Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ami,

Alhamdulilah.
Shukurani zote zinamstahiki Allah.


Alhamdulillah kwa Ilmu unayotupatia katika historia hii,,

Mnamo tarehe 9 september 2000,gazeti la majira lilitoa taarifa kuwa halmashauri kuu ya maaskofu ya baraza la kanisa la pentekoste la tanzania(PCT),Walitoa kitabu chao walichokiita "AMANI KATIKA TANZANIA ITALINDWA KWA KUTENGANISHA DINI NA MAMLAKA YA NCHI",
Walitoa tamko rasmi kuwa kwa tanzania kujiunga na shirika la OIC sharti kuwepo na kura za maoni,tamko hili la maaskofu wa kipentekoste lilitanguliwa na lile la maaskofu wa kanisa la KKKT,lililotolewa kitambo kidogo,lenyewe lilikataa kabisa wazo la tanzania kuijunga na OIC,

lile la maaskofu wa KKKT.LILIFUATIWA NA tamko la KADINALI PENGO wa kanisa katoliki,yeye alipendekeza kuwa wazo hili lazima lipelekwe bungeni,kwenye barua yake aliyomuandikia katibu mkuu wa halmashauri ya waislam tarehe 17.12.1999 mh RAIS MKAPA,KUHUSU suala hilo alisema ya kwamba ni serikali ni lazima iwasikilize wasiokuwa waislam wana maoni gani kuhusu hilo..


Sasa tukirud kwenye MEMORANDUM OF UNDERSTANDING YA 1992 BAINA YA SERIKALI NA MAKANISA ya TEC NA CCT NA MASHIRIKA YA DINI ZA NJE PAMOJA NA SERIKALI ZAO,

Kwanini serikali haikuona umuhimu wa kuwauliza wasiokua wakristo kuhus mambo nyeti kama hayo?na badala yale wakachukua tuh jukum lakufanya maamuz ambayo wanayajua wao tena bila hata bunge kuhusishwa??

Pia kama hizo kura za maoni kuhusu OIC zilikuwa na umuhimu,lini serikali iliitisha kura za maoni kuwahoji wasiokuwa wakristo kuhusu uwepo wa UBALOZI WA VATIKAN AMBAYO NI KAMA TAASISI TUH YA KIDINI NA SI NCHI YENYE MAMLAKA NA RAIA WAKE?

Yaliyofichikana na yanayoleta ukakasi ni mengi sana..
 
MM,

Abdu Sykes aongee nini na Nyerere?
Chama chake TAA cha starehe na Nyerere ana chama chake cha siasa TANU.

Wapi na wapi.

This is too low aisee. Mpaka uchangiaji mada inafikia hapa, mjadara umefika tamati. Mvuto, umakini, usikivu na uvumilivu kwa wachangiaji wakuu vinapokosekana ni kuwa hakuna tija tena hapa.
 
Namba moja ni wewe unayetoa madai usiyoweza kuyathibitisha bali kunukuu maandishi yako mwenyewe.
Ni wewe usiyeweza kutoa tafiti bali tafiti ya warsha ulioifanya wewe chini ya usimamizi wa raia wa Pakistan.

Ni Mohamed Said anayefundisha watu kulalamika bila kuweza kutetea malalamiko yako.
Ni wewe unayechukia wanadam kwasababu tu hawafuati imani yako
Ni wewe unayedhani Umanyema, uzulu na Unubi ni bora kuliko raia mwingine.

Ni wewe unayeeneza uongo, chuki, farki na kufitinisha jamii ili uuze vitabu.
Ni wewe mwenye kiu ya kuona damu ya mwanadamu inamwagika kwa gharama zozote.
Ni wewe usiyetaka kuleta utangamano wa taifa bali kuligawa kwa makundi.

Ni wewe uliyejipa haki miliki ya kuamua nani mwislam nani kafir! hata kama maneno na matendo yako hayakupi nafasi

Anayedhani wewe ni wa kudharauliwa basi ajiulize tena. Wengine wakitumia kalamu kugundua maarifa ya kumkomboa mwanadam wewe unatumia kalam ya kumwangamiza.
Kalamu yako ni kubwa maana ina rangi nzuri na za kuvutia hasa kwa wale wapendao rangi hata kama haina wino.


Hayo unayoyaongea hayabadilishi kitu chochote na wala hayawez i futa uhalisia uliosemwa na unaoendelea kusemwa..

Mihemko imekua mikali bila shaka umeshikwa na jazba,tulia kijana ulambishwe dawa..

