Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mkuu Mohamed Said, nimerejea baada yakuwa kimya kidogo, hii ni kwasababu ya majukumu yakusaka mkate.

Nitaelezea kwa ufupi jinsi kanisa la Tanganyika lilivyoshiriki harakati za ukombozi wa Tanganyika na madhila liliyokumbana nayo.

Ifahamike kuwa vyama vya harakati za ukombozi Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.

Mwaka 1927 – 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima.

Kisa hiki kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake.

Alipoingia askofu Edger Aristide Maranda mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake,

Mfano: 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa.

Juhudi za kanisa kupigania ukombozi ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika.

Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranda pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini. Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.

Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranda aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kassi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranda hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.

Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere zililivutia kanisa na likaamua kumuunga mkono, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu, Askofu Maranda alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni na akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia.

Wazo la Askofu Maranda lilimkaa Mzee Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao.

  1. Elimu,
  2. Woga

Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranda alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranda alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ikahika mkondo wake.

Mnamo tarehe 7/71954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa kanisa Katoliki (Askofu Maranda) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir)


Mpaka hapo ndugu yangu Mohamed Said angalau umepata picha kwa KIFUPI tu ya harakati za uhuru chini ya kanisa.

Nikipata wasaa nitakuletea picha za Mwalimu Nyerere na Edger Aristide Maranda

Sasa nini kilifuata baada ya uhuru? Kwanini Kasisi huyu wa kikatoliki Edger Aristide Maranda hatajwi popote katika historia ya nchi? Kwanini kanisa katoliki halilalamiki kutokuwepo kwenye kitabu cha kivuko?
Yote hayo nitakushushia taratibu kadiri mnakasha huu unavyoenda.

Mkuu asante kwa hili darasa!mungu ukupe afya njema uendelee kutoa elimu hii
 
Ahsante sana kwa historia hii.

Lakini hebu pitia kumbukumbu zako.
Umemtaja Sheikh Issa bin Amir.

Nadhani umekusudia Sheikh Hassan bin Amir.

Hebu niweke sawa yule ni Maranta au Maranda?

Zidi kutupa darsa.
 
quote_icon.png
By Ritz
Yericko Nyerere,

1} Mzee wako alipokuwa hai alikuelezea chochote kuhusu wazee wa kariakoo katika harakati za kutafuta uhuru.

2} Tupe ushahidi kuwa Chifu Maliale ndiyo aliyetoa pesa za kumpeleka Mwalimu Nyerere UN.

3} Kabla Mwalimu Nyerere ajafariki ameishawahi kuuwambia ni nani aliyekuwa rafiki yake kipenzi wakati yupo TANU. /QUOTE]




MAJIBU

1) Swali hilo linajibiwa na nukuu ya mwalimu Nyerere niliyoiweka kwe uzi maalumu pale juu.



2) Kama ulifuatilia vema mjadala wangu na Mohamed Said juu ya kisa hicho nilisema mwezi kesho nitakwenda Butiama nitajitahidi walau kupata picha ya msaada huo wa Chifu Marealle

3) Sikumuuliza na hakuwahi kuniambia, lakini mimi ninajua kuwa alikuwa Mzee Mshume

mkuu, kweli mzee Mshume halafu asiende kwenye maziko yake kama Sheikh Mohamed anavyodai?...hapa pahitaji utafiti.
 
Ahsante sana kwa historia hii.

Lakini hebu pitia kumbukumbu zako.
Umemtaja Sheikh Issa bin Amir.

Nadhani umekusudia Sheikh Hassan bin Amir.

Hebu niweke sawa yule ni Maranta au Maranda?

Zidi kutupa darsa.

Taarifa nilizo nazo ni kuwa aliitwa Shehe Issa bin Amir, na alikuwa ni mzee sana sawa na Kasisi Maranta kipindi wanakutana na kushauriana, huenda alikuwa baba wa Shehe bin Amir. Tuvute subira tafiti zijazo zaweza kuja kung'amua hili.


Ni MARANTA, uandishi tu ulinitereza.
 
Mkuu Mohamed Said,
Neno ngano umelileta nikajua ni wingi wa msamiati yako kama ule wa mnakasha uliotuletea hapa jamvini.
Sikujua laweza kutumbukia nyongo na kuleta muhali. Waungwana wanasema ada ya mja kunena kwa muungwana ni kitendo.

