Yericko wakati mwingine unashangaza sana, hivi unafikili mambo ya ku-doctor picha kwa kupachika au kuondoa sura ambazo hazitakiwi na DORA umeanza leo!! Mbinu hizo zilianza tangu siku binadamu alipogundua jinsi ya kupiga/safisha picha za kudumu i.e mwaka 1826 na baadae usafishaji/upigaji ukaboreshwa zaidi na Eastman Kodak kwenye miaka ya 1880s.
Taifa ambalo lilikuwa limekubuhu katika uchakachuaji wa picha za wanasiasa ni URUSI wakati wa Utawala wa dikteita J.Stalin, wanasiasa wengi na watu mashuhuri walifutwa kwenye Historia ya URUSI na sura zao kuondolewa kwenye picha za pamoja - Looking back now nafikili wanafunzi Watanzania waliosomea Urusi mambo ya siasa za ki Marxists ndio walikuja kuwa washauri wakuu katika mambo ya siasi za kiimla na uchakachuaji wa historia wa Taifa letu - aidha kwa kutaka kujipendekeza au kwa lengo maalumu - ni vigumu kuelewa kilicho kuwa kinaendelea akilini mwao - kwa nini walikuwa wamepania kumfanya binadamu mwenzetu
OMNIPOTENT?
Mimi siamini kama Mwalimu alikuwa anahafiki na kundi hili lilokuwa linampaka mafuta kwa mgongo wa chupa, wengi wao ndio tunawashuhudia wamekuwa mafisadi wa kutupwa baada ya Kambarage kutangulia mbele ya haki, kundi hili lilikuwa linamshauri vibaya Kambarage mpaka anajikuta anakorofishana na watu waliomkaribisha kwenye kundi lao bila ya ubaguzi, wanamtafutia walinzi, wanamtafutia mpishi wakati yuko katika safari za kisiasa mikoani, mpishi anahapishwa asimuwekee sumu kwenye chakula, wanabuni kila mbinu za kuhakikisha usalama wake na mengine mengi - baadae wanakuja kugeuziwa kibao na kuonekana ni watu wabaya SANA wataka shari!!
Hapo juu nimeona ndugu Jericko anazungumzia kuhusu apps za Computer, nafikili anazungumzia micro-computer (PC) kama sikosei, mkuu kwani Chuo Kikuu cha DSM hakijawahi kuwa na Main Frame au Mini Computers, je zilikuwepo tangu miaka gani? Je unajua zina uwezo wa ku-run programs zipi? Kwani unafikili hapakuwepo na programmes nyingine duniani zinazo husiana na michoro/picha kabla ya PHOTOSHOP kuingia sokoni?
Nimalizie kwa kuonyesha wana JF wenzangu picha zinazo thibitisha kwamba michezo ya ku-doctor picha ulianza zamani sana, wala uhitaji Computer kufanikisha hilo - computer haina akili za binadamu, itabaki kuwa a serial processor kwa kusubiri maagizo kutoka kwa binadamu na kufanya mahamuzi yaliyo kuwa programmed na mwanadamu, haina uwezo wa kwenda kinyume cha maagizo.
******************************************************************************************
Picha hapo chini ilipigwa mwaka 1860, hapa wali kuzuga watu kwa kumuonyesha Raisi Abraham Lincoln akiwa amesimama ofisini mwake; ukweli wa mambo ni kwamba walipachika kichwa cha Lincoln kwenye kiwiliwili cha mwana siasa mahili John Calhoun (angalia picha ya kulia)
[h=2]*********************************************************
Picha upande wa kulia ilipigwa mwaka 1936, hapo ni Mao Tse-Tung na wanaharakati wenzake, Po Ku aliposhindwa kuelewana na Mao, basi DORA ikachezea picha (upande wa kushoto) kwa kuondoa sura ya Po Ku wakiwa na madhumuni ya kumfuta katika historia ya wana harakati wa Uchina.[/h]
*****************************************************************************************
2. Picha hapo chini ilipigwa mwaka 1939, Waziri Mkuu wa Canada L.Mackenzie alimuondoa King George VI kwenye original photo na kumbakiza Queen Elizabeth ili baadae atengeneze vipeperushi wakati wa kampeini vimuongezee sifa za kushinda uchaguzi eti kwa kuwa kupiga picha na Queen!!
******************************************************************************************