Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Wickama, MS na wengine,

Mtazamo wa mapinduzi Zanzibar unakinzana sana na kila msimuliaji wayo,

Lakini kila msimliaji katika andishi lake ni lazima amtaje Okello kama ndie aliyeongoza mapinduzi ya mwanzo kabisa na kufuatiwa na sinitofahamu nyingi sana hapa katikati mpaka kuingia kwa Karume mkubwa nakuitwa muasisi wa Mapinduzi,

Ukisoma kila pepa na ukipata simulizi za wahafidhina wa Zanzibar bado hupati nyota ya Karume ilianzia kung'ara wapi hata kuingia katika Mapinduzi haya!

Nayatazama hivi Mapinduzi ya Zanzibar!


Ndani ya Zanzibar John Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi wa meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri.

Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.-

Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu.

Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja.

Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid- akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.

Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.

------------- ?
Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo.

Kuliibuka makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbalimbali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhini ya- fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi- ya pazia la nyuma- la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika lakini hapakuwa na mtazamo wakidini.

?

John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello.

Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi.- Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Jee, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali?- Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono?- Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo?- John Okello alichezesha dadu usiku huo wa mwezi wa Januari.

-

Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo walikuwa mjini Dar).- Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi.- Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa na shuku ya kukata fundo hilo- gumu la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala.-

Hawawalitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao.- Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani.- Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana.

-

?Baadhi ya viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa- "Mapinduzi".- Makundi ya watu wenye fujo yalikuwa huru.- Sheria na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.

Walimiliki- ardhi na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na mauaji yalienea mji mkongwe mzima.- Kwa kweli mji wenyewe uliporwa.

-

Waarabu na Waasia , waliokuwa- wakiunga mkono vyama vingine waliuliwa kwa makundi.- Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyingine baadae maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.

-

?John Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani zake zenye nguvu kijeshi walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba.- John Okello alitangaza vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga yeye.-
John Okello aliamini alikuwa akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza ujumbe ufuatao." Serikali sasa inaendeshwa na sisi… ikiwa mtakuwa wakaidi na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua ninazozichukua hivi sasa" na- "Na ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya wengine….sitokuwa na njia nyingine lakini kutumia silaha nzito.- Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000".

-

Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo.- Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha

"Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na Pemba…Nafikiria kuelekea kijiji cha Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri.- Baada ya dakika 40- nitawamaliza nyote hasa- Wangazija", "na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi, Nitapita Malindi nikiwa nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo.- Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini.- Nataka kuwaona wao wanaimba... Baba wa- Waafrika.- Mungu Mbariki yeye na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu"

-

?Wakati unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za- Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika.- Taifa la chama kimoja lilitangazwa.- Lakini bado Taifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani waliokimbia nchi.- Kile kilichoitwa "wanamapinduzi" hawa baadae walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano wa Tanganyika.- Hii ingeruhusu maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa baadae katika visiwa hivi.- Askari polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni watiifu kwa chama cha TANU na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka ishirini tu
 

Uchambuzi mwema kabisa mkuu,

Lakini ndugu Mohamed Said ameleta sura mpya juu ya hili kwakumhusisha Kambona na Hanga,

Anasema hawa walikuwa bega kwa bega,

Sasa ukiendelea kuchambua na ukisoma maandiko niliyoweka hapo juu unaona kuwa Okello alisimama pekee yake baada ya Sultan kufariki mwaka 1960,

Hivyo bado utata wa hawa wanaotajwa kuwa wana ASP waliokimbilia Dar, walirudije na kuwa sambamba na Mungu wa Afrika ilihali jamaa hakuwa na chama?
 
Mzee Mohamed,

Simulizi hii ya Mwalimu na Abdu kama ya Jakaya na Rostam! Mwalimu aliukana utajiri tangu enzi hizo hadi anafariki hana kitu pamoja na kuwa madarakani kwa zaidi ya miongo miwili.

Nadhani hata Jakaya atakaposimulia namna alivyoupata URAIS wa Jamhuri hatamtaja Rostam.
 
