Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Huwa tunashangaa ujinga, tunashangaa watu wazima wakijidhalilisha pia....

SASA KM UNASIFIA MADRASSA NA KUIPONDA ELIMU DUNIA(KRISTU), HUYU MS ANAPIGANIA NINI NA VITABU VYENYE HADITHI ZA KUSADIKIKA WAKATI WAMESHAPIGA MGONGO ELIMU?HALAFU MKIAMBIWA MLIKIMBIA SHULE WENYEWE MNAANZA BADILIKA NA KURUKA VIHUNZI....MMEAMBIWA MARA NYINGI KUWA WAZEE WENU WALIKATAA MSIENDE SHULE MKAJAKUWA WAKRISTU, HUKU MKIAMBIWA KUWA ILM NDIO KUBWA SANA,NA WAZUNGU WALIIBA NA KUBADILI ILI IWE YAO...MIAKA YOTE HAMJAJIULIZA MASWALI YA MSINGI ..

Kweli spirit iliyowaingia imeondoka na ufahamu wote.
 
Mkuu wa chuo,take note mambo muhimu haya kwa shule yako

hizi ni nondo haswaa zitasaidia katika shule yangu lakini hapa Abu Jahl Ritz amevaa miwani ya mbao na pamba masikioni hasikii wala haoni pamoja na ndugu yake Ahsanta basi hawana hata akili ya ku reasoning we mtu unaambiwa mtu alitoka kwa baiskeli Dar hadi Rufiji kugawa kadi za Tanu mtu unaamini tu...

Ndio mambo yale yale ya Jamaa aliyetoka Geita kwa baiskeli hadi Magogoni Dar es salaam kuja kumpa hongera JK kwa kushinda uchaguzi...

Shule kama hii ni muhimu kwa ajili ya kujifunzia logic...
 
Last edited by a moderator:


Mkuu wa Chuo,
Najua unapata tabu kuamini kuwa Said Chamwenyewe akisafiri kwa baiskeli
kutoka Dar es Salaam hadi Rufiji akiuza kadi za TANU njiani katika vijiji kama
vile najua itakuwa tabu kwako kuamini kuwa na hizo fedha akipata alikuwa
akiziwasilisha ka mweka hazina wa TANU Iddi Faiz Mafongo bila ya yeye kutoa
hata senti moja kwa matumizi yake binafsi.

Hali kadhalika najua itakuwa tabu kwako kuamini kuwa Rashid Ali Meli bila ya
kumshauri yoyote alichukua fedha kwenye safe ya ofisi yake Dar es Salaam
Municipal Council akampelekea Iddi Faizi Mafongo ili atunishe mfuko wa safari
ya kwanza ya Nyerere UNO 1954.

Na kuna mengi ukiwekewa hapa utapata shida sana kuamini.
Nilieleza hapa kuhusu kabati la fedha la Abdu Sykes na watu wengi wakakebehi.

Lakini wenyewe wana TAA/TANU wanajua kuwa Abdu alikuwa ni mmoja wa wafadhili
wakubwa wa harakati kuanzia 1950.

Wazungu wanasema aki-bankroll na hakuna katika viongozi wa wakati ule katika
TAA/TANU ambae hakula fadhila za Abdu.

Ikutoshe tu wana TANU hawakuona nyumba ambayo Nyerere anaweza kukaa kwa
raha bila matatizo isipokuwa nyumbani kwa Abdu Sykes Mtaa wa Aggrey na Sikukuu.

Leo nyumba hiyo ya kihistoria marehemu Ally Sykes amejenga jigorofa kubwa.
Hakika ndugu yangu Mkuu wa Chuo shule kama hizi ni muhimu kwa kujifunzia logic...
 

ha haa haa!!unatumia nguvu nyingi kuandika mpaka mishipa ya kichwa inakusimama, meza hedex vidonge viwil na maji ya vuguvugu.

Baada ya miaka 15 kitabu cha Mohamed Said, kinazidi kupata promo, kitabu kinaitajika mikoani copy hazitoshi tunawashukuru sana nyie kwa kukipaisha kitabu cha Mohamed Said,

Unachofanya wewe ni kuangusha mbuyu kwa bajaji, teh teh teh.
 
Last edited by a moderator:


Wickama,
Hakika dunia ni zaidi ya AA/TAA/TANU/Abdulwahid Sykes na Julius Nyerere.

Umenikumbusha siku ya kwanza kukutana na Dk. Harith Gahassany nyumbani
kwake Muscat.

Niliona grand piano nikamuomba ruksa niitazame.
Nikapiga nyimbo moja ya zamani sana ''Crying in the Chapel.''

Alishangaa sana yeye na mkewe.
Kwao wao sifa zangu zilitangulia kuwa mimi ni ''siasa kali.''

Nakuachia hapo...
Hakika dunia ni zaidi ya mieleka ya jamvini JF.
 

Shariff Ritz,
Jamaa Ibadan imemkwama rohoni.

Kila akizunguka ataishia hapo.
 

Ya Kus Mkuu wa chuo,

Vipi tena hii bayana yako ya chuo nakushauri mtafute Yericko Nyerere, atakueleza mengi yenye logic hivi unajua kama Nyerere alikuwa ananuliwa nguo suti, sox, chupi, bukta, na chifu Maliale mpaka na gari kanunuliwa chukuwa hiyo kutoka kwa Yericko Nyerere,

Ya kus Mkuu wa chuo, nimekununulia cheni yako na dera zuri mikoni mirefu tayari kama ulivyoniagiza kama itakuwa kubwa basi utaibana kwenye hips, ha haa ha.

CC: gombesugu, THE BIG SHOW,
 
Last edited by a moderator:
Utizamwe kwa tahadhari kwasababu ya kauli zako, uchochezi na kuahidi usuluhishi utakaotokana na vita ya kidini na matamshi mabaya sana katika jamii (sijui kama nitaombwa ushahidi)

Nashukuru umekubali kuwa upo kujifunza na si kusomesha kama ulivyokuwa unasema hapo awali
Kazi ya mikono haikosi makosa kahiyo huna sababu za kutisha watu kwa reviews za ulaya, umeshasema ni ya mikono.

Matundu:
-Historia yako haikufuata kanuni za uandishi wa historia. Imeandikwa halafu matukio, nyakati,wahusika vikachomekwa.
-Masimuizi yako hayakufanyika kisayansi na kwa utafiti uliozingatia taratibu za utafiti bali utafiti wa ''infusion'' ya kaka yako mwenye PhD. Hakuna elimu ya infusion kuna elimu ya kusoma na katika utafiti hilo halipo.

-''Historia'' yako ililenga baadhi ya watu, matukio ya kuchagua na nyakati kama ilivyotokea
a)Kumshusha hadhi na kumdhalilisha Nyerere
b)Kuleta uchonganishi na imani zingine na hata kuwatenga wasioamini na wapagan
c)Kuwagawa watu kwa misingi ya imani na ukabila
d)Kujenga majina kwa gharama za watu wengine

-Kutokuwa na vithibitisho
a)Kuwahoji watu uliodhani wameonewa na kukosa sehemu ya pili ya waliodhulumu
c)Kutumia hisia ''inasemekana'' inasemwa, inadhaniwa, yawezekana kama vithibitisho vya tuhuma
d)Kuwatuhumu wakristo bila kuwa na ushahidi bali masimulizi ya siri baina yako na wazee wako waliojaa chuki kama wewe

- Kuficha ukweli
a)Ujio wa Mbuwane Sykes ulikusudia kuua wazalendo na msiba wake ulitokea akienda kuua Watanganyika
b)AA haikuwa mali ya K.Sykes na wala hakutoa wazo, yeye alikuwa mshiriki. Rais alikuwa Matola aliyejua anafanya nini
c)Nyerere alianza siasa kabla ya A.Sykes na alijulikana makao makuu kinyume na madai yako
d)Familia ya Sykes ilishiriki dhulma za mali ya chama kama nyumba iliyotolewa na gavana
e)Mchango wa Nyerere katika kuandika katiba ambayo haikuwahi kuandikwa tangu Mbuwane Sykes hadi Abdul Sykes
f)Nyerere alimshinda A.Sykes katika sanduku la kura mara zaidi ya moja kwa weledi
g)Michango kama ya Maryknol haikuonyeshwa kwasababu ya chuki za kiimani

h)Kifo cha AMNUT ni matokeo ya mifarakano, na ndio walioua EAMWS chini ya Sheikh Amir
i)Sheikh Amir aliendesha siasa majitaka nje ya chama,unafiki
ii)Aliwasaliti waislam kwa kukataa fursa ya kuwatumikia katika serikali
iii)Alihujumu pesa za makao makuu EAMWS na kupelekea chuki mikoani na kujitenga

