Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Zawadi ingine kwa wanajamvi.
[h=1]ALLY SYKES AND JULIUS NYERERE[/h]
 
Gombesugu,
Naomba ruksa yako nikukumbushe jambo.

Aliemuoa Bi Salama Hussein Juma ni Ramadhani Aziz.

Majuzi niko makaburi ya Kisutu nimeliona kaburi la
marehemu Salama.

Sheikh Hussein Juma alikuwa Vice President wa UTP.

In Sha Allah nitakuwekea kitu kuhusu Al Hassanain.

Sheikh Hussein alizaa watoto brilliant kama Prof. Mansour
huyu nadhani ni bingwa wa hisabati, kisha Muhidin huyu
alikwenda Makerere na akawa katika polisi.
 

JokaKuu,

Salaam sana ndugu yangu.

Sasa nazidi kupata picha nzuri ya Ilm na fikra zako. Nafurahi pia kuona mwangazo/mtazamo wako ki-Historia ulipo...yaani umejiagamiza mno na hao "Waalimu wa Kizungu"!?

Lakini nitakua mtovu wa adabu kama nikianza kukulaumu au kukwambia ati yakuwa hujui Historia,hasha abadan na wala si dasturi yangu asilan.

Huyo MwandishiAuthor wako;kwanza kajichanganya kwenye vitu kadhaa. Kwa kuanzia nathubutu tena kwa mapana kusema haijui Historia ya Waswahili wala Kiswahili!

Hivi wewe binafsi unaamini yakuwa Waswahili,ni mchanganyiko wa Wageni/Arabs,Persians na Wabantu tu!?ahaha!!
Kwa hiyo unaamini yakini kabisa yakuwa kabla ya hapo kulikua hakuna Waswahili asilan!?...vipi JokaKuu ndugu yangu mbona nawe pia wataka kuniangusha!? Wajua mie nakutegemea mno hapa jamvini!?

Huyo Author/source yako,pia anaonyesha ule udhaifu ya wale so called "Orientalists" na pia ana ile colonial connotation.

Tayari unakumbuka nilishawahi kukutumia andiko/kitabu mahiri kuhusu Historia ya Waswahili!? Nakushauri kakisome tena/upya kile kitabu nilichokuandikia na pitia ile makala niliyokupa ya; Hali ya kutatanisha ya Kiswahili hivi leo Afrka ya Mashariki by Prof. TSY Sengo.

Tatizo kubwa mno lilipo kwa takriban karne nyingi mno sasa,ni yakuwa Historia ya Watu Weusi huandikwa na wageni,tena kwa mitazamo na maslahi yao.

Takupa mfano kiduchu wa hapa jamvini. Tuna huyu ndugu yetu Mwanakijiji,ambae kwa hapa Jamii Forum,nafikri "anaheshimika" kama ni mmojawapo ya Wasomi wakubwa na Mtaalamu wa hali ya juu!?ahaha!!

Lakini pamoja na vitimbi vyake vyoote vya kumpinga MwanaHistoria Sheikh Mohammed;kwasasa inamlazim huyohuyo Mwanakijiji akasome upya Historia ya Tanganyika tena ati kwa kupitia maandiko ya Wageni/Wazungu kabla ya kurejea upya hapa jamvini,kuja "kupasuana kichwa" na MwanaHistoria Sheikh Mohammed, ambae si tu kwamba ni Nguli wa fani hiyo,lakini pia ni mzaliwa wa kwenye Family ilohusika mno kwenye harakati hizo na maeneo ya hizo harakati zilipokua zikifanyiwa/kufanyika!

Sasa kwa mwenye maarifa na kutulia;ndipo utaona udhaifu ya Watu weusi kiundani...hii nayo ni Topic nyingine ndefu mno inalazim tuiweke kiporo.

Nikirejea tena kwa huyo Author wako;japo amejitahidi mno kudadavua,lakini nahisi kafanza kosa la kitaaluma kuchanganya baadhi ya nukuu kiduchu za Qur'aan kwenye ile bayana yake. Nina imani yakuwa hiyo Qur'aan wala si fani yake na wala haijui kiundani.

Maana alitakiwa pia ajue zile Ayat za Qur'aan,ziliteremshwa kama Wahyi kwa Mtume Muhammad lini,wapi,na kwa sababu/mantik ipi,na kisa kipi kilitokea au kilisababisha hizo Ayat/Surat kuteremshwa!?

Nina hakika kama angelifanza uchunguzi au angalijua japo kiduchu,kati ya hayo basi angejisikia tahayuri hata kufanza zile nukuu zake za kitoto!