Ohhh, Gosh I like this.......... you can be funny haya bwana. Good day.

cc Yericko

Wickama,
Ingekuwa Okello anaijua historia ya Field Marsha Tito
asingethubutu kujiita cheo hicho.

Lakini masikini ya mungu kazi yake ilikuwa kufyatua
matofali Pemba kwa Mazrui.

Sasa ghafla kuja kupewa radio ndiyo lile blanketi akaona
amepata kumbe amepatikana.
 

Wild Card,
Tafadhali sana usiniharibie script ya movie yangu.

Kwanini usimtaje Prof. Malima kama opening scene?
Kisha unapiga "cut!" ya nguvu.

Tunaingia scene nyungine...

Rostam anaingia baadae mambo yamewiva.

Sikiliza WC umesikia jamaa wanawatafuta wachochezi wa
kwenye mitandao na wewe unanichokonoa niseme...

Unataka uje uniletee juisi Segerea?
 
Kama kawaida yako Mzee Mohamed. Huyu bwana angekuwa Muislam bila shaka yoyote simulizi zako zingekuwa tofauti kabisa! Kwa kuwa ni Mkristo lazima aondolewe awekwe Kassim, Ali,...,

DINI yako imekudhibiti sana. Kumbuka tu kuwa Mungu hana DINI.
 
Sheikh Mohammed,

Hivi Bwana Ali mwinyi Tambwe yuhai vile!? Kitambo kikubwa sijapata kukutana nae wala kumsikia...

Ahsanta.

Gombesugu,
Ali Mwinyi amefariki miaka mingi sasa na bint
yake Tanisa nae kafariki Ujerumani.

Mie ndiye mtafiti pekee ambae Ali Mwinyi alikubali
kuzungumzanae.

Ni kisa kirefu.
In Sha Allah tukionana nitakupa kisa hicho.

Hakika Allah anapolitaka lake huwa.
 

Ukisoma kitabu cha Okello yeye anajuta kuwaamini hao jamaa. Alidhani wapo pamoja. Wakina Karume walirudi na boti yenye glass bottom. nadhani kwa fadhila za Julius. Sikiliza huo mkanda. Kwa kweli sijaona ushahidi wa moja kwa moja wa kumhusisha Okello na kambona. sababu ni silaha. Silaha za bara (hizo za kutoka Algeria hazingeweza kuwa hizo za kulindia wafungwa) just have a look at the video. Ziangalie na kisha useme kama ni silaha za nchi kwenda kuiomba nyingine. Automatic rifles zilikuwa hazizidi 5 na hizo walizipora makao makuu ya polisi, moja akabaki nayo okelo. Hizi sio silaha za kina kambona. Kisiasa ni aibu kusema mganda kawapindulieni nchi then kawapeni. Ni embarrassment. Lazima msimame kuwa ni nyie. Lakini sasa ile idadi ya waarabu (raia wasio na silaha iliyouwawa) ndiyo inayofanya mpaka kesho hata ASP wawe low-key nayo; vinginevyo unawezaitwa the Hague kwa crime against humanity. Nadhani you can get his book through established facilities kama Amazon.
 
Kama kawaida yako Mzee Mohamed. Huyu bwana angekuwa Muislam bila shaka yoyote simulizi zako zingekuwa tofauti kabisa! Kwa kuwa ni Mkristo lazima aondolewe awekwe Kassim, Ali,...,

DINI yako imekudhibiti sana. Kumbuka tu kuwa Mungu hana DINI.

Wild Card,
Mie nakueoeza niyajuayo.
 

Wickama,
Hizo bunduki zilikuwa za Ben Bella.

Aliulizwa na Dk. Ghassany uso kwa macho.

Iweje uwape silaha watu wanaopigana na nduguzo Waarabu?

Jibu la Ben Bella ni kuwa wale walikuwa maadui zake sana
kwa kuwa walikuwa upande wa Waingereza wakandamizaji
watu.
 
Ah! Haya bwana. Najua unajua mengi ukiuvua Uislam wako kidogo ukaitazama Tanzania na WATANZANIA kama watu wamoja.


