UCHUMBA WA JF: Timed Bomb!!!

UCHUMBA WA JF: Timed Bomb!!!

M24 Headquarters-Kigali

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
8,199
Reaction score
8,186
Wadau mara kadhaa nimejitokeza hapa JF kutafuta wachumba lakini matokeo yake ni DISASTER tupu maaana nimekutana na vitimbi vya hatari ikiwamo kukutana na Visirani, Gold Diggers,vijizi & Matapeli wa mapenzi .

Leo nitawapa mfano wa mdada mmoja baada ya kuona tangazo langu JF akani-PM na kuniuliza kama nimeshapata mtu nikamuambia hapana basi tukapeana namba za simu, kasha tukapanga kukutana pale KIJIJI CHA MAKUMBUSHO KIJITONYAMA mi niliwahi zaidi yeye alipofika akanipigia kuwa kafika duuh kaja na marafiki zake wa 3, nikawakaribisha tukapata vinywaji na chakula nikalipa bill kiukweli nilishindwa kuongea nae kwa nafasi maana ni kama hao marafiki walikuwa wanapiga stori zisizonihusu. basi tukamaliza tukaagana jioni yake bibie akaniomba nimuazime laki 5 maana kuna mzigo ameagiza Dubai sasa inapaswa alipie kwa agent Duuh nikajiuliza huyu binti

1. ameniletea umati siku ya kwanza tunakutana

2. ananiomba pesa laki 5 ghafla tu. NIKACHANGANYA AKILI ZANGU.

NIKAAMUA KUMPOTEZEA sasa akaanza kunibip nikawa sipokei, sms sijibu mwishoni akaanza kuniporomoshea mitusi gunia. ooh mwanaume gani wewe! hata laki 5 huna, mara mwanaume suruali duuh!!! wadau ukitafuta mchumba JF kuwa makini
 
Back
Top Bottom