Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Umerudi? Hivi huoni haya kuingia kwenye uwanja ambao maswali ya kitoto tu umeshindwa kuyajibu ukakimbia? Sasa unarudi kwenye jamvi unaanza kuleta masuala ya Iraq ambayo hayako kabisa kwenye mada uliyoianzisha mwenyewe!!!!! Unadhani yatakusaidia kufunika udhaifu wako wa tabia ya kuingia mitini kwenye mada za kiume?
 
Mohamed Said tumemuonyesha makosa ya wazi ya kitabu chake na yale yaliyojificha, tena tumemueleza kwa ufasaha na kwa lugha rahisi ya kitaifa,


Sioni sababu ya eti sisi tuwakimbie wafuasi wa Mohamed????

Yaani unaonyesha makosa kwa kuingia mitini!!!!!!!!!!!!!! Kweli nchi hii kazi tunayo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Nyerere hana legitimacy ya kuzungumzia humanity kutokana na mauaji ambayo ameyafanya kwa binadamu wasio na hatia yoyote zaidi ya kutopendezwa na dini wanazoziabudu
 
Hata ungempamba vipi, Mzee Mohamed Said anabakia kuwa muongo wa kutupwa na aliutumia uwongo kinyume na maagizo ya dini yake! Mzee mzima amedharirika hapa!
 

Gombesugu,
Umemtaja Nyakyoma wa Gapex. Maoni yangu ni kwamba James should have been in jail. Aliyoyafanya yeye pamoja na marehemu Muro katika kampuni hiyo si jambo la kusamehewa. Pia James alimtapeli rafiki yake waliyesoma pamoja UDSM ambaye alikuwa amejenga nyumba yake akamshirikisha kwenye mradi fulani na nyumba yake ikawekwa kama dhamana ya mkopo. Walipopata hela Nyakyoma akazificha Uingereza na wakashindwa kulipa deni walilokopa benki ikabidi huyo jamaa nyumba yake ichukuliwe. Lakini hili la kupelekwa faili lake ikulu nadhani zilikuwa njama za marafiki zake waliotaka kumwokoa kwa sababu nilivyomjua Mwalimu alikuwa mkali sana mambo ya fedha. Nyakyoma aliwahi kufanya kazi intelligence na hence alikuwa na watu walioweza kumfichia madhambi yake ndani ya system.
Kuna mifano kadhaa ambako vijana wa intelligence walimficha Mwalimu. Kwa mfano wakati Museveni alipogombana na Obote, wote wakiwa wakimbizi Tanzania, na Obote kumchongea kwa Mwalimu. Mwalimu aliamuru Museveni arudishwe Uganda, lakini maafisa wa usalama, wengine ambao alisoma nao mlimani, wakamficha kati ya Tabora na Karagwe.
Pia kuna wakati Mwalimu alitaka kumfunga Mkono, huyu mbunge wa sasa wa Musoma vijijini. Nasikia alipewa habari na kukimbilia London. Kwa info yako, nadhani na Mohamed ameligusia hili, Mzee Mzena kishatangulia mbele ya haki. Na juzi tu mjane wake amefariki. Mimi pia, kama Mohamed, nikifahamiana na binti zake.
 
Gombesugu, nakusalimu ndugu yangu. Bandiko lako limejaa hamaki hasira na kila aina ya tashtiti. Una haki ya kuelezea hisia zako lakini basi busara itangulie. Umetukana watu kwa lugha ya kiarabu. Nadhani unajua mkanganyiko uliopo kati ya Uarabu na Uislam kwa watu wengi.

