Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ndugu yangu naona jinsi gani nilivyo zimwi katika ndoto zako. Hakuna unachoandika bila kuhakikisha unatumbukiza Nguruvi3.
Mimi ahdi tyangu ni moja, kutomuonea mtu au kumuonea haya. Natumbukiza kisu hadi kigonge mfupa sheikh, ushanfahamu.

Hivi nikikuambia familia yangu ni ya Mndolwa hiyo inasaidia nini katika mnakasha. Tanga nyumbani kwetu. Tena waijua mjni, mimi kuanzia Magoroto, kicheba, mtindiro, mjasani, pongwe, Lusanga, magunga, Mnyuzi, Tengeni tena hapo daah hata usiseme, bonde Muheza nyumbani usinitoe machozi kijana wee! Unaijua barabara ya 10!

Hebu tuendelee na mnakasha maana tutasema mengine na wengine kupatwa na fadhaa kama si soni.

Nguruvi3,

Nikikusoma nafurahika mno kwa vitisho na umahiri wako. Unanikumbusha watu kama Nikita Khrushchev na Slobodan Moilosevic!ahaha!!

Hayo mambo ya kiTanga na Biography ni wewe ndie uliemuanzishia Sheikh Mohammed Said,nami ikanilazim nikunyoshee maneno.

Mbona nami family yangu ni wakulima wa asili kabla hata Wajarumani hawajakua na fikra za kutia maguu yao hapo Tanganyika, na tuna mashamba mpaka kesho yenye hekari nyingi tu kuanzia Daluni, Bwete,Mwele,Magoma,Maramba,Saadani,Ushongo na Mazinde. Bahati mbaya mimi binafsi ni mvivu ndo maana nimekimbilia kujificha huku nchi za watu kwa miaka tarkiban ishirini sasa,Allahmdulillahi.

Hiyo Barabara ya 10 unayoitaja,hapo kale ilikua ni mojawapo ya viunga vyetu vya minazi. Na leo hii tuna nyumba zetu pale mtaani peke yake sita. Nakupa challenge nenda kagonge mlango pale jirani na Msikiti mkubwa wa Al Jumaa, kwa Al Marhum Shariff Nuru(dada yao ni Aunt Mwananuru Shariff aliwahi kuwa Principal Secretary nafikiri Wizara ya Afya hapo enzi ya Rais Mwinyi),wale ni jamaa zetu wa karibu na watakufahamisha uzuri mimi ni nani. Au nenda kamuone Mayor wako pale Tanga akufungulie Archives/shajara na uwasome Wazee wetu kwa utuvu tangia enzi ya Mwarabu na Mjarumani.

Ukishindwa huko koote nenda pale Barabara ya 9,uliza kwa Kina Diwani,nao pia ni jamaa zetu nao watakufahamisha kwa uzuri.

Au muone Salum Shamte wa Mkonge,ambae ni hakika unamfahamu,yule ameoa kwetu kwa hiyo atakupa habri japo kiduchu.

Sasa wewe hiyo Barabara ya 10,nyumba yako/yenu ni ipi,jamaa zako ni nani,au wale kina Khara Wahindi walohamia Canada!?

Mindhal, unasema machozi yanakukurubia tuyaache na tuendelee na mnakasha Insha Allah.

Nakupenda saana Mzee wangu Nguruvi3,na kwa sasa najua wewe ni Uncle wangu from ma Mum's side hapa jamvini,basi nami naringa saana sasa!ahaha!!

Ahsanta.
 
Nanren,
Huyo mwandishi ame generalize ni sawa na kusema Tanzania wanakata viungo vya albino wakti mambo hayo anafanyika sehemu zisizo na ustaharabu na utamaduni wa kiislam.
Barubaru,
Nanren,
Unajuwa katika sehemu zilizofata na kutamalaki mila na desturi za Uislam ndizo sehemu zilizostaharabika sana hakuna mauaji ya vikongwe, watu kutembea na magovi, kukeketa, kuchuna ngozi na kunyofoa viungo vya albino na hata mateso kwa akina mama. Kwani Utamaduni wa kiislam unahimiza sana Utu na kuthamini hilo. "

Je mambo hayo sehemu wanazokaa au zilizotamalaki uislam kama Mtwara, lindi, Pwani, Tanga, Znz na kwingineko yapo? Jiulize kwanini.


