Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Nitakujibu moja tu.
La Nyerere maana hilo ndilo ulipendalo.
Hakuna awezae kushusha hadhi ya Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hapo hakuna ubishi.
Wewe kama kawaida yako mzee unajaribu kushusha hadhi ya Nyerere kwa kutumia mbinu mbalimbali za maneno. Unazungusha maneno na kumdharaulisha mbele ya jamii; unamfanya duni ili uwainue wazee 'wako' na uko tayari kusema lolote dhidi yake kama unavyosema hapa.
Lakini historia ya uhuru haikuanza na yeye.
Historia ya TANU haiwezi kuanza na Nyerere 1954 kama ilivyogongomewa.
Tatizo ni kuwa hakuna mahali hata pamoja hadi leo miaka yote hii ambapo umewahi kuonesha kuwa Nyerere alidai kuwa historia ya uhuru ilianza na yeye au kuwa TANU ilianza na Nyerere mwaka 1954. Hakuna andiko lolote la historia ambapo linasema historia ya Uhuru ilianza na Nyerere. NONE na hujawazeza kuonesha popote. Na hakuna Mtanzania yeyote aliyesoma historia kidogo ya Tanganyika ambaye anaweza kudhania hata kidogo kuwa historia ya Kupigania uhuru ilianza na Nyerere. Hakuna kitabu hata kimoja makini kinachosema hivyo. Wewe mwenyewe hadi LEO HII hujaweza kuonesha wapi Nyerere aliwahi kudai kuwa historia ya uhuru imeanza na yeye au ya TANU kuanza na yeye.
Lakini tumeshakuonesha mara kadhaa kuwa Nyerere mwenyewe amekiri nafasi ya pekee ya wazee wa Dar na amekiri mchango wao kabla ya yeye kufika Dar na siyo wao tu bali pia mchango wa wengine wengi nchi nzima. Historia ya kupigania uhuru haikuanza na Dar na wala historia ya TANU haikuanza na wazee wako wa Dar.
Hata kama Nyerere atakasirika.
Hata angekuwa hai hawezi kukasirika. Kwa sababu unachosema hakina msingi wa ukweli hivyo hakikasirishi.
Hapa ndipo paliponifanya ninyanyue kalamu.
Ndiyo maana leo nimo humu jamvini natoa darsa na kipande ninachodarsisha ni 1929 - 1961.
Lakini unachofanya hata kidogo hakikaribiani na hiyo historia. Wenyewe wanakiita 'historical revisionism"...
You are a true historical revisionist per excellence...