Hayo bwana Barubaru ndio tunayoyapinga
Nafikiri nitakuwa nimekujibu lakin kama utahitaji ziada basi Bismillah
Nimekusoma
Nilikuuliza lile suala la your treatment as Zanzibari arab by your Oman hosts. Je wanakuona ni mwarabu kama wao, au na wewe wanakuita mwarabu pori? (Najaribu kulinganisha na wanaoitwa wangazija pori kule Comoro)
 
Last edited by a moderator:
Nafyonza Ilm tu hapa.

Spike,
Upo kama vile haupo.

Niko 1950 Abdu Sykes na Chief Kidaha.
Akimkubalia kuchukua uongozi wa TAA aunde TANU.

Tewa Said Tewa akikueleza Kidaha alivyokuwa utastarehe.
Alikuwa akisema, "Kidaha alikuwa hodari lakini aliogopa
kumuunga mkono Abdu na hapo ndipo yalipokuja majuto yake."

Taratibu nakwenda na ndugu zangu Insha Allah.
 
Duuuuh ndugu wewe unaelekea kokote upepo unakovuma ilimradi hauathiri udini wako,

jisimamie ndugu yangu,

Mie na wewe nani ajisimamie umeongea uongo mwingi sana kuhusu Al-Qaida kwenye ngano zako.

Nipe darsa mashambulizi ya septemba 11 yalifanywa na nani?
 
Nikusaidie kitu.Enzi za Nyerere professional hazikuwa zinazingatiwa bali mambo yote Chama kimeshika hatamu za uongozi. Kila pahala siasa inatawala.Lakin kumbuka nimekulia Tz na kuzunguka karibu nchi nzima wila zote za Tz Bara najua mengi. Kumbuka kuwa unaposema Mbeya mtu yoyote huko atakwambia wanatoka wanyakyusa lakin kumbuka kuna makabila mengi sana wakiwemo wapangwa, wasafwa na wengine.Unaposema Mara watu wote watakwambiia wanatoka wakurya, lakin kuna makabila mengi sana kule wakiwemo wang'oreme, waikizu, wazanani na wengine wengi tu.Kwa bahati najua sana utendaji na uwezo wa Nyirabu na hata warioba kwani kwa namna moja au nyingine niliwahi kufanya nao kazi hivyo ninachozungumza nalinganisha na uwezo wao kikazi na utendaji wao. wapo wengi lakin naona tuishie hapa kwani ni upendleo wa dhwahir.

Ni Wangoreme au Wangurimi (jina sahihi)
 
WC,

warabu wanasema hivi " Ujinga usio na khasara ni bora sana Kuliko Ilmu isiyo na Faida".

Unajuwa katika sehemu zilizofata na kutamalaki mila na desturi za Uislam ndizo sehemu zilizostaharabika sana hakuna mauaji ya vikongwe, watu kutembea na magovi, kukeketa, kuchuna ngozi na kunyofoa viungo vya albino na hata mateso kwa akina mama. Kwani Utamaduni wa kiislam unahimiza sana Utu na kuthamini hilo.
Barubaru
Egypt wanakeketa wanawake. Mara kadhaa, viongozi wa juu wa kiislam nchini humo wamekuwa wakisisitiza kuwa mwanamke wa kiislam ni lazima akeketwe. Hapa Tanzania (unapojisifia kuwa umetembea na kuzijua sehemu nyingi) warangi na Wamanyema ("Alhamdullilah I have never seen a christian Manyema"-by Moh Said) wote wana hiyo culture, na asilimia kubwa ya makabila hayo ni muslims. Kuhusu ustaarabu wa tamaduni za kiislam kuwa zinajali na kuthamini utu, na kuzuia mateso ya kina mama.... Ngoja tusiingie huko... Maana at times huwa nashindwa kujua ni wakati gani muislam huwa ni "muislam" na wakati gani anakuwa sio "muislam", kwa mfano ni wakati gani Sheikh Yahaya anahesabiwa kuwa ni muislam na wakati gani anakuwa sio...