With all due respect,
embu soma hizo statements zako.. kuna ustarabu na utamaduni wa kiislamu tanzania???

 
Mundungus, Ritz and Kadogoo; Labda nichangie. Kama mmesoma baadhi ya magazeti hasa ya kutoka Marekani, nia ya Marekani kuleta Jeshi la kusaidia kumsaka Kony kule Uganda, ni actually kutumia DRONES kummaliza huyu bwana. Ila by Extension, wakishaweka msingi Uganda na operations kama hizo, uwe na uhakika kwamba kama wana mtu wanamsaka kwa udi na uvumba na wakaambiwa yuko Maswa, ni kwamba mchezo umekwisha. Watamulika hilo anga na wakati mwingine kuua watu wanaodhani ni wewe. Pakistani analia sana na drones lakini huku ni mpokeaji mkubwa wa misaada ya kijeshi toka marekani. Siasa zinajua maslahi tuu
Wickama,

..kama lijitu lina zali zake na Wamarekani na linatafutwa basi tusikubali kulipa hifadhi.

..zaidi, hawa jamaa wakianza kumtafuta mtu basi uwezekano mkubwa kuna kitu amekifanya, or he is about kukifanya.
 
Last edited by a moderator:
Nanren,

Mimi naona tumalize moja twende jingine. Hilo la Misri kama utaliundia mada yake nitakusaidia sana kwani naijua vilivyo Misri na nimekaa hapo kwa takriban miaka 4. hivyo nawajua ndani nje nje ndani na makabila yao.Huyo mwandishi ame generalize ni sawa na kusema Tanzania wanakata viungo vya albino wakti mambo hayo anafanyika sehemu zisizo na ustaharabu na utamaduni wa kiislam.

Lakin hapo hoja ilikuwa tunaizungumzia Tanzania na mimi nimebainisha hivi " warabu wanasema hivi " Ujinga usio na khasara ni bora sana Kuliko Ilmu isiyo na Faida".

Unajuwa katika sehemu zilizofata na kutamalaki mila na desturi za Uislam ndizo sehemu zilizostaharabika sana hakuna mauaji ya vikongwe, watu kutembea na magovi, kukeketa, kuchuna ngozi na kunyofoa viungo vya albino na hata mateso kwa akina mama. Kwani Utamaduni wa kiislam unahimiza sana Utu na kuthamini hilo. "

Je mambo hayo sehemu wanazokaa au zilizotamalaki uislam kama Mtwara, lindi, Pwani, Tanga, Znz na kwingineko yapo? Jiulize kwanini.

Ngoja nikubaliane na hoja yako kwa kuipanua zaidi.

Sehemu ambazo zimetamalaki uislam, watu wote ni wastaarabu, hamna crime, na hamna hata jela. Watu wote huko huwa wanaishi vizuri. Hakuna mauaji, ulevi wa madawa/pombe, uzinzi, ulawiti, kuoneana, domestic violence, FGM, hayo yote hayapo... Ila yatakuwepo tu sehemu ambazo hazina waislam. Hapa nimekubaliana nawe. Ngoja tuendelee na thread ya Yericko..
 
Barubaru
Egypt wanakeketa wanawake. Mara kadhaa, viongozi wa juu wa kiislam nchini humo wamekuwa wakisisitiza kuwa mwanamke wa kiislam ni lazima akeketwe. Hapa Tanzania (unapojisifia kuwa umetembea na kuzijua sehemu nyingi) warangi na Wamanyema ("Alhamdullilah I have never seen a christian Manyema"-by Moh Said) wote wana hiyo culture, na asilimia kubwa ya makabila hayo ni muslims. Kuhusu ustaarabu wa tamaduni za kiislam kuwa zinajali na kuthamini utu, na kuzuia mateso ya kina mama.... Ngoja tusiingie huko... Maana at times huwa nashindwa kujua ni wakati gani muislam huwa ni "muislam" na wakati gani anakuwa sio "muislam", kwa mfano ni wakati gani Sheikh Yahaya anahesabiwa kuwa ni muislam na wakati gani anakuwa sio...

