SoC04 Uchumi katika kilimo na maeneo ya kilimo

SoC04 Uchumi katika kilimo na maeneo ya kilimo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mnzavatekina

New Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
3
Reaction score
0
Nchini Tanzania, Sekta ya Kilimo ni muhimili wa maendeleo ya uchumi. Sekta hii inachangia kiasi cha nusu ya pato la Taifa, robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na chanzo cha chakula pamoja na utoaji wa fursa za ajira zaidi ya 75% ya Watanzania. Hali hii inatupa uhalisia na yakini kwamba kilimo ni uti wa mgongo katika taifa la Tanzania.

Kuimarisha uchumi wa Taifa letu, ni vema kama Taifa tukaamuwa kujikita katika kilimo kama ambavyo Raisi Mh. Dkt Samia Suluhu Hasani raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alivyojikita katika kuwaimarisha vijana na kuwawezesha katika kuwapa mafunzo ili wapate ujuzi katika swala nzima la kilimo hapa nchini.

Katika chapisho langu hili nitajikita katika uwekezaji wa kilimo katika maeneo mbalimbali hapa nchini ilikulifikia lengo la Mh. Dkt Samia Suluhu Hassani katika miaka ya mbeleni.

Tanzania ni Eneo lenye kilometa za mraba 947,303 (nchi ya 31 duniani); na Idadi ya watu kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 ilikuwa 61,741,12, (nchi ya 24 duniani) kutoka 44,928,923 waliohesabiwa katika sensa ya mwaka 2012, likiwa ongezeko la 3.2% kwa mwaka.

Kulingana na takwimu hizi, Tanzania ni nchi yenye ukubwa wa kutosha kuhakikisha tunajikwamua kiuchumi kupitia kilimo tija chenye manufaa kwa Taifa letu. Kama nchi tunaouwezo mkubwa wa kuhakikisha tunalisha nchi za Afrika Mashariki zote na kuwa na uhakika wa akiba kubwa ya chakula ndani ya nchi.

Naamini ardhi tulio nayo inaweza kutuwezesha kufanya Zaidi ya hapa tulipo ndani ya miaka mitano kuhakikisha kwamba uchumi ndani ya nchi yetu unakuwa kwa asilimia kubwa kulinganisha na miaka mingine ya nyuma.

Yapo maeneo ambayo kama nchi tunahitajika kuchukua uamuzi mzito wa kuhakikisha tunayatumia kikamilifu katika kulikwamua Taifa katika uchumi wa kijani. Mfano wa maeno hayo ni eneo lililopo kisangara mkoa wa Kilimanjaro (shamba la katani), eneo lililopo barabara Toka Tanga hadi Kihaba pwani, eneo lililopo kambi ya jeshi Dodoma baina ya mashamba ya jeshi na wananchi chihikwi pamoja na maeneo mengine makubwa ambayo mazao hayatupi tija sisi kama taifa.

Haya ni baadhi ya maeneo tu lakini yapo maeneo mengi katika nchi yetu tumeyaacha na yanakuwa kama mapori katika nchi, bila kujua thamani yake. Tunahitajika kuyatumia kuleta mabadiliko yenye tija katika taifa letu.

Maeneo haya yanahitaji nguvu kubwa ya serikali kuweka miundombinu iliyobora ya kufika katika maeneo haya na kuboresha miundombinu katika maeneo mengine ambavyo yanafikika kwa tabu. Katika muktadha huu, serikali inahitajika kuweka utaratibu wa kilimo bora cha umwagiliaji na kuhakikisha kama taifa tunatumia jeshi letu, wafungwa na kuajiri vijana wengi ambao hawajapata ajira ili kuhakikisha tunazalisha mazao mengi ya biashara pamoja na chakula.

Sambamba na hilo kama taifa tutakuwa tumetatua swala la upungufu wa ajira katika nchi yetu kwani tutakuwa tumeajiri wafanyakazi wa kutosha katika maswala mazima ya utayarishaji wa mashamba kwajili ya kilimo, waendesha mitambo ya kulimia mashamba, wataalamu wa umwagiliaji, wataalamu wa ufatiliaji wa tabia ya ardhi ya zao linalokubali katika eneo hilo, watoaji huduma katika mashamba katika maswala ya maradhi katika mazao, wavunaji wa mazao kwa njia ya kisasa kabisa kwa kutumia mashine, watunza maghala ya mazao yetu tulio yafuna, wasafirishaji wa mazao kutoka shambani hadi kwenye maghala, wasafirishaji wa mazao kutoka maghalani hadi kwa mtumiaji (mnunuzi nnje ya nchi). Hizi ni baadhi ya ajira ambazo taifa tutazitengeneza kama tukiamuwa kujikita katika kilimo chenye tija kubwa katika taifa letu.

Sambamba na hilo tutafanikiwa kupata chakula kwajili ya magereza yetu nchini, mashuleni na taasisi nyingine mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali. Nchi ya Tanzania ni nchi ambayo imejaaliwa maeneo mengi ambayo yapo hayatumiki na si katika maeneo ya hifadhi za mbuga za Wanyama.

Kilimo chenye tija kubwa cha umwagiliaji katika maeneo hayo ni kama ulimaji wa mahindi, alizeti, maharage, mpunga na aina nyingine mbalimbali kulingana na aina ya eneo ambalo litatumika katika wakati huo. Sisi kama taifa hatuna budi kujipanga kikamilifu kuhakikisha maeneo yote yenye tija kwa taifa yanawekewa miundombinu bora ikiwemo:-

  • Barabara zinazofikika
  • Maji ya kutosha kwajili ya umwagiliaji
  • Uwepo wa umeme kwajili ya usindikaji mzuri wa mazao yetu
  • Mashine za kisasa za upandaji, uvunaji, na ubambuaji kwa aina ya mazao na
  • Miundombinu mingine yenye kuhitajika kuwepo katika maeneo hayo ya mashamba.
Jambo hili, linaweza kukamilika kama taifa tutashirikiana na wawekezaji wa ndani ya nchi wenye uwezo kwa kuhakikisha haya tunayo yapanga watayafanya kikamilifu au kuwa na ubia nao katika ufanyaji wa shughuli hii kubwa ya kilimo katika nchi yetu.

Taifa letu linaloongozwa na mama yetu mpedwa Rais Mh.Dkt Samia Suluhu Hasani ikiamuwa kikamilifu kuyatumia maeneo haya ambayo nchi imeyaacha tu bila ya kuyatumia inaweza kulisaidia taifa letu na kulifanya kuwa taifa lenye uchumi mkubwa baada ya miaka kumi.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom