Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Ritz,
Ahsante sana shariff.
Kuna watu wanataka wajibiwe maswali yao.

Kumekucha na Dk. Harith!
Wahenga wamesema, ''Usilojua usiku wa kiza.''
 
DR HARITH, kumbe kafanya utafiti wa kina kuna mengi hayajulikani kwenye Mapinduzi ya Zanzabari.

Nafyonza Ilm.

Spike; M/Mungu amzidishie huyo bwana bidii na tuzo. Hapa kwa hakika hatutakosa subira ya kupata JIBU la MASWALI tuliyotanguliza. Dr Harish kaonyesha vizuri, nani alikuwa anamsaidia nani ili afanye nini. Na hata yeye mwenyewe kwenye hicho kitabu kawanakili CIA wakionyesha ASP wakipokea silaha toka kwa kina Oscar Kambona. NDIYO MAANA TUNAULIZA MISAADA HII NA ILE YA SAKURA YA WAMAKONDE WA KIPUMBWI, ALIYEMWOMBA MWENZIE NI NANI? NANI ALIYEKUJA NA AGENDA YA KUTAKA KUIANGUSHA SERIKALI YA ZENJ? NI TANU AU ASP? NA MBONA MWOMBAJI HAPEWI WA MSAADA HALAUMIWI ANALAUMIWA MTOAJI?

TUMEKWAMA. GARI HAINA 4WD
 

Spike Lee,

Huyu Mohamed Faik alikuwa mtu wake sana Ahmed Rashad Ali
enzi Rashad anatanga za Radio Free Africa, Cairo katika 1950s.
Mohamed,
Ungemsaidia basi Ghassany kuandika Kiswahili sanifu. Kuanzia badala ya kuanziya.
 
Ritz,
Ahsante sana shariff.
Kuna watu wanataka wajibiwe maswali yao.

Kumekucha na Dk. Harith!
Wahenga wamesema, ''Usilojua usiku wa kiza.''

Mohamed Said,

Dkt Ghassany ameacha maswali mengi katika andiko lake ambayo kimsingi yanahitaji majibu yake/yako,

1) Mapinduzi ya Zanzibar ni HALALI au HARAMU?

2) Kwanini wazanzibar WOTE wanaadhimisha mapinduzi ya Zanzibar kila mwaka?

3) ASP iliomba msaada wa Mapindizi kwa TANU?

Nk.........!

Hoja zetu zinasimama kama zilivyo!
 
Ritz,
Ahsante sana shariff.
Kuna watu wanataka wajibiwe maswali yao.

Kumekucha na Dk. Harith!
Wahenga wamesema, ''Usilojua usiku wa kiza.''

Sheikh Mohamed Said,

Kitabu cha Dr Harith kina majibu mengi sana kimejaa tafiti za kina.

Mwandishi kafanya sana kazi kwenye utafiti wa kukusanya ushahidi.

Watu wangekisoma hicho kitabu wala wasingekuwa wanaangaika kuuliza masuali.

Watu wawe na subra majibu yapo mengi Wanaukumbi ndiyo watakaoamua mimi takishusha kitabu chote humu chenye kurasa 500 watu wafyonze ilm.
 
Last edited by a moderator:
Ritz,
Ahsante sana shariff.
Kuna watu wanataka wajibiwe maswali yao.

Kumekucha na Dk. Harith!
Wahenga wamesema, ''Usilojua usiku wa kiza.''

Mzee MS; Swali la nani alimwomba mwenziwe msaada wala halihitaji taabu. Bora wewe umeshajitoa KULIJIBU. Kwa sababu unajua FIKA kuwa yule aliyekuwa anakusanya Wamakonde (popular guys) kwenda kumpigia kura wakati wa chaguzi za Zenj anajulikana (Ref. Kwaheri Uhuru....) ANAJULIKANA.

SWALI NI; JEE ASP WALILAZIMISHWA KUPOKEA MSAADA WA SILAHA NA ASKARI (WAMAKONDE WA KIPUMBWI) AU WAO NDIO WALIOUOMBA MSAADA HUO TOKA KWA UONGOZI WA TANU/TANGANYIKA?