Ni vema na vziur na wewe ukatoa hisia zako Nguruvi3' histohisia..

Lakini haitasaidia kitu,abadan asilan..

Ukweli dawa yake ni kuupokea tuh,na sio kuugeuza geuza na kuuchukia kama mnavyofanya wewe na jamaa zako..
 
Last edited by a moderator:
MM,

Sheikh Hassan bin Amir katajwa?

Vipi Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Halima Selengia, Fundi Muhindi,
Shariffa bint Mzee, Amina Kinabo, Abdallah na Maulid Kivuruga, Sued
Kagasheki, Abdallah Rutabanzibwa, Salum "Ndege Mwema" Abdallah...

Umekutana na majina haya?

Omar Suleiman, Haruna Taratibu, Ali Migeyo, Shariff Attas, Msham
Awadh, Bantu Group, Saniyyat Hubby, Al Watan, Egyptian, Bomba
Kusema...

Ingekuwa mimi naamini nimeandika historia yote nisingekuhimizeni
nanyi muandike.

Mikasa kabla na baada ya uhuru...
Nimekusoma hata hivyo.

Haya majina yalitenda kitu gani kilichotukuka that devalue historia yote wasipotajwa?
 
Haya majina yalitenda kitu gani kilichotukuka that devalue historia yote wasipotajwa?


Kama huna cha kuandika na hujui mantiki kuu ya kinachozungumzwa hapa ni bora tuh uchukue mbuzi na nazi ukae chini uandae tui..

Lakini kuendelea kuzungumza mashudu na pumba pumba ni kuonesha jins pishi lako la ujinga lilivyo jingi..
 
Kama huna cha kuandika na hujui mantiki kuu ya kinachozungumzwa hapa ni bora tuh uchukue mbuzi na nazi ukae chini uandae tui..

Lakini kuendelea kuzungumza mashudu na pumba pumba ni kuonesha jins pishi lako la ujinga lilivyo jingi..

Acha upumbavu tafuta mwingine wa kubishana nae na kutukanana nae.
Acha nijibiwe na niliyemuuliza. Am not ur type.
 
Haya majina yalitenda kitu gani kilichotukuka that devalue historia yote wasipotajwa?

Menyidyo,

Katika miaka ya 1990 wakati Kitwana Kondo ni Meya wa
Dar es Salaam alibadili majina ya mitaa na kuipa majina
ya wazalendo waliopigania uhuru.

Mabadiliko yale yalileta malalamiko mengi katika magazeti
hasa kwa kuwa majina yote yalikuwa ya Waislam.

Sarah Dumba wa RTD akafanya mahojiano na Kitwana Kondo
kuhusu kadhia ile.

Mzee Kondo akamwambia Sarah Dumba kuwa ikiwa kuna watu
wasiowajua wazalendo wale bora waulize watafahamishwa.

Menyidyo,


Majina yalotajwa ni mengi na kukuwekea hapa nani alikuwa nani
ni kazi kubwa.

Lakini ikiwa unapenda kuwajua na kujua majina hayo na nini yalifanya
katika kupigania uhuru wa Tanganyika itabidi usome kitabu changu
''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...''
 
Nguruvi,
Umeghadhibika.

Mtu akighadhibika uungwana ni kumtuliza kwanza.
Utakapotulia Insha Allah ntakujibu yote.


......

Pole kwa yote ndio ukubwa, lakini tatizo linakuja ukiwa wewe muislam ukielezea dhulma wanayofanyiwa waislamu ktk jamii ya tz ukubali litakalo kufika na kuitwa kila jina,ukirusha jiwe kizani atakae piga kelele ndie lililompata.
 
Acha upumbavu tafuta mwingine wa kubishana nae na kutukanana nae.
Acha nijibiwe na niliyemuuliza. Am not ur type.


......


Hakuna wa kubishana na wewe either. Uwe na adabu basi katika lugha zako,hatuwez kukuacha unaongea kauli zenye shombo hapa.
 
Acha upumbavu tafuta mwingine wa kubishana nae na kutukanana nae.
Acha nijibiwe na niliyemuuliza. Am not ur type.

Menyidyo,

Nakuwekea hapa kutoka kitabu changu ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes...''
Utakutana na majina ambayo lau sikuyaandika katika post ulosoma lakini naamini
itasaidia kukupa picha ya historia ya kupigani uhuru wa Tanganyika.

Ikiwa una maswali zaidi tafadhali niulixe nami Insha Allah nitakujibu ikiwa ninayo
majibu yake:

Tabora 1954

Soonafter the formation of TANU in 1954, an elder's council which had about 170members was formed at the headquarters. [1]

It was an all-Muslim committee of elders with Sheikh Takadir as its firstchairman.

