Hata mimi nilikuwa sielewi kuwa wamakonde wa kipumbwi walipelekwa na Nyerere kule znz kumuondoa Sultan.
Ninapochanganyikiwa ni kuwa, hivi kati ya TANU na ASP nani aliomba msaada wa wamakonde wa Kipumbwi?
Halafu hawa akina Thabiti Kombo Jecha, Nassor Moyo, Natepe, Jumbe na Mwinyi na wengineo wamefanya kazi na huyu ''kafir'' Leo wanaitwa wana mapinduzi, je ni wanamapinduzi kwa heshima au ni wasaliti.
Ninapochanganyikiwa zaidi na 200K wanaomsikiliza mzee ni kuona wazanzibar wanasherehekea Mapinduzi.
Sasa ni halal au ni haramu?
Na pia nataka nielewe kutoka kwa Mohamed kama haya mapinduzi ya kuumaliza Uislam visiwani ni halali au haramu.
Hapo ndipo namwalika mzee aongee na 200K maana miongoni mwao wamekwama!
Anapokaa kimya ndio uchochezi wenyewe unaosemwana sitaki kuamini kama ni uchochezi labda akiendelea kukaa kimya.
Vipande vya vijitabu havieleweki, tuwafanyie tahfifu hawa 200K wanotaabika na vijihoja vidogo.
Ima akiendelea kukimbia basi uchochezi utakua mubashara aje hapa aweke bayana.
Spike lee naona tutulie tumsikilize Mohamed Said, hiyo ndiyo tarbiya al islam.
cc Twalib, Swahba, Al-akhyi, al watan na wanajamvi.
Nguruvi3
Crusade war haitakusaidia,na chuki zako dhidi ya uislam hata kama unajaribu kuzificha na kuzionesha tambua ya kwamba pia na hiyo haitakusaidia,
Unapokuja na kuubeza uislam kwa kutoa kauli zako za kuzunguka mbuyu sisi tunakuona umefili hata kabla hiyo mission yako hujaianza,
Na hakuna aliekuambia hapa kwamba Kuondolewa kwa sultan zanzibar basi ni kuanguka kwa uislam,
Labda nikuulize,unauliza hilo kwa dhati ya kutaka kujua au kwa mantiq ya kuuvaa na kuukejeli uislam??
Kipindi sultani anatawala zanzibar kulikuwa kunaendeshwa kama dola ya kiiislam??
Kama ni kweli weka uthibitisho,kama si kweli jipime mwenyewe na uone chuki yako ni ya kiwango gani dhidi ya uislam na waislam??
Inawezekana kabisa ya kwamba walikuwapo waislam ambao walikuwa wanaish zanzibar kipindi hicho cha usultani na walikuwa hawaufurahii uongozi wa kisultani kwa namna moja ama nyingine,unalizungumzaje hilo?
Je unafaham uislam uliingia lin zanzibar??kabla au baada ya usultani???
Tunachokuambia hapa ni kwamba mumeshindwa kuuonesha uchochez wa Moh Said,na mnachokifanya ni kuangaza huku na kule kutafuta kitu ambacho mtaegemea kutafuta uthibitisho lakini bahati mbaya sana mmekosa,
Moh Said hayupo hapa kuweka ligi na mtu au kuweka ubishani,yeye yupo hapa kuweka uhalisia wa historia,
Kama umeshindwa kuiamini na kuikubali ni juu yako,wapo wanayoiamin na ni wengi wenye weledi wao,kama wewe umeshindwa kuafiki kwa kuona Juhudi za ukristo na wakristo hazipewa nafasi kama unavyojaribu kuongelea ni sawa pia,
Lakini uhalisia uko hivyo,na utabakia kuwa hivyo....