Nguruvi3
Crusade war haitakusaidia,na chuki zako dhidi ya uislam hata kama unajaribu kuzificha na kuzionesha tambua ya kwamba pia na hiyo haitakusaidia,
Unapokuja na kuubeza uislam kwa kutoa kauli zako za kuzunguka mbuyu sisi tunakuona umefili hata kabla hiyo mission yako hujaianza,
Na hakuna aliekuambia hapa kwamba Kuondolewa kwa sultan zanzibar basi ni kuanguka kwa uislam,
Labda nikuulize,unauliza hilo kwa dhati ya kutaka kujua au kwa mantiq ya kuuvaa na kuukejeli uislam??
Kipindi sultani anatawala zanzibar kulikuwa kunaendeshwa kama dola ya kiiislam??
Kama ni kweli weka uthibitisho,kama si kweli jipime mwenyewe na uone chuki yako ni ya kiwango gani dhidi ya uislam na waislam??
Inawezekana kabisa ya kwamba walikuwapo waislam ambao walikuwa wanaish zanzibar kipindi hicho cha usultani na walikuwa hawaufurahii uongozi wa kisultani kwa namna moja ama nyingine,unalizungumzaje hilo?
Je unafaham uislam uliingia lin zanzibar??kabla au baada ya usultani???
Tunachokuambia hapa ni kwamba mumeshindwa kuuonesha uchochez wa Moh Said,na mnachokifanya ni kuangaza huku na kule kutafuta kitu ambacho mtaegemea kutafuta uthibitisho lakini bahati mbaya sana mmekosa,
Moh Said hayupo hapa kuweka ligi na mtu au kuweka ubishani,yeye yupo hapa kuweka uhalisia wa historia,
Kama umeshindwa kuiamini na kuikubali ni juu yako,wapo wanayoiamin na ni wengi wenye weledi wao,kama wewe umeshindwa kuafiki kwa kuona Juhudi za ukristo na wakristo hazipewa nafasi kama unavyojaribu kuongelea ni sawa pia,
Lakini uhalisia uko hivyo,na utabakia kuwa hivyo....
Nadhani kama yupo anayesimama mimi ni mmojawapo. Nimeshawahi kusema hapa kuwa Uislam ni dini ya mwenyezi mungu.
Mimi ninapozuia watu wasiunasibishe uislam na hadithi au chuki zao ni jambo jema kuliko wale wanaoshangilia uislam kutumika kama ngazi ya watu kuzua uongo, kueneza chuki na fitna na kuudhalilisha.
Mohamed amesema mara nyingi nia ya Mapinduzi ni kuua Uislam kule Zanzibar.
Kwa wale waliosoma vitabu na kufuatilia hoja zake hapa hawana shaka na hili.
Hivi karibuni ikafika mahali pa kusema wale waislam wa Tanga walioshirikiana na Nyerere ni ''punda'' akiwataja kama Punda wao. (ushahidi upo)
Ghassany na Mohamed katika kitabu chao wanasema Zanzibar ilikuwa shwari hadi pale Nyerere alipoleta fitna yake.
Juzi akiwa Kibanda Maiti Seif alisema Zanzibar ni nchi ya Kiislam. Madai hayo yameshadidiwa na suala la OIC hata kama tunafahamu kuwa si kweli kuwa ni nchi ya kiislam bali nchi yenye waislam wengi. Kuna tofauti.
Mohamed ameanisha watu kuwa wamakonde wa Kipumbwi ndio walipelekwa ZNZ kufanya mapinduzi kwa maelekezo ya Nyerere na misaada mingine. Lengo la Mohamed nikuonyesha kuwa Nyerere alikuwa na chuki na wazanzibar si kwasababu nyingine ni kwasababu ya Uislam. Ni chuki hiyo hiyo ya Nyerere ndiyo ilimuondoa Sheikh Amir.
Kabla 200K haijaondokewa na shaka juu ya Mohamed tumemuuliza
Je, Wamakonde wa Kipumbwi walipelekwa kwa ombi la nani, TANU au ASP au ilikuwa unilateral decision ya Nyerere kuua Uislam kama anavyodai na wala si mimi ninayesema hayo.
Pili, Mapinduzi ni halali au ni haram?
Tatu, wznz wanaposherehekea mapinduzi ya Nyerere yalilyolenga kuua uislam wanafanya jambo jema au ni wasaliti
Tatu,akina Thabiti Kombo, Jumbe na Wanamapinduzi wengine waliofanya kazi na Nyerere ni wanamapinduzi au wasalaiti?
Haya ni maswali muhimu sana hasa ukiangalia suala la Kipumbwi, Nyerere na madai ya Uislam yatolewayo na Mohamed.
Mnaponishambulia mimi ninayeuliza ili kuweka hoja sawa badala ya kumtaka mtoa madai athibitishe ninawashangaa sana.
Mimi nitasimama na ukweli, najua inawakera sana kuona mzee ameshindwa kuwaambia 200K juu ya madai yake.
Mzee anazidi kutia hofu 200K kwasababu kila mara amekuwa anatoa madai asiyoweza hata kujaribu kuyatetea.
Najua inawauma kuona mzee kasimama mbele ya kadamnasi mambo yakiwa kombo sasa mnatafuta mahali pa kumuokoa.
Mumejitahidi na nukuu na picha haikuwezekana, kama kawaida yenu mna chomeka mambo ya dini mkijua kuwa hoja itakufa kwavile sisi wengine tunaheshimu sana imani za watu na hata wale wasio na imani au wasio amini. T
unaheshimu kila mtu.
This time around mnapaswa msimame na kumwambia Mohamed ima aombe radhi kwa 200K kwa kutoa madai asiyoweza kuyatetea au asimame na atetee kile anachojua.
200K haiwezi kudanganywa kila mara na kuacha mambo yapite. 200K ina kiwewe cha mambo lukuki ikiwemo Ibadan, sasa mnaachia na huu msumari wa moto juu ya donda! ndugu zangu tuwaonee watu huruma. 200k ni idadi kubwa sana kudanganywa kirahisi.
Lakini pia mwambieni mzee kuwa anaposema wznz ni ndugu zake basi awaambie ukweli kuwa mapinduzi ni haramu, la sivyo awaambie ni halali.
Kusema ukweli ni sifa ya mwislam.
Ni wakati sasa msimame na kumwambia Mohamed asinasibishe maneno yake na iman.
Pamoja na yote niliyosema hapo juu 200K wanasubiri majibu.
Mohamed Said Waambie 200K jambo kuhusu uliyoulizwa.
NB: Tafuteni mstari au fanyeni spinning ili kumuokoa mzee. Msitumbukize imani kwasababu hiyo mnaifanya silaha yenu.
Nime stick mzee awaambie wasomaji wapatao 200K ukweli, hamtaweza kuniondoa katika mada kwa spinning au kuchomeka mambo ya dini.
Naambiwa na wenyeji wa JF haijapata kutokea, watu 200K! Sasa awaambie ukweli.