Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

hongera Sheikh, Mtaalam, mjuzi, mpembuzi, mbunifu, researcher na sijui nikupe cheo gani. Hao wanapinga tu. kama wanaglikuwa wanajua wanachofanya wangalitoa angalau kimakala kimoja kupitia magazetini. Hongera Mungu akupe umri mrefu

mkuu wengi tupo kwenye mjadala huu ila hatutii neno. Unamharibia mzee wetu MS.
 

Labda hujui historia ya nchi hii.

Soma Sivalon ndiye aliyetuambia kuwa Kanisa Kaltoliki linaona Uislam kama adui.
Inaelekea Bwana Jasusi wewe ni mgeni katika mambo haya.

Sisi tumebobea tuna rejea lukuki.
Usidhani tumo humu kutania.

Angalia hapa chini:

The second book is by Dr John C. Sivalon, who in his expose, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, [1] unmasks a conspiracy in the government to subvert Islam. Sivalon revealed that the Catholic Church as far back as 1961 was worried by two prospects. First, was the unity between the Muslim madhheb (sect) of Sunni, Bohora, Ismailia and Ithnasheri in Tanganyika; and the second, was the transfer of the headquarters of the East African Muslim Welfare Society (EAMWS) from Mombasa to Dar es Salaam. The Church was worried that the resources in the hands of rich Asian Muslim community in East Africa, coupled with the political power of African Muslims, particularly in Tanganyika, would endanger Christian interests in East Africa. The Church therefore declared Islam as its enemy in the country and plotted to thwart its progress.[2]

[1] John C. Sivalon, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, (Ndanda, 1992).

[2]Ibid. p 37.
 

Kaka kuna tofauti kubwa kati ya malezi na ustaarabu wa Musoma na Dar es Salaam. Pwani mtu yeyote mwenye umri wa baba yake ni mzee wako.

Tuendelee kusemezana.
 

naam shekhe...!
Wanipa raha sana,mnakasha ukipotea wewe waurudisha kwenye track,,
yan wakisima nchale wakikaa nchalee..!
Yani hoja kwa hoja,bali wengi wao si wenye kuutaka ukweli,ila wewe wape tuh kwa manufaa ya wengi.
 
Na Karume je? Unamweka kundi gani? Naye alitumiwa kuhujumu Waislamu?

Jasusi,

Hiyo kazi pevu ya Karume.

Itabidi tuanze Kipumbwi na mamluki wa Kimakonde wakifanya
mazoezi kuja kuvamia Zanzibar.

Wanaambiwa mnakwenda kuwakomboa ndugu zenu kutoka
utawala wa Waarabu.

Safari hii ni ndefu.
Hili lisubiri kwanza Insha Allah tutastarehe ukumbini.

Hapo una Hanga na Karume Dar es Salaam na Zanzibar.
Tanga yuko Jimmy Ringo.

Usisikie habari ya ati mapinduzi wamefanya Umma Party.
Hizo ndizo porojo.

Karume ataingia na utamwona nini ilikuwa nguvu yake
alipowekwa kitini.

Vuta subira ngoja nimalizane na uzi huu.
 
Mohamed,
'keep your eye on the ball'' fair enough!

Ulipotaja kuwa EAMWS iliuawa na kanisa na Nyerere tayari ulikuwa na ushahidi.
Kama hukuwa nao hilo tunaweza kusamehe, kwa lugha nyingine ni kuwa 'umehisi''.

Hata hivyo uliposema hivyo ni lazima utakuwa na mzingira ya kiushahidi kuwa kanisa lilihusika.
Hicho ndicho wasomaji walitaka kuelewa, je, logic ya ushiriki wa kanisa ipo vipi.

Endapo hakuna ushahidi au ushahidi wa kimazingira basi tungekushauri uondoe kauli hiyo.
Vinginevyo hiyo tu inaondoa thamani nzima ya ''social research''.

