DOKEZO Uchotwaji pesa za mfuko wa jimbo la Musoma Mjini zaidi ya Tsh 59,981,000. Tunaiomba TAKUKURU iingilie kati

DOKEZO Uchotwaji pesa za mfuko wa jimbo la Musoma Mjini zaidi ya Tsh 59,981,000. Tunaiomba TAKUKURU iingilie kati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hii ni baada ya wananchi kuhoji matumizi ya fedha hizo bila majibu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 15, ndipo wameamua kuitisha mjadala kwenye group la CCM Musoma Mjini ambapo mbunge wa jimbo hilo Vedastus Mathayo, akaelekeza katibu wake aweke mitasari ya vikao vya kamati ya mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo akianza na mwaka wa fedha wa 2021/22 ambapo kikao hicho kwa inaonekana hakikufuata utaratibu wa kisheria kwa kuwekwa wajumbe ambao hawakutajwa na sheria Na 16 ya mwaka 2009 iliyotungwa na bunge inayosimamia mifuko ya majimbo Bara na Zanzibar

Hata hivyo manunuzi yaliyofanyika hayakufuata taratibu za manunuzi kitu ambacho kimezua mjadala mkali na mbunge kutoa majibu yasiyoridhisha akidai kama kuna mwanachi hakuridhika waende katika vyombo vinavyohusika na kuelekeza katibu wake aweke muhtasari wa mwaka wa fedha wa 2022/23 na 2023/24

Baada ya mitasari hiyo kuwekwa ndipo diwani mmoja ambaye ni mmoja wa wajumbe katika kamati ya mfuko wa jimbo ameshangaa kuona kuwa kikao hakijawahi kufanyika katika mwaka wa fedha wa 2023/24 na matumizi ya fedha kiasi cha sh milion 59,981,000 kinaonekana kutumika katika miradi ambayo ilishafanyika katika kipindi cha 2022/23 ndipo mzozo mkubwa kwenye group hilo ukaibuka na hatimaye katibu wa CCM wilaya akalifunga group hilo kwa muda kisha akalifungua mijadala ikaendelea ambapo wananchi hawakuridhishwa na report ambazo dhahiri, zimeghushiwa na kutaka majibu fedha hizo

Baadaye leo tarehe 28 usiku mwenyekiti wa CCM wilaya ndugu Magiri akataka mijadala ya mfuko wa jimbo isitishwe katika group hilo, hali iliyoleta taharuki, mitasari yenyewe ipo na ninaiambatisha hapa, tunaomba "TAKUKURU"mkoa wa Mara ifanye uchunguzi wa sakata hili na kuwahoji wahusika maana hata mitasari ya vikao yenyewe inaleta mashaka makubwa

Na kwa mujibu wa vyanzo vya ndani kwa maana ya watumishi ni kwamba fedha za mfuko zilizotoka mwaka wa fedha 2023/24 zilienda kulipa wakandarasi waliofanya kazi ya ufunguaji wa barabara zilizokuwa hazipitiki katika kata 10, kazi iliyofanyika mwaka wa fedha wa 22/23 kiasi chote cha sh 59,981,000, hii ikiwa ni baada ya wakandarasi hao kudai fedha hizo kwa muda mrefu bila mafanikio huku meya na mbunge wakijibu kuwa pesa za jimbo hazijatoka hali ya kuwa pesa hizo zilirejea kutoka hazina
 

Attachments

Pesa za mfuko wa jimbo huwa ni za kupiga tu, sionagi manufaa yake zaidi ya kutokuwa na hsabu zilizo wazi
 
Back
Top Bottom