Sweke 34 kasema hujayatendea haki maoni yangu kwa kukimbia kupitia mlango wa ''ngano''
Platoozoom kasema yaweza kuwa ni maoni yangu kama unavyoniambia kila siku kuwa si lazima kuamini usemacho

Pamoja na yote hayo, nakusihi tuachane na ngano ili akina Warioba.E na wengine waliokuja kupata faida
waipate inshallah kwa mnakasha.

Kwa heshima ya wanajamvi naondoa neno lako ngano katika maoni yangu, basi nawe uwe radhia maridhyatan na utende haki kwa kujibu haya :

Mkuu Jokakuu,
Nimesoma maelezo ya Mohamed Said kuhusu Mshume Kiyate alivyomkirimu mwalim hadi kumpa pesa, chakula n.k.
Mohamed akaenda mbali zaidi na kusema Ditopile alipoelezea mchango wa Kiyate, Magazeti yalipotosha kwa kusema alimdhalilisha Nyerere kwa maneno ''kulishwa''. Hapa Mohamed anatuambia kuwa kuna kusoma habari na kupotosha habari kunakoweza kutokea. Fair enough!

Ukisoma maelezo ya vitabu tuhumiwa utaona kilichotokea ni kuchukua baadhi ya mistari na kupoteza dhana nzima.
Sina maana kila kinachosemwa hakikuandikwa, ninamaanisha kuwa kuna sehemu imechukuliwa sentensi tu na kuacha maudhui ya aya nzima. Sina hakika kama hakuna upotoshaji kama ule aliofanyiwa Ditopile.

Lakini pia lazima watu wasoma vitabu vya Mzee Said wafaham kuwa yapo mambo yaliyokuwa pre-determined kuandikwa na hivyo hutafutiwa eneo tu.

Ukisoma majibu kwa Yericko Nyerere kuhusu Mshume Kiyate, Mohamed ameelekeza tuhuma zake kwa Nyerere hasa pale anapodai kuwa kulikuwa na hujuma za jina lake kutopewa mtaa.
Kwamba Nyerere alifanya hivyo kama sehemu ya dharau na chuki kwa wazee wake.

Anachosahau Mohamed ni kuwa Tangu Uhuru, madiwani wa jiji la Dar es Salaam kwa asilimia zaidi ya 80 hadi sasa ni Waislam wakiongozwa na Mameya(mfano, Kitwana Kondo, K.Sykes, Abou Juma, Adam Kimbisa,Abdulkareen kwa uchache tu. Wakuu wa mikoa na wenyeviti wa CCM ni kama akina Ditopile, Hemed Mkali, Ramadhan Nyamka, Kandoro Abas n.k

Hakuna kumbu kumbu kama walifanya chochote na kuzuiwa zaidi ya wao kuwa sehemu ya mabadiliko ya majina kama UWT/Bibi Titi n.k. Why Nyerere na sio madiwani? Kwanini Moshi waenzi watu wao Dar washindwe? Ni kosa la nani!

Mohamed nadhani unajua chama cha wazawa wa Dar es Salaam na wazee wa Saigon.
Wote hao hukuona kama walikuwa na wajibu na hawakutenda wajibu kuwakumbuka wazee wako bali ni Nyerere tu.
Je, hapa hakuna chuki au matokeo ya kupangwa kabla ya mchezo(kuandika kitabu).

Tuambie hadi leo Dar es Salaam ina Land Mark gani kama sehemu muhimu sana ya harakati za ukombozi na sehemu ya heshima ya wakazi wake. Vijana wangapi wanajua Mzizima na asili yake.

Ni nani mwenye dhima ya kuweka mambo hayo sawa! Je, bado Nyerere anasubiriwa azaliwe upya!
Kwanini uone kiwanja cha Ponda kama sehemu muhimu sana ya maendeleo ya Waislam na usiangalie picha kwa urefu na upana wake.

Chama cha wazawa na Saigon wanafanya nini kuboresha hali za maisha za wakazi wa Jiji hasa wenyeji.
Kwanini Nyerere atupiwe lawama kwa mambo yaliyo katika uwezo wa watu ambao wamegoma kuona mbali.