Cha muhimu ujue kuwa mambo anayofanya anayejiita muislam katika maisha ya kawaida (mnayohusisha na ustaarabu) kama vile kutumia maji chooni, kutahiri, kusaidia wasiojiweza, huwa pia yanafanywa na watu ambao hawaujui huo uislam. Na ujambazi, ujangili, uzinzi, uasherati na kuuza madawa ya kulevya na kutumia pombe and other vices, vinafanywa na watu wa aina zote hata wale wanaohesabika kuwa ni waislam...

Narudia tena kukuambia JF siyo sehemu ya POROJO tupe majina ya hao viongozi wa dini ya Kiislam Misri waliotoa "fatwa" wanawake kukukeketwa.

Fatwa ya masuala ya Uislam Misri yanatolewa na Mufti of Egypt All Gomaa.

Wewe umeitoa wapi watu hawauitaji link za wakurdi wanaitaji majina ya hao viongozi uliowataja.

Cc.. gombesugu, Kadogoo, Ami, Barubaru,
 
Last edited by a moderator:
Mohamed,
Umeuliza swali zuri. Kipi kilichofanya Kikwete ampe marehemu Abdulwahid na Ally Sykes medali baada ya miaka 50 ya uhuru? Jibu lake linaweza kuwa VERY interesting. Lakini nadhani ni bora kila mtu aspeculate kivyake vyake.
Kaka Jasusi,
Hakuna haja ya speculation hapa. Hata Mwalimu alipewa medali hiyo siku hiyohiyo, mjane wake akaipokea kwa niaba yake. Ikumbukwe kuwa TANU haikuongozwa na mtu mwingine yeyote, mbali na Mwalimu, tangu inaundwa, inazinduliwa( tarehe 7.7.1954) hadi inakufa kifo cha kinyonga( nasikia kinyonga akizaa hufa muda huohuo!) tarehe 5.2.1977. Historia ya TANU ndio hiyo. Ile ya kufikirika ya Mzee wetu Mohamed inayoanzia Burma na TAA aendelee kuifundisha misikitini na huko anakojua yeye.
 
maswali yako hukufikiria sana nani wa kumuuliza. Unapaswa kumuuliza Mohammed Said kwanini hakuandika historia kama ilivyotukia au kwanini alipowaangalia wazee aliamua kuwabagua - kati ya wale Waislamu na Wakristu. Sasa unaniuliza miye nijibu historia ni lazima ukubali kwanza mapungufu ya histohisia ya Mohammed Said.
Hayo mengine ni katika kunogesha mjadala na kwenda down memory lane. Usikwazike sana na vitu vidogo.

Mwanakijiji,

Haina neno ndugu yangu,tuko pamoja na niwie radhi kama nimekukera.

Hata hivyo bado kuna baadhi ya mambo napitia hapa jamvini na bado nina maswali kadhaa kwako binafsi Insha Allah.

Lazim kwanza ukubali kuwa mimi binafsi na wewe tuna mitizamo tafauti mpaka hapa tulipofikia kwenye huu mnakasha, na kwa sababu zetu kadhaa. Na labda pia tafauti ya kuelewa vitu kadhaa au pia ku-over look vitu vingine vingi tu. Kwa hiyo huku tukiendelea na mnakasha ni vizuri kuheshimiana tafauti zetu nyingi mno.