Nifahamu ndugu yangu JokaKuu,hapa sijaribu kutetetea Qu'raan,sababu hiyo Qur'aan ni kitabu kilicho kamili na mara zoote hujiteteta chenyewe kwa minyambulisho yake iso shaka...lakini tu kwa wale wenye kujua...wanaitwa "Inkutum Taalamuna".

Tafrani nyingine kiduchu alofanza huyohuyo Author wako/wetu,amejaribu(tena hii ni dasturi saana ya maluuni wengi wa kizungu),ku-suffocate Historia yoote ya Watu weusi.

Sasa hapa naomba upitie upya kitabu hiki kama ulishawahi kukisoma:

The Destruction of Black Civilization by Chancellor Williams.

The Black Athena by Martin Bernal.

Is Roman Catholicism Christian!? by Dr. John Henry 2001.

Orientalism by Prof. Edward Said.

Afrika and other Civilizations: Conquest and Counter-Conquest by Prof. Alamin Mazrui.

The Waswahili: The Social History of an Ethnic group by W. Arren. The original draft of this paper was presented at the 1972 Toronto Meeting of the Amerikan Anthropogolical Association.

Tafadhali,inanilazim nirejee tena kukwambia yakuwa mimi sitetei asilan ukweli wowote uliopo kuhusu vitimbi na unyama walofanza hao Waarabu japo nina damu yao kiduchu!ahaha!!

Wanataaluma wengi wa Social Anthroplogy,nahisi wakiona paper ya huyo Author wako/wetu,watamdhihaki pita kiasi.

Sina hakika,kama aliofanza kusudi au kwa kutokujua tu!?...lakini kaacha kugusia ule unyama,udhalimu na ushenzi mkubwa mno aliokua akifanza Kabaka pale Buganda,kabla ya kufanza urafiki/kujuana kwa karibu na Watawala wa Zanzibar karne hizo. Hii khabari nayo ni ndefu mno pita kiasi...lakini nina imani nayo pia waijua japo kiduchu!?

Sasa kukosekana kwa story/khabari hii,kwenye hiyo bayana yako,ndipo inaashiria japo kiduchu kutokujua majambo ya Ki-Historia kiundani kwa ya yule mwandishi/Mzungu wako,au amefanza makusudi kuficha baadhi ya vitu kwa khofu ya labda kuwapa credit japo kiduchu hao Waarabu au Uislamu!? Ama kwa hakika kwa hapa mimi nawe ndugu yangu nakhis hatuna yakini.

Pia kuna ile connection ya MwanaMutapa na pale Kilwa pia haikuonyeshwa!? Hatujaamabiwa ile khabari mashuhuri ya wale Watu weusi/Watumwa waliokua wakiomba wenyewe bora wende Kilwa Utumwani kwa hao Waarabu kuliko kubaki na Mfalme wao MwanaMutapa,kwa ule unyama,ushenzi na vifo aliokua akiwafanzia wenzie!

Cha mwisho,jiulize kwanini huyo Author,kwenye aidha conclusion au background yake hajaweka kile kisa kikuu ili kufahamisha Historia ya Watu weusi wengi tu,tena baadhi yao walikua Rich Merchants pale Makkah na Medina na baadhi ya sehemu nyingi za ardhi za Uarabuni,kabla hata ya Mtume Muhammad hajazaliwa!?

Nina hakika kuna connection anaijua itatokea na kuwapa credit Waarabu/Uislamu au hao Watu weusi/Watumwa...ndo maana imefichwa.

Kuna myth kubwa inaendelea mpaka kesho,yakuwa Watu weusi waliokua Waislamu wa mwanzo ati walikua ni Watumwa tu waliokombolewa...bakhti mbaya hii myth hata baadhi ya Waarabu/khasa Serikali zao hazitaki kukemea kwa maslahi yao fulani ya kidunia. Na labda pia kuogopa kuwapa nafasi/credit Watu weusi katika Historia ya kweli ya Kiislamu.
Hii nafikiri,tuache maana hapa si pahala pake,na pia ni issue/Topic nyingine ndefu pita kiasi!

Kuna kisa cha "The Elephant Year"...ni kisa maarufu kimetajwa kwa kirefu kwenye Qur'aan. Wasomi wengi Manguli wa Historia na wanataaluma wa Anthropology na sciences nyinginezo wamekithibitisha kisa hiki kutokea.