Kwa vile Nyerere ''alikula njama'' za kuwahujumu waislam wasijenge chuo mwaka 1967, je chuo hicho kingejengwa kingemsaidia vipi mtu wa Nyamato, kimazicha Mkamba, Ikwiriri na Somanga ambako hakujawahi kuwa na shule hadileo hii.

Unadhani ilikuwa muhimu kujenga chuo kikuu au kujenga shule za kuwaanda wanafunzi watakaoandaa wanafunzi kwa ajili ya chuo kikuu?

Mohamed, katika ukanda wa Afrika ni nchi gani iliyowahi kujenga chuo kikuu cha kiislam miaka ya 1960-1970 ambayo tunaweza kuifanya kama model ya kuthibitisha kuwa hujuma za EAMWS ilikuwa na impact kubwa sana kwa maisha ya waislam

Mfano huu ni kuonyesha kuwa yapo mazingira yaliyoandaliwa ili kujenga mazingira yenye ushahidi usiokuwepo.
Hapo ndipo ''vitabu husika'' huelezwa kwa undani kwasababu kuna mstari mmoja au miwili inayoweza chomolewa na ku-fit the purpose.

Fikiria hivi, mambo yote yaliyotokea kati ya 1954 hadi 1985 yalimhusu Nyerere kama mtu. Leo Mohamed anasema serikali ikae na Waislam iongee nao kuhusu tatizo. Kwanini Waislam wasitake kukaa na Mwinyi, Mkapa au Kikwete bali serikali.
Lini mambo ya taifa yametoka kwa mtu na kuwa serikali? Mbona huko nyuma haitajwi serikali anatajwa Nyerere na kwanini leo hatajwi Kikwete inatajwa serikali.

Nitamwelewa kama atasema hivi, Waislam wanataka kukaa kitako na Kikwete kuelezea kadhia yao wasikilizwe.
Asiishie hapo tu, ni lazima na ni wajibu wa mtu anayetafuta suluhu kuweka kila kitu mezani.
Mohamed hawezi kutuambia kuna kadhai lakini hatuambia anafikiri suluhisho ni nini.

Hii ni kwasababu tayari ameshajenga mazingira ya ''wasikilizwe'' na wala si kusikilizwa bali kutekelezewa.
Hiyo ndio pre-determined condition ambazo zinashangaza ndani ya masimulizi na ngano za mzee wetu.

Ametoa madai kitabu kimepigwa marufuku, hajaeleza ni tamko la nani na lini! Ameshauriwa viwekwe hapa anatoa bei ya vitabu! Yote haya ni kwa kujua kuwa vitabu hivyo vikitua jamvini kwa wale wasiovisoma awali au waliosoma kwa ushabiki, ngano inaweza kuchukua mweleko mpya kabisa.

Kwa minajili ya mnkasha nisingependelea uchague maswali. Ningependelea uyajibu kama yalivyo.

Ahsante
 
Mkuu Mohamed Said,
Neno ngano umelileta nikajua ni wingi wa msamiati yako kama ule wa mnakasha uliotuletea hapa jamvini.
Sikujua laweza kutumbukia nyongo na kuleta muhali. Waungwana wanasema ada ya mja kunena kwa muungwana ni kitendo.

Sweke 34 kasema hujayatendea haki maoni yangu kwa kukimbia kupitia mlango wa ''ngano''
Platoozoom kasema yaweza kuwa ni maoni yangu kama unavyoniambia kila siku kuwa si lazima kuamini usemacho

Pamoja na yote hayo, nakusihi tuachane na ngano ili akina Warioba.E na wengine waliokuja kupata faida
waipate inshallah kwa mnakasha.

Kwa heshima ya wanajamvi naondoa neno lako ngano katika maoni yangu, basi nawe uwe radhia maridhyatan na utende haki kwa kujibu haya :



Kwa minajili ya mnkasha nisingependelea uchague maswali. Ningependelea uyajibu kama yalivyo.

Ahsante

Naaaam mkuu, bila shaka Mzee Said atajibu kwakuwa naamini ametawaliwa na busara za kiafrika.
 