Kuna uwezekano akatokeo mtu nakusema umetukana kwa kutumia Uislam, hapo utakuwa umefanya dhalili katika dini. Ningeshauri wakati mwingine utumie busara ili kujitambua na kutambua kuwa si kila jambo linaandikwa kwa utashi wa mtu.
Yapo yanayoathiri jamii hata kama ni ya mtu. Naomba nilirejee bandiko lako kwa uchache tu na kadri ninavyoweza na kujaaliwa
gombesugu;6223813]Ritz,Huyo jamaa ni psychological fragile,angalia tu ile mada yake halafu ameweka Sheikh Issa Bin Ameir badala yaSheikh Hassan Bin Ameir...kama kwenye legal technicalities basi
Barrister mahiri anakwambia Case dismiss
Kwa utaratibu huo basi kesi ya Mohamed ni dismissed. Kusema kawawa alikuwa makamu wa rais mwaka 1988 Barrister mahiri angeshasema case dismiss.Kwamba balozi amehutubia bunge hakimu angebubujikwa na machozi
Inastaajabisha na ni viroja pasi mfano,hao mashangingi wa shughuli kutukataza kumjadili huyo Nyerere kama vile sisi hakuwa Rais wetu!? Hawa watu maluuni saana
Ustadh soma maneno yako haya ili watu wasipate tabu kujua nani hasa ni maalun
Gombesugu:Kwa hiyo msione watu tumekaa kimya,ati mkafikiri tumevamia tu hili jamvi au hatujui mam
o au huyo Nyerere wenu hatumjui au mambo nyeti takriban yoote, ati kwa sababu tu ni watoto wa Mdarasa
halafu tena hapa
Hapa kilichobaki kwa ufupi ni kurembeana fedhuli na kibri kingi tu,labda zaidi wanatumia
udhalimu wao wa kumuuliza makhanatha Sheikh Mohammed ili wamuumize kichwa
na kumalizia ukasema hivi
Kwa masuala haya muulizeni Mzena mwenyewe kama yuhai. Mkitaka zaidi nitakupeni majina ya watu makhusus tena Wakristo wenzenu mkaulize
Kama Nyerere ni rais wa wote haya maneno''hamtujui,wao,wenu'' yanatoka wapi?
Hapo maalun nani aliyesema au aliyekaa kimya
Na haiingii akilini hata chembe ati watu tusimjadili Nyerere,mtu aloleta nakma na zilzala ziso mipaka hapo Tanzania na kwingineko Hapana
Nyerere ni mwanadamu hana immunity ya kutojadiliwa1 ajadiliwe tu hakuna shida. Lakini si umesema haya manenomwenyewe
Gombesugu:Habari za Nyerere ni nyingi mno wala hazishi kwa hapa Jf hata siku moja
Pengine ni kwasababu he was great man vinginevyo kwanini ajadiliwe!
Yule kunguni wa hoja a.k.a Abu Jahal,mimi pia nilimtoa maanani kitambo pale alipoleta ule uTarime/Ukabila wake,na ati kujaribu kumtetea Nyerere tena kwa kutumia Khadith na Qur'aan tukufu. Yule Kunguni Wallahi ni Khabith Al maar
Uislam hauna hati miliki. Kama ametumia Qur'aan na hadithi kuna ubaya gani?Pengine yeye ana weledi mkubwa kuliko yule anayedhani bila kujua Qur'aan na hadithi zinasemaje.Hebu angalia hapa ambapo hukutumia Qur'aan au hadithi unavyojiweka dhalili Kwa mtazamo wako kwa vile kuna maalun mmoja anatukana Marekani basi ni vema Muislam Mohamed naye atukane. Uislam hausemi kuhusu kuiga mabaya, umehimiza katika kutenda mema na kuusia kuacha Maaswi. Sasa unapochukua tusi la Marekani ukijua ni kinyume na taratibu za uislam na utamaduni wetu hapo huna Qur'aan, hadithi au sunna. Ni afadhali mwenzako aliyetumia kuliko wewe uliyeshindwa kutumia sheikh tena unatilia ubani kabisa
Na bila ya kufanza hivi,tutawezaje kuzungumzia History!?
Hewala kama ndivyo basi Mshauri Mohamed aongee yale ya chumbani kwa Nyerere ili historia ikamilike.Vipi historia ikamilike kwa Nyerere peke yake kudhalilishwa? Sasa jamani si kila siku manasema watu waandike vitabu, inakuwaje ninyi manotaka watu waandike ndio wa kwanza kufurumusha matusi? Kama hukubaliani naye mchalenji Hapa unatupa habari mbili na nikushukuru.
Habari ya kwanza ni kuhusu Abdallah Nungu na Zacharia Maftah. Hawa ni watu wakubwa katika uongozi wa sehemu nyeti. Kumbe basi zile lawama kuwa waislam hawakupewa nafasi zinatoka wapi? Maana tulisikia vitengo muhimu vilipewa mfumokristo, sasa hivi kama si muhimu, je muhimu ni vipi?