Cha muhimu ujue kuwa mambo anayofanya anayejiita muislam katika maisha ya kawaida (mnayohusisha na ustaarabu) kama vile kutumia maji chooni, kutahiri, kusaidia wasiojiweza, huwa pia yanafanywa na watu ambao hawaujui huo uislam. Na ujambazi, ujangili, uzinzi, uasherati na kuuza madawa ya kulevya na kutumia pombe and other vices, vinafanywa na watu wa aina zote hata wale wanaohesabika kuwa ni waislam...
 
Last edited by a moderator:
Barubaru
Egypt wanakeketa wanawake. Mara kadhaa, viongozi wa juu wa kiislam nchini humo wamekuwa wakisisitiza kuwa mwanamke wa kiislam ni lazima akeketwe. Hapa Tanzania (unapojisifia kuwa umetembea na kuzijua sehemu nyingi) warangi na Wamanyema ("Alhamdullilah I have never seen a christian Manyema"-by Moh Said) wote wana hiyo culture, na asilimia kubwa ya makabila hayo ni muslims. Kuhusu ustaarabu wa tamaduni za kiislam kuwa zinajali na kuthamini utu, na kuzuia mateso ya kina mama.... Ngoja tusiingie huko... Maana at times huwa nashindwa kujua ni wakati gani muislam huwa ni "muislam" na wakati gani anakuwa sio "muislam", kwa mfano ni wakati gani Sheikh Yahaya anahesabiwa kuwa ni muislam na wakati gani anakuwa sio...

Cha muhimu ujue kuwa mambo anayofanya anayejiita muislam katika maisha ya kawaida (mnayohusisha na ustaarabu) kama vile kutumia maji chooni, kutahiri, kusaidia wasiojiweza, huwa pia yanafanywa na watu ambao hawaujui huo uislam. Na ujambazi, ujangili, uzinzi, uasherati na kuuza madawa ya kulevya na kutumia pombe and other vices, vinafanywa na watu wa aina zote hata wale wanaohesabika kuwa ni waislam...

nanrem,

JF siyo sehemu za porojo hebu tutajajie hao vingozi wa dini ya Kiislam ambayo walikuwa wanawataka wanawake wakeketwe.

Usichanganye mila za watu na dini ya Kiislam.

Kwa faida ya wanajamvi tuwekee hao viongozi wa Kiislam kama usipowaweka basi takuweka kwenye list ya udaku na umbeya wa JF utakuwa kapo moja na watu wa mipasho.

Tunasubiri hao viongozi kaka tuwasome.
 
Last edited by a moderator:
Asante kushukuru Wickama;

Kwa kweli nimesoma jinsi mambo ya Tanga yalivyo basi hadi nimesikia uchungu. Nimeishi Tanga maisha yangu ya utoto na ujana na kukulia miongoni mwa Waislamu. Nimesoma na Waislamu toka darasa la kwanza hadi sekondari. Sasa siyo kusoma tu hivi hivi lakini kuwa na urafiki wa karibu kiasi cha kwenda nao kwenye Maulidi ya Mtume, na utotoni hata kupiga nyimbo za daku - na unajua bana hakuna wanakofanya vizuri kama Tanga (sijui siku hizi). Ni Tanga ambako miye sikujua wapo Waislamu ambao walikuwa hawajaendelea; nimekua nikiwaona wanafanya biashara, wana maduka, wana mabasi (na hapa sizungumzii Waarabu tu - kina Mabrouk) la hasha nawazungumzia hawa weusi tii wenzetu. Tulipokuwa shule tukisoma pamoja niliwaona uwezo wao darasani; mtu mmoja darasani alikuwa best wangu na tulikuwa tukishandana sana aliitwa Saleh Khalfan (alikuwa ni mswalihina hadi mtu unaona wivu); baba yake Mzee Khalfan akiishi pale Majani Mapana karibu na duka la Chako ni Chako. Binti aliyekuwa anatutesa wote, mpole kwelikweli - Mwanahawa Salim alikuwa ni Binti wa Kiislamu; mwingine ambaye alikuwa anatuzingua darasa aliitwa Mpaji Juma akiishi pale kijijini cha Mwamboni (sijui kama bado kipo). Dada zangu wamesoma ile shule ya Jumuiya (pale karibu na stendi). Mwenyewe nikaenda kusoma Pangani. Kote huku - nisamehe kwa kutembelea kumbukumbu za zamani - niliishi nikiamini kabisa kuwa sisi sote tulikuwa tunashindana vizuri darasani na wenye kipaji walikuwa na kipaji - sikufikiria kabisa suala hili la dini. Na kweli niliwaona vijana wa Kiislamu wakipasua darasani vizuri tu na wengi wameenda mbali leo hii. Na niliwaona watoto wa Kikristu wakiharibu darasani na leo maisha yao yako duni vile vile.