Nasubiri mchango wa kanisa katika kupigania uhuru wa Tanganyika kama ulivyoahidi juzi.
Ukikamilisha tafadhali tushushie humu jamvini.
Hakuna mtu wala taasisi iliyopigania uhuru wa Tanganyika. Tulidai kistaarabu uhuru wetu kupitia UN na Waingereza walikuwa waelewa kwamba wao hawakuwa wakoloni wetu, wakatukabidhi nchi yetu, wakaondoka.
 
Hakuna mtu wala taasisi iliyopigania uhuru wa Tanganyika. Tulidai kistaarabu uhuru wetu kupitia UN na Waingereza walikuwa waelewa kwamba wao hawakuwa wakoloni wetu, wakatukabidhi nchi yetu, wakaondoka.

Sio kweli mkuu, watu walipigania uhuru wa nchi hii,

Hata Mkwawa, Kinjekitile, Mangi Sina nk walipigania uhuru

Soma makala ndogo niliyoieleza hapo juu
 
Taarifa nilizo nazo ni kuwa aliitwa Shehe Issa bin Amir, na alikuwa ni mzee sana sawa na Kasisi Maranta kipindi wanakutana na kushauriana, huenda alikuwa baba wa Shehe bin Amir. Tuvute subira tafiti zijazo zaweza kuja kung'amua hili.


Ni MARANTA, uandishi tu ulinitereza.

Itabidi nami niulize walionipita umri.

Sina kumbukumbu ya Sheikh Issa bin Amir sheikh ambaye alikuwa
na ushawishi kwa Waislam kiasi atafutwe na Father Maranta kuzungumzia
mambo makubwa ya nchi.

Lakini jambo ambalo nina hakika ni kuwa sheikh huyo hawezi kuwa baba
yake Sheikh Hassan bin Amir hata kwa mbali.

Nakushauri ujaribu "Sheikh Idrissa bin Saad" maana katika wakati huo usemao
yeye ndiye alikuwa sheikh maarufu kupita wote Dar es Salaam.

Sheikh Idrissa bin Saad alikuwa akikaa Mtaa wa Narung'ombe na Bonde nyumba
yake ikitazamana na msikiti wake.

Zipo taarifa kuwa kulikuwa na padri akimtembelea Sheikh Idrissa pale nyumbani
kwake na wakifanya mazungumzo ambayo hayakuwa ya faragha.

Hebu pita na huko.

Wajukuu wa Sheikh Idrissa bin Saad wapo na wanaishi nyumba hiyo hiyo
ya babu yao.

Ahsante kwa darsa.
 
Itabidi nami niulize walionipita umri.

Sina kumbukumbu ya Sheikh Issa bin Amir sheikh ambaye alikuwa
na ushawishi kwa Waislam kiasi atafutwe na Father Maranta kuzungumzia
mambo makubwa ya nchi.

Lakini jambo ambalo nina hakika ni kuwa sheikh huyo hawezi kuwa baba
yake Sheikh Hassan bin Amir hata kwa mbali.

Nakushauri ujaribu "Sheikh Idrissa bin Saad" maana katika wakati huo usemao
yeye ndiye alikuwa sheikh maarufu kupita wote Dar es Salaam.

Sheikh Idrissa bin Saad alikuwa akikaa Mtaa wa Narung'ombe na Bonde nyumba
yake ikitazamana na msikiti wake.

Zipo taarifa kuwa kulikuwa na padri akimtembelea Sheikh Idrissa pale nyumbani
kwake na wakifanya mazungumzo ambayo hayakuwa ya faragha.

Hebu pita na huko.

Wajukuu wa Sheikh Idrissa bin Saad wapo na wanaishi nyumba hiyo hiyo
ya babu yao.

Ahsante kwa darsa.

Kwa kuongezea kaburi la Sheikh Idrissa bin Saad lipo hapo hapo msikitini kwake mtaa wa Narung'ombe.
 
