Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar



Yericko[/B]; Miaka ya Nyuma nilisoma kitabu cha Okello. Hakuna mahali alipotaja kushirikiana na Mzee Karume. Okello pia haonekani kipumbwi kwenye mbinu za kivita na wenzie (assuming alikuwa part of that army). Binafsi nilimsoma kama mtu aliyebobea uafrika dhidi ya uarabu. This is confirmed kwenye hiyo video (Mungu wa waafrika!!!!!) Mahali fulani kwenye kitabu chake alisema alibakiwa na jeshi dogo sana la watu jasiri waliokubali kulishana AMINI (paka walichinjwa na matambiko)na hao ndio aliofanya nao hayo mapinduzi siku hiyo. Mwenyewe alivamia kituo cha polisi akamuua askari na kupora silaha. Angalia hiyo video niliyopost inaonyesha kabisa aina ya bunduki zao. Ni zile askari walikuwa wanalindia wafungwa for so long. Haiwezekani hizo ziwe zile zilizoagizwa Algeria. NO WAY.

Kama unaweza kuwahisi waingereza kutoa msaada ni kule kupunguza maofisa polisi wazungu toka 26 hadi 5 wakati hayo yanatokea. Kwenye kitabu cha marehemu Ali Muhsin amelaumu kuwa hao wazungu walienda na fungo za ghala ya silaha kiasi kuwa siku hiyo askari walikuwa wamebeba silaha tupu. Japo, hii pia inaweza ikawa ni matayarisho ya yale mapinduzi toka bara.

Ukizingatia kwamba Karume, Babu, na wengi tayari walishaondoka zenj same week kuwa Dar. Inaelekea hawa viongozi walikuwa wanatarajia mapinduzi, sawa, lakini for sure sio haya ya Okello. Ndio maana mwandishi anatoboa kuwa ya kwao (ASP) ambayo Tanganyika (Nyerere) angesaidia ilikuwa yafanyike wiki moja BAADAE. Ni kwamba Okello aliwakata bogi. Kwa maana hiyo kulikuwa na siri ndani ya siri. Mwandishi ameeleza wazi kuwa Okello hakutaka kuwaamini wanasiasa juu ya mpango wake.

Sasa kama watu wameshapindua huwezi sema sisi tumepanga yetu. No wonder wao walitumiwa post zao za urais na uwaziri over the radio na kama hayo bila kutarajia. Na hiyo explains why in the long run huyu Okello lazima angekuwa an embarassment kwao kwa vile wewe utakuwa rais, sawa, lakini aliyepindua ni huyu, sasa who is the king here?

Kwenye kitabu chake, Okello yupo bitter na jinsi Nyerere alivyom-handle na kum-mislead hadi kufikia akafukuzwa kwenda kwao Uganda. Analalamika kuwa hakuwa mkweli kama alivyompima Kenyatta. Sasa kama ingekuwa wao ndio waajiri wake, for sure lazima angebaki loyal kwao na asingekuwa tishio kwa serikali iliyofuata baada ya mapinduzi. Lakini the fact kuwa ilibidi aondoke ni ushahidi kuwa viongozi wa ASP wasingeweza kutawala vyema in his presence. Katika hiyo video wanampa credit Mr. Hanga kuwa huenda alishirikiana na Okello, lakini inawezekana ilikuwa in the absence ya viongozi wengine wa ASP kujua.

Haya ya kuua watu wengi, yeye Okello aliyasema "SIKU HIYO KADRI YA WAARABU 13,000 waliuwawa. Sio WAISLAMU. Waswahili na wazungu walibaki salama. Ulitakiwa kuvaa au kuninginiza kitambaa cheupe. Testimony ya chuki za Urangi. Kwa hiyo Zenj palishagawanyika na infact hata jina la ASP linaonyesha kuna jamii ya watu fulani walishajihisi wanyonge. Huu ulikuwa ni Urangi na Ukabila hakuna dini hapa. Wote walikuwa Waislamu pengine kasoro OKello. Ni sawa na nyakati za Zimbabwe, Angola, South Africa (Christians versus Christians). Hii kuua ya waislamu ni recent politics. Kama vile zimbabwe umlaani Mugabe kuwa ZANU-PF waliuwa Anglican Christians (white settlers) katika kujikomboa.
 