Badala ya kutaka kwa ulazim na kwa haraka haraka kukubali hayo mapungufu ya kitabu cha Sheikh Mohammed,nijaalie muda kiduchu tuangalie atakapoishia na soote kwa pamoja, ndo tukate shauri la kujua nani mkweli na nani ni mrongo/alokosea. Halafu ndipo pia tutarejea tena kujua huko kukosea, je kunahalalisha na kutosheleza malengo ya hii mada kama ilivyoletwa hapa jamvini na Yericko Nyerere!?

Kwa kifupi,haya yoote tusumbukayo hapa jamvini,lakini la muhimu zaidi ni kuthibitisha shutuma dhidi ya Sheikh mohammed Said. Na pia tuangalie,je hata kama hizo shutuma dhidi yake tukizithibitisha,alizifanya kwa makusudio au ni tafran na dhahama tu za kiuandishi zilimzidi kimo,lakini moyoni mwake alikua na bado anayo makusudio mema kwa Watanzania wenzie na nchi yake!?

Ahsanta.
 
Nafyonza Ilm tu hapa.
Fyonza tu wewe kama ndege kwenye mauwa
Spike,
Upo kama vile haupo.....................
Huyu kijana uwepo wake ni wa kiaina.Safari ya mwanzo alifyonzaa weee.Aliposhiba akaingia ukumbini kupigana mieleka.Jamaa wakaanza kulalamika kama kawaida yao.Nusura wamuitie polisi jinsi alivyowabwaga mmoja mmoja.
 
Narudia tena kukuambia JF siyo sehemu ya POROJO tupe majina ya hao viongozi wa dini ya Kiislam Misri waliotoa "fatwa" wanawake kukukeketwa.

Fatwa ya masuala ya Uislam Misri yanatolewa na Mufti of Egypty All Gomaa.

Wewe umeitoa wapi watu hauitaji link za wakurdi wanaitaji majina ya hao viongozi uliowataja.

Cc.. gombesugu, Kadogoo, Ami, Barubaru,

Acha uvivu.
Hizo links nimekupa, zisome zote kwa undani. Umeiona hiyo ya Muslim brotherhood?
Kama hutaki acha.
Sheikh mkuu wa Egypt mwaka 1995 akiwa anapingana na mambo ya mkutano wa Beijing, alitangaza (Nilimsikiliza kwenye BBC) akisema kuwa ni wajibu kwa mwanamke wa kiislam kukeketwa.
Kama huamini haya nisemayo, basi acha. Ngoja Barubaru (akiamua kusema ukweli this time) akwambie, labda ndio utaamini.
 
Mimi siumi maneno, mimi nasema nachoamini.Kwa hiyo wewe Unachotaka kuniambia Wamarekani wanawavamia hizi nchi simply kwasababu ni waislamu?????
marekani waliivamia iraqi kwa kudai saddam alikuwa na silaha za maangamizi! matokeo yake wamepeleka makampuni yao ya mafuta ili wanufaike na mafuta ya iraqi! baada ya kumnyonga saddam wamegawa silaha kwa makundi ya kidini leo wairaqi wanachinjana wenyewe kwa wenyewe! huko afganistani alivamia ili kumkamata osama lakini wanadai wamemtupa baharini baada ya kumsalia sala ya maiti! leo wamarekani bado wako afganistani hatujui ni kwa malengo gani! baada ya hapo wameivamia libya kwa kusaidia uasi ili wanufaike na mafuta yao na baada ya gaddafi kuuwawa leo libya haina usalama kwa sababu ya uvamizi wa nchi za kikristo! sasa jiulize kwanini marekani haivamii nchi kama korea kaskazini au zimbabwe au venezuela? kwa mujibu wa bush junior alitangaza vita vya msalaba wakati anaivamia afganistani na iraqi ronald regan wakati anaondoka madarakani aliitangaza dini ya kiislamu kuwa ni adui aliyebakia baada ya ukomunisti! sasa mundus sijui unataka ufahamishwe vipi ili utambue hali halisi!
 
MUNDUGUS; hapa kwetu tuna sheria ya ugaidi lakini sheria hii inawahusu waislamu tu! ndio maana tundu lisu kashangaa lwakatware kahusishwa na ugaidi wakati sheria hii inawahusu waislamu tu!
 
