Ndugu yangu naona jinsi gani nilivyo zimwi katika ndoto zako. Hakuna unachoandika bila kuhakikisha unatumbukiza Nguruvi3.
Mimi ahdi tyangu ni moja, kutomuonea mtu au kumuonea haya. Natumbukiza kisu hadi kigonge mfupa sheikh, ushanfahamu.
Hivi nikikuambia familia yangu ni ya Mndolwa hiyo inasaidia nini katika mnakasha. Tanga nyumbani kwetu. Tena waijua mjni, mimi kuanzia Magoroto, kicheba, mtindiro, mjasani, pongwe, Lusanga, magunga, Mnyuzi, Tengeni tena hapo daah hata usiseme, bonde Muheza nyumbani usinitoe machozi kijana wee! Unaijua barabara ya 10!
Hebu tuendelee na mnakasha maana tutasema mengine na wengine kupatwa na fadhaa kama si soni.
Nguruvi3,
Nikikusoma nafurahika mno kwa vitisho na umahiri wako. Unanikumbusha watu kama Nikita Khrushchev na Slobodan Moilosevic!ahaha!!
Hayo mambo ya kiTanga na Biography ni wewe ndie uliemuanzishia Sheikh Mohammed Said,nami ikanilazim nikunyoshee maneno.
Mbona nami family yangu ni wakulima wa asili kabla hata Wajarumani hawajakua na fikra za kutia maguu yao hapo Tanganyika, na tuna mashamba mpaka kesho yenye hekari nyingi tu kuanzia Daluni, Bwete,Mwele,Magoma,Maramba,Saadani,Ushongo na Mazinde. Bahati mbaya mimi binafsi ni mvivu ndo maana nimekimbilia kujificha huku nchi za watu kwa miaka tarkiban ishirini sasa,Allahmdulillahi.
Hiyo Barabara ya 10 unayoitaja,hapo kale ilikua ni mojawapo ya viunga vyetu vya minazi. Na leo hii tuna nyumba zetu pale mtaani peke yake sita. Nakupa challenge nenda kagonge mlango pale jirani na Msikiti mkubwa wa Al Jumaa, kwa Al Marhum Shariff Nuru(dada yao ni Aunt Mwananuru Shariff aliwahi kuwa Principal Secretary nafikiri Wizara ya Afya hapo enzi ya Rais Mwinyi),wale ni jamaa zetu wa karibu na watakufahamisha uzuri mimi ni nani. Au nenda kamuone Mayor wako pale Tanga akufungulie Archives/shajara na uwasome Wazee wetu kwa utuvu tangia enzi ya Mwarabu na Mjarumani.
Ukishindwa huko koote nenda pale Barabara ya 9,uliza kwa Kina Diwani,nao pia ni jamaa zetu nao watakufahamisha kwa uzuri.
Au muone Salum Shamte wa Mkonge,ambae ni hakika unamfahamu,yule ameoa kwetu kwa hiyo atakupa habri japo kiduchu.
Sasa wewe hiyo Barabara ya 10,nyumba yako/yenu ni ipi,jamaa zako ni nani,au wale kina Khara Wahindi walohamia Canada!?
Mindhal, unasema machozi yanakukurubia tuyaache na tuendelee na mnakasha Insha Allah.
Nakupenda saana Mzee wangu Nguruvi3,na kwa sasa najua wewe ni Uncle wangu from ma Mum's side hapa jamvini,basi nami naringa saana sasa!ahaha!!
Ahsanta.