Asante sana mkuu kwa maelezo murua,


Naaaaam mnakasha sasa umeingia patamu,

Kuna jambo ambalo nafurahi kuona mkuu umetembea kwenye akili yangu,

Kwanza tutambue katika kile kilichoitwa mapinduzi,

Li pinduzi lipi la kwanza?

Ni la Okello?

Ni Kasim Hanga?

Je Karume aliongoza mapinduzi yapi?

ASP lifanya nayo mapinduzi yake kama mwandishi anavyoeleza katika video hii ama waliamua kuunga mkono yale ya Mungu wa Afrika (Okello)?

Ikiwa siyo, hebu tubainishe kwa uwazi kuingia kwa Mzee Karume akiungwa mkono na Tanganyika kulikuwaje?


Hapa namuona Hanga nae akitajwa kuwa ni kiongozi wa kile kilichoitwa Mapinduzi,

Je yeye alisimama na Okello ama na Karume?
 

Asante sana Mohamed Said kwa maelezo murua,

Lakini umeleta ladha tofauti katika suala hili,

Naolo ni Kasim Hanga!



Naaaaam mnakasha sasa umeingia patamu,


Kwanza tutambue katika kile kilichoitwa mapinduzi,

Li pinduzi lipi la kwanza?

Ni la Okello?

Ni Kasim Hanga?

Je Karume aliongoza mapinduzi yapi?

Kipi kinachoitwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar?

ASP ilifanya nayo mapinduzi yake kama mwandishi anavyoeleza katika video hii ama waliamua kuunga mkono yale ya Mungu wa Afrika (Okello)?

Ikiwa siyo, hebu tubainishe kwa uwazi kuingia kwa Mzee Karume akiungwa mkono na Tanganyika kulikuwaje?


Hapa namuona Hanga nae akitajwa kuwa ni kiongozi wa kile kilichoitwa Mapinduzi,

Je yeye alisimama na Okello ama na Karume?
 
"Nitashangaa kama watanzania hawataasi kutokana na kudhulumiwa na watawala wa leo, ndio nitawashangaa, na watakuwa ni wajinga na wapumbavu" nukuu ya Julius Nyerere 12/3/1992

Swali kwako Ritz,

Je mwalimu alitukana?

Yericko Nyerere,

Hapo si tu yakuwa Nyerere aliwatukana mno WaTanzania, bali pia makusudio ya matamshi/matusi yake yanaashiria ni mtu aliekuwa anataka kuleta chokochoko,uchochezi na ukosefu wa amani kwenye nchi.

Labda tu,kwa hayo matusi yawezekana kusamehewa kwasababu yeye Kiswahili ilikua si lugha yake ya asili japo alikuwa akijitahidi mno kufurukuta nacho.

Hizo ni dalili za "Kiongozi" alopoteza dira kabisa ndani ya kichwa chake. Kiasi yakuwa alikua haoni tena hata hatari na athari ya matusi na matamshi yake,na nini yaweza kuwa nakma na machafuko kwenye nchi. Kiongozi yeyote responsible,asingeweza asilan kutamka hayo majambo hadharani,hasa ukizingatia sababu kadhaa za mazingira ya wakati huo.

Acha,kutumia emotions na mahaba yako juu ya Nyerere;kwa hili nakusuhi ipitie tena hiyo comments halafu zichambue kwa kina,huku ukizingatia influence ya Nyerere hapo Tanzania na hali halisi ya nchi wakati yeye Nyerere anatoa matamshi yale.

Shukran.

Cc;Ritz
 

Yericko Nyerere,

Kwa ihsan yako,naomba utuorodheshee vitabu vyoote ulivyosoma na kupitia wewe binafsi kuhusu hayo "Mapinduzi ya Zanzibar".

Kama pia kuna sources nyingine zozote pia ulizopitia tafadhali tufahamishe...kabla hujenda mbali saana na haya mambo ya Zanzibar.

Shukran.

Cc;Ritz,The Big Show,Sheikh Mohammed Said,JokaKuu
 

Taratibu mkuu,

Sijui hapo umekusudia nini maana mjadala huu kuhusu kile kinachoitwa mapinduzi matukufu ya Zanzibar unahitaji utulivu na hekima ili kutoingiza itikadi za kidini

Umenihoji kiimla mno ndugu yangu,

Lakini mimi nimelelewa na kufunzwa katika mafundisho mema, hivi nitakujibu kama ifuatavyo!

