Nilipo RED.
naomba usahihishe hapo. Zanzibar hakuna UDINI kwani raia wa nchi hiyo more than 99.9% ni waislam, Je udini huo utatoka wapi?
Fuatilia katika wabunge wake wa kuchaguliwa na wanchi more than 99% ni waislam na wawakilishi wake wa kuchaguliwa na wanchi 100% ni waislam .
Je udini huo utatoka wapi?
Barubaru hapa si suala la quantity tu, udini ni pamoja na tolerance.
Wazanzibar wanaposema Wakristo wanakuja znz kufanya abdc huo ni udini.
Waznz wanaposema Nyerere alipeleka ukatoliki huo ni udini
Lakini udini zaidi ni pale wznz wanaposema wao 99.9% ni waislam.
Sijui Uislam unautafsiri vipi kwasababu kupata 99 ni jambo linalohitaji fikra zaidi.
Je 1% mbayo ni sawa na 12,000 kwa population ya 1.2m ni idadi ndogo ya kuweza kuondolewa katika population
12,000 kwa upande wa znz ni jimbo la uchaguzi. Kwahiyo huwezi ku-ignore constituent hiyo.
Je, kila anayeitwa Mohsin ni mwislam. Vipi wale wenzetu ambao si rizki nao wanaingia katika uislam na kama hawaingii wanaingia wapi! 1% au wanaongezea idadi n.k.
Hoja yangu kubwa ni kuwa majina kwa asilimia 99 ni ya kiislam lakini si lazima wawe waislam na hivyo ku-justify kuwa kisiwa kina 99% ni ku-ignore facts nyingine.
Unapomchapa mtu risasi eti kwasababu tu anaimani tofauti huo ni udini (nakusubiri hapa maana utakuja na hoja fulani)
Unapochoma nyumba ya ibada kwasababu hutaki iwepo znz huo ni udini.
Unapomwita mtu asiye mzanzibar kafir huo ni udini.
Tukiangalia kwa namna za kufyonza ilm ni kweli 99% ni waislam, tukiweka fikra si kweli na idadi iliyobaki inapuuzwa kwasababu tu si waislam. Huo ni udini.
Kwahiyo udini si suala la namba ni suala la analysis hasa tukiangalia tolerance,mtazamo wa jamii husika kuhusu imani,na jamii inaangalia vipi wale wasiofanana na jamii hiyo!
Naweza kusema Iran siyo wadini kama Zanzibar! ipo hoja hapa