Pili, file la Kiwira, meremeta, Dowans, IPTL, Buzwagi, Richmond, Radar hayajulikani yalipo. Hata zile karatasi zilizonyofolewa hapo hakuna. Madudu yote yanawagusa akina Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Ni vema ungeendeleza mlolongo wa matatizo usiachie kwa Nyerere hata mimi nakuunga mkono kuorodhesha hayo lakini basi usichague, mwaga kila kitu huo ndio uadilifu Hoja yako hapa ni nini? nashindwa kuelewa ni endapo ni raia wa Zanzibar ndani ya meli au vipi. Ninavyokusoma (kama sijakosea) hizi ni njama za kuumiza waislam. Kwamba meli ikishambuliwa watakufa raia waislam wa Zanzibar na wala si askari. Wakati wa vita ya Kagera madereva walikuwa raia.Sijui hapo unasemaje. Lakini basi kama ni msaada kwa mkatoliki mwenzake Samora, vipi kuhusu Sahara Magharibi na Palestina? Vipi Afrika kusini, Zimbawe n.k.

Unachotakiwa ufahamu ni kuwa meli haikuwa hatari kama vile vijiji vilivyopakana na kambi za wakimbizi kule Mkimbizi Iringa, Dakawa na Mazimbu au maeneo ya kusini indi na Mtwara. Mbona hujaona hatari maeneo hayo? Wewe ulichokiona ni hatari ya waislam wazanzibar
wa kifupi,Sheikh Mohammed hakumtusi Nyerere ati kwa kusema alikua akisaidiwa kitoweo na nduguye Bwana Mshume Kiyate,hasha!
Wickama ameto tafsiri ya kusengenya kama unakubaliana nayo basi ni tusi kama hukubaliani nayo kama Uislam usemavyo upo sahihi.
Hoja kama nilivyoielewa ni kuwa yale aliyokuwa anafanya Sheikh Yahya ni sehemu ya Uislam? Awe amemfanyia Nyerere, Obote au mwingine swali linabaki je ni Uislam ndivyo usemavyo? Hapa utusaidie maana unaweza kuwa na ufahamu zaidi yetu, endapo huna jibu basi liacje suala hili kama lilivyo maana litazua mengine yasiyohitajika Kumbe ajali ilikuwepo! kuna habari hapa kuwa IGP alikimbia nawe unathibitisha kuwa ajali ilikuwepo. Kwani nini kilitokea hasa? na kwanini Nyerere huyo huyoaliyemsulubu Hamza ampe ulaji?
 
Yeriko sijui utaficha wapi sura yako...hawa watu mnaowaita wa maddrasa wanastaha na maarifa mengi sana. Kuna mengi ambayo yakianikwa hapa hata ile sifa kidogo ya mzee wetu nyerere inaweza ikayeyuka, RIP JKN yeye alitambua kuwa kunabbaadhi ya maeneo alifanya makosa na alikiri makosa yake kabla ya kufariki dunia...naamini yeye kumuomba Ghadaffi kisha akakubali kumjengea msikiti katika hatua za mwisho za uhai wake ilikuwa ni kuu-enzi uislam na waislam kwa michango yao mingi waliompatia katika maisha yake ...Wakati mwingine kuukubali ukweli ni njia nzuri kufikia maridhiano na suluhu ya kudumu kwa mustakbali wa watu wetu ...
 
Ukimmaliza Mwalimu umeimaliza TANZANIA. Hakuna namna ya kuitaja Tanzania ukaacha kumtaja Mwalimu. Watu hapa wanajaribu kupambana na HISTORIA. Hawataweza.
 

Jasusi,
Sikujua kama yule Bi Mkubwa amefariki.

Akinijua vyema na kunipenda kama mwanae.
Mara ya mwisho nilimuona kasimama nje ya
nyumba yake pale Regent na tukasalimiana.

