Ndugu zangu Watanzania,
Mpaka sasa haieleweki ni nani alishauri ,kuwashauri na kuwapa mawazo ya kishetani BAWACHA kuchoma vitenge hadharani.kitendo walichofanya BAWACHA na kuungwa mkono na chama kizima pasipo kukemewa wala kuonywa na kujitenga na kitendo kile cha kishetani ni laana kubwa sana ambayo imeingizwa ndani ya CHADEMA.
Huwezi ukachoma moto kitenge kizuri .wakati huo huo mtaa unaotokea kuna wajane wenye shida za mavazi,kuna wajane wenye kushindia kitenge kimoja wiki nzima,kuna wajane wameachiwa watoto wadogo au wachanga na wanakosa hata kitenge cha kubebea mtoto mgongoni halafu wewe unakwenda unachoma kitenge hadharani?
Unachoma kitenge wakati huohuo mtaani kwako kuna wazee wanakosa kitenga au hata kanga tu ya kuvaa? Unachoma kitenge wakati kuna binti yatima jirani yako hana hata kitenge cha kujifunga au hata kuvaa? Unachoma kitenge wakati pengine hata mama yako mzazi aliyepo kijijini au mtaa wa pili ana shida ya nguo na huna hata uwezo wa kumvika ,ila kwa ulimbukeni na kufuata Mkumbo unatoka hadharani na kujipiga picha unachoma kitenge?
Hivi BAWACHA walitumia nini kufikiria mpaka kufikia maamuzi hayo? Kwanini wanakosa akili ,ufahamu na busara? Unachomaje vitenge wakati kuna vituo vya kulelea watoto yatima vinahitaji vitenge na vinatamani hata kupata kitenge hata kimoja tu kwa ajili ya kuwapa watoto wanaowalea?
Kwanini uchome kitenge mtu mzima mwenye akili Timamu na unayejitambua? Ndugu zangu Watanzania kiroho ni laana kubwa sana ambayo wanawake hao wa CHADEMA wameleta ndani ya CHADEMA ,ambayo itakiteketeza chama kwa moto mkali sana kupita ule wa kuchoma vitenge.
Ni laana imeingia ndani ya CHADEMA,hawatakaa wawe na amani maishani mwao wasipofanya kutubu,hawatakaa wapate amani ya moyo,hawatakaa waache kuweweseka kila wawapo usingizini,hawatakaa waache kuona mikosi ikiandama maisha yao,hawatakaa waache kuona mambo yao yakiharibika na kukosa muelekeo.
Gadhabu ya Mungu itakuwa juu yao na wataona uzito mzito ukiwa juu ya maisha yao,mipango yao kamwe haitafanikiwa na itakuwa ikivurugika hovyo hovyo kwa kila wapangacho.watakuwa ni watu wa kuhangaika na kutanga Tanga muda wote bila mafanikio wala matunda ya kazi yao.kila watakachoshika na kugusa kwa mikono yao hakitafanikiwa.Ni laana imebebwa na kubebesha uzao wao.kila kizazi kitaikuta laana hiyo iliyopandwa,kitakuta mbegu ya laana ikiwa imekomaa vizuri na ikitafuna vizuri bila huruma.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.