Na hili ni kweli siyo hapo Tanga tu; nimebahatika nami kupita sehemu kubwa ya nchi yetu. Ni mikoa mitano tu ambayo sikujaliwa kufika kabisa; Mtwara, Lindi, Rukwa (Katavi), Kigoma na Pemba. Sehemu nyingine zote nimefika; nimefika Mwera, Boza, Muheza, Maramba, Dunga, Ileje, Ndala, Unguja, Kisarawe n.k ni sehemu nyingi. Nimekuja kuelewa kitu kimoja ambacho Mohammed Said na wengine wenye kuamini histohia hii hawajajaribu basi kuangalia - maendeleo Tanzania yameenda kimaeneo zaidi (geographical). Kwamba kuna maeneo ambayo yamefanikiwa sana kutokana na historia yake bila kujali makabila yaliyomo ndani yake. Leo hii huwezi kushangaa kuwakuta Wahaya Waislamu waliosoma sana; huwezi kushangaa kukuta Wachagga Waislamu ambao ni wasomi vile vile n.k

Lakini cha kushangaza sana; utaona kuwa wanaodai kuwa Waislamu wamedhulumiwa hawawezi kuelezea mafanikio ya Waarabu Waislamu, au Wahindi Waislamu, au hata Wahindu wa Tanzania. Mfumo Kristu ambao unapendelea Wakristu unaweza vipi kuachilia Waislamu wa makundi mengine wakafanikiwa? Wanatolea mfano hapa wa kuvunjwa kwa EAMWS kama mfano mmoja wa jinsi Uislamu ulivyopigwa vita; lakini hawahawa hawawi wa kweli kusema kuwa Aga Khan (muasisi na mfadhili mkuu wa EAMWS) aliendelea kuwekeza Tanzania na mahusiano yake na utawala wa Nyerere hayakuingia mawaa hata chembe.

Kwangu mimi kurahisisha tu kudai kuwa haya yote ni kwa sababu Waislamu/Uislamu unapigwa vita.

Mwanakijiji nashukuru kwa mawazo yako mapana. Huu ni mwaka wangu wa 20 hapa tanga mjini. Believe me, familia za kiarabu ni among zinazosomesha wasichana kwa kiwango kidogo sana. Wengi wakibahatika kumaliza darasa la saba ni kwamba mchezo umekwisha. Wavulana wa kiarabu wanaohimizwa kuendelea na sekondari nikilinganisha na mali wanazomiliki kama jamii ni kidogo pia. Wengi wao ni wapenzi wa biashara. Vijana wa kiarabu niliosoma nao SUA hadi leo nawajua na huwa wakija Tanga tunatafutana. Mji huu kwa kitambo umeiga sana desturi za wenzetu hawa. Na athari yake imezama sana hadi kwa jamii iliyo karibu sana nao. Sijawahi kuelewa kutosomesha kwao watoto kwa bidii kama pale Machame ni kwanini. Labda wanaogopa NECTA. Nitaiachia hapo. Huu ni mwaka wa 12 nafanya agricultural research (soils) kwenye Western Usambara mountains (Lushoto), been every piece of these mountains. Lakini, itakushangaza Mwanakijiji, kuwa hata ile familia unayoiona ni maskini bado ina-struggle sana watoto wasome. Naomba anitoe dosari yeyote katika hili jamvi kama sio kweli kwamba jamii ya kisambaa ambayo ilikuwa inabezwa sana huko awali, leo ni the most advanced mkoa huu. Hii haikuja kwa kulaumu wadigo, au wabondei, au wapare. The guys worked and toiled for that position. Wapo waliosema sana humu JF kuwa watumishi wa serikali ni wenye aibu na soni katika kuutetea uislamu na kuufatilia. Inategemea mtu umekutana na kina nani. Hivi kwenye laptop yako unasubiri kijana wa kikiristo akuwekee Qasida? Mbona yeye kaweka gospel music? nani kamzuia mwislamu kuwa na mahubiri kwenye laptop yake au hata kuwa na flash disc akatembea nayo. Unyonge haujui elimu. Internet ndio hii inatuleta pamoja lakini wapo wanaoitumia kuangalia madudu. Ni menu.