Namkumbuka na gari yake Peugeot akiwabeba
wanae kuwaleta kwenye parties zetu.

Jasusi nakurudisha nyuma...
Mick Jagger and The Rolling Stones.

Wakati umekwenda.
 
THE LABEL OF "ISLAMIC FUNDAMENTALISM" TO MOHAMED SAID & WALAMBA BUTI ZAKE...

With reference to religion,the concept of fundamentalism originated in Protestant Christianity,especially in the Puritan tradition in United States.In Christianiaty "fundamentalism" is a perojative word.In his famous book,'Fundamentalism' Barr(1981;2)says the word is disliked even by 'the people to whom is applied'.,it is regarded as " a hostile and opprobrious term suggesting narrowness,bigotry,obscurantism'
In Christianity,fundamentalism is associated with characteristics which most Christians disapprove of,because they are considered extremist and indefensible.Among its chief characteristics are the following;

1.a belief that the bible in its entirety is literally the word of god

2.'a very strong emphasis on the inerrancy of the bible and the absence from it of any sort of error'

3.'an assurance that those who do not share their religious viewpoint are not really 'true christians' at all (Barr,1981;1)

4.a very strong emphasis on prophecy and its ultimate fulfilment.

Serious problem arise when that concept of fundamentalism is transferred to Islam.It is a universal belief of all MUSLIMS,no matter how one would wish to qualify them,that the Qur'an,is Literally the word of ALLAH and is free from any sort of error.THEREFORE,if the concept of religious fundamentalism is applied to MUSLIMS,All Muslims would have to be considered fundamentalists.And any Muslim who is not a fundamentalist ceases to be a MUSLIM.

Here in Tanzania,the concept of "islamic fundamentalism".,can very easily slide into political tool for religious oppression and control.Everything Muslim would be "fundamentalist" and therefore Dangerous,,especilly when he tries to speak the truth and reality..

KWA NAMNA HII BASI TUTALAMBA TUH BUTI ZA MOH SAID KWA HESHIMA NA TAADHIMA ZOTE...
 
Nguruvi3, Wickama, MS, Ritz, Mag, Platozoom, Yericko, Barubaru et al.

Wakati manakasha ukiendelea, hebu tujikumbushe Baraza la Mwalimu JK Nyerere kama lilivyotolewa na Nyongeza ya Ngurumo, Jumanne tarehe 11 Okctoba 1960.
 

Attachments

  • Baraza la Nyerere 1960.jpg
    778.8 KB · Views: 93

Jasusi,

Salaam. Nashukuru sana kwa bayana yako. Wewe ni mmojawapo wa watu wachache mlonikaribisha uzuri hapa jamvini.

Nyakyoma namjua vizuri saana nae anamjua na kumwogopa saana Mzee wangu! Bint yake Nyakyoma mmoja Alice, alikua rafiki yangu kitambo enzi ya "Ujahil" wakati nilipokua England!ahaha!!

Kwa wale wanaojua system,hasa "enzi ya Mwalim",watakuhakikishia umahiri na unyama wa Zacharia Maftah. Cabinet nzima ilikua inamwogopa huyo kiumbe. Kwa hiyo mtu yeyote asingeweza asilan, ati kudadavua ile file ya Nyakyoma kwenye mikono ya Maftah bila ya Nyerere ku-sanction/authorise...hii haina ubishi ndugu yangu. Barua zipo mpaka kesho pale Takukuru,Nyerere ame-sign file iende kwa Abdallah Nungu kwa geresha na kutoka hapo imfuate yeye pale State House. Kama unataka kujua zaidi,muulize Mzee Kitwana Kondo,siku zile alipokua Mkurugenzi Mtendaji wa State Motors Corporation,na Hatibu Idd as General Manager...J.W. Ladwa yule baniani wa pale Upanga, ilimlazim akimbilie Canada kwa muda akapumue!ahaha!! Maftah ilkua kitu ingine ndugu yangu. Ghafla kaingia "Sheikh Ali" madarakani,akamuondosha bila hata sababu yoyote ya maana. Brigadier Ntukamazima aliwahi kuongelea upuuze ule kwa undani japo nae alikua mwoga fulani hivi kunusuru madaraka yake. Lakini sisi tunajua kwanini ilitokea vile!ahaha!!...again..."Funika Kombe Mwanaharasha apite". Sasa tutafunika makombe mangapi hapa jamvini!?ahaha!!

