Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Acha uongo si ujibu umeambiwa waislamu wakiambiwa ukweli wanakasirika, eti unawaheshimu yaani heshima ni bora kuliko ukweli funguka acha ubabaishaji.
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kunitajia marais wangapi duniani ambao ni Wakatoliki ambao wamekidhi vigezo ivyo na kutangazwa wenye heri kisha watakatifu.
Ritz,Hata hiyo hatua ya Mwalimu kuitwa Mwenye Heri haijafikiwa. Ni kazi ngumu sana kuifikia hatua hiyo kuliko hata kutangazwa Mtakatifu.
 

Mkuu Ngongo,

Sidhani kama huu mnakasha unaelekea ukingoni bado ni endelevu kuna mambo mengi sana wanaukumbi wanaitaji kupewa darsa.
 
Last edited by a moderator:
Vipi kuhusu ukubwa wa taasisi kristo(Uwingi wa wakristo na mataasisi,miradi mbalimbali wanayoiendesha kuisaidia jamii-vitu ambavyo hupelekea kuomba misamaha ya kodi mfano vituo vya watoto yatima,makanisa,vyuo,mashule nk) ukilinganisha na ukubwa wa taasisi islamu(uwingi wao na upana wa wigo wa mambo wanayo yafanya)? Vipi kuna upendeleo wowote kwa taasisi za kiislamu zinazotoa huduma kwa jamii au misikiti kukataliwa misamaha ya kodi wakiomba serikalini? Ahsante!
 

Yericko,
Kuna mengi sana ya kusimulia katika haya kwani siku ya mapinduzi mimi nilikuwepo kabisa na niliona kila kitu namna tulivyozuiliwa watu wa shanghani tusitoke mjini.

Sikubaliani na wewe hata kidogo unapoita mapinduzi ya OKELLO. Tujiulize Okello mmoja aliweza fanya mapinduzi hayo pekee kuanzia mjini mpaka ng'ambu? au alitumika kama Muwa tu baada ya kuisha utamu unatupwa.



 
zomba,a.k.a Mzee wa hints...!
Naona umerudi kwa kishindo wengine washaanza kupata stress...!!
 
Last edited by a moderator:

JokaKuu

Salaam. Sijakusikia kitambo ndugu yangu.

Niwie radhi kwa kuingia kati ya suala lako kwa Al Akhiy Kadogoo.

Hilo suala la Biafra,napingana na wewe kwa kina kingi mno. Hizo elements za ukabila yawezekana zilikuwapo lakini zaidi ile ilikua ni vita ya Udini. Nina sababu na facts kadhaa,ambazo nitazibainisha Insha Allah wakti wake kifika.

Kumbuka mimi nawe tuna ile miadi ya ile thread yetu nyingine kuhusu masuala ya Mozambique na Nyerere. Nafikiri kwa sababu zilezile tuliuzokubaliana awali kusitisha kwa muda yale majadiliano yetu,pia tufanze kwa jambo hili. Nafikiri mle tutapata kuchanganya mawazo,fikra na majambo mengi tutakayo,khasa kuhusu "Mtakatifu" Nyerere na Afrika...sabra huvuta kheir!

Labda kabla sijakwacha,nipa fursa kukuuliza visuali kiduchu ili unisaidie katika ule "mpambano" wetu ujao:

Je unajua au ulipata kusikia ile khabari/fununu ya Nyerere kuhusishwa na yale mauaji ya Eduardo Mondlane pale D'salaam!?

Unajua ni nani alikua OCD na RPC wa wakati ule hapo D'Salaam!? Unajua kwanini hao jamaa walipata "matata fulani" na Nyerere na kupewa instructions makhusus tokea Usalama wa Taifa!?

Unajua ni nani kati ya viongozi wakuu kutoka Police na Usalama wa Taifa waliofika kwa haraka sehemu ya tukio siku ile ya mauaji/mlipuko!?

Haina haja ya kunijibu kwa sasa,nakutayarisha tu kwa ule "mpambano"/"mduara" wetu.

