N
Basi mmekalia Nyerere, Nyerere, Nyerere tu?
Ukitaka kujua habari za kanisa msome Sivalon.
Mzee Said sasa hapa hututendei haki; tatizo ni kuwa hisia zako zinakufanya uamini vitu visivyokuwepo. Hivi kati ya wote tunaokosoa maandishi yako kuna hata mmoja aliyesema "Nyerere peke yake" au "Nyerere tu" au "Nyerere ndiye muasisi pekee wa taifa hili?" nani kasema hivyo?
Yericko Nyerere?
Mag3
Nguruvi3
Jasusi
Nanren
Wildcard
Tatizo unafikiria tunapokosoa histohisia yako tunafanya hivyo kwa sababu tunaamini ni "Nyerere peke yake". Hakuna sehemu yoyote katika historia palipowahi kuandikwa kuwa Nyerere peke yake ndiye aliyeasisi TANU au ndiye pekee aliyefanya harakati za Uhuru. HAKUNA.
Hujawahi katika maandishi yako yote kuonesha mahali popote - iwe kwenye mihadhara yako ya ndani au ya nje ya nchi - kuwa Nyerere mwenyewe aliwahi kudai ndiye aliyeanzisha TANU peke yake, au kuna mahali wana historia waliandika kuwa Nyerere alianzisha TANU peke yake akiwa Pugu. Hakuna.
Hakuna MAHALI POPOTE ambapo imewahi kuandikwa na wanahistoria makini kuwa Nyerere ndiye muasisi pekee wa taifa na kuwa peke yake ndiye aliyeleta uhuru. Sifa pekee ya Nyerere ni kuwa ndiye kiongozi mkuu wa wapigania uhuru wote. Huwezi kuandika historia ya wapigania uhuru wa Tanganyika halafu ukamuweka Nyerere wa pili. Ukiandika historia hiyo Nyerere anakuwa wa kwanza na siyo tu wa kwanza anatambulika kama Baba wa Taifa (Father of the Nation). Sifa hii haijaanza kuitwa leo tangu miaka ya sitini wazee wa Dar walimuita hivyo na maandishi ya wakati huo yalionesha hivyo. Siyo sifa ambayo amekuja kupewa baadaye baada ya kufa au baada ya kutoka madarakani.
Mchango wa pekee, mkubwa zaidi na wa kina zaidi wa Nyerere haujawahi kufikiwa na kina Sykes, Mhando, Kyaruzi, Mwapachu n.k. Leo hii vijana wakimsifia Messi kwa uchezaji wake na kumsifia na kuvaa jezi zake na watu kumtuza kwa kila tuzo unafikiri ni kwa sababu yuko peke yake uwanjani!? La hasha bali kwa sababu ya vipaji na mchango wake wa pekee.
Huwezi - hata kwa kujaribu uliko jaribu - kumfanya Nyerere namba mbili.
Alikuwa wa kwanza kati ya wengi, na wa pekee kati wengine wake. He was the leader among leaders! Wazee wako walimtambua hivyo, walimheshimu hivyo, walimpenda hivyo na wengine hadi leo wana moyo wa shukrani kwa kuweza kuwa naye katika harakati.