A similar committee was also formed in Tabora in 1956, and Mzee FundiMuhindi, a veteran politician, founder member of the African Association inTabora in 1945 and founder member of TANU in Western Province in 1955, waselected its first chairman.

After the founding of TANU the leadership beganworking on the plan to take its case before the Trusteeship Council of theMandate Territories and to seek Tanganyika's independence.

This was to be thesecond time that Africans of Tanganyika were taking their case to the UnitedNations.

The first time was in 1952 when Kirilo Japhet went to the UnitedNations to present the Meru Land Case.

TANU came to realise that the reports by United Nations visitingmissions had very little influence on Britain. Learning from Japhet'sexperience at the United Nations, TAA had been working towards sending its owndelegate to the United Nations Trusteeship Council to plead for Tanganyika'sself-rule. It is in Nyerere's trip to the United Nations that we meet Idd FaizMafongo.


[1] The listof names of TANU Elders Council is in Elders Council Section File 376. CCMArchives.


  1. Sheikh Suleiman Takadir alikuwa mwenyekti wa Baraza la Wazee TANU HQ
  2. Mzee Fundi Muhindi alikuwa mwenyekiti Baraza la Wazee wa TANU Tabora
  3. Japhet Kirilo ni Mtanganyika wa kwanza kuhutubia UNO
  4. Idd Faiz Mafongo alikuwa mmoja wa wanachama wa mwanzo kujiunga na TANU,
na alikuwa ndiyo mwekahazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na TANU. Yeye
ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kukusanya fedha za safari ya Nyerere UNO mwaka 1954



 
Pole kwa yote ndio ukubwa, lakini tatizo linakuja ukiwa wewe muislam ukielezea dhulma wanayofanyiwa waislamu ktk jamii ya tz ukubali litakalo kufika na kuitwa kila jina,ukirusha jiwe kizani atakae piga kelele ndie lililompata.

Isalia,
Nimeishi na hali hii kwa muda mrefu sana.
 
Menyidyo,

Katika miaka ya 1990 wakati Kitwana Kondo ni Meya wa
Dar es Salaam alibadili majina ya mitaa na kuipa majina
ya wazalendo waliopigania uhuru.

Mabadiliko yale yalileta malalamiko mengi katika magazeti
hasa kwa kuwa majina yote yalikuwa ya Waislam.

Sarah Dumba wa RTD akafanya mahojiano na Kitwana Kondo
kuhusu kadhia ile.

Mzee Kondo akamwambia Sarah Dumba kuwa ikiwa kuna watu
wasiowajua wazalendo wale bora waulize watafahamishwa.

Menyidyo,


Majina yalotajwa ni mengi na kukuwekea hapa nani alikuwa nani
ni kazi kubwa.

Lakini ikiwa unapenda kuwajua na kujua majina hayo na nini yalifanya
katika kupigania uhuru wa Tanganyika itabidi usome kitabu changu
''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...''

MS
Thanks for this,
Nina afiki kwa njia moja au nyingine mashujaa ni vyema wakatambulika na kuenziwa na michango yao.
Angalizo ni kuwa focused kwa baadhi ya majina ni rahisi kuleta mgawanyiko. Nikimaanisha bila ya uzalendo tutaanguka. Uzalendo ule wa machifu kukubali kuvuliwa nyazifa katika himaya zao na kuwa na common goal.
Let us not look for mistakes our fore father did but concentrate on unity that no peace, hammony and development can occur.
Afu hata itakuwa busara
ukawa-pm hawa mabwana wakubwa ambao they just attack with no reason.
 
Acha upumbavu tafuta mwingine wa kubishana nae na kutukanana nae.
Acha nijibiwe na niliyemuuliza. Am not ur type.


......

Kama unapenda ujibiwe na mtu mmoja ungemtumia PM hii ni forum ukiweka kitu chako unajibiwa na yeyote.
 
Hivi kweli unafikiri kuna historia inawataja kila mtu ili kuonekana mtu yuko fair? Hakuna mtu anayeandika historia akaweza kuwataja wote hadi watu aliokuwa anasalimiana nao subject. Kweli kabisa katika uelewa wako wote ulitegemea historia ni lazima iwataje watu wote wa Dar-es-Salaam ambao walifahhamiana na Nyerere? Hivi kweli unafikiri wote ambao waliotoa mchango wao kwa namna moja au nyingine katika harakati za uhuru wametajwa au walipaswa kutajwa?