SWALI LINASIMAMA KAMA LILIVYO
 

Utakuwa umefanya la maana Ritz; Ila katika page zake (500pgs) zote hakuna mahali kaonyesha kuwa ASP walilazimishwa kupokea msaada, ambalo ndilo swali husika kwa tunavyojadiliana. Hakuna. Sijaliona across the entire book. Jaribisha na wewe labda nilikhalifika.
 
Last edited by a moderator:

Yericko,

Mimi nisingetegemea wewe kuuliza masuala kama haya. Kwani kwa kila jambo lazima liwe na negative side na positive side. Na hata mapinduzi yoyote Duniyani lazima yatakuwa na positive side na negative side kwa wananchi. Hivyo ni jukumu lako kusoma kitabu na kisha kufanya maamuzi kuwa kwa mtazamo wako mapinduzi hayo yanasimamia wapi.

Kumbuka kuwa kazi ya mwandishi ni kuielimisha na kuipasha habari jamii NA WALA SIO KUIAMULIA JAMII ifate msimamo upi.

Kwa mantiki hiyo utaona fika unalazimisha mwandishi akupe msimamo wake jambo ambalo ni jukumu la msomaji kujiona anaweza simamia wapi.

Lakin vile vile siku hiyo kusherehekewa hilo ni wazo na matakwa ya Serikali kwani ni kama siku ya Nyerere day au Karume day kuwa siku za ijaz kwenu na wanaweza sema hata siku ya kuzaliwa mama wa Taifa iwe Ijaz. Hilo lisikupe mushkira ni maamuzi tu ya kikundi cha watu wenye maslahi nayo na kuinasibisha na wananchi wengia.

Zamani wa Tz wote walikuwa wanapumzika siku ya taarih 5 Feb siku ya kuzaliwa CCM. iwe mwanachama au sio mwanachama basi unapumzika na wenye sherehe ndio wanasharaheka.

Kumbuka kuwa kuna KUSHEREHEKEA na KUPUMZIKA, hivi ni vitu viwili tofauti.

pole sana
 

Mimi ninachofanya ni kuweka bayana habari za Mapinduzi kutoka kwa Dr Harith kuna wanaukumbi wengi hawajuhi hizi habari hayo masuali yako wala hayana tija yoyote kitabu cha Dr Harith kimemaliza kila kitu.
 


Naam.,

Mwaga nyuki hapa,walishaanza kuwatangazia jamaa zao kwamba wana ghahawa wamekimbia ukumbi...!

Wanapewa taarifa za utafiti na rejea zake,badala ya kuzisoma wao wanakimbilia kuuliza maswali yasiyo na tija...
 
Mimi ninachofanya ni kuweka bayana habari za Mapinduzi kutoka kwa Dr Harith kuna wanaukumbi wengi hawajuhi hizi habari hayo masuali yako wala hayana tija yoyote kitabu cha Dr Harith kimemaliza kila kitu.

Sawa kabisa
 
Wanajamvi,
Maswali ni rahisi sana wala hayahitaji kishikizo kiwe cha nukuu au picha.

1. Wickama anasema hivi anashawishika kabisa kuwa mapinduzi yalikuwa na chagizo fulani.
Kinachomtatiza ni kitu kimoja, hivi hawa Wamakonde wa Kipumbwi walipelekwa na TANU kwa nguvu au kulikuwa na ombi kutoka kwa ASP?

2. (a)Nguruvi3 nauliza, hivi mapinduzi ni kitu halali au haram kwa kuzingatia maandiko ya Gahssany na Mohamed Said
(b)Hivi haya maandamano ya kushangilia mapinduzi wanayofanya wznz ni halali au harama ?
(c)Hawa akina Mwinyi, Jumbe n.k. wanaangukia kundi gani la wanamapinduzi au vibaraka wa Nyerere.