Pia nina miadi na Al Akhiy Barubaru ya thread nyingine kuhusu masuala ya Tanga na mwambao wa East Afrika,itanilazim niwe mindful wa schedulle yangu Insha Allah.

Ahsanta kwa kunisikza huo uchechefu wangu...nipa fursa nikamnyoshee maneno kiduchu nduguyo Jasusi.

Cc;Barubaru
 

Vema sana mkuu, ikiwa kuna mengi yakusimulia uyajuayo kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa fahari kwa wanajamvi kupata elimu hiyo mkuu,

Naaam, Okello pekee ni kweli hange weza kupindua utawala wa kisultani Zanzibar yote,

Alichokifanya ni kutengeneza ushawishi na uungwaji mkono toka kwa makundu ya vijana majabari zaidi ya 300,

Utawala wa Okello pale Zanzibar ulidumu kwa miezi sita, wahafidhina husema ni miezi sita ya mkono wa chuma,

Sasa wewe ukisema Okello si chochote sijui miezi sita hii unaiweka kundi lipi la maisha ya Zanzibar?
 

Jasusi,

Mbona unaleta mambo ya dinner table ya Nyerere's Clan hapa jamvini!?
Yaani mazungumzo ya Nyerere na Wakristo wenzie wana-discuss na kupongezana religious war/conflict at the dinner table ambayo yeye Nyerere amehusika kwa kina...halafu unaleta hayo mazungumzo hapa jamvini ili iwe ndio kianzio cha discussion!?

Kama ni hivyo,haina neno maana nasisi wengine pia tunazo saana hizo stori za "vinyozi wa Kipata na Mkunguni" kama mnavyoziita!

Hivi vitu si ndo siku zote nyinyi mnamkebehi Sheikh Mohammed hapa jamvini!? Mimi binafsi hicho kitabu chako nilipitia kiducu kitambo,lakini nikakitupa sababu yule mwandishi wako tayari alikua na agenda zake!

Zipo sources credible na vitabu vingine vingi kwa mwenye kutaka kujua mtafaruku ule wa Biafra.

Huo ni mtazamo wako binafsi na wenzio. Nyerere aliingia kule kwa mtizamo wa kidini.

Nipa fursa kukuuliza suali kiduchu.
Nahisi wewe ni mmojawapo kati ya wanaodai yakuwa Nyerere hakuhusika wala haku-influence yale maafa ya Zanzibar 1964!? Kwanini unafikiri Nyerere hakufanza hivyo kusikitisha yale mapinduzi haramu dhidi ya ile Serikali ya mseto ilochaguliwa kihalali!?

Ahsanta.
 
Unaweza kunitajia marais wangapi duniani ambao ni Wakatoliki ambao wamekidhi vigezo ivyo na kutangazwa wenye heri kisha watakatifu.

Labda nikufahamishe tu kuwa kigezo cha uteuzi wa Julius Kambarage Nyerere kuingia kwenye mchakato wa kuwa mwenye heri na kisha mtakatifu hakikuwa URAIS wake Tanganyika/Tanzania,

Sababu kubwa ilikuwa ni ukatoliki wake na matendo yake mema kwa dunia!

Lakini kubwa zaidi ni kuwa hili suala haliwahusu wasio wakatoliki, hivyo kulilia kwa kudadisi kwenye mizani yakulipinga ni kuingilia uhuru wa dini nyingine na uhuru wa watu kuabudu!

Hivyo ndugu wewe Ritz muislamu mtiifu kwa mungu wako kitendo chochote utakachofanya cha kikaonyesha kupinga mchakato huo wa kanisa ni kuwa utakuwa unavunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977!

Yakatoliki waachiwe wakatoliki na ya Muislamu waachiwe Waislamu,

Vivyo hivyo ya RastaFari waachiwe MarastaFari na ya Mpagani wa achiwe Wapagani!
 

Ritz,

Salaam,Al Akhiy.