Hao watu maluuni na makhabithi waliotoka kwenda kuvunja ile Q'aaba pale,wengi ya Viongozi wao walikua ni watu Matajiri Weusi wakiongozwa na Wajukuu/Virembwe wa Bint Ngola ambae aliekua Malkia wa hii leo Angola...wakti huo ulikua mmojawapo ya Falme kubwa mno na zenye kutisha duniani!

Sasa ukishajaribu kuunganisha hizo connections zoote na nyinginezo nyingi mno,siku zote itakua Historia haikupi taabu ndugu yangu JokaKuu!?

Kwa kifupi,kuna vitu kiduchu huyo Author nakubaliana nae...lakini hiyo paper yake/Research,nina hakika hata Mwanafunzi wangu wa Second Year atainyambua tena huku kafumba macho.

Mwisho ndugu yangu JokaKuu,pamoja na kukushukuru kwa kunisikiza,lakini binafsi nahisi twapelekana mbali zaidi/nje na hizi mada za "uchochezi,uhaini na ugaidi wa Sheikh Mohammed"!?

Nastaajabu hata nami pia nimejikuta nimo katikati ya malumbano!?ahaha!!

Tuendelee na mnakasha wetu kwa utaratibu Insha Allah ndugu yangu.

Ahsanta.

Cc;Ritz,Barubaru
 

Usijali mzee MS; mwambie Uchina ni kitoweo kama kisamvu. Bora nimwekee part 2. Ziko part 6 nitajaribu kuwa mkarimu inshallah.

The Daring Dobermans - Part 2 - YouTube

Mzee MS, ladha halisi ya content tunaijua sisi wafugaji (mimi na wewe) wa wanyama hawa!!!!! Barabara zingine huwa zina speed limit Sheikh ili viumbe hawa nao wapite. hahahahahahah. Ila nakusifu kwa kuchagua kufuga Dobermans angalia walivyo watiifuu wakitumwa Sheikh!!!! umeona huyo aliyepeleka barua benki kwenye part 1. Nilitishwa kuwa lazima wamshambulie mmiliki wao katika maisha yao. Nikuache upumzike ndugu yangu maneno yako ya meli kutia nanga Johannesburg ni matamu na yamenikumbusha maneno ya WAZEE wangu wa MZIZIMA kuwa si hekima kudai kodi hospitalini. tena wodini. hahahahah. Sina hamu.

Tuko pamoja MS, kucheka ni Sunna, ruksa, usijizuie.
 
gombesugu,

..thanks for ur long response.

..kuna mwana JF alibisha kwamba WAARABU hawakuhusika na biashara ya UTUMWA ktk eneo la TANGANYIKA, ZNZ, na AFRIKA MASHARIKI.

..sasa hii makala nadhani inamaliza ule "mzozo" kama ni kweli Waarabu walishiriki au hawakushiriki ktk udhalimu huo.

..masuala ya tafsiri ya Kuran mimi sina utaalamu nayo. pia sina utaalamu wa tafsiri ya biblia. zaidi, naogopa sana kugusa maeneo hayo kwa kuogopa kudhalilisha imani za watu.

..mwisho, nadhani makala niliyoileta iko balanced kwa kiasi kikubwa.

NB:

..inaelekea unapenda mambo ya lugha ya KISWAHILI. sasa ulizuka "mzozo" ktk blog za wa-Zanzibar kuhusu asili ya lugha hii, kama ni lugha za Kibantu, au Kiarabu.
 
Last edited by a moderator:

Sheikh Mohammed,

Ahsanta saana,kwa kunibainishia...namkumbuka saana Bwana Ramadhani Aziz nafikiri ndo maana nikaweka pale ile "Step Father In Law",ili kutabainisha yakuwa si IGP Hamza Aziz aloowa bali ni nduguye...!ahaha!! ndo yale yale chembilecho cha nduguyo Mark Twain!ahaha!!

Nalisikitika mno kusikia kifo cha Aunt Salama Hussein maskini...Wallahi,zamani nikiwa mduchu akinipenda mno na kuniita "Mchumba wangu",huku Al Marhum Ramadhan Aziz akinitisha yakuwa ati "nikimuoa" Mkewe basi haturejeshi tena nyumbani kwetu...basi mimi nikianza kulia mno!ahaha!! Wallahi,ndugu zetu wengi wamekwenda zao,Inna Lillahi Wa Inna Illahi Raj'un

Siku nyingine kinipa fursa takuwekea kisa cha Prof. mansour Hussein na Nyerere pale Lagos Univ. wakti huo akifundisha pale.