Nimekuelewa kwa ustaarabu wa mazungumzo yako. Nami nina mengi pita kiasi,la muhimu tuyaache na kuwastiri Wazee wetu..."Funika Kombe Mwanaharasha apite".

Siku moja tukikutana nitakupa kisa cha Kitwana Kondo na jamaa yako Sinde Warioba,utacheka saana. Matokeo yake ikabidi Mwinyi amrudishe Sinde Warioba toka Uwaziri Mkuu awe Waziri wa Serikali za Mitaa na Miji. Kufika pale,Sinde akaanza kutumia umahiri wake wa kisheria kumchachafya upya Kitwana Kondo. Ikabidi Kitwana Kondo ajibu mashambulizi,akatumia System wakamuweka mtu wao ati "Muislamu" na kumsaidia kwa karibu yule jamaa na akamwangusha Sinde Warioba pale Bunda. Mwinyi akapata excuse nzuri ya kutomrejesha tena!ahaha!! Yaani hapo Mzizima kama ujuavyo pana mengi mno na viroja vingi Wallahi!!

Mimi binafsi sina chuki kwa Nyerere nilishawahi kusema awali;Mzee wangu kamfanyia kazi zake nyingi saana na nzito. Lakini tunapokua baina yetu Watanzania kwa Watanzania ni muhimu saana kuzungumzia kiundani matatizo yaliyopo,yalipotokea,chanzo chake nini,nani walosababisha,tumejifunza kitu gani,tufanye nini ili kurekebisha na kivipi twende mbele ya safari kwa umoja na mapenzi. Kwa hiyo ukweli wenye maana na ushahidi lazim tunene.

Lakini ghafla,wanapokuja viwavi fulani wasojua mambo na kuanza kutoa amri,Wallahi mimi hupata simanzi mno.

Huyo Nyerere, mimi hapa nilipo na kila nchi nyingine niendazo;mara zoote nikikutana na jamaa wa mataifa mengine hasa ya ki-Afrika na wanapoanza kuleta maneno ya makhanatha na kumkashifu bila ya sababu za msingi. Kwa kukosa kwao fadhila au kutucheka yakuwa Watanzania hatujasoma na ni maskini...basi mimi huwawekea darsa kutwa nzima,na kumsifia Nyerere kwa mengi na muhanga tulojitoa Watanzania kwa wenzetu. Mwisho wa darsa jamaa hunitaka radhi na kushikana mikono. Huwa sikubali asilan,mtu mpumbavu tena sio Mtanzania aanze kashfa za kipuuzi dhidi ya Nyerere. Lakini kuna topics nyingine huwa naacha mdomo wazi,hasa inapokuja mambo ya Uganda,Mozambique na Biafra!ahaha!! Tuyaache haya ndugu yangu,labda siku tukijaaliwa kukutana.

Huyo kijana Yericko,kuna kitu amekosea na nina hakika amewakera mno kina Mama Maria, Uncle Andrew na ndugu zake.

Tuendelee na mnakasha.

Shukran na nakutakia siku njema ndugu yangu.
 
bwana mohamedi saidi, nina wasiwsi na uwezo wako wa kufikiri na kupembua mambo.
 
Ha ha haa Nguruvi3, wewe kweli kiboko! Ngoja nitulie kwanza kidogo...kazi ndiyo inaanza.

Mag3,

Acha kutulia muungwana hapa shughuli hii ni nzito saana. Mpe salaam Uncle yangu Nguruvi3 a.k.a Vunja Mifupa...mwambie aache uwoga na kupunguza mambo ya biography za Tarime. Kama anayaweza kikweli mwambie amwingie Zali la Mentali a.k.a Mchimba Chumvi !ahaha!! Aache au apunguze kumuonea Sheikh Mohammed!ahaha!!