Nimesoma kitabu cha Dk Harith Ghassany ambacho hata mzee wetu Mohamed Said anatumia kama rejea,

Pia nimesoma maandiko ya watu wengi sana ikiwemo video za mapinduzi hayo na nk!

Mfano nimemsoma Okello akizungumza yake ya moyoni,

Nimemsoma Bargash nae anazungumza juu ya mapinduzi hayo,

Lakini kila mmoja akibeba dhana yake, ndiomana hata hapa ukimsoma Wickama na Mohamed Said utaona wanatofautia katika dhana!

Vivyo hivyo Mwanakijiji nae anamtazamo wake katika suala hili na mimi pia ninamtazamo wangu!

Naaam jf ni uwanja mpana, sasa ni wakati mnasibu kukutanisha fikra zetu na kujenga mtazamo chanya juu ya mapinduzi ya Zanzibar na dhana yake!
 

Yericko,

Makusudio yangu ilikua kutaka kujua ni kwa kina kipi unayajua na kubobea nayo matata na maafa ya Zanzibar kabla na baada ya hayo "Mapinduzi ya 1964",na nini athari zake mpaka hii leo. Ili mtu ajue hayo mambo,ni muhimu pia kuijua kiundani historia halisi ya Zanzibar tangia karne nyingi zilizopita,tena kwa mitazamo na vina tafauti.

Nashukuru umenifahamisha huo uelewa wako kiduchu. La muhimu kwa sasa mpatie fursa Sheikh Mohammed atunyambulie kiundani kwa faida ya soote.

Ahsanta.
 
Ritz,
Katika historia ya TANU kuna mambo TANU yenyewe ilikuwa wanayaogopa
na hili limekuja kurithiwa na CCM.

Sheikh Suleiman Takadir anaogopwa kama vile anavyoogopwa Abdu Sykes.
TANU haikuipenda kueleza michango ya wazalendo hao.
Abdu anaogopwa kwa lipi? Hakuwahi kuwa KIONGOZI wa maana wa TANU iliyoundwa tarehe 7.7.1954 mbali ya kuwa muasisi wake kama wale wengine 16.

Mzee Mohamed, unamkuza sana Abdu bila sababu. Afadhali hata mdogo wake aliwahi kuwa Balozi wetu Italia kuliko Abdu ambaye baada ya kushindwa Urais wa KWANZA wa TANU ni kama alijing'atua kwenye siasa hadi kufariki kwake.
 

Wild Card,
Abdu Sykes alihofiwa kuwekwa katika historia ya TANU kwa sababu
yeye alikuwa na mchango muhimu kuifikisha TAA pale ilipofika na
TANU ikaasisiwa.

Kama unavyoona hapa nilipomrejesha Abdu katika historia kurudi kwake
kumewaleta wazalendo wengi na visa vingi katika historia ya TANU.

Katika hali kama hii yeyote atakaesoma habari za Abdu hataacha kuguswa
na mchango wake pamoja na ndugu zake wawili na baba yao katika kuipa
Tanganyika mwelekeo.

Historia ya Abdu haikupata kuwa ya kugombea nafasi na kupanda jukwaani
kuhamasisha.

Historia ya Abdu Sykes imejengeka zaidi katika kukujenga chama cha TAA
kisha TANU na katika kumpa Nyerere kila aina ya msaada katika Dar es Salaam
ile ya mapema 1950.

Nadhani utakumbuka mzozo wa "chumba cha Abbas Sykes" na "kabati la fedha
la Abdu Sykes."

Wapo katika TANU baada ya uhuru wakichomwa nyoyo na roho kuuma kwa historia
hii.

Kwa sababu za uchungu huu ndiyo maana historia ya Abdu Sykes ikawa inaogopwa
kuingizwa katika historia ya TANU lau kama mikutano ya siri wakifanya nyumbani
kwake Aggrey Street au nyumbani kwa mama yake Bi. Mluguru biti Musa Kirk Street
na hela ya kuendesha chama akitoa yeye.

Ukipenda nilirefushe darsa nifahamishe In Sha Allah.
 

