Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

JF ni shule tosha, nilipigiwa simu kuufwatilia huu mjadala. Umenifanya nijiunge kuwa member Jf.
 
Wanaukumbi neno "ngano" lina maana gani.

Inamaana mbili,


  1. Hadithi fupi ambazo wazee huwasimulia watoto.

2. Mmea jamii ya nafaka ambao una suke kama la mpunga lenye punje fupi na nene kuliko za mpunga.

Katika dhana ya mjadala huu, tunamaanisha Hadithi fupi ambazo wazee huwasimulia watoto.
 
JF ni shule tosha, nilipigiwa simu kuufwatilia huu mjadala. Umenifanya nijiunge kuwa member Jf.

Ndiyo haya nisemayo tufanye staha na mijadala ya busara na adabu kiasi iwavute watu kuja kusoma humu.
Ikiwa mijadala yetu ni ghadhabu, kejeli na matusi hakuna atakaetaka kubisha hodi humu.
 
Ndiyo haya nisemayo tufanye staha na mijadala ya busara na adabu kiasi iwavute watu kuja kusoma humu.
Ikiwa mijadala yetu ni ghadhabu, kejeli na matusi hakuna atakaetaka kubisha hodi humu.

kweli kabisa mzee wangu, kwa leo mimi naomba kuwa msikilizaji/msomaji.
 
Itakuwa vizuri kama tunaweza kupata hiyo barua ambayo Nyerere aliliandikia Kanisa. Katika kitabu changu niemandika maneno haya yafuatayo kueleza mambo yalivyokuwa:

''...baada ya kupatikana kwa uhuru, ile nguvu ya Waislam iliyotumika kupambana na Waingereza kuleta uhuru, ikaonekana haina maana yoyote na haifai kitu tena. Kuvunjwa kwa Baraza la Wazee ndiyo ilikuwa kishiko cha mwisho cha Waislam katika TANU.

Baada ya hapo Kanisa lililokuwa pembeni wakati wa kudai uhuru sasa likajitokeza waziwazi kuwapiga vita Waislam katika TANU.

Katika kitendo ambacho kanisa halikupata kufanya, Kanisa Katoliki Bukoba liliteua wagombea wake wenyewe wapambane wa wagombea Waislam walioteuliwa na TANU kugombea nafasi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kanisa lilisema limeweka wagombea wake binafsi kwa kuwa wana elimu kupita wagombea wa TANU Waislam.

Kampeni kama hii ilifanyika vilevile Kigoma. Hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kuwa Nyerere, serikali au TANU yenyewe ilichukua hatua zozote dhidi ya Kanisa kwa kuchanganya ''dini na siasa.''
Mohamed Said,

..kuna mwana JF mwenzetu Companero anasema hiyo barua inapatikana kwenye index ya kitabu cha Van Bergen.
 
Last edited by a moderator:



attachment.php



attachment.php


attachment.php




attachment.php



wimbi la mbele,

Achalia mbali kasoro za percentage (angalia tables) hebu tuangalie tena mgawanyo wa msamaha wa kodi.
Kielelezo No 3. kinaonesha kuwa misamaha wa kodi 2007 wakristo ilikuwa 70%, waislam 7% na wengineo 23%. Lakini ukiangalia Jedwali la pili toka juu, kuna taasisi kwa majina. mfano KCMC, Bugando. Pia kuna Designated District hospitals ambazo nyingi zinamilikiwa na Kanisa. Nina maswali mawili:

1. Waislam wana hospitali ngapi? (including Designated District hospitals)

2. Misamaha ya kodi inatolewa kulingana na idadi ya taasisi (i.e hospitali) au hutolewa bila kigezo chochote?
 
Yericko Nyerere,

1} Mzee wako alipokuwa hai alikuelezea chochote kuhusu wazee wa kariakoo katika harakati za kutafuta uhuru.

2} Tupe ushahidi kuwa Chifu Maliale ndiyo aliyetoa pesa za kumpeleka Mwalimu Nyerere UN.

3} Kabla Mwalimu Nyerere ajafariki ameishawahi kuuwambia ni nani aliyekuwa rafiki yake kipenzi wakati yupo TANU.

Mkuu Yericko Nyerere,

Maswali yangu naomba majibu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mohamed Said, nimerejea baada yakuwa kimya kidogo, hii ni kwasababu ya majukumu yakusaka mkate.

Nitaelezea kwa ufupi jinsi kanisa la Tanganyika lilivyoshiriki harakati za ukombozi wa Tanganyika na madhila liliyokumbana nayo.

Ifahamike kuwa vyama vya harakati za ukombozi Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.

Mwaka 1927 – 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima.

Kisa hiki kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake.

Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake,

Mfano: 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa.

Juhudi za kanisa kupigania ukombozi ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika.

Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini. Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.

Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kassi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.

Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere zililivutia kanisa na likaamua kumuunga mkono, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu, Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni na akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia.

Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mzee Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao.

  1. Elimu,
  2. Woga

Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ikahika mkondo wake.

Mnamo tarehe 7/71954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa kanisa Katoliki (Askofu Maranda) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir)


Mpaka hapo ndugu yangu Mohamed Said angalau umepata picha kwa KIFUPI tu ya harakati za uhuru chini ya kanisa.

