SoC02 Uchumi na Utawala Bora Tanzania

SoC02 Uchumi na Utawala Bora Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

YAHAYA YANGE

New Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
1
Reaction score
0
MADA; UCHUMI NA UTAWALA BORA  TANZANIA.
UTANGULIZI
nchi yeyote ile Ili ikue kiuchumi inahitaji serikali iliyo bora na imara, Kwa maana ya kwamba serikali ambayo misingi ya democrasia na haki za raia. Serikali ambayo itasimamia rasilimali za taifa lake Kwa umakini mkubwa, kuziendeleza na kutengeneza ajira Kwa kiasi kikubwa. Mfano Tanzania inaweza kujifunza kupitia nchi kama Marekani, Uingereza na Japani ni nchi ambazo zimeendelea Kwa kiasi kikubwa hii ni kutokana na kuwa na serikali ambazo ni imara katika kuboresha mahusiano ya raia wake, Uchumi na usimamizi wa rasilimali zake, kupitia democrasia, Demokrasia ambayo inawapa watu uhuru wa kuchagua, pia mifumo imara ya biashara na uwekezaji.

Rufiji_Mission.jpeg
#credit: Picture by embassy of republic of Tanzania
KIPI KIFANYIKE KUBORESHA UCHUMI NA UTAWALA TANZANIA.


Kuunda sera bora na kuzisimamia.
kama nchi inatakiwa kuwa na sera ambazo zinamanufaa Kwa taifa, Sera zenyelengo la kuinua na kusimamia uchumi. Kwa miaka mingi sana Tanzania imekuwa ikipitia kwenye sera za kubadilika badilika, kitu ambacho kinasababisha sekta mbali mbali kushindwa kuendelea na hii inatokana na mitazamo tofauti tofauti ya viongozi ambao wanaliongoza taifa.Mfano Raisi wa awamu ya tatu Mh. Mkapa alikuja na sera kama "Tanzania bila  UKIMWI inawezekana", Raisi wa awamu ya nne mh. Jakaya Mrisho Kikwete alikuja na sera kama "Hali mpya nguvu mpya na Kasi mpya" mwaka 2005, ikafuatwa na awamu nyingine ya serikali chini ya Raisi John Joseph pombe magufuli ambaye alikuja na sera kama "Tanzania ya viwanda". Hizi ni sera tofauti tofauti ambazo kama taifa linapitia kutoka katika viongozi tofauti tofauti Kwa vipindi tofauti, sera kama hizi za kubadilika badilika zinaliweka taifa katika njia panda, lakini Kwa kiasi kikubwa zinakosa utekelezaji hivyo kupoteza ufanisi, zimekuwa kama kauli tu za kisiasa na maono ya viongozi husika tu.

Kama taifa ni bora likawa na sera za kudumu ambazo zimechanganuliwa vizuri, zenye uwezo wa kuinua na kuimarisha uchumi,kujenga taifa na misingi bora ya kiserikali na kiuongozi Ili Kila kiongozi ambae anaingia madarakani aweze kuzisimamia Kwa ufanisi na zifanywe kama sheria.

2. Kulinda haki za raia na kuzisimamia
Kila raia anahaki ambazo zinapaswa kulindwa kama ambavyo zilivyoorodheshwa katika katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kuanzia ibara ya 12 mpaka ibara ya 29katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi ambayo inakumbukumbu mbaya zaidi katika kusimamia haki za raia na democrasia hii inatokana na Sheria ambazo ni kandamizi na zisizo angazia haki za raia. Mfano mwaka 2020 bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania lilifanya mabadiliko katika Sheria zake (Basic rights and duties enforcement Act, Cap 3, R;E 2014) wakibadili kifungu namba 4Basic rights and duties enforcement Act, Cap 3, R; E 2014, ambacho kina mpa mtu uhuru wa kufungua kesi mahakamani ikiwa moja wapo wa haki zake au haki za mtu mwingine zikiwa zimevunjwa kama zilivyoorodheshwa katika katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.Lakini mabadiliko yaliyofanywa kupitia Sheria(written laws (miscellaneous amendment)No. 3) Act , 2020, kifungu Cha 7(b),(2)written laws (miscellaneous amendment)No. 3) Act , 2020, mabadiliko hayo yanazuia kufungua kesi mahakamani inayohusiana na uvunjaji wa haki za msingi za raia kama zilivyoorodheshwa kwenye katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, mpaka mtu aweze kuthibitisha kuwa ameathirika na uvunjaji wa haki za msingi za raia yeye binafsi, hii inawanyima raia haki zao za msingi, mfano kuna makundi maalumu kama watoto, walemavu, wazee, ambao wanahitaji kuwakilishwa na kutetewa haki zao, lakini pia mabadiliko haya yanazuia taasisi mbali mbali na makundi ya kiraia katika kutetea haki za raia, kama ilivyotokea katika kesi ya Rebbeca gyumi dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali.

Kinachotakiwa kufanyika hapa, serikali inapaswa kulinda haki za raia na misingi ya kidemokrasia Kwa kuunda Sheria ambazo sio kandamizi hii itapelekea uhuru wa kujieleza na uhuru wa kuikosoa serikali pale inapofanya vibaya, hii itaboresha utawala bora na itachochea uwajinikaji, hivyo kuleta mabadiliko chanya nchini.