Gombesugu,
Profesa wangu alinitaka nimpe reference ya jambo nilosema
kuhusu historia ya TANU.

Jibu langu lilikuwa mimi ndiyo hiyo reference.
Kapata mshtuko.

Nikamwambia hayo nilosema yamefanyika nyumbani kwetu
na babu yangu mwaka 1947 na wala hapo hajasikia jina la
Nyerere.

Yericko anategemea maandishi sisi hao walopindua ni ndugu na
jamaa wa wazee wetu.

Nimeweka hapa jamvini kisa changu na Ali Nabwa.
Nani atayajua mapinduzi ya Zanzibar kumshinda Nabwa?

Mimi Nabwa ni rafiki na ndugu yangu.
 

Yericko,
Nitakujibu la Hanga na nguzo yake alosimamia.

Hanga alisimama na Oscar Kambona.
Kambona alikuwa akimwakilisha Bwana Mkubwa.

Imetosha au niongeze?
 
Yericko,
Nitakujibu la Hanga na nguzo yake alosimamia.

Hanga alisimama na Oscar Kambona.
Kambona alikuwa akimwakilisha Bwana Mkubwa.

Imetosha au niongeze?

Nitakushukuru ukifafanua kwamapana zaidi usharika wa Kambona na Hanga na tofauti yao na Mungu wa Afrika ambae mimi namuona kama ndie Baba wa Taifa la Zanzibar!

Kati yao yupi aliyeongoza kufanya mapinduzi ya mwanzo?

Ni Okello au Hanga+Kambona?
 

Jasusi,

Kama unadai yakuwa ulishavisoma vile vitabu vyoote na source nilokuorodheshea,sasa kwanini ulileta ile misleading statement/"analysis" hapa jamvini!?
Huoni ile statement/"analysis" yako ingeleta sura nyingine na isiyo ya ukweli kwa mtu asiejua/asofuatilia kiundani historia ya JFK,Martin Luther KingJr. na Civil Rights Movement?


Zile harakati za kummaliza Lumumba zilikua ni ndefu na zilihusisha watu/mataifa kadhaa,hata baada ya huyo Lumumba mwenyewe kuwa alishatoweka hapa duniani.

Kuhusu habari za tarehe,tumshukuru pia Sheikh mohammed pale alipoingilia kati kuturekebisha kiduchu. Ndo barka za kuwa na Watu Wazima wenye hikma na busara hapa jamvini. Kwa maana hii ule "mpini" wangu woote wa mwanzo unastahiki kusimama vilevile na palepale.

The main aim was to sabotage and eventually destroy Lumumba's ideology within the mass movement of peasants,workers,the urban unemployed,students and lower civil servants under the eager leadership among Lumumba's lieutenats,most of whom had regrouped to establish a National Liberation Council-CNL in Brazzaville.

Since Lumumba's physical elimination had removed what the "West"(the US,UK and Belgium in particular) saw as the major threat to their interests in the Kongo. "Internationally"-led efforts were undertaken to restore the authority of the "moderate" and pro-Western regime in Kinshasa over the entire country.

These resulted in ending the Lumumbist regime in Kisangani,the secession of south Kasai and Katanga secession end of 1965.

Tunajua kwa yakini yakuwa mwanaharakati mahiri hata akiuwawa au kutoweka,lakini cheche zake huwa si rahisi kuzimwa kwa kipindi kirefu mno kama si milele.

Tuna mifano ya Chavez na Venezuela,Cuba na Che Guevara,Vietnam na Ho Chi Mihn,Iran na Ayatollah Khomein,Sudan na John Garang na leo tupo hapa jamvini kumsikiza Sheikh Mohammed juu ya Tanganyika/Tanzania na Abdilwahid Sykes.


Kuhusu,hiyo habari ya Matabeleland italazim tuifunge. Maana sasa unadai yakuwa huna/umeishiwa na facts!? Sasa kwanini uliingia kwa kishindo kikubwa vile ndani ya hoja bila kuwa na facts za kina!? Haina neno nafikiri nilivyochanganua mimi inatosheleza kwa sasa.


Kwa kifupi, sio siri yakuwa Nyerere's regime was harsh and extremely secretive possibly similar to that of his own idol Kim Il Sung of North Korea. The only way/method we can know many things and atrocities is through credible sources,as there's no definitive answer to many questions/atrocities.