Kuwagawa na kuwadharau Watanganyika
a)Kudharau jitihada za kwingineko kuhusu mapambano dhidi ya ukoloni
b)Kuifanya Tanganyika kama Narung'ombe na Kipata
c)Kuwafanya Wamanyema, Wazulu na Wanaubi kama wakombozi wa nchii hii(WWW)
d)Kuwapiga vita waislam kwa misingi ya AMNUT, ubara na (WWW)

Historia kuongoza ushawishi uliofikiriwa kabla ya historia
a)Madai yasiyo na ushahidi ya Namba za mitihani na Malima. Imehdihirika ni uzushi
b)Hotuba ya Nyerere ya kuaga, umeshindwa kutoa vielelezo vya chanzo cha matamshi uliyoyanukuu mwenyewe
c)Madai kuhusu ugaidi. Paper ya Ibadan iliandikwa kwa kunukuu bila kuangalia nukuu. Utafiti wa infusion. Uongo
d)Nyumba ya AA na TAA ilijengwa Jumapili, si kweli ilitapeliwa na kukarabatiwa jumapili na familia ya Mbuwane Sykes
e)Wamakonde wa Kipumbwi, umeshindwa kutoa ushahidi wa hilo kwa kuzingatia wakati tulio nao.

Kuwatenga Wazalendo wengine kwasababu ya Imani zao
a)Hukuwahi kumhoji Vedastus Kyaruzi hadi alipofariki hivi karibuni. Kyaruzi alikuwa kiongozi kabla ya Sykes katika siasa
b)Hakuna mahojiano na Kawawa hadi alipofarii hivi karibuni
c)Hukuwahi kufanya jaribio la kumhoji Nyerere bali ulisikia kupitia prof Othman
d)Mchango wa familia kama za Bomani haukuandikwa kama wa Mshume Kiyate na bi Farijala
e)Hukuwahi kumwelezea John Rupia zaidi ya Mshume au Idd Mwafongo kama si bi Mluguru

Kuiteka historia
a)Kuifanya historia kama ya waislam hata kama waislam wanaikataa kwa maneno
i)Abdul alisema(Mohamed)......ni kwa ajili ya ukombozi wa Mwafrika
ii)AMNUT walikataliwa na waislam wa Tanganyika
iii) Kutumia maneno sisi kuipa historia hisia zako na si za washiriki na matukio.

Kuchomeka ndoto zako kama historia
a)A.Sykes kuanzisha chama kwa fikra, katiba na mageuzi mengine yafanywe na Nyerere
b)A.Sykes hakushindwa uchaguzi mkali bai alimwachia Nyerere. Alishindwa na Nyerere katika uongozi wa TAA na TANU
c)Kumfanya A.Sykes Rais wa TANU. Hakuwahi kuwa Rais wa TANU hata sekunde moja
d)ASykes alikuwa Rais wa Tanganyika kuanzia Burma, hakuwahi kuwa hata mkuu wa Wilaya
e)Nyerere alichukiwa, Nyerere alipendwa kuliko kiongozi mwingine wa nyakati hizi na zilizopita
d)AMNUT watarudi kutawala, si kweli na wanapigwa vita na kila Mtanzania mwenye akili timamu.

Hii ni 1/100 ya sehemu ya matundu yasiyozibika kwa patex au super glue. Serious intellectual abuse,
Ningeendelea ngoja kwanza nifute machozi kutokana na hisia za uwezekano wa kizazi kijacho 'kunajisiwa'
Dah inatia uchungu sana!



-
 
Shariff Ritz,
Jamaa Ibadan imemkwama rohoni.

Kila akizunguka ataishia hapo.

Sheikh Mohamed Said,

Wewe mtu mbaya sana unawafanya watu wanataka kuchizi aisee!! ha haa haa.

Umetulizana tuli unakula faluda tu taratibani huku unarusha mipini, watu povu linawatoka ovyo.

CC: gombesugu,
 
Last edited by a moderator:

Vipi historia ya Yericko Nyerere, imefuata kanunu au wewe unaimeza mazima kama mamba wala hauitaji kuhoji chochete vipi umeishatapa nakala ya kitabu cha ugaidi kutoka kwa gwiji lenu la historia toto la Nyerere.

Kitabu cha Mohamed Said, kimefumua kabisa mfumo wako wa ubongo, ha haa ha.
 
