Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
- Thread starter
-
- #17,181
Utizamwe kwa tahadhari kwasababu ya kauli zako, uchochezi na kuahidi usuluhishi utakaotokana na vita ya kidini na matamshi mabaya sana katika jamii (sijui kama nitaombwa ushahidi)
Nashukuru umekubali kuwa upo kujifunza na si kusomesha kama ulivyokuwa unasema hapo awali
Kazi ya mikono haikosi makosa kahiyo huna sababu za kutisha watu kwa reviews za ulaya, umeshasema ni ya mikono.
Matundu:
-Historia yako haikufuata kanuni za uandishi wa historia. Imeandikwa halafu matukio, nyakati,wahusika vikachomekwa.
-Masimuizi yako hayakufanyika kisayansi na kwa utafiti uliozingatia taratibu za utafiti bali utafiti wa ''infusion'' ya kaka yako mwenye PhD. Hakuna elimu ya infusion kuna elimu ya kusoma na katika utafiti hilo halipo.
-''Historia'' yako ililenga baadhi ya watu, matukio ya kuchagua na nyakati kama ilivyotokea
a)Kumshusha hadhi na kumdhalilisha Nyerere
b)Kuleta uchonganishi na imani zingine na hata kuwatenga wasioamini na wapagan
c)Kuwagawa watu kwa misingi ya imani na ukabila
d)Kujenga majina kwa gharama za watu wengine
-Kutokuwa na vithibitisho
a)Kuwahoji watu uliodhani wameonewa na kukosa sehemu ya pili ya waliodhulumu
c)Kutumia hisia ''inasemekana'' inasemwa, inadhaniwa, yawezekana kama vithibitisho vya tuhuma
d)Kuwatuhumu wakristo bila kuwa na ushahidi bali masimulizi ya siri baina yako na wazee wako waliojaa chuki kama wewe
- Kuficha ukweli
a)Ujio wa Mbuwane Sykes ulikusudia kuua wazalendo na msiba wake ulitokea akienda kuua Watanganyika
b)AA haikuwa mali ya K.Sykes na wala hakutoa wazo, yeye alikuwa mshiriki. Rais alikuwa Matola aliyejua anafanya nini
c)Nyerere alianza siasa kabla ya A.Sykes na alijulikana makao makuu kinyume na madai yako
d)Familia ya Sykes ilishiriki dhulma za mali ya chama kama nyumba iliyotolewa na gavana
e)Mchango wa Nyerere katika kuandika katiba ambayo haikuwahi kuandikwa tangu Mbuwane Sykes hadi Abdul Sykes
f)Nyerere alimshinda A.Sykes katika sanduku la kura mara zaidi ya moja kwa weledi
g)Michango kama ya Maryknol haikuonyeshwa kwasababu ya chuki za kiimani
h)Kifo cha AMNUT ni matokeo ya mifarakano, na ndio walioua EAMWS chini ya Sheikh Amir
i)Sheikh Amir aliendesha siasa majitaka nje ya chama,unafiki
ii)Aliwasaliti waislam kwa kukataa fursa ya kuwatumikia katika serikali
iii)Alihujumu pesa za makao makuu EAMWS na kupelekea chuki mikoani na kujitenga
Kuwagawa na kuwadharau Watanganyika
a)Kudharau jitihada za kwingineko kuhusu mapambano dhidi ya ukoloni
b)Kuifanya Tanganyika kama Narung'ombe na Kipata
c)Kuwafanya Wamanyema, Wazulu na Wanaubi kama wakombozi wa nchii hii(WWW)
d)Kuwapiga vita waislam kwa misingi ya AMNUT, ubara na (WWW)
Historia kuongoza ushawishi uliofikiriwa kabla ya historia
a)Madai yasiyo na ushahidi ya Namba za mitihani na Malima. Imehdihirika ni uzushi
b)Hotuba ya Nyerere ya kuaga, umeshindwa kutoa vielelezo vya chanzo cha matamshi uliyoyanukuu mwenyewe
c)Madai kuhusu ugaidi. Paper ya Ibadan iliandikwa kwa kunukuu bila kuangalia nukuu. Utafiti wa infusion. Uongo
d)Nyumba ya AA na TAA ilijengwa Jumapili, si kweli ilitapeliwa na kukarabatiwa jumapili na familia ya Mbuwane Sykes
e)Wamakonde wa Kipumbwi, umeshindwa kutoa ushahidi wa hilo kwa kuzingatia wakati tulio nao.
Kuwatenga Wazalendo wengine kwasababu ya Imani zao
a)Hukuwahi kumhoji Vedastus Kyaruzi hadi alipofariki hivi karibuni. Kyaruzi alikuwa kiongozi kabla ya Sykes katika siasa
b)Hakuna mahojiano na Kawawa hadi alipofarii hivi karibuni
c)Hukuwahi kufanya jaribio la kumhoji Nyerere bali ulisikia kupitia prof Othman
d)Mchango wa familia kama za Bomani haukuandikwa kama wa Mshume Kiyate na bi Farijala
e)Hukuwahi kumwelezea John Rupia zaidi ya Mshume au Idd Mwafongo kama si bi Mluguru
Kuiteka historia
a)Kuifanya historia kama ya waislam hata kama waislam wanaikataa kwa maneno
i)Abdul alisema(Mohamed)......ni kwa ajili ya ukombozi wa Mwafrika
ii)AMNUT walikataliwa na waislam wa Tanganyika
iii) Kutumia maneno sisi kuipa historia hisia zako na si za washiriki na matukio.
Kuchomeka ndoto zako kama historia
a)A.Sykes kuanzisha chama kwa fikra, katiba na mageuzi mengine yafanywe na Nyerere
b)A.Sykes hakushindwa uchaguzi mkali bai alimwachia Nyerere. Alishindwa na Nyerere katika uongozi wa TAA na TANU
c)Kumfanya A.Sykes Rais wa TANU. Hakuwahi kuwa Rais wa TANU hata sekunde moja
d)ASykes alikuwa Rais wa Tanganyika kuanzia Burma, hakuwahi kuwa hata mkuu wa Wilaya
e)Nyerere alichukiwa, Nyerere alipendwa kuliko kiongozi mwingine wa nyakati hizi na zilizopita
d)AMNUT watarudi kutawala, si kweli na wanapigwa vita na kila Mtanzania mwenye akili timamu.
Hii ni 1/100 ya sehemu ya matundu yasiyozibika kwa patex au super glue. Serious intellectual abuse,
Ningeendelea ngoja kwanza nifute machozi kutokana na hisia za uwezekano wa kizazi kijacho 'kunajisiwa'
Dah inatia uchungu sana!
-
Mkuu
Asante sana kwakushusha ukweli wa mambo!