Yaani najua huwa mnanikumbuka ndugu zangu,asubuhi hii nimeona comments zenu ati mnanijibu basi nimevunjika mbavu kwa kicheko Wallahi!ahaha!!

Leo nasafiri na family kiduchu,takujibuni nikijaaliwa labda on Tues. Insha Allah

Naona Nguruvi3,biography zake zoote sasa anajaza Masheikh na Misikiti tu,au anataka kuingia Uislamu kinyemela!ahaha!! Mwambie tunamkaribisha lakini asije kupata akili za Madrasa kama sisi!ahaha!!

Ile lobbying yangu kwa Sheikh Mohammed Said,ili akutoe kwenye "ile Shit List" bado inaendelea kwa hiyo fanya sabra kiduchu!ahaha!!

Ahsanta na tupendane ndugu zangu.
 

NGURUVI;

Nashukuru kwa dua lakini ili dua ikubaliwe na Mola uliemtaja kuna masharti haya ya kufanya kabla ya kuomba dua: The Azanian Sea: ADABU ZA KUOMBA DUA
 

Nguruvi3,

Nakusalim ndugu yangu. Mbona unawatia aibu wenzio,wao walidhani yakuwa wewe ndo Shujaa wa kumwingia Zali la Mentali,naona unatoa excuse ati humtaki "hana maana". Inakuwaje leo uko kiwanjani uchague wapinzani wa kuwakaba...tafadhali Mzee Vunja Mifupa,punguza hadaa za kijitu kizima!

Kuhusu kutaka kunijibu mimi ni kwamba huwezi na wala mantiki zangu hutazifikia asilan,labda tu itaishia mimi nawe kulumbanana na haina haja tufikie huko,maana wewe ni Uncle wangu kutoka Tarime!ahaha!! Kwa hiyo ilobaki,kama dasturi yangu narejea kuwa msikivu mtiifu wa Sheikh Mohammed.

Pia nachelea kumkera Maalim wangu Sheikh Mohammed,maana kwa ustaarabu alonao, hapendi sisi Wanafunzi wake tulomkubali kwa dhati kunena mengi hapa jamvini. Na jana alinikanya kiduchu hapa jamvini. Kwa hili nakufahamisha yakuwa nitakua kimya mpaka itakapolazim kunyoosha tena maneno Insha Allah.

Mfahamishe Mag3,yakuwa ile bayana yangu haikuwa na matusi asilan, na wala yale si maneno mughali kwa mwenye kujua kutumia kiswahili kwa hiba na madaha. Au zile Istilahi na Lahaja zimemsumbua kiduchu!? Basi Wallahi nitakie saana radhi kwake na naomba anisamehe. Najua kuna wengine walinitukana ati kwanini nimeandika kiarabu!?ahaha!!

Kwaheri nakuachia mtaalam mwenzio Mchimba Chumvi!ahaha!!

Insha Allah.
 

Mzee Ms, baada ya Salaam. Nashukuru kwa maneno mazuri. Haya ya kina Babu na Wazenj na Mapinduzi mimi wala siyazungumzi (angalau kwa leo). Infact moja ya kitu nachotamani kitokeze kwenye tume ya kina Waryoba ni kuwa tupige kura ya kubaki au tusibaki na muungano na kama tunabaki nao uwe ni upi. Sioni taabu kukuambia ikitokea fursa hiyo, mimi ni mmoja wa watakaopiga kura ya kuuvunja. Kikubwa ni kuwa i would rather live alone rather than with a bitter and unhappy neighbor. The sooner mabwana hawa wakipewa chao nitashukuru. Then they can fulfill their "tarnished" dreams. Mimi nasubiri fursa ya kura. Kuhusu suala la wewe kuandika issues za Sheikh na Nyerere lazima niwe mkweli sijasoma umeandika nini. Lakini tangu ukomae na ukatoliki wake, then kuhamia kwenye Kupishwa chumba alae na Ally, then Nyerere kukopa hela za mboga kama part ya "struggle against the British colonialism" i will seriously treat your coverage on him with caution. And you can easily see why. Shukran.
 