Kwa kweli ungeweza kabisa kuwataja wale wengine waliotoa mchango katika harakati za Uhuru bila a. Kumshambulia Nyerere na b. Kuwaacha wengine kwa sababu ya dini zao. Ulichokifanya kwa kweli ni disservice to the nation. Umeingiza udini kwenye historia na sasa historia ya Tanganyika inasomwa katika sehemu mbili "Waislamu Vs. Wakristu". Ulichokifanya ni kibaya zaidi kuliko unavyofikiria. Unaweza ukafikiri umepata sifa na heshima mbele ya Waislamu lakini kwa kweli umewafanyia faraka ndugu zako na utakuwa muungwana ukitambua hilo na kulirekebisha. Hakuna sifa katika faraka.

Kaka unataka kutuambia hawa wazee aliowataja MS walikuwa wanasalimiana tu na Mwalimu Nyerere wala hakuna haja ya kuandikwa kwenye historia?
 
This is too low aisee. Mpaka uchangiaji mada inafikia hapa, mjadara umefika tamati. Mvuto, umakini, usikivu na uvumilivu kwa wachangiaji wakuu vinapokosekana ni kuwa hakuna tija tena hapa.

.......

Menyi,

Mimi hawa watu ninaowaleza ni wazee wangu na katika mjadala
huu nimejitahidi sana kueleza historia yao.

Katika uhuru wa Tanganyika ni tabu kukwepa ''Muslim symbols.''
Mtafiti yoyote hili atakutananalo na lipo wazi bila kificho.

Kwa bahati mbaya hicho ndicho kinachowakera wengi humu.
Matokeo yake ikawa ni matusi, kejeli na kebehi.

Sasa na mimi mara moja moja nawalipa kwa sarafu ile ile yao
wenyewe.

Lakini ikiwa mtu atakuja kwangu kwa adabu na kutaka kujua
mimi nitajibishananae kiistarabu na wala si lazima akubaliene
nami.
 
Haya majina yalitenda kitu gani kilichotukuka that devalue historia yote wasipotajwa?
mmh kweli wee mbaguzi.

yaani hujui kabisa hio ndio miamba na majabai makubwa sana katika kuijenga TANU?

Ama kweli umekosa fadhwila.
 


Katika uhuru wa Tanganyika ni tabu kukwepa ''Muslim symbols.'' Mtafiti yoyote hili atakutananalo na lipo wazi bila kificho.


........

Hapa ndio mara nyingi unaonesha jinsi usivyo makini katika kujenga hoja. Hakuna mtu anayetatizika na "Muslim symbols". Unafikiri kuwa sisi ni kama Wamarekani au watu wengi wa magharibi ambao kwao Uislamu ni "dini nyingine".

Unavyozungumza ni kana kwamba sisi wengine wote tunauona Uislamu kama adui au Waislamu kama siyo wenzetu. Hili ni kosa kubwa la kimantiki. HIvi umemuuliza nani humu kujua kuwa anakwaza na alama za Uislamu?

Nyerere kwenda kuombewa na wazee wa Kiislamu iwe Bagamoyo au Mnyamani Tanga yeye akiwa ni Mkatoliki je iwakwaze Wakatoliki? Kwanini? Kinyume chake inawafanya watu wamuone Nyerere kama the most tolerant, inclusive leader we have ever had.

Kwamba kwenye mikutano ya Nyerere wanasoma Qurani na kumuombea dua wazee wa Kiislamu iwe kikwazo? why? Labda useme inakukwaza wewe kuwa Mkristu tena Mkatoliki Nyerere alikubalika hivyo, kupendwa, kulindwa na kuheshimiwa na wazee wako wa Kiislamu kiasi kwamba inakushangaza.

Kitu ambacho hujaweza kukisema yumkini ni kuwa wazee wako hawakupaswa kumkirimu na kumpa heshima na uongozi huyu Mkristu Mkatoliki. Kwa sababu ni "mwingine"!

Wengi wetu hapa unapotusimulia jinsi Waislamu na Wakristu walivyoshirikiana katika kupigania uhuru na kulinda umoja wa kitaifa, udugu na heshima ya Mtanzania tunaona fahari.

Tunawaona wazee wetu wa Kiislamu kutoka Tanga wakisimama dhidi ya baadhi ya wazee wako waliotaka kuleta udini kwenye siasa; tunawaona wazee wa Kiislamu wakisimama na Nyerere kumheshimu na kumpenda. Wengi wao hawakudai lolote zaidi ya kusema na wao wametoa mchango wao.