Somewhere niliona maneno ya kutoshukuru jinsi ile university complex ya Morogoro kwa waislamu ilivyopatikana. Imeniuma kwa vile nakumbuka the amount sleepless nights and toil ambayo many people including mwalimu wangu wa Agricultural Engineering pale SUA (Prof Salim, wa kondoa huyu bwana) waliipata kuandika convincing arguments za kuiomba. Prof Salim broke into tears in the presence of Mzee Kitwana Kondo siku Mkapa aliwakubalia. Lakini hapa JF all that is seemingly little. Mmoja wa watu waliokuwa na Mh.Mkapa kwa karibu sana (a muslim, school mate of mine, no name ) accompanied Mkapa to Tripoli Libya. He never knew what was cooking. But the Product of that tour ni Masjid Gaddafi ya Dodoma (almost exact replica of that very imposing Kampala Mosque also built by same Gaddafi). Kwa culture ya haa JF hiyo ni "nothing" Ukiuliza walio-serve under Mkapa (the inner group staff), the guy used to fast ramadhani na his muslim staff. A catholic.

Huwa najiuliza sana Mwanakijiji; Hivi leo Kikwete akienda kuomba ufadhili wa ujenzi wa a better Cathedral kupita ile ya pale forodhani front kwa ajili ya Dodoma, assuming akapewa. Hawa wanaopiga kelele na kuchonganisha watu kwa uislamu na ukiristo watamwacha kweli? Hutasikia wakikubali ahudhurie baraza la maulid tena. Wakae na Kafiri???? That is the sad side of this community.

Namshukuru sana Mungu kuwa kazi nayofanya ina contact na ground zero. Najua ground zero wanataka kujengewa matumaini kuwa "come on guys you can make it, just work and plan hard". Lakini ukiisikiliza sana jumuiya ya KEYBOARD utasahau wajibu wako to ground zero. Ili ku-illustrate kuwa hawa jamaa akili zao ni ndogo sana huwa huwajui baba na mama yako wanaweza kuwa ni wakiristo huku wewe ni mwislamu. Kwa wao landscape yote ni miti hawajui kuna majani chini.
 
Hilo halipo huku bara tu. Ni tatizo katika jamii nyingi. Na ndio hasa sehemu ya huu mnakasha. Watu wanaacha kutafuta kiini cha tatizo, wanabaki kutafuta simple solutions. Mfumo wa kifisadi unamnyima kazi kijana wa kikristo/kiislam/asiye dini, badala ya watu kuangalia tatizo la ufisadi kwa ujumla wake, mwingine anaibuka anasema Yule kijana wa kiislam amenyimwa kwa sababu ya dini yake. Wakristo na waislam wa Lindi hawataki shule labda wanapendelea kuvua samaki zaidi, au wakristo na waislam na wapagan kwenye jamii za wafugaji wanakataa shule kwa kupenda zaidi ufugaji na uwindaji, halafu mtu anaibuka na kusema, waislam kwenye jamii hiyo wamebaguliwa na mfumo kristo… Nafikiri hata huko Oman uliko, kuna watu wana mentality hiyo, ikitokea uprising because of social discontent, kuna watu hawatawia kuilaumu Marekani, badala ya kuangalia kiini cha matatizo ya wananchi…

