Kadogoo,
..naomba nianze na suala la Biafra kwanza.
..kwa mtizamo wangu Nigeria kulikuwa na vita ya kikabila, siyo vita ya kidini. sidhani kama ilikuwa vita baina ya Wakristo vs Waislamu, kwasababu huo upande unaodaiwa kuwa na Waislamu ulikuwa na wanajeshi Wakristo. Olusegun Obasanjo, Mkristo, alikuwa upande wa federal gov of Nigeria.
..kwa hiyo Nyerere alikwenda kusaidia Waibo, waliokuwa wakichinjwa na Wanigeria wenzao.
..mimi ningekushauri utafute hotuba iliyotolewa na C.Y.Mgonja[waziri wa nchi ofisi ya Raisi ] kuelezea kwanini Tanzania iliamua kuitambua Biafra. naamini kabisa kama uko open minded utakubaliana na hoja zilizotolewa na serikali ya Tanzania.
..Hata mimi nashangazwa sana na hii process ya kumfanya Mwalimu Nyerere mwenye heri na baadaye Mtakatifu. Mimi namuelewa zaidi Mwalimu kama mwanasiasa, yes he was a devout Catholic, lakini sidhani kama alifanya mambo yoyote yale ya "kiroho" au "kitume" kustahili ngazi ya wenyeheri and eventually utakatifu.
..Lakini Mwalimu amepewa sifa nyingi sana, na wakati mwingine hata yeye mwenyewe alikuwa anashangaa. Kuna kipindi India walimpa nishani ya amani na unaharakati wa kuzuia silaha za nuklia[naomba kusahihishwa kama kuna makosa]. Mwalimu katika hotuba ya kushukuru alisema bayana kwamba ameshangaa yeye kupewa nishani hiyo ukizingatia kwamba siyo mara moja ambapo aliunga mkono mapambano ya silaha.
..Umeuliza kuhusu mauaji ya Zanzibar na Mwembechai kama yangeweza kutokea wakati wa Mwalimu. Kwa mtizamo wangu naweza kusema yasingeweza kutokea. Nasema hivyo kwasababu Mwalimu na vyombo vyake vya usalama walikuwa na tabia ya "kunyakua" vinara wa machafuko kabla hawajaleta madhara kwa jamii nzima.
..Mwalimu pia alikuwa haogopi kujibu shutuma zozote zile dhidi ya serikali yake. Kwa mfano, hawa jamaa wanaohubiri mfumo Kristo wasingeachiwa wakatamba nchi nzima kwa miaka kadhaa bila kujibiwa na Mwalimu mwenyewe, au kutiwa kizuizini.
..Mwisho, nadhani Mwalimu alichukia dhuluma kwa namna ya kipekee kabisa. Kutokana na msimamo huo ndiyo maana unaona alikuwa radhi kwenda kinyume na OAU charter kuwatetea Waibo wa Biafra. Ndiyo maana akakubali Tanzania ikose misaada ya kiuchumi toka Uingereza kwa msimamo wetu wa kuwatetea wananchi wa Zimbabwe. Kwa kuchukia dhuluma hakuogopa kutoa msaada wa kijeshi kwa Frelimo waliokuwa wakipambana na Wareno, wanachama wa NATO.
cc:
Jasusi,
Kudi Shauri,
gombesugu,
Ritz,
Wickama