Nashangaa tumeamua kukata vipande vya vitabu kana kwamba havijasomwa. Tumesoma sana ndio maana tuna duku duku na baadhi ya hoja kwa maana hatuzielewi. Tusaidieni tufyonze ilm
 
Mimi ninachofanya ni kuweka bayana habari za Mapinduzi kutoka kwa Dr Harith kuna wanaukumbi wengi hawajuhi hizi habari hayo masuali yako wala hayana tija yoyote kitabu cha Dr Harith kimemaliza kila kitu.
Ha ha haaa, ya Al Akhiy Mohamed Said bado na sasa kaingia Dr. Harith...Al Akhiy Ritz, je kuna lolote umejaribu kuhoji kutokana na maandishi ya huyo dokta au kama kawaida ni kumeza tu? Mohamed Said na Dr. Harith ni kama mtu na pacha wake, wamekuwa wakicheza boli bila refa wala timu pinzani lakini watamazaji watiifu duh, kwa kushangilia mchezo ulivyonoga! Hakuna hata shabiki moja anayeuliza kulikoni? Haya, chenga mwawala ingawa hawaonekani...hata chandimu kiboko! Hebu tuendelee...

Sultani Jamshid bin Abdullah baada ya vitisho vya kiongozi wa Mapinduzi Field Marshall John Okello ule usiku wa tarehe 12 Januari, 1964, aliamua kuikimbia Zanzibar. Aliwakusanya wanafamilia wake, ndugu zake, rafiki zake woote wakiwa ni Waarabu akawajaza kwenye boti na kuondoka. Cha ajabu ni kwamba hakuwakumbuka hata marugaruga weusi waliokuwa ndani serikali yake na badala yake aliwaacha at the mercy of His Exellency Field Marshall John Okello, mwenyekiti wa kwanza wa baraza la MAPINDUZI!

Kama ilivyotegemewa Kenya iliwakatalia kutia nanga mjini Mombasa na hivyo kubaki wakitangatanga baharini wasijue la kufanya kwani hata Oman hawangepokelewa, mahusiano yaliishavurugika kitambo tu. Ni Mwalimu Nyerere aliyewaokoa na janga hilo kwa kuwapa hifadhi mjini Dar es Salaam wakati juhudi zikifanyika kutafuta nchi itakayokuwa tayari kuwapokea. Pamoja na usafiri wa ndege kupatikana kuwapeleka Uingereza, hiyo ndege haikuweza kutua kwenye uawanja wa Heathrow kama ilivyopangwa awali na ilibidi watue kwenye uwanja wa Manchester na hadi leo hii wanaishi huko.

Ninayo matumaini kuwa hadi leo Ex-Sultan Sayyid Jamshid bin Abdullah Al Said popote pale alipo atakuwa anakumbuka fadhila, utu na moyo wa huruma aliokuwa nao Baba wa Taifa...lakini kama na yeye anaungana na wachochezi kumtukana Mwalimu, nadhani kama ni laana haitampita kando. Je, Al Akhiy Ritz, katika hivyo vitabu unavyovisifu kwa kufichua yaliyofichwa kuna popote wameandika harakati za Sultani huyo kutafuta hifadhi na alivyoweza kunusurika na hiyo kadhia maanake leo huenda tungekuwa tunasimuliana mengineeee...!

Kwa kumalizia kuna kitu nimekigundua humu kuhusu shariff Ritz, naona kila ukibanwa unafanya mojawapo katika haya mawili;

  1. Kulilia huruma kwa dai la Uislaam kudhalalishwa/kutukanwa.
  2. Kuweka nukuu ndeefu kutoka maandishi yale yale tunayoyapinga.
shariff toka mjadala uanze ukiacha hayo, huna chochote kipya unachochangia sana sana unapiga tu chorus, yaani huna tofauti na kasuku, kwa nini usikae kimya ukafyonza kama Spike Lee hata kama unachofyonza hakina rutuba? Tusiwe kama wazee wetu walivyopokea neno "shikamoo" bila kuhoji lina maana gani...
Jibuni maswali mnayoulizwa kuhusu mapinduzi, acheni kuzunguka mbuyu.. Ritz na Mohamed Said.
 
Last edited by a moderator:
THE BIG SHOW,

Majibu kwa wanaukumbi nadhani umeyaona taratibani tutaendelea kuleta bayana za mapinduzi ya Zanzibar kutoka kwenye kitabu cha Dr Harith.
Badala ya kuquote kitabu cha Dr. Ghassany, unaweza kutoa majibu juu ya maswali yaliyoulizwa na Wickama, Nguruvi3 na Yerricko kuhusu mapinduzi? Samahani kama nitakuwa nimekukwaza kwa swali hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…