Mohamed Said mara kadhaa amesema Nyerere hakuasisi TANU! Tukipinga hili mnasema tunamtetea Nyerere kwasababu ni mkristo mwenzetu, na tuna chuki na uislam. Na kila anayepingana nanyi, mnafikiri ni mkristo tu
Na sisi hatukatai kuwa kulikuwa na waasisi wengine. Walikuwepo lakini Nyerere alikuwa ndio kinara. Au unataka kinara awe Abdul ambaye hakuwa na uongozi wowote ndani ya TANU kuanzia 1954???

Kama umemsoma Mohamed Said vizuri, na umetusoma na sisi vizuri bila jicho la udini, utaona kuwa hatupingi hadithi za nani alimpa Nyerere baiskeli, au nani alikuwa anampokea kikapu pale sokoni. Hata akidai kuwa Nyerere alikuwa anaenda sokoni bila pesa, kama ni ndio ukweli, sisi ni nani hata tupinge? Tunachopinga ni kufichwa baadhi ya facts ili kumdunisha mmoja na kumkweza mwingine. Tunapinga hisia zinazoingizwa kwenye masimulizi na kufanywa kama sehemu ya ukweli. Mathalan anaposema "the speech was farce, the TRUTH was muslims were no better than they were before independence" bila kueleza hiyo TRUTH ameipataje. Kuna bandiko analirudi rudia eti "The church declared islam as its enemy" wakati hiyo declaration is his own imagination. Anaposema watu walifungwa kwa uislam wao wakati actually walifungwa kwa kukaidi sheria za wakati huo (ikiwa ni pamoja na wasio waislam), huoni kuwa ni hisia tu ambazo zina lengo la kugawa wananchi? Mpaka amefikia hatua ya kutuma vijana na masheikh kuzunguka misikitini kuwaambia waislam wasichague Chadema ili wamchague muislam Kikwete? Hayo bwana Barubaru ndio tunayoyapinga

Nimekusoma
Nilikuuliza lile suala la your treatment as Zanzibari arab by your Oman hosts. Je wanakuona ni mwarabu kama wao, au na wewe wanakuita mwarabu pori? (Najaribu kulinganisha na wanaoitwa wangazija pori kule Comoro)

Nanren,
Umesema mengi lakini mie nimevutiwa na mawili tu na hayo ndiyo nitakayoeleza hapa.

La kwanza Kanisa Katoliki na Uadui na Uislam:

Angalia kitabu ''Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985'' cha Dr. John C. Sivalon.

Sivalon anasema maneno haya ''...Utume wa Kanisa wa Jamii Kitaifa walijaribu kutumia Utume huo
kama mkakati wa kupambana na yaliyodhaniwa kuwa maadui wa Kanisa: Ukomunisti na Uislam.''
(Benedictine Publication Ndanda - Peramiho, 1992 uk. wa 37).

La Pili mimi katika kitabu changu niliita hotuba ya Nyerere ''farce'' yaani puruzai.
Nakuwekea hapa Prof. Njozi na yeye anasema nini kuhusu hotuba ile ya Nyerere kuweka haki
baina ya Waislam na Wakristo wakati wa utawala wake:

The Limits of "Suffering without Bitterness"
[SIZE=+0]In his moving farewell speech at the Diamond Jubilee Hall on 4th November, 1985 Mwalimu Nyerere made two statements, of great moment, about Muslims in Tanzania. In a way, those statements encapsulate and crystallise both Tanzania's looming political tragedy and the fading hopes of averting it. In the first part Nyerere paid glowing tribute to Muslims for their political maturity and patience, qualities which greatly contributed to the country's enduring peace. He acknowledged the existence of enormous religious disparities against Muslims in education and employment when the country became independent. And that the inferior status of Muslims was so conspicuous that it could have easily been used to divide the nation. He said that attempts were indeed made to use those imbalances to disrupt the unity and solidarity of Tanzanians, but Muslims spurned them. In the second part Mwalimu Nyerere expressed his satisfaction that as he was stepping down from government leadership Tanzania had already successfully rectified whatever imbalances that existed between Christians and Muslims in education and employment.[/SIZE]