Wajua hizi tamaduni za hawa wenzetu wa kizungu na sisi ni tafauti nyingi mno...mfano wale Ma-Brotherman,nasi kwa Kiswahili nafikiri ndo tukiwaita Mabwankaka!?ahaha!!

Niwie radhi,kuna kitu nataka ku-correct kiduchu kwenye bayana yangu kwa ndugu yetu JokaKuu.

Ahsanta.

Cc;Ritz
 
Kila mara nimekuwa nasoma watu wakijinasibu ''watu wa madrasa'' katika kuonyesha hali fulani.
Niseme wazi kuwa ni katika hali ya kuonyesha unyonge.

Watu lazima waelewe kuwa elimu ni elimu tu hata ile ya jando na unyago ilikuwa elimu muhimu sana.
Ningefarijika sana kama watu wangejinasibu na elimu ya madrasa kuliko kujisikia wanyonge wa elimu hiyo.

Kinachotokea hapa ni sumu ya Mohamed Said kuathiri jamii. Kwamba, Mohamed ameifanya jamii iamini kuwa ni dhalili.
Siku zote ukitaka kumshinda mtu jambo la kwanza mfanye ajisikie dhalili hapo utapiga kadri unavyotaka.

Kabla ya mpambano wa ngumi, mara nyingi utasikia tambo za wanamasumbwi '' yule nyanya sana, bwaba lile raundi mbili kwisha, hana lolote minyama tu n.k.'' yote hiyo ni kumdhalilisha kwanza mpinzani kabla ya kuingia ulingoni.

Lakini pia kama watu wanaona elimu ya madrasa ina mushkeli, je wanafanya nini kuioboresha?
Na hapa pia Mohamed anabeba lawama za kuchomeka fikra za kulalamika na wala si kutenda.
Si ajabu atakuja na hoja za eneo flani kutaka kujenga madrasa na mfumokristo kukataa! pathetic

Ujumbe wangu kwa wale mnaosema ''elimu ya madrasa, sisi wa madrasa n.k.'' mnashindwa kuelewa kuwa mnaitia elimu hiyo udhalili wenyewe na mnaonyesha kuwa kuna tatizo katika elimu yenyewe, now it's time to do something.

Jitambueni na acheni kuchukua unyonge wa kufundishwa na Mohamed.
You take the confidence away halafu unaingia ulingoni!

Mohamed amefanikiwa sana kuwafanya watu wawe kama vizuka, wengine wanasema wanaonewa! ukimuuliza wapi hana jibu, wengine elimu ya madrasa ukimwambia inatatizo gani hana jibu.

Acheni kusoma hadithi, sasa ni wakati watu wajiulize zile madrasa zinaweza kuwa tranformed vipi na kuingiza mitaala mingi ili kuzifanya bora na zinazoenda na wakti!

Ni wakati wa kujiuliza, je walimu wa madrasa wanaswifa za kutosha kumuandaa mtoto katika mazingira yaliyopo.
Ni wakati wa kujiuliza je,kuna mitaala ya madrasa ambayo mtoto akitoka Kilwa na kuja Dar hatachanganyikiwa
Ni wakati wa kujiuliza walimu wa madrasa wanalipwa stahiki za maisha au ndio kusubiri mzee fulani ajitolee kumlipa.
Ni wakati wa kujiuliza kuna taasisi ya kuandaa walimu wa madrasa

Nashkuru nadhani nimetumia tarbiya al islam na nawanukuu Al-akyi wote, Talib Barubaru, Swahib, Shariff Ritz, Alwatan Gombesugu,Mag3, JokaKuu, Prishaz, Wickama, Jasusi, Mkuu wa chuo,mfyonza elimu spike lee, mtoto wa Alaska na wanajamvi wote.
 

JokaKuu,

Nimekunyambulia japo kwa kistaarabu,lakini kukuonyesha yakuwa huyo Professor wako hamna kitu...Waswahili tunaita "Zumbukuku".

Nimezunguka vile na kuandika kwa kirefu kwa maana yangu makhusus,sasa hata kunipa pongezi kiduchu kwa kushinda kwenye hii keyboard ndugu yangu!?

Kuhusu tafsir ya Qur'aan mimi binafsi sina uwezo wala utaalamu nayo kwa kujitanafasi mbele ya wenzangu,afadhali wewe mwenzangu labda itakua unaijua hiyo Biblia yenu japo kiduchu.