Ndo maana hata Nyerere mwenyewe hakuthubutu asilan kuandika Biography yake,sababu alijua kuwa his entire political life was full of contradiction. Kama asemavyo Sheikh Mohammed;hata huyo Nyerere angetaka kuandika/kujibu je angeanzia wapi!?

Kuhusu hicho kitabu cha Dr. Ghassany;nakukumbusha yakuwa mwandishi wa kitabu hicho hicho pia ndie aliekua mwandishi wa ile paper iloletwa hapa jamvini kutoka google search na Wickama ikielezea harakati za Mufti Sheikh Hassan Bin Amir.

Nafikiri unakumbuka jinsi wewe binafsi na wenzio; mlivyokua mkipiga chereko,vigegele,vifijo na nderemo kushangilia jinsi Wickama alivyokua akimnyambua Sheikh Hassan Bin Ameir kwa kashfa,na huku akimwita ndumila kuwili,mrongo na kebehi nyingine kadhaa kwa kutumia paper iloandikwa na huyo Dr. Ghassany!?

Sasa inakuwaje leo unamkataa mwandishi huyo huyo Dr. Ghassany,kisa kazungumza mambo usotaka kuyasikia!? Hujui yakuwa unapokua selective kwenye masuala haya utapunjika kwa mengi!?


Hiyo habari ya Jacqueline Kennedy,kwa kifupi ilileta rabsha na athari kadhaa wakati huo. Mtu yeyote mwenye akili timamu na kuyafahamu mambo haya,hawezi asilan ati kudharau kauli za Jackie Kennedy kwa wakati huo,na hasa ile impact na effect ilosababisha.

Kwa kuwa wewe nasikia ni mtu wa Chadema nakuuliza suali kiduchu;hivi kauli yoyote atakayotoa leo hii Mke wa Dr Padri Slaa kwa Rais Kikwete itakua haina uzito au haitaleta rabsha zozote!? Halafu unajua fika jinsi gani wenzetu wa siasa na media huku nchi za magharibi wanavyofuatilia na kushabikia masuala kama haya. Kwa hili nafikiri tuwaache wengine wapime hapa jamvini...

Hizo habari za race issue in Amerika nakuachia mwenyewe na hizo stereotypes na prejudice ulizonazo. Hii ni haki yako ya asili kama mwana-Adam.

Shukran


Cc;Ritz,Nyambala,JokaKuu,Sheikh Mohammed
 

Wickama,
Okello atafika vipi Kipumbwi na yeye si key player?

Pale alikwapo Victor Mkello, Mohamed Omar Mkwawa
na Jimmy Ringo.

Kipumbwi pakilindwa kama "War Zone."
Hapaingiliki ovyo.

Mamluki wakifanyishwa mazoezi pale na katika watu
walokuwa wanajua kinachoendelea pale ni Jumanne
Abdallah alokuwa Mkuu wa Mkoa na Ali Mwinyi Tambwe.
 

Yericko; Mimi sio authority kwenye masuala haya. Ila kwa kila atakayeangalia ule mkanda wa video na akajakuta huko mbeleni bwana Hanga anapata matatizo, sio taabu sana kuichorea ramani. Hii ni ramani yangu ya matukio-fikirika na HUENDA ikawa 100% WRONG;

1. Kwamba Hanga anashiriki kuvamia vituo vya mapolisi na kupora silaha na ... kupindua bega kwa bega na Okello (hii inaelekea ndivyo-angalia hiyo video na msikize mwandishi)na pengine aliyapanga haya na Okello kibinafsi bila ridhaa ya chama kuogopa leakage (possible, sikiliza mkanda)

2. Kisha, Hanga bado anaitii ASP na kuwaita mabosi wake kwa kushirikiana na Okelllo warudi waongoze zenj (inaelekea ndivyo). Okello hana chama cha siasa zaidi ya Mungu wa Waafrika!!!!!.

3. Hanga anabakia makamu wa rais, Okello karidhika rank ya Field Marshall na Rais ni mwingine (Karume). Mazingira haya lazima yanajenga aina ya uswahiba na kuheshimiana sana kati ya Hanga na Okello. Wote ni mashujaa.