4by7660bb0f3571z0r4_800C450.jpg
#Credit: picture by pars today.
3. Kuweka mifumo bora ya uwekezaji na ukusanyaji kodi.
kama nchi inapaswa kuhakikisha mifumo ya uwekezaji inakuwa rafiki na rahisi, hii itasaidia kuvutia wawekezaji hivyo kuja Kwa wingi nchini kuja kuwekeza, kuunda Sheria zenye nia njema na dhabiti ya kusimamia na kukuza uwekezaji hii itachangia Kwa kiasi kikubwa katika ukuzaji wa uchumi kupitia ukusanyaji kodi na kutengeneza ajira nchini hivyo kupunguza wimbi kubwa la ukosaji wa ajira. Katika nyakati tofauti Tanzania imekuwa na Sheria na sera mbovu katika uwekezaji, mfano mzuri serikali iliyoingia madarakani mwaka 2010, haikuweza kuwa na sera na Sheria bora za uwekezaji, wawekezaji walitozwa kodi zaidi ya mara mbili hii ilipelekea kuzorota Kwa uwekezaji nchini.

Katika ukusanyaji kodi Tanzania inapaswa kama nchi kuhakikisha inatafuata na kuunda Sheria na njia nzuri za ukusanyaji mapato na kusimamia, kuondoa kodi kandamizi na zisizo na malengo bora Kwa raia na nchi, hii itasaidia ukusanyaji mapato Kwa wingi na kuhamasisha ulipaji kodi bila shuruti. Mifumo mibovu ya ulipaji kodi imekuwa ni moja ya sababu ya kuharibu uwekezaji na kuchochea umaskini nchini, mfano uanzishwaji wa tozo za miamala ya Simu na Benki, tozo hizi zimekuwa kero Kwa wananchi na wawekezaji kiasi kwamba wawekezaji na makampuni ya Simu na Benki wanaingia hasara kwasababu imepelekea raia kuacha na kupunguza kutumia Simu na Benki katika kufanya miamala, kodi kama hizi ambazo sio rafiki zinazorotesha uwekezaji na kuyaingiza katika hasara makampuni ya biashara, mfano, kampuni ya Simu ya Vodacom imetangaza hadharani kuwa tangu kuanzishwa Kwa hizi kodi imeingiza hasara zaidi ya billion 103.8 Tozo zaisababishia Vodacom hasara ya Tsh. Bilioni 103.8.

4. Kuboresha mifumo ya elimu.

Elimu pia ni moja ya nyanja muhimu sana katika kukua Kwa nchi na maendeleo ya taifa, mifumo ya elimu ya Tanzania imekuwa mifumo sugu katika kuchochea umaskini nchini hii ni kutokana na mfumo huo kuwa mrefu na usio na tija, mfano mwanafunzi anasoma kuanzia darasa la kwanza mpka darasa la Saba akiwa na masomo yote kama kiswahili, kiingereza, sayansi, na maarifa ya jamii na elimu Kwa ngazi ya msingi hutolewa Kwa lugha ya kiswahili,ngazi ya pili ni elimu ya sekondari ambayo hii hufundiswha Kwa kiingereza, hapa mwanafunzi yule yule ambaye amesoma kiswahili Kwa zaidi ya miaka Saba elimu ya msingi, elimu ya sekondari anaianza Kwa kiingereza hii imewawia vigumu wanafunzi wengi na kusababisha kufeli hivyo kuzorota Kwa elimu.

Mbili, changamoto nyingine ni katika masomo ambapo mwanafunzi anapata nafasi ya kuchagua masomo anapokuwa katika ngazi ya tatu ya elimu ya sekondari, lakini Huku nyuma kote mwanafunzi huyu anasoma masomo yote, hii inapoteza mda lakini pia inamfanya mwanafunzi kutoelewa vizuri haya masomo.
Changamoto ya tatu, ya elimu hapa nchini ni katika kutengeneza ajira hasa kwa vijana wanapomaliza elimu ya vyuo vikuu, elimu iliopo nchini haimtengenezi mwanafunzi kuwa na uwezo wa kujiajiri hivyo anapomaliza elimu ya chuo kikuu mwanafunzi huyu hana pa kwenda zaidi ya kukaa na kusubiri kuajiriwa jambo ambalo ni gumu hapa nchini, elimu kama hii inapotezea watu muda na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

Ili kuboresha elimu nchini kama taifa linapaswa kuangalia mifumo bora ya elimu, mfano katika lugha ya kufundishia ni bora ikachaguliwa lugha moja ikatumika Kwa ngazi zote za elimu kulikp hii ya kubadilika badilika Kwa lugha inachanganya wanafunzi hivyo kuzorotesha mfumo mzima wa elimu, na katika uchaguzi wa msomo ni bora serikali ikaangalia namna nzuri ya kumfanya mwanafunzi kuchagua masomo mapema na akaendelea nayo kwenye ngazi zote, mfano labda mtoto anapewa fursa ya kuchagua masomo ya kusoma akiwa darasa la Saba, hii itamfanya ayaelewe vizuri kuliko ya kuja kuchagua masomo katika ngazi ya elimu ya sekondari hii inachosha na inapotezea muda, pia kama serikali inapaswa kuangalia namna nzuri ya kutoa elimu ambayo itawezesha wanafunzi wanapomaliza wawe na uwezo wa kujiajiri, mfano kuboresha utoaji wa elimu ya ufundi(VETA) na ujasiria Mali Kwa vijana wote kwani ndiyo elimu zenye ufanisi mkubwa katika kujiajiri.

istockphoto-1323715308-1024x1024.jpg

#Credit: picture by iStock.


 
Upvote 0
Back
Top Bottom