Katika ''reserach'' yako uliweza kutumia maneno ''inasemekana'' dhidi ya Nyerere.
Hata kama hakuna mahali aliponukuliwa au kuhojiwa bado uliweza kufanya link kati ya mlezi wake padre wa kikatoliki, nafasi zake za masomo na kikazi na hata kuunganisha ajira yake na utata katika kupigania uhuru.
Vipi unashindwa kutumia mwenendo huo kutueleza ushiriki wa kanisa katika kuua EAMWS?
 
naam shekhe...!
Wanipa raha sana,mnakasha ukipotea wewe waurudisha kwenye track,,
yan wakisima nchale wakikaa nchalee..!
Yani hoja kwa hoja,bali wengi wao si wenye kuutaka ukweli,ila wewe wape tuh kwa manufaa ya wengi.

Alhamdulilah,

Sisi hatusemi uongo Allah kakataza.

Hii ndiyo siri ya sisi kung'ara humu ndani juu ya
kuwa tu wachache.

Nilikianza kitabu changu na Bismillah Rahman Rahim.
Publisher kanikatalia kitabu kisianze hivyo.
 

Nyerere, Nyerere, Nyerere...
Nyie hamtaki kujua mchango wa Ali Migeyo, Idd watatu wale niliokutajieni?

Idd Faiz aliyempeleka Nyerere UNO, Idd Tosiri aliyempeleka Nyerere Bagamoyo
kwa Sheikh Mohamed Ramia Khalifa wa Quadiriyya.

Ukimpata Sheikh Ramia una maelfu wa wanachama katika TANU.
Hawa ni murid na Sheikh Ramiya ndiye Khalifa.

Hutaki kujua habari za Idd Tulio wasukaji wa mambo ndani ya Baraza la Wazee wa TANU?

Basi mmekalia Nyerere, Nyerere, Nyerere tu?

Ukitaka kujua habari za kanisa msome Sivalon.
 
Alhamdulilah,

Sisi hatusemi uongo Allah kakataza.

Hii ndiyo siri ya sisi kung'ara humu ndani juu ya
kuwa tu wachache.

Nilikianza kitabu changu na Bismillah Rahman Rahim.
Publisher kanikatalia kitabu kisianze hivyo.
Mohamed! Mohamed Said Abdallah Salum Mwekapopo Samtungo!
Hivi uliposema Nyerere aliingizwa katika siasa na Abdul Sykes mwaka 1953 ulikuwa ukweli huo?

Hivi uliposema Nyerere alianzia siasa Dar ili hali tunajua alianzia Makerere ni ukweli huo!

Hivi uliposema mapinduzi ya Zanzibar yaliandaliwa na kuletwa na Nyerere ni ukweli huo!

Hivi unapsoema kanisa limeua EAMWS bila ushahidi ndivyo uislam unavyosema kweli!
 
Oh,Mohamed yaani ungejua tunavyowathamini Watanganyika waliojitolea kuikomboa nchi hii usingesema hayo.

Habari za akina Sykes, Nyerere, Lugazia, Mwapachu, Kyaruzi, Amir, Tosi, Bomani, Ramiya, Migeyo, Bomani, Fundikira, Steve Mhando, Danstan Omar, Phombeah,Rupia, Kasella Bantu, Tatu binti Mzee, Aisha binti Mohamed n.k. kweli zinatufanya tuwapende mashujaa kwa utumishi wao ingawa historia yao inageuka kuwa hisia iliyojengwa katika ngano tamu sana.

Je, upendo huo ndio utulazimishe tuamini kuwa EAMWS iluawa na Kanisa hata kama tunajua kuwa hakuna ushahidi wowote au wa kimizangira achilia mbali logic.

Je, tujue habari tu kwa kumeza kama makinda ya ndege bila kutumia vichwa vyetu tulivyojaaliwa na Mwenyezi mungu.
 
Ukitaka kujua habari za kanisa msome Sivalon.
Sivalon hakuandika kuhusu kifo cha EAMWS! Uliyeandika ni wewe na ni wewe mwenye dhima ya kutetea hoja yako.

Mohamed Said, waambie wanajamvi Kanisa liliua vipi EAMWS! hiyo ndiyo hoja.
Kama itakosa majibu basi, izike kauli hiyo kama ulivyzika tuhuma za namba za mitihani.

Hatumezi kama makinda ya chole au mbayu wayu tunduni, tunatumia akili zetu! Hapa ni Jamvini kila kitu hadharani, haonewi au hasamehewi mtu!
 