4. Ghafla Okello anafukuzwa, sababu hazieleweki vizuri. HII LAZIMA ILIWAUMA WALE WALIOKUWA MSTARI WA MBELE WA MAPAMBANO NA YEYE WAKATI WA KUPINDUA.

5. Mazingira hayo yanazaa fitna na mashaka na kutoaminiana kati ya wale waliomfukuza Okello na wapinagaji wake. Recall, wengine walichinja nae paka nk.

6. Okello keshafukuzwa, jee, ukituhumiwa kuwa unawasiliana nae, itakuwaje!!!!!

7. Ukishafikia hapo YERICKO una makundi mawili. Moja linaona; jamani sisi tumepambana mpaka kukomboa hii nchi, sasa hawa jamaa mbona wanatubana hivi? wameshamfukuza kamanda wetu. Hawa jamaa hawana fadhila bora hata tusingewaita toka Dar. Tungetawala sisi.

8. Wengine wao watakuwa wanahofia yao; hawa washenzi wanamlilia Mganda wao .....ngoja tuone

9. Nani atatangulia kuuliwa na nani ni SANDAKALAWE ......AMINA.......

10. Bwana KATWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE

Kwa hiyo naamini Hanga alikuwa mtiifu na alisimama na Karume kwa kigezo cha mkanda huo nilio-post. Lakini kiongozi hufanya mambo kwa ushauri wa waliomzunguka. Hakuna anayejua ushauri wa mbeleni aliopewa Karume au yeyote juu ya huyu bwana.

Hii ni dhana binafsi na inaishia hapo. Huenda ni wrong by 100%.
 

Wickama,
Wenyewe Wazanzibari wanasema huku wakicheka kuwa Okello
alivishwa blanketi na likamwenea khasa na akalipenda.

Kwa nini alipende blanketi?
Sababu alikuwa mjinga.

Alidhani yeye ni Field Marshal wa kweli kumbe wenzake
wamemfanya karagosi.
 
Wickama,
Wenyewe Wazanzibari wanasema huku wakicheka kuwa Okello
alivushwa blanketi na likamwenea khasa na akalipenda.

Kwa nini alipende blanketi?
Sababu alikuwa mjinga.

Alidhani yeye ni Field Marshal wa kweli kumbe wenzake
wamemfanya karagosi.

Ohhh, Gosh I like this.......... you can be funny haya bwana. Good day.

cc Yericko
 

Sheikh Mohammed,

Salaam Al Khiy.

Mimi nakufahamu kwa utuvu mwingi,ndo maana kuna wakti hucheka peke yangu pale jamaa wakijaribu ati kufurukuta na wewe.

Kweli dunia ina vihoja...ati leo atokee mtu kuitwa Yericko na akae kilingeni kushindana na wewe khabari za Zanzibar!?

Lakini,nilimpa tahadhari kiduchu asubuhi hii nafikiri kanifahamu.

Insha Allah Mola taongeza sabra, na naendelea kukusoma kwa utuvu. Nimeiona pia ile barua ya Bwana Ali Sykes ulotuwekea kiduchu hapa jamvini.

Nimeona pia ile khabari yako ya Guitar na Piano. Mimi yoote hayo taabani,lakini mara chache hupiga drums. Lakini Wifey hapa ni mzima saana wa Piano. Siku ukijaaliwa kututembelea hapa nitafurahi mno kukutanisheni,nami nipata wasaa kukusikilizeni umahiri wenu!ahaha!!

Nakumbuka Babu Shariff Abdallah Al Attas;aliwahi kunipa kisa fulani cha safari ya Lebanon miaka ya sitini...kuna mmojawapo kati ya mabwana Ali,Abdilwahid au Abbas nasikia alikua ni mahiri kwa kupiga saxophone. Aliwashangaza saana jamaa pale Lebanon kwenye Concert; wakti alipopewa na kucharaza saxophone kwa ustadi mwingi...Wallahi wakti unakwenda zake!

Ahsanta.
 

Mzee MS; You???? again!!! Looks like ulikuwa ume-delegate!!!!!! to a young colonel???? my condolences for the temporary set. Let me laugh back. Ohhhh, No the glass is actually half empty not half full!!!!!
 

Sheikh Mohammed,

Hivi Bwana Ali mwinyi Tambwe yuhai vile!? Kitambo kikubwa sijapata kukutana nae wala kumsikia...

Ahsanta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…