Nasikitika masuali yako/yetu huwa ati wanadai hayaonekani/hawayaoni!? Na hayo uloyaweka hapo juu, ndo ushukuru Mola,maana majibu hakuna asilan. Nastaajabu,ati jana pana jamaa hapa kaorodhesha vile vituko/"maswali" yao ambayo "hayajajibiwa"!?

Mambo mengi na zongo la nyaraka limetanda hapa jamvini lakini ndo uzuri. Kama aalivyousia Sheikh Mohammed,yakuwa na nyinyi leteni hizo Historia zenu tuzione.

Nimecheka asubuhi pita kiasi Wallahi, maana naona imekulazim kumtaka radhi jamaa hapa ati kwa kumshindilia ile "mipini ya roho"!aahaha!! Halafu ukamwongeza na "mpini" mwingine hapohapo!ahaha!! Wewe kiumbe "mkorofi" mno Wallahi!ahaa!

Mbona kuna wengine wanatangaza yakuwa ati shughuli ishakwisha!? Vipi ile khabari ya "uchochezi na uhaini" nayo imeishia wapi...maana mpaka sasa hatujaona lolote wala chochote!?

Basi Insha Allah,wacha nipitie baadhi ya vituko hapa kiduchu.

Ahsanta.
 
Kwa baadhi ya watu humu hakuna jema lolote alilofanya Mwalimu tangu anakuwa Rais TAA baadae kidogo TANU/CCM. Muda wote alookuwa Rais wa KWANZA wa Tanganyika na baadae kidogo Rais wa Jamhuri hii nako hakuna jema alilofanya! -Mapinduzi matukufu ya Zanzibar alishiriki kijinai/kidini; -Uendeshaji wa NCHI, TANU/CCM ulikuwa wa KIDINI; -Ukombozi wa Afrika alikosea sana kote; -Mambo ya Biafra angetakiwa kuwa The Hague; -BAKWATA ndio kabisa alifanya kosa kubwa sana kuua EAMWS; -Ujamaa na vijiji vyake ndio balaa; -Kuungana na Zanzibar ni Balaa;Mimi nadhani hata kuzaliwa kwake ndani ya nchi lilikuwa ni kosa la Mungu!
 

Mkuu naomba nijue mambo machache toka kwako ili twende sawa na mnakasha huu,

Kwanza naomba kujua, Je unatambua Okello ndie aliyeongoza mapinduzi yale?

Pili nikuwa, je utawala mkono wa chuma wa Field Marshal au Mungu wa Afrika kama alivyopenda kuitwa wa miezi sita ndani ya ardhi ya Zanzibar ulikuwa na mkono wa Nyerere?

Hebu naomba ujibu hayo ili tujenge hoja hapo na zijibiwe hoja kwa hoja!
 

Yericko Nyerere,

Nashukuru umeamua kwenda na mimi taratibu,maana unajua akili za Madrassa majambo mengi sisi hutupa taabu kuyajua kwa wepesi kulinganisha na nyinyi wenzetu...

Lile suali nimemuuliza huyo nduguyo kwa maana yangu makhusus...lakina haina neno mindhal umeamua kuja wewe maana natambua yakuwa damu ni nzito kuliko maji.

Hayo masuali yoote mimi binafsi sina majibu yake na wala siyajui,ndo maana nikaanza kwa kumdodosa huyo nduguyo.
Lakini kama dasturi ya hili jamvi letu,naona na wewe badala ya kunisaidia majibu unaniletea furushi la masuali mengine!?

Tumuombe Shariff Ritz,labda aeza kuwa na jibu japo kiduchu...au watoa ushauri gani ndugu yangu Yericko!?

Shukran.

Cc;Ritz
 

Haina neno mkuu,

Sio kwamba nimeuliza kwakuwa sijui, laa hasha!

Nimeuliza ili kama unayafahamu vema basi nipate fursa yakujenga hoja kulingana na majibu yako mkuu!


Kama Ritz atajibu kulingana na maswali yalivyo ni jambo jema!

Nasubiri
 
Haina neno mkuu,

Sio kwamba nimeuliza kwakuwa sijui, laa hasha!