Nikipata wasaa nitakuletea picha za Mwalimu Nyerere na Edger Aristide Maranta

Sasa nini kilifuata baada ya uhuru? Kwanini Kasisi huyu wa kikatoliki Edger Aristide Maranta hatajwi popote katika historia ya nchi? Kwanini kanisa katoliki halilalamiki kutokuwepo kwenye kitabu cha kivuko?
Yote hayo nitakushushia taratibu kadiri mnakasha huu unavyoenda.
 
quote_icon.png
By Ritz
Yericko Nyerere,

1} Mzee wako alipokuwa hai alikuelezea chochote kuhusu wazee wa kariakoo katika harakati za kutafuta uhuru.

2} Tupe ushahidi kuwa Chifu Maliale ndiyo aliyetoa pesa za kumpeleka Mwalimu Nyerere UN.

3} Kabla Mwalimu Nyerere ajafariki ameishawahi kuuwambia ni nani aliyekuwa rafiki yake kipenzi wakati yupo TANU. /QUOTE]




MAJIBU

1) Swali hilo linajibiwa na nukuu ya mwalimu Nyerere niliyoiweka kwe uzi maalumu pale juu.



2) Kama ulifuatilia vema mjadala wangu na Mohamed Said juu ya kisa hicho nilisema mwezi kesho nitakwenda Butiama nitajitahidi walau kupata picha ya msaada huo wa Chifu Marealle

3) Sikumuuliza na hakuwahi kuniambia, lakini mimi ninajua kuwa alikuwa Mzee Mshume
 
TITI MOHAMED, NYERERE  NA BARAZA LA WAZEE WA TANU.jpg

Hakika tulikuwa pamoja

Katika picha hii yupo Mohamed Jumbe Tambaza, Bibi Titi Mohamed, Julius Nyerere, John Rupia na baadhi ya wazee katika Baraza la Wazee la TANU. Picha hii ilipigwa miaka ya mwanzo ya harakati.
 
Yericko asante kwa darasa; keep it up.

Kwa kawaida inatamkwa darsa kwa ''sekne.''
Wewe umeweka ''alif'''

Kwa lugha ya Kiarabu ambako ndiko asili ya neno lenyewe unakuwa umelikosea.
Lakini sisi ukisema ''darasa'' yote sawa.

Maana ikiwa ''darasa'' unapoteza kabisa ile filosofi yenyewe ya neno ''darsa.''
Katika darsa huwa na adabu zake.

Hakuna kejeli hakuna tusi hapo.

Wanafunzi wamepiga goti wanasoma wameinamia vitabu wanamsikiliza maalim.
Na darsa ina adabu zake wanafunzi wanasomeshwa.

Ndiyo maana mimi napata shida kufanya mnakasha mtu akikejeli au akitukana.

Naweka hapa chini zawadi kwako.

MSHUME KIYATE.jpg

Huyo ndiye Mshume Kiyate.

Rafiki kipenzi wa Nyerere kuanzia 1953 pale alipojulishwa kwake na Abdulwahid Sykes katika kundi lile la wafanyabiashara wa Karakoo Market.

Mzee Mshume ndiye alikuwa dalali mkubwa wa samaki pale sokoni biashara ambayo ilimtajirisha.

Abdulwahid alikuwa ndiye Market Master.

Mzee Mshume alikuwa mfadhili mkubwa wa TANU na alikuwa katika Baraza la Wazee wa TANU.

Nyerere alipolivunja baraza hili mwaka 1963 chini ya uenyekiti wa Mzee Idd Tulio wazee wale walisonononeka sana.
Kutokana na ustaarabu wa pwani ukifukuzwa hurejei wazee hawa wa baraza la TANU hawakurudi tena pale ofisi ya TANU yalipokuwa makao yao.

Taratibu mmoja baada ya mwingine wakafa na kuzikwa bila ya heshima yoyote ya chama au serikali.
Idd Tulio aligongwa na gari na kufa akazikwa na nduguze Waislam kimya, kimya, Mshume Kiyate aliugua kwa muda mrefu Muhimbili.

Kiongozi pekee aliyekwenda kumtembelea Mzee Mshume alikuwa Oscar Kambona na ilikuwa kumuaga maana alikuwa yuko njiani kutoroka nchini.

Hata siku ya maziko yake Mzee Mshume Mtaa wa Matumbi Dar es Salaam TANU wala serikali haikuonekana mazikoni.
Allah ana shani yake.

Pale yalipokuwa maziko yake nyumba ile ilikuwa karibu sana na mahali ambapo mwaka 1955 au 1956 Mzee Mshume alikutana na Nyerere (Cameron/Morogoro Road maarufu Mwembe Togwa sasa Faya au United Nations) akielekea sokoni wakajuliana hali na Mzee Mshume akatoa rundo la fedha kumpa Nyerere kisa ambacho nimekieleza huu ukumbini.

Kipindi hiki ni kipindi kigumu sana katika historia ya Waislam na chama cha TANU maana baada ya uhuru kupatikana zilianza kuingia fitna baina yao na Nyerere.

Hii ilipelekea kutolewa risala kwa Nyerere maarufu kwa jina ''Moto wa Waislam Ukiwaka'' risala iliyosomwa na Bilali Rehani Waikela kwa Nyerere katika ufungaji wa mkutano wa mwaka wa 1963 wa EAMWS. Inasemekana risala ile ilikuwa kalamu ya Sheikh Hassan bin Amir.

Historia ya TANU na Waislam ina mengi sana.
Mzee Mshume wanaukumbi msingemjua kama nisingemtaja humu ukumbini.
 
Back
Top Bottom