[SIZE=+0]Nyerere's second statement has baffled me, and I hope many other Tanzanians since. And like many Tanzanians also, I have too much respect for Mwalimu to accuse him of lying. But how could he commit such a grave factual error in his public farewell speech? There are several logical possibilities. The first one is that he sincerely believed religious imbalances had been redressed. It is a possibility which is difficult to accept. Throughout his political career Nyerere kept himself very well informed about local and international affairs. The position of Muslims in Tanzania is a subject which even the dullest students could hazard a correct answer, how could their teacher, and one who ruled the country for twenty five years, have got it so wrong? The other possibility is that Nyerere like everyone else knew that those imbalances had not been corrected and that in some cases like political appointments the Muslims were even worse off in 1985 than they were in the early sixties. Nyerere had promised Muslims in 1959 that their lowly position could only be set right after independence. After ruling the country for a quarter of a century and after acknowledging the enduring patience of Muslims throughout that long period, Nyerere found it difficult to admit his failure in that regard. But again that is very uncharacteristic of Mwalimu.

Way back in 1962 Nyerere wrote Tujisahihishe. The onus of his narration in that small booklet was to underline the need for acknowledging and correcting our mistakes. And in his leadership Nyerere displayed admirable courage in admitting mistakes and even failures without equivocation. The Arusha Declaration: Ten Years After is but one example. But why was Nyerere suddenly unable or unwilling to admit failure in religious imbalances?[/SIZE]
[SIZE=+0]We may never know why Mwalimu made that puzzling statement but many Muslims have been forced to suspect a trace of religious prejudice against them. One can understand why in his book, Said (1998) has described that speech as a "farce". Muslims argue that Nyerere could not have possibly been ignorant of their situation. Nor could he have been embarrassed by his failure to keep his promise. For if that were the case he could have easily ignored that subject altogether as he had done throughout his rule as president. He was under no pressure to raise it. Nyerere not only raised the matter but also attempted to close the Muslim file by misrepresenting it. It was mentioned in chapter one how Nyerere, a Catholic, had vowed to do everything in his power to strengthen Catholicism in Tanzania. Was Nyerere afraid that the new president, a Muslim, would also misuse his power to strengthen Islam in the country? In any case, Nyerere had failed to fulfil his promise.

Why was he now deliberately discouraging future leaders from addressing that problem? Did he believe Muslims would perpetually continue with their suffering without any bitterness? A year before Nyerere made that statement Mazrui and Tidy (1984:377-378) noted in their book, Nationalism and New States in Africa that the political leverage of Muslims in Tanzania was well below commensurate levels and that ‘Most observers do not even realise that there are more Muslims than Christians in Tanzania'. They also wrote, (and in retrospect quite prophetically) that while Tanzania had fared better in terms of religious harmony, ‘but the risk that Muslims might become increasingly discontented as they witness a disproportionate share of privilege enjoyed by Christians continue to hang over Tanzania, especially in the years which would follow the departure of Mwalimu Julius Nyerere'.[/SIZE]


Nanren,
Ningeweza kuweka hapa mifano lukuki lakini kwa muda huu hiyo hapo juu inatosha.

Nahitimisha kwa kusema kuwa Jasusi alipata kunipinga kuhusu Kanisa Katoliki kuutangaza Uislam
kama adui na akataka ushahidi kutoka kwa Sivalon.

Nilimpatia ushahidi na hadi leo amekaa kimya.
Lakini mie hilo halikunishtua.

Nimelazimika kumleta Jasusi jamvini ili kauli yangu ithibitike kuwa mimi siwezi kuzua uongo si kama
nimemleta kwa ajili ya kusutana.