Hizi unazoiita "alama za Waislamu" ukweli ni kuwa ni alama zetu pia. Hivi leo tukifanya shughuli yoyote siyo kwamba tunawaita watu wa dini mbalimbali wakatoa dua zao kwa mujibu wa imani zao? Tumefanya hivyo toka zamani kwanini tukwaze?

Hivi unajua kama kuna kitu ambacho Watanzania tunaporudi nyumbani kama tukiwa nje (hasa hizi nchi za Magharibi) hakuna kitu kinakufanya ujisikie uko Bongo kama kusikia Muazin anaitisha Swala!

Lakini hizi alama za Uislamu ni nini basi? Kama Wakristu hawakwazi na alama hizi za UIslamu na hakuna Mkristu ninayemjua ambaye amewahi kulalama kwanini watu kama wewe ukwaze na alama za Wakristu katika nchi yako?

Prof. Mazrui alisema vizuri sana na labda ujifunze kwake - huu ni urithi wetu wa pande tatu. Uafrika, Uislamu na Ukristu ni urithi wetu sisi watu wa Afrika ya Mashariki. Mimi binafsi kwa mfano, hadi leo hii kutokana na mazoea yangu ya kukulia na kusoma miongoni mwa Waislamu nyama zote ninazonunua nanunua kwenye duka la Waislamu.

Siyo kwa sababu za kidini bali najua naweza kufikiwa na wageni marafiki zangu Waislamu hivyo sitaki kuwalisha haramu. Na siyo mimi tu wapo Wakristu wengi tu ambao toka zamani wamewaheshimu ndugu zao Waislamu, wamesaidiana, wameoloeana na kuuguzana na kuzikana; wameshirikiana katika furaha na machungu. YOte wameyafanya bila kujali dini zao.

Hadi ulipotokea wewe na siasa zako za utengano, chuki, kisirani na kisasi. Usipoangalia mzee wangu historia itakukumbuka vibaya kweli kwa kushindwa kutumia yale unayojua kuponya taifa lako na badala yake unajitahidi kila kukicha kueneza propaganda za chuki na itikadi ya mfarakano.

Mzee Said simama uhesabiwa katika kujenga taifa letu; tumia historia uijuayo kuwaleta Watanzania pamoja. Usifanye dhulma ile ile kwa Wakristu ambayo unadai Wakristu wameifanya kwa Waislamu. Si msamaha ni bora zaidi kuliko kisasi Quran inafundisha? Mzee Said tafuta upendo zaidi kuliko chuki, umoja kuliko utengano, uponyaji kuliko kujeruhi.

Imeandikwa: ...Wa Bil-Wālidayni 'Iĥsānāan Wa Bidhī Al-Qurbá Wa Al-Yatāmá Wa Al-Masākīni Wa Al-Jāri Dhī Al-Qurbá Wa Al-Jāri Al-Junubi...Surat Al Nisa (Mwanamke) 4:36

Mzee Said watendee wema (hisan) wote hao na majirani zako walio karibu na waliombali. NI mapenzi ya Mungu hayo. Sijui kama una ndugu Wakristu lakini ungekuwa nao ungeelewa hisia zao kutokana na unachokifanya. Umeambiwa uwafanyie wema ndugu zako pia. Haikusema ndugu zako wa dini moja tu.
 
Kaka unataka kutuambia hawa wazee aliowataja MS walikuwa wanasalimiana tu na Mwalimu Nyerere wala hakuna haja ya kuandikwa kwenye historia?

......

GG,

Mwanakijiji kapwelewa.

Nyambala kanishushia Hansard na akafuatisha na maneno makali ya kebehi kwa wazee wetu kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini kwa hiyo hakuna cha Abdu Sykes wala bastola yake nk.nk.

Mimi nikamwekea TAA HQ 1950 Political Subcommittee ya akina Sheikh Hassan bin Amir na kutiwa Earle Seaton katika TAA kama mwanasheria asaidie katika masuala ya udhamini wa Tanganyika.

Jamaa kanihamakia. Soma post yake.

Dullah kawaambia hamtuwezi. Kinachowauma ni kuwa wazee wetu haya wameyafanya 1950 ndani ya TAA
na Nyerere hayupo.

Unajua wanashindwa kukubali ukweli kuwa ni baada ya Nyerere kutoka UNO ndipo akaanza kuwika Tanganyika nzima.

Kusema hivi si kumvunjia staha yake bali ni ukweli wa historia ya uhuru na ukweli wa maisha yake.
 
Back
Top Bottom