Really? Nani alikuwa Mkurugenzi wa TBC wakati huo? na TBC ilikuwa chini ya serikali ya Nyerere huyo huyo mwenye chuki dhidi ya Waislamu?

Ndipo ninaposema nyie mambo haya hamyawezi.

Basi manashindwa hata kusoma kidogo.
Utafiti kidogo.

Hiyo ilikuwa Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC) 1963.

Nyie ni mafundi wa ubishi.
 
N

Basi mmekalia Nyerere, Nyerere, Nyerere tu?

Ukitaka kujua habari za kanisa msome Sivalon.

Mzee Said sasa hapa hututendei haki; tatizo ni kuwa hisia zako zinakufanya uamini vitu visivyokuwepo. Hivi kati ya wote tunaokosoa maandishi yako kuna hata mmoja aliyesema "Nyerere peke yake" au "Nyerere tu" au "Nyerere ndiye muasisi pekee wa taifa hili?" nani kasema hivyo?

Yericko Nyerere?
Mag3
Nguruvi3
Jasusi
Nanren
Wildcard

Tatizo unafikiria tunapokosoa histohisia yako tunafanya hivyo kwa sababu tunaamini ni "Nyerere peke yake". Hakuna sehemu yoyote katika historia palipowahi kuandikwa kuwa Nyerere peke yake ndiye aliyeasisi TANU au ndiye pekee aliyefanya harakati za Uhuru. HAKUNA.

Hujawahi katika maandishi yako yote kuonesha mahali popote - iwe kwenye mihadhara yako ya ndani au ya nje ya nchi - kuwa Nyerere mwenyewe aliwahi kudai ndiye aliyeanzisha TANU peke yake, au kuna mahali wana historia waliandika kuwa Nyerere alianzisha TANU peke yake akiwa Pugu. Hakuna.

Hakuna MAHALI POPOTE ambapo imewahi kuandikwa na wanahistoria makini kuwa Nyerere ndiye muasisi pekee wa taifa na kuwa peke yake ndiye aliyeleta uhuru. Sifa pekee ya Nyerere ni kuwa ndiye kiongozi mkuu wa wapigania uhuru wote. Huwezi kuandika historia ya wapigania uhuru wa Tanganyika halafu ukamuweka Nyerere wa pili. Ukiandika historia hiyo Nyerere anakuwa wa kwanza na siyo tu wa kwanza anatambulika kama Baba wa Taifa (Father of the Nation). Sifa hii haijaanza kuitwa leo tangu miaka ya sitini wazee wa Dar walimuita hivyo na maandishi ya wakati huo yalionesha hivyo. Siyo sifa ambayo amekuja kupewa baadaye baada ya kufa au baada ya kutoka madarakani.

Mchango wa pekee, mkubwa zaidi na wa kina zaidi wa Nyerere haujawahi kufikiwa na kina Sykes, Mhando, Kyaruzi, Mwapachu n.k. Leo hii vijana wakimsifia Messi kwa uchezaji wake na kumsifia na kuvaa jezi zake na watu kumtuza kwa kila tuzo unafikiri ni kwa sababu yuko peke yake uwanjani!? La hasha bali kwa sababu ya vipaji na mchango wake wa pekee.

Huwezi - hata kwa kujaribu uliko jaribu - kumfanya Nyerere namba mbili.

Alikuwa wa kwanza kati ya wengi, na wa pekee kati wengine wake. He was the leader among leaders! Wazee wako walimtambua hivyo, walimheshimu hivyo, walimpenda hivyo na wengine hadi leo wana moyo wa shukrani kwa kuweza kuwa naye katika harakati.
 

If the Catholic church was worried about the unity between Muslim madhheb, their worry was misplaced. There has been much antagonism among Muslim groups, or sects, which eventually led to the banning of EAMWS in Tanzania. But then worrying is one thing but it is another thing to come and claim that the church led a crusade against muslims in Tanzania. You have not proven that.
 
Tunajiifunza mengi sana hapa.

Kwanza naona tofauti kubwa ipo kati kinachosimamiwa, katika kufuatilia hoja nimeona MS ameegemea upande wa imani yake na kundi jingine limeegemea katika uTaifa.

