Wickama
JF-Expert Member
- Mar 8, 2009
- 1,466
- 1,196
Mkuu Wickama:
Nadharia nzima ya mapinduzi ya Zanzibar inabebwa na Okello,
Japokuwa inaelezwa kuwa Okello aliwazidi kete wahafidhina wa ASP ambao inaelezwa kuwa walishapanga kufanya mapinduzi wiki moja mbele ya yale ya Okello,
Mkanganyiko kwangu unakuja kutuama kwa Mzee Karume,
Je Karume alikuwa kwenye jeshi la Okello ama alikuwa kwenye kundi la mapinduzi la ya ASP ambayo yalipangwa kufanyika wiki moja mbele ya Okello?
Hebu tupeane elimu hapa mkuu!
Yericko[/B]; Miaka ya Nyuma nilisoma kitabu cha Okello. Hakuna mahali alipotaja kushirikiana na Mzee Karume. Okello pia haonekani kipumbwi kwenye mbinu za kivita na wenzie (assuming alikuwa part of that army). Binafsi nilimsoma kama mtu aliyebobea uafrika dhidi ya uarabu. This is confirmed kwenye hiyo video (Mungu wa waafrika!!!!!) Mahali fulani kwenye kitabu chake alisema alibakiwa na jeshi dogo sana la watu jasiri waliokubali kulishana AMINI (paka walichinjwa na matambiko)na hao ndio aliofanya nao hayo mapinduzi siku hiyo. Mwenyewe alivamia kituo cha polisi akamuua askari na kupora silaha. Angalia hiyo video niliyopost inaonyesha kabisa aina ya bunduki zao. Ni zile askari walikuwa wanalindia wafungwa for so long. Haiwezekani hizo ziwe zile zilizoagizwa Algeria. NO WAY.
Kama unaweza kuwahisi waingereza kutoa msaada ni kule kupunguza maofisa polisi wazungu toka 26 hadi 5 wakati hayo yanatokea. Kwenye kitabu cha marehemu Ali Muhsin amelaumu kuwa hao wazungu walienda na fungo za ghala ya silaha kiasi kuwa siku hiyo askari walikuwa wamebeba silaha tupu. Japo, hii pia inaweza ikawa ni matayarisho ya yale mapinduzi toka bara.
Ukizingatia kwamba Karume, Babu, na wengi tayari walishaondoka zenj same week kuwa Dar. Inaelekea hawa viongozi walikuwa wanatarajia mapinduzi, sawa, lakini for sure sio haya ya Okello. Ndio maana mwandishi anatoboa kuwa ya kwao (ASP) ambayo Tanganyika (Nyerere) angesaidia ilikuwa yafanyike wiki moja BAADAE. Ni kwamba Okello aliwakata bogi. Kwa maana hiyo kulikuwa na siri ndani ya siri. Mwandishi ameeleza wazi kuwa Okello hakutaka kuwaamini wanasiasa juu ya mpango wake.
Sasa kama watu wameshapindua huwezi sema sisi tumepanga yetu. No wonder wao walitumiwa post zao za urais na uwaziri over the radio na kama hayo bila kutarajia. Na hiyo explains why in the long run huyu Okello lazima angekuwa an embarassment kwao kwa vile wewe utakuwa rais, sawa, lakini aliyepindua ni huyu, sasa who is the king here?
Kwenye kitabu chake, Okello yupo bitter na jinsi Nyerere alivyom-handle na kum-mislead hadi kufikia akafukuzwa kwenda kwao Uganda. Analalamika kuwa hakuwa mkweli kama alivyompima Kenyatta. Sasa kama ingekuwa wao ndio waajiri wake, for sure lazima angebaki loyal kwao na asingekuwa tishio kwa serikali iliyofuata baada ya mapinduzi. Lakini the fact kuwa ilibidi aondoke ni ushahidi kuwa viongozi wa ASP wasingeweza kutawala vyema in his presence. Katika hiyo video wanampa credit Mr. Hanga kuwa huenda alishirikiana na Okello, lakini inawezekana ilikuwa in the absence ya viongozi wengine wa ASP kujua.
Haya ya kuua watu wengi, yeye Okello aliyasema "SIKU HIYO KADRI YA WAARABU 13,000 waliuwawa. Sio WAISLAMU. Waswahili na wazungu walibaki salama. Ulitakiwa kuvaa au kuninginiza kitambaa cheupe. Testimony ya chuki za Urangi. Kwa hiyo Zenj palishagawanyika na infact hata jina la ASP linaonyesha kuna jamii ya watu fulani walishajihisi wanyonge. Huu ulikuwa ni Urangi na Ukabila hakuna dini hapa. Wote walikuwa Waislamu pengine kasoro OKello. Ni sawa na nyakati za Zimbabwe, Angola, South Africa (Christians versus Christians). Hii kuua ya waislamu ni recent politics. Kama vile zimbabwe umlaani Mugabe kuwa ZANU-PF waliuwa Anglican Christians (white settlers) katika kujikomboa.