Last edited by a moderator:
Ishakuwa "thriller in manila" itabidi sweet Ritz utupe taulo ulingoni au mpiganaji anaweza kuharibikiwa

Lady Alaska,

Mnakasha bado mpichi wala usihofu.

Hapa sisi tutakaa hata miaka tunafanya promo kitabu sasa hivi kitatafutwa kila kona ya Tanzania.

Unadhani bila JF tungepata wapi nafasi ya kuweka wazi Wazee wetu wa Mzizima.
 
Last edited by a moderator:

Kila siku nakuambia unata tatizo kubwa kwenye ubongo, kwa hiyo wewe pamoja na kujitapa msomi unaamini utamaduni wa mwafrika ni kutembea uchi?
 
Jana usiku nililala ndo maana sikujibu baadhi ya post,lakini naona kuna majibu yametolewa,nikipata muda nitaendelea na huu mnakasha.asubuhi njema wanajamvi
 

Al majununu fununu, we Abu Jahl mi na dera sijui na cheni wapi na wapi? Usifikiri kama we unavaa hivi vitu basi ni watu wote...

Si unaona sasa umekwisha beba andiko bila ku reasoning unaleta tu na mimi nimeze hapana inabidi mtu ufikiri nje ya box...
 
Last edited by a moderator:
Sheikh Mohamed Said,

Wewe mtu mbaya sana unawafanya watu wanataka kuchizi aisee!! ha haa haa.

Umetulizana tuli unakula faluda tu taratibani huku unarusha mipini, watu povu linawatoka ovyo.

CC: gombesugu,


Shariff Ritz,
Mimi nimewanyazisha Kivukoni College na kile kitabu chao cha historia
ya TANU si kwa kuuliza maswali ya kebehi, matusi na kejeli.

Nimesikizwa na ulimwengu mzima kwa kuja na historia mbadala na kusema
kuwa ile ya Kivukoni si historia ya kweli.

Hawa ndugu zangu wanasema wao hawataandika kitabu watalala jamvini
si kitu jamvi liwaumiuze mbavu.

Tatizo ni hili.
Na mimi nashinda na kulala hapa JF na kitabu kipo kinasomwa vyuoni
Ulaya na Marekani.

Na kila mwanafunzi ajaye kutoka huko waalimu wake wanamwelekeza kuwa
akifika Dar lazima aje afanye mahojiano na mimi.

Hivi ninavyoandika kuna kijana mara ya kwanza alikuja kwangu kama mwanafunzi yapata
miaka kumi imepita.

Kaja hivi sasa ananiambia kuwa sasa yeye ni mhadhiri wa chuo kikuu Idara ya Historia
safari hii amekuja kufanya utafiti kama mhadhiri anataka msaada.

Huyu binti nilipokuwa New York alikuja hotelini kwangu Manhattan na mumewe na wakanichukua
Brooklyn Height kunitembeza na kunionyesha maisha ya Wamarekani.

Hapa Brooklyn Height ndipo alikpokuwa akiishi Dr Hustable ''The Cosby Show.''
Hii show ilipendwa sana khasa na watoto.

Wakanionyesha na Financial Centre ya NYC kutoka Brooklyn Bridge.

Ipo hisani kubwa sana kati yangu na wasomi wa Kimarekani hawapungui kwangu.

Kama hali ndiyo hii vipi hawa jamaa wataweza kushindana na mimi?
 

Ya kus Mkuu wa chuo, A.K.A kasumaak narabuk, vipi nasikia uliongozana na Padre Slaa, nchini Ujerumani kwema huko? hivi ilikuwa ziara ya Chadema au alikuwa ziara binafsi?

CC: gombesugu, zomba, Kadogoo,
 
Last edited by a moderator:
Ya kus Mkuu wa chuo, A.K.A kasumaak narabuk, vipi nasikia uliongozana na Padre Slaa, nchini Ujerumani kwema huko? hivi ilikuwa ziara ya Chadema au alikuwa ziara binafsi?

CC: gombesugu, zomba, Kadogoo,

inaonekana Abu Jahl kila sehemu unamuwaza tu Dr Slaa...

Ukiendelea hivyo ipo siku utakuja kuwa kamanda, Insha Allah ipo siku ...
 
Last edited by a moderator:
Kwa niaba ya rafiki zangu,familia yangu na mimi mwenye nashukuru kwa kutumwagia dondooo kama hizi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…