Umeusikia ule msiba wa Geita ambao ng'ombe alishindikana kuchinjwa?
 

Mzee MS; kwenye huo mkanda Okello kapewa a direct credit ya kuvamia headquarters za police station, killing a sentry, breaking into the arms store and distributing the guns to his soldiers. Another credit kapewa ni ya kumchukua a politician at gun point kuwapeleka kwenye kituo cha radio. Vyeo apart, LETS GIVE THE DEVIL HIS DUE, HE WAS BRAVE TO HAVE RISKED HIS LIFE WAKATI WENGINE WAPO SALAMA ACROSS THE OCEAN. TOFAUTI NI HIYO Of course na yule Mungu wake wa Waafrika!!!!!!!
 

Yericko,
Nisome kwa makini.

Nimesema Hanga alikuwa na Kambona na Bwana Mkubwa.
 

Umeziona hizo bunduki mzee MS? Please revisit ile video link. Nimepitia JKT na najua huku bara zilikuwa zinatumika prisons hadi miaka ya hivi karibuni. Sio bunduki za nchi kuiomba nyingine. Hata za Mgulani JKT zingekuwa bora.
 

Hehee daah,

Nilionya mwanzo kuwa tunapoingia kwenye suala hili la Mapinduzi ya Zanzibar ni vema kuwa watulivu na wastahimilivu,

Tukiruhusu hisia za kibinadamu zitutawale bila shaka tutatekwa na mitazamo hasi ambayo dhahiri ni UDINI

Sasa kwa aina hii ya mtazamo wako kwa Okello ni dhahiri kuwa dini yake ndio veto kwako mkuu!
 

Gombesugu,
Saxphonist alikuwa Ally Abdu yeye akipiga Clarinet
na Abbas guitar.

Mzee Matesa drums, Said Kastiko bass, Msikinya nadhani
piano, Dome Budohi Drums,Khomo sax, Martin trumpert.

Hii ni bendi yao watoto wa Gerezani ikiitwa The Skylarks kisha
ikaitwa Blackbirds kisha Shell Merry Makers.
Hiyo ni 1947/48.

Khomo na Msikinya walikuwa wanatoka Afrika ya Kusini.
Budohi na Martin wakitoka Kenya.

Band Patron Kleist Sykes na ndiyo alowanunulia wanae vyombo
vya muziki.

Hawa wote nimewaona wengine wakija nyumbani.
 

Mohamed Said,

Nikisoma mipini yako kuhusu mapinduzi ya Zanzibar walaahi najisikia mustarehe.

Kituko Yericko naye anajitokeza kuchambua mapinduzi ya Zanzibar nabaki nacheka sawa sawa watu tunakula Mandi ya mbuzi anatokea mtu analeta ugali wa udaga na furu...ha haaa.

Ukimuuliza Yericko, John Gideon Okello amefariki lini hajui.

gombesugu,
 
Last edited by a moderator:
Umeziona hizo bunduki mzee MS? Please revisit ile video link. Nimepitia JKT na najua huku bara zilikuwa zinatumika prisons hadi miaka ya hivi karibuni. Sio bunduki za nchi kuiomba nyingine. Hata za Mgulani JKT zingekuwa bora.

Wickama,
Hilo sijui lakini za Ben Bella zilifika zikashushwa Kunduchi.
 

Haaaaaa; this is strange wewe tena????? Mzee MS leo masuala ya Qadar vipi? Kama wanatafuta watu ni kwamba saa hizi tayari wanasoma pages na pages za huko nyuma za miaka. Hawa wakina JF kazi yao ni kutoa address husika ya computer iliyotumika (ndio kazi ya wanachoita cookies!!!!!). MS hata uiuze, aliyeinunua mwisho wa siku atakufata na jamaa wamevaa miwani za jua. Wewe endelea, na thread wakati unasubiri Qadar Sheikh hahahahah
 

Ulionya wewe nani? Kwa hiyo wewe ulitaka mtu ambaye ni Muislam asipingane na Okello?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…