Sio kweli mkuu, watu walipigania uhuru wa nchi hii,

Hata Mkwawa, Kinjekitile, Mangi Sina nk walipigania uhuru

Soma makala ndogo niliyoieleza hapo juu
Wote hawa hawakupigania uhuru wa TANGANYIKA. Walipigania uhuru wa himaya zao. Tanganyika haikuwepo wakati huo. Tanganyika imekuwepo baada ya vita kuu ya kwanza. Iandikeni historia ya Tanganyika kama ilivyo.
 
unaleta taarifa ambazo hujazifanyia utafiti.Labda utafiti wako unaufanyia hapa JF.haya maelezo yako yanaangukia neno lako kwamba ni ngano.Unachojaribu kuandika kipeleke kwa Mohamed Said akusahihishe kama anavyofanya hapa
Taarifa nilizo nazo ni kuwa aliitwa Shehe Issa bin Amir, na alikuwa ni mzee sana sawa na Kasisi Maranta kipindi wanakutana na kushauriana, huenda alikuwa baba wa Shehe bin Amir. Tuvute subira tafiti zijazo zaweza kuja kung'amua hili. Ni MARANTA, uandishi tu ulinitereza.
 
Last edited by a moderator:
mkuu, kweli mzee Mshume halafu asiende kwenye maziko yake kama Sheikh Mohamed anavyodai?...hapa pahitaji utafiti.

Yapo maneno yakizungumzwa na wazee wa Dar es Salaam kuhusu kushiriki kwa Nyerere katika maziko ya wanaharakati Waislam.

Wanasema kuwa baada ya maneno yaliyosemwa baada ya maziko ya Abdu Sykes Nyerere aliona itakuwa bora ajitenge nao kwa mbali sana.

Unafahamu ikiwa Nyerere atahudhuria maziko ya mtu yoyote watu watataka kujua ule uhusiano kati yao.

Mathalan alipohudhuria maziko ya Abdu Sykes na akatembea kwa miguu nyuma ya jeneza la Abdu kutoka Mtaa wa Lindi hadi Msikiti wa Kitumbini kisha kutoka hapo hadi Makaburi ya Kisutu wasiojua uhusiano wa Abdu na Nyerere hata ndani ya TANU na serikali wakati ule walipigwa na mshangao mkubwa.

Jambo la kustaajabisha magazeti ya TANU chini ya Benjamin Mkaoa hayakupa uzito msiba ule ila walichoandika ni kuwa Nyerere kahudhuria mazishi ya Abdu Sykes.

Hawakueleza chochote katika mchango wake wa kumpokes Nyerere Dar es Salaam wala wa kufadhili TAA hadi TANU wala mchango wake katika kuasisi chama.

Rafiki zake Abdu kama Ahmed Rashad Ali na hata baba yangu wakawa wanasema inaelekea Nyerere hapendi kunasibishwa na historia yake mwenyewe.

Iweje Abdu asiandikiwe taazia sawa na makamu na heshima yake?
Hata binti yake Abdu alikasirishwa na jinsi historia ya baba yake ilivyopuuzwa na hawa wote walielekeza shutuma zao kwa Nyerere.

Sasa hata alipokufa Sheikh Hassan bin Amir Nyerere hakuhudhuria maziko yake, Sheikh Mohamed Ramia, Idd Tulio, Jumbe Tambaza, Dossa Aziz nk.

Swali likaja kuwa ule udugu watu hawa waliomfanyia Nyerere umekwenda wapi?
Mbona picha iliyojitokeza ni kama watu hawa hawakupata hata kujuana?

Ndiyo tena yakafuatia na haya mengine ya hao wote kufutwa katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Leo gari alotoa Dossa kumpa Nyerere kwa ajili ya shughuli za TANU New Street hakuna ajuae inaulizwa gari ya Chief Thomas
Marealle ambayo iko Butiama.
 
unaleta taarifa ambazo hujazifanyia utafiti.Labda utafiti wako unaufanyia hapa JF.haya maelezo yako yanaangukia neno lako kwamba ni ngano.Unachojaribu kuandika kipeleke kwa Mohamed Said akusahihishe kama anavyofanya hapa

Pole sana mkuu, soma mantiki ya nilichokieleza,

Muulize Mohamed Said anaelewa maana ya tunachojadili hapa!
 
Last edited by a moderator:
Wote hawa hawakupigania uhuru wa TANGANYIKA. Walipigania uhuru wa himaya zao. Tanganyika haikuwepo wakati huo. Tanganyika imekuwepo baada ya vita kuu ya kwanza. Iandikeni historia ya Tanganyika kama ilivyo.

Mkuu naomba utupe 'darsa' kwa faida ya wengi,kunaweza ibuka mkanasha mwingine hapa ninavyoona
 
Back
Top Bottom