Ndipo pale nikamshangaa,yule Professor/Author wako,ati kunukuu Ayat za Qur'aan pahala wala isipokhusu au kulazim!?

Kiswahili si yakuwa nakipenda tu,bali pia huona fakhari iso kifani kukizungumza na kuringia nacho...maana mimi ni Mswahili kwa kila kitu;asili yangu,matendo yangu na hata kibri changu!ahaha!!

Poleni nyingi kwa huo "mzozo" ulozuka kwenye hiyo "Blog ya Wazanzibary"....kama ulivyoiita!

Ahsanta sana.
 



Muheshimiwa Nguruvi3,

Salaam ndugu yangu.

Tatizo lako yaelekea una ghadhabu,chuki na hamaki zisizo mfano ndugu yangu kipenzi... hivi umekumbwa na nini Yarabi!?

Hujioni yakuwa wewe hapa ndo utakua na unaonyesha ni Mnafiki na Mzandik wa hali ya juu(niwie radhi kutumia maneno haya,maana miaka yoote,nilikua nikijua ni matusi mpaka hivi juzi ulivyotufahamisha vingine!)!?

Mimi binafsi nilipoingia hapa jamvini,hilo neno "Watu wa Madrassa","wapuuzi wa Kariakoo","wanywa gahwa" na kashfa na kebehi nyinginezo nyingi mno ndo zilizokua zimetanda na kutolewa na hao wafuasi wako watiifu!

Sisi tukaamua kwa kistaarabu,ili kuepusha zogo na tafrani hapa jamvini bora tukubali hayo majina. Ndo maana nafikiri ikalazim tuanze kujiita na kuji-proud na hivyo vyoote, mvionavyo nyinyi ati ni "upuuzi".

Haya maneno na maelekezo yako kwa hao Waislamu uwaonao ati wamelala,nafikiri ni mema na mazuri mno.

Binafsi nafikiri tatizo lako limo kwenye hiyo lugha utumiayo;nahisi Waislamu wengi wakisoma bayana zako watakuona unawa-patronise na kuwadharau. Niwie radhi hapa sina maana ya ku-question communication skills yako,lakini najaribu kukuasa tu kiungwana na hiyo dasturi yako.

Kumbuka sisi hapa tumeshaitwa mambo mengi mno,mfano ati ni-ma-"Radical Muslims" na Wachochezi;kisa tu tunakubaliana na hoja za Sheikh Mohammed!?

Kwasisi kujiita au kujinasibu na Madrassa,wala sikutie shaka asilan. Nafikiri ni sawa na mwingine kusema ati alikua anahudhuria Sunday School bila ya kukosa!

Huo "ushauri wako wa kitaaluma" kuhusu "kuwasaidia" Waislamu kielimu au kurekebisha hizo Madrassa zao,hivi unahisi Waislamu wenyewe woote au hata mmoja hapo Tanzania hawaoni hivyo vitu na kujaribu kuvishughulikia,au unahisi wanaviona na wameamua kukaa tu chini kupumzika na kucheza zumna/bao!?

Tafadhali ndugu yangu Nguruvi3,japo najua yawezekana umesoma Missionaries,lakini achana na prejudices na stereotypes zao.

Natumai utajaribu kunifahamu japo kiduchu kwa huo uchechefu wangu.

Nakushukuru mno kwa kunisikiza.

Ahsanta.

Cc;Shariff Ritz,Al Khalifa The Big Show,Alhaj Boko Haram,Swahib Al Maarifa Kadogoo.
 
Aya ya Quran inaweza kuwa khaaswa (mahsus) kwa mtu au watu fulani lakini katika lafdhi hugeuka kuwa aamma (kwa wote).

Mfano aya hii:
Quran 3:103. Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu..."
Aya hii ilishuka Madina hasahasa kwa Swahaba wawili mmoja kutoka kabila la Al-aws na mwingine kutoka kabila la Al-khazraj makabila ambayo kabla ya Uislamu yalikuwa katika vita kubwa sana mara kwa mara.
Na Mayahudi wa Madinah ndio waliokuwa wauzaji silaha wakubwa wakati haya makabila yakipigana vilevile katika baadhi ya vita ilikuwa ni mayahudi ndio wanaowachohea ili waingie katika vita na kukuza mauzo yao ya silaha.

Ulipokuja Uislamu haya makabila yakasilimu na kufuta uadui wao wote wakaw ni ndugu.