Narudia tena kukuambia JF siyo sehemu ya POROJO tupe majina ya hao viongozi wa dini ya Kiislam Misri waliotoa "fatwa" wanawake kukukeketwa.

Fatwa ya masuala ya Uislam Misri yanatolewa na Mufti of Egypt All Gomaa.

Wewe umeitoa wapi watu hawauitaji link za wakurdi wanaitaji majina ya hao viongozi uliowataja.

Cc.. gombesugu, Kadogoo, Ami, Barubaru,

Ritz,

Ni kweli,nahisi haya mambo ya technology na kurahisishwa kwa source of information inaharibu saana baadhi ya watu. Ghafula mtu waeza kujiona unajua mambo mengi, kumbe ni ile jamaa zangu Wahindi wa Kimamba wanaita "machele punga"!ahaha!!

Lakini haina neno na tuendelee na mnakasha.
 
Acha uvivu.
Hizo links nimekupa, zisome zote kwa undani. Umeiona hiyo ya Muslim brotherhood?
Kama hutaki acha.
Sheikh mkuu wa Egypt mwaka 1995 akiwa anapingana na mambo ya mkutano wa Beijing, alitangaza (Nilimsikiliza kwenye BBC) akisema kuwa ni wajibu kwa mwanamke wa kiislam kukeketwa.
Kama huamini haya nisemayo, basi acha. Ngoja Barubaru (akiamua kusema ukweli this time) akwambie, labda ndio utaamini.

Naona bado unazunguka kwenye kichuguu kama nguchiro tupe ushahidi wa hao viongozi na majina yao hizi links sijawaona viongozi wakuu wa dini kutoka Misri wakiruhusu ukeketeji, usichanganye mila za watu na Uislam.
 
MUNDUGUS; hapa kwetu tuna sheria ya ugaidi lakini sheria hii inawahusu waislamu tu! ndio maana tundu lisu kashangaa lwakatware kahusishwa na ugaidi wakati sheria hii inawahusu waislamu tu!
Kadogoo,

..wewe una kengeza la UDINI.

..kama sheria ya Ugaidi inawahusu Waislamu, kama unavyodai, kwanini basi Lwakatare na Ludovick wanashtakiwa kwa sheria hiyo wakati wao ni Wakristo??

..umejaribu kupotosha utetezi wa Tundu Lissu kwa Lwakatare.
 
Last edited by a moderator:
MUNDUGUS; hapa kwetu tuna sheria ya ugaidi lakini sheria hii inawahusu waislamu tu! ndio maana tundu lisu kashangaa lwakatware kahusishwa na ugaidi wakati sheria hii inawahusu waislamu tu!

ulimsikia akisema hivyo?
 
Ritz,

Ni kweli,nahisi haya mambo ya technology na kurahisishwa kwa source of information inaharibu saana baadhi ya watu. Ghafula mtu waeza kujiona unajua mambo mengi, kumbe ni ile jamaa zangu Wahindi wa Kimamba wanaita "machele punga"!ahaha!!

Lakini haina neno na tuendelee na mnakasha.

gombesugu,

"Fatwa" hutolewa na Maulamaa wenye Ilm siyo Bejing, ha haa haha.

Chele Punga...
 
Last edited by a moderator:
quote_icon.png
By Kadogoo

MUNDUGUS; hapa kwetu tuna sheria ya ugaidi lakini sheria hii inawahusu waislamu tu! ndio maana tundu lisu kashangaa lwakatware kahusishwa na ugaidi wakati sheria hii inawahusu waislamu tu!
Kuna wakati binadamu huwa tunapitwa na jambo fulani...Unaweza kunisaidia/kunikumbusha labda ni waislam wangapi hapa Tanzania wameshafikishwa mahakamani au wameshashtakiwa kwa kutumia hii sheria ya Ugaidi?
 
Back
Top Bottom