Sidhani kuwa hoja za MS zimetokea hewani kuna ukweli japo jinsi unavyowasilishwa unawaza tia shaka hapa na pale, katika historia ya kanisa katoliki kuna mengi machafu yamewahi kufanyika aidha kwa jina la kanisa(kutetea/kueneza) au kutokana na akili za viongozi wa wakati huo. yeyote anayejiona kuwa mhanga wa hayo haitakuwa ajabu akiwa na msimamo mkali dhidi ya kanisa

Sidhani kama MS anakosea kuamini anachoamini kuegemea imani yake lakini nafikiri anakosea kuunganisha uongozi wa kisiasa wa dola na imani za kidini. Mtizamo wangu ni kuwa Nyerere aliweka taifa kwanza kabla ya mambo mengine na pale alipoona kuna umuhimu wa kulilinda taifa dhidi ya yeyote anayetishia kuvunja umoja wa kitaifa alifanya hivyo bila kuangalia ni mtu wa taifa, kabila au dini gani.

Kuna malalamiko dhidi ya Nyerere kutoka kwa wasomi, wafanyabiashara na wengineo kwamba hakuwatendea haki lakini hapohapo tunapata picha kwamba halikuwa kundi moja lililoathirika kwahiyo hakufanya aliyoyatenda kwa kuwakomoa bali aliamini uamuzi aliuchukua ulikuwa ni kwa manufaa ya wengi.

Natamani watu kama ninyi mnaofahamu historia ya nchi yetu mngekaa pamoja tupate historia isiyo na mapengo mengi bila kuweka 'ego' ili iweze kujenga misingi imara ya huko tuendako kwasababu tutajua tulipotoka.
 
Ndipo ninaposema nyie mambo haya hamyawezi.

Basi manashindwa hata kusoma kidogo.
Utafiti kidogo.

Hiyo ilikuwa Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC) 1963.

Nyie ni mafundi wa ubishi.

dharau hii si ya lazima hata kidogo; kwani unafikiria sijui kuwa ilikuwa ni TBC ya wakati ule? Hujajibu swali hapa. Nyerere Mkristu kapakwa na shehe hadharani na TBC ikarusha matangazo yale nchi nzima. Je Mkurugenzi alichukuliwa hatua yoyote na serikali? Je serikali ilijaribu kuacha kurusha matangazo hayo? Hujibu haya maswali.
 

Nguruvi3,

I admire your courage.
Ntakupa kisa cha George Foreman na Joe Frazier nini Foreman alisema kuhusu Frazier. Kisha nitakupa nini Muhammad Ali alisema kuhusu George Foreman. Hifadhi akilini kisha nikumbushe.

Sasa nisikize.

Nyie mambo haya hamyajui kwa sababu mambo yenu yote ''have been taken care of.'' Sisi tumehangaika kuyajua kwa sababu tunajiuliza iweje sisi tuwe hivi ilhal ni wazee wetu walipigania uhuru wa nchi hii kuondoa dhulma? Ndiyo maana nyie hamtaki hata kusikia Mshume Kiyate akitajwa au Jumbe Tambaza au Sheikh Hassan bin Amir. Watu muhimu katika historia lakini mmekaa maisha yenu yote hamna habari zao.

Sasa hebu soma hapo umsikie Sivalon anasema nini:

The second book is by Dr John C. Sivalon, who in his expose, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, [1] unmasks a conspiracy in the government to subvert Islam. Sivalon revealed that the Catholic Church as far back as 1961 was worried by two prospects. First, was the unity between the Muslim madhheb (sect) of Sunni, Bohora, Ismailia and Ithnasheri in Tanganyika; and the second, was the transfer of the headquarters of the East African Muslim Welfare Society (EAMWS) from Mombasa to Dar es Salaam. The Church was worried that the resources in the hands of rich Asian Muslim community in East Africa, coupled with the political power of African Muslims, particularly in Tanganyika, would endanger Christian interests in East Africa. The Church therefore declared Islam as its enemy in the country and plotted to thwart its progress.[2]

[1] John C. Sivalon, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, (Ndanda, 1992).

[2]Ibid. p 37.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…