Kaka yangu Jasusi naamini atanielewa.
Jasusi akimjua vizuri sana Bwana Abdu Sykes akenda hadi nyumbani kwake.
 
Nilipo Blue.

Al akhiy Gombesugu umegusa saaaaaana saaana kama nawaona hawa baadhwi ya masheikh uliowataja. naona umesaha vitongoji vngine Muhimu kama Ndumi na darini kisiwani kwani huko ndio chimbuko na bahri kubwa ya ilmu kwa wengi.

Mimi nashauri tuweke uzi maalum tuichambue TANGA ilivyokuwa kabla ya uhuru na baada ya uhuru kwanini Tanga imedidimia kiuchumi wakti kila kitu wanacho kuanzia bandari na hali ya hewa safi kuona dhulma walizofanyiwa.Upande wangu nitachambua sana kiuchumi kwani nina data nyingi sana za huko na wapi waliwakona na kuwadhulumu.

Nimefurahi sana uchambuzi wako na Allah akubariki sana.

maa salaam
Itapendeza sana kama mtajadiri mambo hayo "objectively"bila kutafuta visingizio vya mfumo kristo!
 
Wanajamvi leo tumeingia page # 649,Mzee wetu Mohamed Said anaelekea kukubali makosa ya kitabu chake namwona hatu lugha anayoitumia si ile ya mwanzo ana weka tahadhari kubwa kabla hajachangia hoja si kama kule mwanzo.

Napenda kuwapongeza Mag3 Nguruvi3 Mzee Mwanakijiji Jasusi platozoom WildCard Wickama .......Kazi mliyoifanya si haba Mzee wetu Moh kajivunza mambo mengi hakujua Nyerere alishaingia Dar kabla ya mwaka 1950.Hakuwa anajua Nyerere alikuwa kiongozi wa AA mwaka 1945 huko Tabora.Hakupenda wasomaji wake wafahamu Rais wa kwanza wa AA alikuwa Cecil Matola angetokea Gerezani angeandika page 10 kumwelezea uhodari wake,usomi wake ......Mzee wetu kwa maksudi alitaka kutudanganya kwamba Abdul Sykes ndiye aliyemtambulisha Nyerere katika siasa za Dar hakujua Nyerere alionana na Dossa Aziz mwaka 1945 bila shaka Abdul Sykes wakati huo hakuwa na ushawishi wowote na kama alikuwa nao basi ulikuwa hauvuki Gerezani.

Nasema tena nawashukuru sana kazi mliyoifanya ni kubwa na mnastahili nishani ya uraia wema uliotukuka.Uchambuzi na hoja mbali mbali hakika ni funzo kubwa kwa anayetaka kujifunza.

Ngongo; You are welcome and thanks for your good words
 
Last edited by a moderator:
Mzee MS, nina hoja ndogo. Nijuze specifically why you went and what you did kule Iran. Na kwa asseessment yako uli-achieve nini na ni kwanini unadhani ni muhimu kwa watu kama wewe kwenda kule Please.
 
Naona sasa unataka kulazimisha Bao.

Pole sana

Barubaru,
Katika ibra za Allah ni mambo kama haya ya Abdu Sykes na Nyerere na urafiki wao.

TANU chama alichokiasisi Abdu kikaja kuwa mbele kumkana muasisi wake.
Leo zaidi ya miaka 60 tuko hapa tunabishana na wakati mwingine kutukanana.
 
Ntachangia hoja zangu kwenye huu mchango wa Kanisa kwenye kudai Uhuru paragraph kwa paragraph ili niweze kupata majibu ya uhakika kwenye kila dhana badala ya kudadisi dhana zote kwa wakati mmoja. Naanza na dhana hii hapa

Nitaelezea kwa ufupi jinsi kanisa la Tanganyika lilivyoshiriki harakati za ukombozi wa Tanganyika na madhila liliyokumbana nayo.



Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini. Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.

Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kassi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.