Siku moja Myahudi mmoja (jina limetoka kwa sasa) alipita na kuwaona swahaba wawili mmoja mu-Aws na mwengine ni Mu-Khazraj wamekaa wanazungumza kwa furaha na kutaniana, yule Myahudi akakasirka sana akaenda kumwita Myahudi mwenzake ambaye hapana shaka yoyote alikuwa na kipaji cha uchonganishi ili akawochonganishe wale swahaba wawili.

Yule Myahudi akaanza kuwakumbusha uadui wao wa zamani, mshairi ya kiuadui waliyokuwa wakitungiana, na mambo mengine mpaka wale Swahaba wakaanza kuchukiana na kutoleana mapanga kutaka kupigana!

Baada ya kutenganishwa Mtume swalalahu alyhi wasallam akaja kwenye tukio na katika aliyowaambia ni kuwa wasirudie katika hali yao ya ujahiliya, ndipo ilipoteremshwa aya hii (3:103)

sasa mtu akiangalia sababu za kuteremshwa kwake ataona kuwa ni khaaswa (mahsusi) kwa hawa swahaba wawili LAKINI KATIKA LAFDHI (tamko) INAMAANISHA NA NDIO KUSUDIO NI KWA UMMA MZIMA.
 

Sideeq,

Salaam.

Ahsanta sana kutujaalia hishma na kubainisha kwa utuvu.

Nilihisi lazim pangetokea Mwanajamvi mwengine kuja kuturekebishia na kutushereheshea. Ilikua ni katika mazungumzo tu kiduchu ya kistaarabu na ndugu yangu JokaKuu.

Lazim nikiri, nami umahiri wangu kwenye "minyambulisho mikali"ya Qur'aan si mzuri saana.

Insha Allah,Mola takulipa kwa fadhila yako hii na nyinginezo.

Ahsanta.
 
Sijui kama nimekuwa mnafiki na mzandiki kama usemavyo. Mimi nilidhani kuwa natoa mchango wangu na katika kufanya hivyo nisingependa kumuudhi au kumpendeza mtu. Siku zote nasema nitasema ninachotaka kusema si kile mtu anachotaka kusikia.

Lazima utambue kuwa baadhi ya kejeli zinakaribishwa na wahusika. Mohamed anasema Nyerere alipokuja alikuta watu wa mjini tayari kwa maana nyingine kuna washamba huko alikotoka hakuna miji.

Kaenda mbali na kuonyesha Kaptura(mwaka jana) na kusema alitambulishwa kwa wazee wa jiji na akina Abdul waliomkweza hadi kileleni. Kwa mwingine hilo ni kama dhereu na hapo mtu mwingine atatafuta neno, mathalani, watu wa kariakoo n.k kama kujibu.

Na ieleweke kuwa katika mnakasha kuna watu wenye hulka, haiba, ilm na tarbiya tofuati na hivyo kuvumiliana ni sehemu muimu sana ya mnakasha kama ninavyokuvumilia unaponiita mzandiki na mnafiki ambayo ni haki yako kabisa kama ilivyo kwangu nifanyavyo hivyo.

Pili, nimeeleza kuwa kama mtu anajivunia madrasa(jambo jema) afanye hivyo kwa dhati na si kwa unyonge. Kinachotokea hapa ni kuwa watoto au vijana wanaona kuna udhalili fulani ukiwa wa madrasa. Break the circle of inferiority complex and build the sense of confidence

Madrasa ni sehemu ya kupata maarifa, na maarifa si physic au chemistry tu hata tarabiya al islam ni maarifa ya kuishi na jamii. Ndivyo elimu zote zilivyo hata kama zina utofauti huko mbeleni.

Sijui lugha yangu imekuwa na tatizo gani na ningepaswa kusema nini lakini nina hakika mwenye kutizima hoja zangu na si Nguruvi3 bila prejudice ataelewa ninasema nini.

Kuhusu waislam kushughulikia mambo yao kama madrasa, endapo hilo linatokea ni jambo jema sana na liungwe mkono, nisichokubalina nacho ni kutafuta sababu zisizo na mashiko kama zile za chuo cha ufundi kibaha na kuzifanya agenda hata kama hazina ukweli.

Kuhusu radical muslims na wachochezi, wanaokubalina au kukataa hoja za Mohamed in a way hawapo katika kundi hilo kwasababu mnakasha lazima uwe na watu wenye mitizamo tofauti. Nadhani unakubali kuwa sote tunajiufunza kutokana na mnakasha.

Hii haiondoi ukweli wa mchochezi anayezusha mnakasha na malumbano kama mzee wetu ambaye mara nyingi ameshindwa kusimama na kutetea hoja zake.