Nimeuliza ili kama unayafahamu vema basi nipate fursa yakujenga hoja kulingana na majibu yako mkuu!


Kama Ritz atajibu kulingana na maswali yalivyo ni jambo jema!

Nasubiri

Yericko Nyerere,

Mimi pia nilishahisi yakuwa jibu unalo kibindoni...maana wewe ni mjuzi mzuri, MwanaHistoria mahiri na mwandishi stadi.

Kwanini tu usitoe ulonalo,mpaka ufanze kwa kutegeshea!? Yakhusu nini kusubiria ilhali jawaba ulinkalia!? Mbona watufanzia inda...watutamanisha khabari halafu wafanza kuringishia!?

Tafadhali fanza kila njia ututoe hii kiu ulotuletea hapa jamvini.

Shukran.

Cc;Ritz
 
Gombesugu,
Kama kuna vitabu ambavyo wewe unaviona ndivyo credible katika suala la Nigerian civil war vitaje ili na sisi tuvidadavue.
Usibanie ilm. Hiki nilichokitaja nilikuta kinakubaliana na yale niliyoyajua kuhusu vita ya Biafra. Kama wewe una sources nyingine unazizipachika jina credible, zimwage hapa sote tuchote ilm. Kama dinner ya Nyerere clan imekuchefua ungechefuliwa siku nyingi na stori za Nyerere kununuliwa chakula Kariakoo. Kuhusu mapinduzi ya Zanzibar sina hakika kuwa Shamte alichaguliwa kihalali. Hayo nawaachia akina Nassor Moyo. My hands are full with our problems kule Mara.
 
Kaka Jasusi,
Kokote ambako MAPINDUZI yalifanyika, waliopinduliwa hawajapata nafasi nzuri ya kulipiza kisasi cha nguvu, yaani nao wapindue, waue na kurudisha madaraka yao, ni vigumu kuwasamehe wale waliowapindua. Tatizo hili liko Zanzibar tangu mwaka 1964. Wanajua wazi kikwazo kikubwa kwao waliopinduliwa ni Mwalimu na Muungano huu. Hawatamsema vizuri Mwalimu kwa lolote lile. Mimi nimemsifu na kumheshimu sana gombesugu kwa uwazi wake juu ya mapinduzi haya anayoyaita haramu.

gombesugu amekwenda mbali zaidi na kusema wazi kuwa mwaka 1972 nao walijaribu kupindua. Hawakufanikiwa lakini yule "Mnyasa" aliuwawa.
 
Last edited by a moderator:
Sasa naanza kumwamini Commando, Dr Salmin Amour, alipodai kuwa naye alitaka kupinduliwa na akina Maalim Seif mwaka ule. Nisichokijua ni vipi jambo hili lingewezekana katika "NCHI" ambayo imo ndani ya nchi nyingine!
 

Naaam

Nilifanya hivyo ili ninapoleta hoja zisisigane na uamini wako mkuu,

Kwanza nitaanza kujibu hivi,

1) Ninatambua na kuyaheshimu mapinduzi yale yaliyoongozwa na Field Marshal John Okello, na zaidi ninaamini John Okello ndie baba halali wa mapinduzi matukufu ya Zanzibar!

2) Pamoja na mwalimu kuunga mkono mapinduzi yale, lakini utawala wa mkono wa chuma wa Okello ulidumu kwa miezi sita haukumfurahisha mwalimu,

Kwakuwa Okello hakuwa mwanachama wa chama chocho katika mapinduzi na utawala wake, Mwalimu aliunga mkono juhudi za ASP katika kuleta utangamano Zanzibar!

Katika mizani hiyo dhana ya udini inatoweka na siasa,rangi na ukabila vinastawi katika visiwa hivyo vya karafuu!

Mijadala iliyotanda siku ya mapinduzi ilikuwa ni ukabila na rangi, na vilevile Okello alitangaza wazi kuwa atakaepinga utawala wake atakuwa kaikataa roho yake mwenyewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…