Kwa maelezo haya ina maana kwamba Askofu na mapadre walikutana na Mashekhe ili waone jinsi gani wataingia rasmi kwenye harakati za kudai uhuru. Kwa maana hiyo mpaka mwaka 1948 Kanisa lilikuwa halijaingia rasmi kwenye harakati za kudai uhuru kwa muundo wa chama wakati Masheikh waliingia rasmi katika muundo wa chama tangu 1929 wakati African Association (AA) kilipoanzishwa. Kwa nini Maaskofu na Mapadre walikuwa waoga kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kudai uhuru wakati wenzao Masheikh waliingia mapema?

Lakini cha ajabu hapa ni kwamba Askofu Maranda alipokwenda kukutana na Sheikh Issa, alishauriwa watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi wajiunge navyo kama wao wanapigwa marufuku. Askofu akajenga hofu kama ndani ya vyama hivyo kuna wasomi. Sasa suali la kujiuliza hapa ni kwamba wasomi walikuwa wapi wakati huo kama hawakuwapo kwenye vyama vya harakati? Kama Askofu alijenga hofu kwamba ndani ya vyama vya harakati hakuna wasomi, kwa nini alimfuata Sheikh Issa? Kwa nini asiende kwa wasomi na kupanga nao mikakati badala yake amfuate Sheikh Issa?
 
Nilipo Blue.

Al akhiy Gombesugu umegusa saaaaaana saaana kama nawaona hawa baadhwi ya masheikh uliowataja. naona umesaha vitongoji vngine Muhimu kama Ndumi na darini kisiwani kwani huko ndio chimbuko na bahri kubwa ya ilmu kwa wengi.

Mimi nashauri tuweke uzi maalum tuichambue TANGA ilivyokuwa kabla ya uhuru na baada ya uhuru kwanini Tanga imedidimia kiuchumi wakti kila kitu wanacho kuanzia bandari na hali ya hewa safi kuona dhulma walizofanyiwa.Upande wangu nitachambua sana kiuchumi kwani nina data nyingi sana za huko na wapi waliwakona na kuwadhulumu.

Nimefurahi sana uchambuzi wako na Allah akubariki sana.

maa salaam

Barubaru,

Ahsanta,Jazaak Allahu Kheir Al Akhiy. Ameen kwetu soote. Nafurahika kwa bayana zako hapa jamvini.

Ile habari ya nduguyo Bwana Julius Rweikiza imenitia simanzi ya dhati. Insha Allah Mola takulipa kwa fadhila zako na kukuongezeni mapenzi na mahusiano mlonayo baina yako na wale watoto wa marehemu.

Inshallah,siku ikapatikana fursa ya kufunguliwa ile thread ya Tanga basi uwaalike na ndugu zetu Nguruvi3,Mwanakijiji na Wickama.

Wale watu wenye zogo woote nishawatia kwenye ile "shit list" ya Sheikh Mohammed Said na nitahakikisha hatuwaaliki!ahahaha!!

Kwaheri Al Akhiy,Wallahi hii barza ina vituko na vichekesho viso mfano.

Ahsanta.
 
Mzee MS, nina hoja ndogo. Nijuze specifically why you went and what you did kule Iran. Na kwa asseessment yako uli-achieve nini na ni kwanini unadhani ni muhimu kwa watu kama wewe kwenda kule Please.

Wickama,
Nilialikwa katika hawli ya Imam Khomeni.

Sikuwa peke yangu palikuwa na ujumbe kutoka vyombo
vya habari vya serikali na binafsi vya Tanzania.

Tulihudhuria kongamano la Fikra za Khomeni.

Nilifanyiwa mahojiano ya TV na radio.

Ama kuhusu umuhimu ni kuwa kusafiri peke yake ni elimu na hapo
ndipo ulipo umuhimu wa watu kutembeleana.

Na nilikwenda kwa kuwa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran ndiyo
iliyonipa mwaliko.

Na ni uungwana ukialikwa kuitika.
 
Back
Top Bottom