Ni lazima pia uelewe kuwa hakuna kupingana au kukubalina, kuna uchambuzi wa hoja.
Hivi nitapinga nini kuhusu K.Sykes kuwa katibu wa AA? Nisichokubalina nacho ni kuwa yeye peke yake ndiye muasisi na kuficha majina ya waasisi halisi kama Matola.

Nadhani lugha yangu ni njema kabisa kama mtu ataangalia hoja, na ni mbaya sana kwasababu ya kusema ukweli bila kuupaka manukato, au kunyunyizia hamira. Inategemea unaangalia vipi maoni ninayoita ''hoja'' kama ulivyowahi kuniambia huko nyuma.

Niwatake radhi wanaokereka na hoja zangu lakini sitaomba radhi kwa hoja zangu. Ninasima nazo kama zilivyo kwasababu ninaziandika nikiwa nafahamu naandika nini.

Na mwisho, je hayo niliyosema kuhusu madrasa,mitaala na walimu au chuo cha kufunza walimu yana makosa? Ni uongo? Je, kuwashauri watu wawe na confidence ni makosa?

Ningeshauri watu wajibu hoja badala ya kuwa na curiosity ya communication skills zangu. Kila mtu ana namna yake ya communication na wala sijisikii vibaya nikaambiwa nina the worst communication skills kwasababu wapo wanaoniambia nina the best communication skill. The beauty is on the eye of the beholder
 

Muheshimiwa Nguruvi3,

Nashukuru ndugu yangu. Nimekusoma na nimekufahamu kwa makini.

Basi naomba tuendelee na mnakasha kwa usalama na staha,sisi soote ni wamoja/Watanzania.

Ahsanta.
 
Ndugu zangu Waislam nadhani mmeona ushauri mzuri mliopewa na ndugu yenu Nguruvi3, anawapendeni sana na ana mahaba mazito na nyie, hebu apa chini tumsome anapokuwa katika chama chake cha Chadema kinachoongoza na Padri wa zamani kama wao wanavyomuita.
Mbunge wa Jimbo la Karatu Mchungaji Israel Natse (CHADEMA) na mbunge wa jimbo la Iringa mjini
Mchungaji Peter Msigwa Chadema wana makanisa yao kabisa lakini wao wakiongea na ndugu zao kanisani hakuna tatizo.
Leo kwa mtu mwenye weledi na fikra timamu itamchukua muda sana kufikiria kujiunga na CUF kwasababu tayari chama hicho kimepoteza maana ya chama cha siasa na kimepoteza kitu kinaitwa Diversity(mchanganyiko)
Huyu kosa lake ni kuongea na Waislam wenzake Msikitini ndugu zangu Waislam wazee wa Madrassa mimi nawaacha ni vikazi kidogo nafanza.
 
Last edited by a moderator:
Ritz, nimeshasema sana kuwa spinning si kitu kizuri. Ingawa watu wanakutetea na pengine kudhani nakuonea mwenyezi mungu analeta heri zake.

Hiyo nukuu umeichukua ''Duru za siasa''.
Kwanza nisema kuwa sina chama cha siasa kama unavyosema. Pitia maandiko yangu yote uone jinsi gani ninavyokichambua kila chama kwa mujibu wa maoni na tahmini zangu.
Hili la kusema mimi ni mwancham wa Chadema umeniwekea, kama ningelikuwa hivyo sina sababu ya kukataa.

Kitu kimoja ambacho kipo kwenye rekodi yangu ni kuwa sipendi CCM na nimesema hata PPT maendeleo ikichukua nchi nitafurahi kwa kuangalia miaka 50 iliyopita. Ipo katika rekodi za JF.

Kwenye hiyo nukuu kutoka duru za siasa, kuna sehemu kuu mbili.
Sehemu ya kwanza nimeelezea kuhusu Lipumba, sehemu ya pili nikaelezea kuhusu Edwin Mtei na kauli zao.
Nikafanya ulinagnifu wa kauli ya Lipumba na ya Mtei na nimesema kama Lipumba anakuwa responsible na kauli zile basi Meti atakukuwa responsible equally.

Ukisoma heading utaona nimeandika nini. Na katika maandishi yangu sikuwahi kusema kwanini amezungumza msikitini.
Nimesema kuhusu kauli zake tu. Sasa hiyo spinning unayofanya siyo nzuri.

