Jamani, msilie na hii mikataba kwani kanuni yake ilikuwa ni ndogo sana. Na michezo yenyewe ilikuwa kama ifuatavyo.
Kimsingi Bepari hakufutii deni hata siku moja. Mliposikia kuwa Mkapa kafanikisha kufuta madeni kulikuwa na gharama ya kulipa vile vile. Gharama yake ndio ilikuwa kulilipa deni hilo kupitia madini, indirectly. Tukajisifu sana kwa kufutiwa madeni, kumbe tuliliwa. Sasa mchezo umeanza, mnalilia nini. India walipotaka kufutiwa walikataa, mnajua kwanini? Kwasababu walijua gharama yake ilikuwa kubwa zaidi. Hivi kweli nyie watanzania mliamini kuwa tumefutiwa deni hilo kabisa, hata kifutia jasho wao wasipate? Hiyo sahau kabisa, nafikiri mmesahau Nyerere aliwaitaje hawa "mabepari, wanyonyji, kupe" na kila aina ya jina ilimradi tu ionyeshe jitu fulani lisilokwenda kwa hasara.
Mkapa aliambiwa na alifahamu na akatuacha majuha kama Nyerere alivyotuacha na kipindi cha miezi 18 ya shida baada ya Vita vya Uganda. Kumbe alielewa ni milele, na imetoka. Hata hivyo hii ni fundisho kwa Watanzania. Watanzania amkeni, msipende vya bure!!!!!!!!!