Nguruvi3,
Nakutumia bayana hii fupi kukwambia mie sikutukana na wala sikuzungumza "Kiarabu" asilan. Ni sawa vile mtu asojua mambo vizuri ati akamtuhumu Mwingereza kuwa katukana kwa kutumia ki-French au ki-Latin!?

Lakini napenda kuchukua fursa hii kwako binafsi, na wengineo nyoote mlojihisi dhuluma imekinza mioyoni mwenu kutokana na ile bayana yangu. Labda nilikua na muhma wala si hamaki asilan,na ndo udhaifu wa kibinadamu.

Kuhusu hiyo "ajali",nisingependa tuirudie tena...kwa sababu kadhaa na hishma ya wahusika ambao mimi ni watu wangu wa karibu. Lakini kama utatumia fikra,usomi ulonao na mantiki na pia kuondoa Udini na Ukabila;basi ni muhimu saana ujiulize. Hivi ni kwanini Nyerere aliamua kumuweka chini ya Surveillance IGP wake mwenyewe takriban kwa miaka kadhaa. Bila ya huyo IGP kushukiwa au kufanza lolote baya,na bila ya kufuata ushauri wa Marehemu Mzee Mzena ambae alipinga saana jambo lile!? Mzena alimfahamisha Nyerere implications na consequences za jambo hilo,na je IGP akipata fununu itakuwaje na tutatoa justification gani!? Vipengele vya Sharia vilipoletwa,Nyerere hakutaka kabisa kusikia. Bahati nzuri kwa Nyerere,IGP hakujua hii kitu mpaka siku ile alipopatwa na "ajali" na kwenda kukutana na Nyerere na baada yake ndio akagundua "tambara" zima. Tuwache haya mambo tafadhali,huwezi jua jinsi Mzee Mzena na Hamza Aziz walivyokua kikaribu na kuheshimiana kikazi. Lakini baada ya haya kutokea palikua na friction na indifference kubwa baina yao...pia iliathiri "makundi fulani" ndani ya Idara zao. "Funika Kombe Mwanaharasha apite"...wewe ni mtu mzima tuyaache haya mambo,hao woote ni Wazee wetu soote ok!

Msalimie Mag3,natumai nae pia amenisamehe kwa kile "Kiarabu" cha kwenye bayana.
Ahsanta.
 
Gombesugu,
Kaka yangu basi inatosha.

Mzena ni marehemu.

Wakati niko shule nilikuwa karibu sana na wanae.
Tukisoma shule moja.

Sheikh Mohammed,

Asalaam Alaykum Al Akhiy.

Nipokelea bayana yangu hii dhaifu kwako.

Nimekufahamu na nimesikitika. Hawa jamaa kila tunapowaambia kuwa hawa watu woote sisi ni Wazee wetu,nafikiri hawafahamu asilan kuwa tunamaanisha nini.

Ndo maana mimi tangia nilipongia nalikubali kuwa chini yako ili nikusikive kwa utuvu na nitape Ilm. Nikaonekana ati ni Mfuasi wa Madrasa sitaki kutumia maarifa na wala "Historia ya Tanzania" ati siijui!?ahaha!!

Kuna wakti ulizungumzia na kujiuliza Zohal gani ilowasibu hawa jamaa. Sina hakika lakini najua pana ile "Zohal Sumaku" ambayo ni mughali kukutoka ikishaganda. Au pia pana "Kisirani Shida",nayo pia ni bahri nyingine.

Leo nasafiri nakwenda pale Westerplatte Danzig(najua unaijua kwa uzuri historia ya pahala hapa,hasa kunako wiki ya mwanzo ya WWII),kwa weekend na family hapa...Insha Allah tarejea siku ya Jumanne Penye uhai na majaaliwa.

Lile neno Shangingi,wala si neno baya wala si matusi asilan. Naona jamaa hapo limewakera lakini nishiwataka radhi. Hili neno asili yake khasa ni Wamasai. Ni neno la fahari kubwa kwa Wamasai kuitwa Sangiki...lakini Insha Allah tuyaache maana nayo pia ni bahri nyingine.

Nakutakia Kheir na fanaka na mapumziko mema ya W'end Insha Allah.



Ahsanta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…