Naweka kila nilichokiandika PROF LIPUMBA HATAGOMBEA TENA UONGOZI WA NCHI
KAULI ZA MZEE MTEI ZAGEUKA KUWA SHUBIRI KWA CHADEMA
ili watu wasome na waone jinsi gani spinning zako zinavyoharibu, kuudhi na kukirihisha watu wengine. Na hapa namualika Gombesugu aliyesema unaumia kwa lobbying zangu kwa invisible.

nitaweka hapa chini kile nilichokisoma hata kama link ipo ili ukweli utawale
Halafu nitahoji kauli za Ritz alizoniwekea mdomoni
 
YERICKO NA MOHAMMED SAID;
Inaninibidi niwa-address nyote wawili kwa vile nimeona jambo ambalo kama halitarekebishwa basi huenda hata huu mnaksha hautakuwa na tija kwa wanaotusoma.

1. Mada ya mnakasha huu sio ya dini. Mada inaeleweka na sio ngumu. Kinachotakiwa ni Yericko kutuwekea wazi (hata ikibidi kurudia-ili kukumbusha) kwa nini unadhani MS ni Mchochochezi na yeye MS atueleze umma wa TZ kwanini yeye sio Mchochezi. Muhimu lazima maana ya UCHOCHEZI ieleweke ili MS apime kama anachokifanya ni uchochezi ili naye ajitetee. Watu waweze kupima tuhuma na utetezi.

2. Hadi sasa, mnakasha umeachiwa kuingiza mambo mengi tena yasiyouhusu kwa kiasi kikubwa sana. Ni kwamba sasa kila anayesoma ataona ni kama vile uislamu na ukiristo ndio vinalumbana. Mada haikuwa kutafuta mbora kati ya dini hizi au historia zake katika nchi zetu hizi au kwingine. Binafsi sioni kama ni njia nzuri ya mwelekeo na wala siamini kuwa baada ya kuzilumbanisha dini hizo mbili ndio suluhu ya tuhuma zilizotolewa kwenye uzi huu zitapatikana. Kwa hiyo nawashauri nyote wawili mrudishe jahazi kwenye mada mama. Forum za dini zipo na anayezitaka azifuate kwa wakati wake.

3. Kutokana na (2) mnakasha unawagawa wachangiaji katika dini na sio mada wanazosimamia. Wanaowagawa wachangiaji katika matakwa ya dini wameachwa huru kufanya desturi hii bila aina yoyote ya kuwajibika na hii inawapa ari ya kuwatia uoga wasomaji wengine kuchangia ili wasionekane hawaendi kama kundi lao linavyoenda wakati ambapo mawazo yao yangenufaisha wasomaji wengi kwa mifano yenye tija na kupanua uelewa wa watu wengi

4. Itakuwa ni hasara kama baada ya muda wote wa kuwa hewani tutaambulia kutojua nini kifanyike katika haya tunayojadiliana hivi sasa. Na hili huenda likawa sio la kushangaza kama hizo point tatu zilizotangulia hazitawekwa sawa

5. Kama tuhuma zilishatolewa na kujibiwa tunaomba kuzijua na ikiwezekana tuelewe nini hatma yake. Kama hakuna kitu kama hicho cha makubaliano (pia ni uungwana) sio mbaya kambi hii tukaifunga ikapisha nyuzi zingine tukachangia.

Wasalaam
 
Wanajamvi hiki ndicho nimeandika kule Duru za siasa.
Someni halafu linagnisheni na kauli za Ritz#15962 ili muone spinning na jinsi alivyoniwekea maneno.
Alichokifanya si kuchukua dhana ni kukata mistari ili kuleta maana isiyokusudiwa.

Natumaini Gombesugu atachangia hili katika kumtetea Ritz, ningependa sana kusoma maoni yake, na nitashangaa kama hatamtetea


 
Leo mda mfupi uliopita kupitia TBC taifa katika kipindi cha "Wosia wa Baba"

Hotuba ya kuwaaga wazee wa jiji la Dar imerushwa hewani, hakika imerushwa kama ilivyo hapo juu na maeelezo mengine mengi sana katika sehemu iliyosalia ya hotuba hiyo hapo juu!
 
Nguruvi3;
Nimekusoma shukrani sana. Ni kawaida ya wanasiasa kuwatumia watu ili kujinufaisha. Siasa ni maslahi sio Taqwa. Sasa huyu Prof yupo kwenye exit of political career. Kama kawaida ya watu wa aina hiyo ataanza kukumbuka wakina sheikh fulani wako wapi ili aungwe mkono. Infact ni ile hali ya kuona shida ya kuingia kwenye political museum.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…