NGUVUMOJA
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 1,347
- 328
Leo 2013, ndio unaliona hili, vipi kwa yule aliyesimamia kwa nguvu zake zote kuhakikisha anauvunja mshikamano wa Waislam wa Afrika ya Mashariki (East African Muslim Welfare Society) na kuwawekea chombo chenye katiba inayofanana na ya TANU?Suala la BAKWATA mimi naungana na wanaotaka mageuzi juu ya chombo hiki,
Nilazima kutazama kama kinamanufaa kwa waislamu ama kinamanufaa kwa serikali na chama tawala,
Misingi inayoleta viongozi wa chombo hii ni lazima itazamwe upya!
Manung'uniko kwa waislamu juu ya chombo hiki ni lazima yasikilizwe ama sivyo huku ni kuhatarisha ustawi wa uislamu Tanzania!