Nguruvi,Hayo mengine uloandika sitayazungumza.Nitazungumza kuhusu kauli ya Sheikh Ilunga kuhusu ''kisasi.''Sheikh Ilunga kazungumza kuhusu kisasi.Katika Uislam kisasi ni haki.Haya ni maneno yake Allah mwenyewe.Hata hivyo Allah kaeleza mengine katika hicho kisasi.Kuna kusamehe pia.Filosofi ya kisasi ni kuwa kinafanya watu waogope kuwafanyia ubaya wenzao kwa kujua kuwa na wao yatawakuta.Huu ni uwanja wa maulamaa.
Uislam umekataza mtu kuzungumza kitu usichokuwa na ujuzi nacho.
Ukiangalia mazingira aliyoongelea Ilunga ni yale ya mauaji ya Sheikh Rogo. Na kwa mujibu wake mauaji hayo yamefanywa na serikali.
Yeye anasema kwa uchache sana kuwa njia ya kuzuia hayo ni kutafuta Askofu mmoja na kuua kama kulipiza Kisasi.
Akanukuu aya inayozungumzia Kisasi ingawa sijui kama aliinukuu yote. Ninachojua hakueleza kisasi hicho kimetafsiriwa vipi kwa mifano, hadithi n.k. hadi kufikia hapo. Kwa maneno mengine amechukua mistari michache tu na kuwalisha wasikilizaji wake. Hilo sina ujuzi nalo na wala sitaki kulizungumzia kwa maana ya tafsiri n.k.
Lakini basi busara zinasema iweje mzozo wa Kenya aufanye uwe wa Tanzania? Na kwanini mazingira ya Kenya ayafananishe na Tanzania. Ni kwanini mzozo wa waislam na Polisi uingize watu wengine. Kwa mantiki yako Mohamed, ninani anatishwa hapo na kwasababu gani, ni Polisi au Maaskofu na kwa nini.
Kuna connection gani kati ya maaskofu na Polisi wa Tanzania
Kwa vile kauli hiyo imeleta utata sana miongoni mwa wenye weledi basi ni hatari sana kwa akina 'sisi'' wanao amini kuwa dini ni yale anayosema sheikh wala si kisomo na fikra. Hawa ndio tunaona wanabeba maneno ya ''kisasi ni haki'' ili mradi kasema sheikh na mabalaa yameonekana.
Kama mtu huyu angekuwa na Ilm kweli kauli ile asingeitoa katika mazingira yale na kwa wepesi ule kana kwamba kuua ni kama kupopoa embe Ng'ongwa. Kwamba Uislam umeagiza kufanya hivyo.
Tunaambiwa(na hapa nisahihishwe) kuwa kuzini tu hukumu yake inahitaji mashahidi walioona na si kuona walioshuhudia utupu mmoja ukiingia kwingine(ashakum) kwa macho yao. Hapo ndipo Fatwa inaweza kutolewa.
Tazama ugumu wa kutimiza jambo hilo, leo iweje Ilunga asikie hadithi za Kenya ambazo hajui kiini chake na azitumie katika kutoa Fatwa dhidi ya watu wasiohusika kwa maneno rahisi na mepesi kiasi kile? Hebu nieleimishwe hapa.
Hata ukichanganya vitu vinne, Sheikh Rogo, Polisi, Kenya, Tanzania na Maaskofu hakuna flow of information zinazounganisha habari nzima. In other words alitumia tu jina la Rogo na Uislam kuchochea mauaji bila kuwa na msingi wa kauli zake. Ndiyo maana tunaonya sana kuwa majina na matukio ni njia nyepesi sana ya kupandikiza chuki iwe kwa mahubiri au historia.
Kila mtu ana namna ya kueleza hisia zake,Ilunga kaelezea hisia zake kwa style anayoiona yeye ni muafaka kulingana na uelewa wake yeye kidini huku akinasibisha na hali halisi iliyotokea kwenye jamii yake,
Kumuuliza muislam mwingine kuhusu uhalali wa yale aliyoysema Ilunga ni kutaka kupima yeye upande gani kuhusu yale aliyoyazungumza Ilunga,ndio tunakujibu sasa Maulamaa kazi yao ni kutoa fatwa'a katika vipengele tata vinausisha sharia za kiislam na hekima inayostahiki kutumika,,
Jiulize kwanin mtu kama ilunga aibuke leo kuongea haya,miaka yote alikuwa wapi?,je ni ishara ya kukosa uvumlivu au ishara ya kuona unyonge umeongezeka upande wao kutokana na wao kutozungumza yanayowasibu?
Kila tukio tulionalo sasa halikuja kwa bahti mbaya..
Kwangu mimi kilichonivuta ni kauli ya Mohamed kuwa Ilunga ana Ilm kubwa. Nadhani ana Ilm lakini je anaitumiaje Ilm hiyo? Ndipo nikamuuliza Mohamed kuhusu msimamo wake kwa mtu anayemtaja kuwa ana Ilm na mentor wake. Kikubwa zaidi ni kile alichowahi kukisema Mwanakijiji kuwa generalization katika maongezi na maandishi ni kitu kischo sahihi.
Unaposema Ilunga ametumwa na waislam akahubiri kuhusu mfumokristo, swali ni kuwa ni waislam wapi hao? Maana kuna BAKWATA, Shia, Ismaili, Kamati ya mali za waislam, kamati ya haki, Baraza kuu, Muslim foundation n.k. Sasa ni kundi lipi ambalo Ilunga anliwakilisha na kwanini kundi la Ilunga liwe waislam?
Kuhusu Ilunga kuonyesha hisia zake hilo nalo lina utata. Mathalani, kwanini yeye ahimize watu wakaue kwa siri? Kwanini wasiende kuua hadharani ili wawe mashahidi na waonyeshe hisia zao( ni mfano kwasababu siafiki mauaji ya kiumbe chochote). Endapo angekwenda yeye hadharani hilo lingekuwa hisia, lakini kuwaambi watu ua kwa siri usijulikane hapo hakuna hisia kuna uhalifu kwa mwenyezi mungu (mtazamo wangu).
Sijui ni Maaulamaa wangapi wamekaa na kuwafikia wale waislam waliokuwa wanamsikiliza Ilunga. Watu wale waliondoka na kutawanyika wakijua kuwa ''kisasi kwa Askofu ni haki'' sasa utawapata wapi kuwaelezea kiini, chimbuko na maana nzima iliyokusudiwa kwa hilo lenye utata.
Sidhani kuwa kauli zake zinatokana na kukosa uvumilivu. Kama kuna kukosa uvumilivu kwasababu hawasikilizwi tutauliza je wale Wasomali wamekosa uvumilivu wa kutosikilizwa na nani? Je, wale Sunni wanaowalipua Shia kule Iraq na Pakistan nao wamekosa uvumilivu kwa kusikilizwa na nani? Nataja huko kwasababu hakuna sababu ya kukosa uvumilivu mahali penye asilimia 100 au 99 ya waislam.
Mtu kama Ilunga na wengine walikuwepo,na huko nyuma hawakusema hayo.
Kinachotokea ni kuwa wachungaji wenye dhamana wameamua kukaa chini ya mti ili wachome nyama ya mbuzi na kuacha makundi ya ng'ombe,kondoo na mbuzi yakijiendea bila uelekeo. Fisi, Chui na Simba wanatumia fursa hiyo kushibisha matumbo yao.